MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NYOYO ZETU

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: NYOYO ZETU
#1
NYOYO ZETU
Kwa moyo mie nakiri, Natamka kwa ulimi
Nyota nimeitabiri, Nikawa sina usemi
Bora nifichue siri, Ninayempenda mimi
Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida

Macho hayakukosea, Yalipokuona wewe
Na nafsi kungojea, Nikangiwa na kiwewe
Huu wangu upokea, Moyo nakupa mwenyewe
Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida

Zama za tokea enzi, Nilikupenda kwa dhati
Moyo kujawa mapenzi, Kukupata ni bahati,
Naeleza kwa utenzi, Maandishi yenye hati
Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida

Waja wa kale wanena, Ya kweli usikatae
Mahaba yenye kufana, Mpende akupendae
Simfanyie khiyana, Moyo wake uutwae
Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida

Penzi sitie ukungu, Sitochoka kukungoja
Asali isiwe chungu, Wewe ndiwe namba moja
Usinitie machungu, Moyo damu ukatoja
Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida

Kila jambo la msingi, Ndani yake lina kheri
Tutavikwepa vigingi, Tuepukane na shari
Mahasidi kwetu wingi, Usinambie kwaheri
Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida

Penzi la watu wawili, Kulipangua mashaka
Nimeshapima akili, Kuamua nakutaka
Nakupenda kikamili, Sitoitoa talaka
Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida

Unikumbuke kwa huba, Usingizini na ndoto
Tuitane mahabuba, Huku kipeana joto
Ulojaliwa mahaba, Na mapenzi motomoto
Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida

Wala sione aibu, Na kuniwacha njiani
Unitibu nikutibu, La azizi u’mwandani
Tulishane na zabibu, Tukiwepo kitandani
Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida

Tamati nimeshafika, Namalizia shairi
Nimechoka kuandika, Nimepungukwa na ari
Nakupenda kwa hakika, Mpenzi usighairi
Ingawa tu mbalimbali, Nyoyo zetu si baida

Na.
TRT Swahili
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)