08-01-2021, 11:54 AM
KIPINDI CHA PILI NA CHA TATU
(Angalizo: Hivi ni lazima viwe vimepishana kwa wiki kadhaa )
Kabla ya kusoma
Uliza tena maswali kuhusu muundo wa hadithi na jinsi maneno na picha vinavyochangia katika muundo huu.
Baada ya Kusoma
Imechukuliwa kutoka: Swain, C. Gazeti Msingi la Kiingereza (The Primary English Magazine)
Andika hadithi ubaoni, lakini usiandike kichwa cha hadithi wala sentensi mbili za mwisho (‘Alitoa shuti – chini kuelekea kulia. Goli zuri!’) ubaoni mpaka sehemu ya mwisho kabisa ya somo lako.
[Kukimbilia utukufu na Mark Northcroft (umri miaka 12 )]
Alikimbia tena na tena. Miguu yake iliuma kama tindikali. Aliweza kusikia waliokuwa wanamfukuzia wakiwa wanamkaribia. Alihisi kuwa asingeweza kukaa nao sana na kwa muda mrefu lakini alijua lazima afanye vile. Hatua zilikuwa zinamkaribia. ‘Haraka! Haraka!’alilia. ‘Siwezi! Siwezi!’ alijibu. Alijisikia nguvu kutoka sehemu fulani ndani ya mwili wake. Sasa alijua kuwa atafanikiwa.
Ghafla mtu alitokea kusikojulikana. ‘Nipate sasa au nisipate kabisa,’ alifikiri.
[Alipiga shuti – chini kuelekea kulia. Goli zuri!]
Tanbihi
‘Miguu yake iliuma kama tindikali’ – Tashbiha hii au ulinganisho huu si rahisi kuueleza lakini unaweza kusema kuwa mwanaume au mvulana huyu alijisikia maumivu katika miguu yake kana kwamba kulikuwa na mchanganyiko wa kemikali iliyokuwa inachemka.
Maswali ya kuwauliza wanafunzi katika maandalizi ya uandishi wa mwanzo na mwisho mbadala wa hadithi hii
(Angalizo: Hivi ni lazima viwe vimepishana kwa wiki kadhaa )
Kabla ya kusoma
- Umeshafikiri kuhusu kile kitabu tangu tulipokisoma kwa mara ya mwisho?
- Ungependa kukisoma tena?
- Nisimulie unachokumbuka zaidi kuhusiana na kile kitabu.
Uliza tena maswali kuhusu muundo wa hadithi na jinsi maneno na picha vinavyochangia katika muundo huu.
Baada ya Kusoma
- Umegundua kitu chochote wakati huu ambacho hukukigundua kabla?
- Unajisikiaje kuhusiana na hadithi hii baada ya kuisoma tena?
- Unapofikiria kitabu hiki sasa, ni kitu gani muhimu kuliko vyote kwako kuhusiana na kitabu?
Imechukuliwa kutoka: Swain, C. Gazeti Msingi la Kiingereza (The Primary English Magazine)
Nyenzo-rejea 3: Hadithi
Nyenzo-rejea ya mwalimu kwa ajili kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunziAndika hadithi ubaoni, lakini usiandike kichwa cha hadithi wala sentensi mbili za mwisho (‘Alitoa shuti – chini kuelekea kulia. Goli zuri!’) ubaoni mpaka sehemu ya mwisho kabisa ya somo lako.
[Kukimbilia utukufu na Mark Northcroft (umri miaka 12 )]
Alikimbia tena na tena. Miguu yake iliuma kama tindikali. Aliweza kusikia waliokuwa wanamfukuzia wakiwa wanamkaribia. Alihisi kuwa asingeweza kukaa nao sana na kwa muda mrefu lakini alijua lazima afanye vile. Hatua zilikuwa zinamkaribia. ‘Haraka! Haraka!’alilia. ‘Siwezi! Siwezi!’ alijibu. Alijisikia nguvu kutoka sehemu fulani ndani ya mwili wake. Sasa alijua kuwa atafanikiwa.
Ghafla mtu alitokea kusikojulikana. ‘Nipate sasa au nisipate kabisa,’ alifikiri.
[Alipiga shuti – chini kuelekea kulia. Goli zuri!]
Tanbihi
‘Miguu yake iliuma kama tindikali’ – Tashbiha hii au ulinganisho huu si rahisi kuueleza lakini unaweza kusema kuwa mwanaume au mvulana huyu alijisikia maumivu katika miguu yake kana kwamba kulikuwa na mchanganyiko wa kemikali iliyokuwa inachemka.
Maswali ya kuwauliza wanafunzi katika maandalizi ya uandishi wa mwanzo na mwisho mbadala wa hadithi hii
- Unafikiri ‘A’ ni nani?
- Unafikiri yuko wapi?
- Unafikiri nini kitamtokea?
- Nani ‘mwanamume’?
- Watu gani wengine wanaweza kuwa sehemu ya hadithi hii?
- Kutakuwa kumetokea nini kabla ya sehemu hii ya hadithi?
- Nini kinaweza kutokea baadaye?
Mwl Maeda