MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
NADHARIA YA U-MARX

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
NADHARIA YA U-MARX
#1
Maana ya Umarx:
Wamitila,(2006:182) anasema, umarx ni falsafa ya kiyakinifu hasa kwa kuwa pana msisitizo mkubwa kwenye msingi wa hali za kiyakinifu za maisha kama mazingira ya kuishi kuliko mawazo katika maisha ya binadamu (ikimaanisha kwamba mawazo yake hayategemezi kwenye dhana dhahania kama urembo, ukweli au ndoto bali anayategemeza kwenye uhalisia unaoonekana.
Nadharia ya umarx ilianzishwa na Karl Marx mwaka 1818-1863 na Fredrich Engles (1820-1895).Katika nadharia hii Marx amejikita katika historia na miundo ya kijamii kwa kupitia hoja kuu zifuatazo.
Historia ya maisha ya binadamu inaweza kuelezeka katika misingi yakinifu ya kiuchumi ambayo itachunguza njia za uzalishaji mali pamoja na miundo ya kiuchumi na pia huathiri uzalishaji mali na usambazaji wa mali hizo. Hivi vyote kwa pamoja huunda misingi ambapo kwenye misingi hiyo huunda maadili, itikadi, dini na utamaduni.
Hoja nyingine ni kuamini kuwa historia ya binadamu inadhihirisha au kuakisi harakati zinazoendelea katika matabaka ya kiuchumi-jamii. Marx alisema “Historia ya maisha ya binadamu ni ya harakati za kitabaka”.
Harakati za kitabaka katika jamii. Nadharia ya ki-marx inaangalia matabaka katika ngazi mbalimbali kama vile ngazi ya familia, dini na elimu.
Ubepari kama njia ya uzalishaji mali na mara nyingi huharibiwa na tabaka la chini, hivyo ubepari hujitengenezea njia za kujiharibu wenyewe. Kutokana na unyonyaji na ukandamizaji unaoufanya kwa tabaka la chini.
Njia ya kuondokana na ubepari huu jamii lazima ikemee.
Mshikamano uliopo baina ya tabaka tawaliwa. Kwa mujibu wa marx ili kuondokana na mfumo wa unyonyaji na ukandamizaji, jamii lazima iungane ili kubadilisha mfumo uliopo.
Matamanio ya kitabaka yanaakisi jamii hiyo au itikadi ya jamii iliyopo. Kwa mujibu wa nadharia ya umarx tabaka la chini itikadi yao ni kupambana na tabaka la juu ili kuondokana na unyonyaji na ukandamizaji na tabaka la juu itikadi yao inaonekana kuwa ni halali kulikandamiza tabaka la chini.
Fasihi inayojitokeza inaweza kuyaakisi au kuyadhihirisha mahusiano ya nguvu katika jamii, matamanio na matakwa ya matabaka yaliyopo katika jamii yanaakisiwa katika itikadi iliyopo katika jamii.
Sifa za Uhakiki wa kimarx:
Kuna muelekeo mkubwa wa kuitazama sanaa katika nadharia hii kwa kutilia mkazo mkubwa kwenye dhamira.
Ni mkabala ambao unaingalia fasihi kwa kuhusisha na mazingira yake ya kihisitoria pamoja na shughuli zingine za kibinadamu.
Ni nadharia inayopinga au mtazamo wa kubagua au kutenga fasihi na mazingira yanayoizaa kama ilivyooneshwa kwenye nadharia nyingine kadhaa.
Kwa kuhimiza kuchunguzwa vipengele vya kijamii na kiuchumi uhakiki unaelekea kupanua uwanda wa fasihi.
Udhaifu wa nadharia hii ya Kimarx:
Uhakiki wa Ki-marx unaishia kuidunisha na kuipuuza kazi ambayo ina sifa za kiwango cha juu sana za kiujumi au kisanaa kwa kuwa ni dhaifu kiitikadi licha ya kuwa itikadi sio kaida au kanuni ya sanaa au ubunifu. Hatuwezi kupuza kazi kwa misingi ya kiitikadi tu.
Hivyo huzichunguza sifa mbalimbali za kazi ya kifasihi pale tu zinapoingiliana na miundo ya kihistoria jamii au kiuchumi kwa kufungamana na itikadi yake.
Matokeo ya mtazamo huu wa kuyamulika zaidi masuala ya kidhamira yanaifanya nadharia hii kutoangaza vipengele vingine vidogovidogo ili kutathimini ubunifu au upekee wa kazi inayohusika.
Unaelekea kuchunguza muktadha wa kihisitoria kwa kuelemea mno kwenye vigezo vya kiuchumi.
Jamii ni kielelezo kinachoshikiliwa kama upeo wa kuendelea na kusambaratika kwa mfumo wa kibepari unaoelekea kuwa na elementi za kinjozi.
Namna ya kutumia uhakiki wa Ki-marx katika kazi za kifasihi.
Miaka ya hivi karibuni uhakiki wa kazi za kifasihi umezidi kupanuka katika kuelezea masuala ya kijamii na kisiasa. Hivyo unapotumia uhakiki wa ki-marx katika kazi za kifasihi lengo ni kuonesha tofauti za kijamii, kisiasa, kiuchumi kulingana na maelezo yalivyo katika kitabu. Hii inaonesha itikadi ya kijamii ya mwandishi na kuweka uhusiano kati ya uzoefu wa kijamii wa mwandishi na wa wahusika wake.
Katika kutekeleza itikadi za uhakiki wa ki-marx kuna hatua tano za kufuata ili kuhakiki kazi ya fasihi kwa ufanisi.
Kueleza jinsi wahusika wanavyohusiana: Uhusiano baina ya watu, muingiliano wao utaonesha madaraja na ishara fulani zinazoendana na tofauti za matabaka ya kijamii.
Kutathimini kazi za wahusika:
Uhusika wao umejikita katika mifumo ya kimatabaka ambapo kazi anayofanya mhusika inaashiria moja kwa moja sehemu alipo katika mfumo. Kiwango cha anasa na kiwango cha utendaji kazi navyo vinaonesha sehemu alipo katika mfumo.
Kuonesha jinsi wahusika wanavyotumia muda wao wa mapumziko. Nadharia ya ki-marx inaeleza kuwa mtu anauwezo wa kutumia muda wake wa mapumziko kwa namna ya uzalishaji mali au anavyopenda yeye. Huu muda wa kupumziko huashiria namna mtu anavyoishi na jamii inayomzunguka.
Kutathimini jukumu la serikali,
kuonesha mfumo wake, vyombo vya utekelezaji na jinsi jamii inavyopokea mafanikio yake.
Kurejea waandishi wengine wa ki-marx na kutafiti vipindi ambavyo kazi hiyo ya kifasihi imechapwa na kisha kuhusianisha mawazo yaliyotolewa na kipindi hicho
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)