MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

LEO KATIKA KAMUSI ‘Watumiaji wa lugha wanavyochanganya viambishi ko-po na mo-‘

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
LEO KATIKA KAMUSI ‘Watumiaji wa lugha wanavyochanganya viambishi ko-po na mo-‘
#1
Karibu katika KAMUSI.
KAMUSINI LEO tunaangazia kuhusu namna watumiaji wa Lugha ya Kiswahili wanavyochanganya na kukanganya baadhi ya viambishi/ vipashio vinavyodokeza : hali ya kuwa pahala pa jumla, muhususi na ndani ya…
Viambishi hivyo ni : – ko , – po na – mo.
Tutazame mifano hapa chini:
( i) Kiselekete yuko Tanzania
(ii) Leo yupo kijijini kwao. Maneremango.
(iii) Muda huu yumo msikitini.
Ukichunguza sentensi hizo tatu katika mpangulio huo kutoka i hadi iii mtawalia, utabaini kuwa kuna maneno yanayodokeza kuwapo sehemu fulani..
Mathalani:
Katika ( i ) yuko , hii – ko hapo hudokeza kuwa sehemu ya jumla. Yaani haijabainishwa dhahiri kuwa Kiserekete anapatika sehemu gani mahususi nchini Tanzania. ( Yuko sehemu fulani Tanzania).
Katika ( ii ) Kuna – po , hiyo po hudokeza sehemu mahususi. Sehemu inayofahamika katika maeneo maalum. Hapo hata ukimwitaji Kiserekete unajua anapopatikana huko kwao Mwanaromango.
Katika ( iii) kuna – mo, hiyo mo hudokeza sehemu ndani ya kitu.
Kwa hiyo, Kiserekete katika sentensi hiyo ya iii inadokeza kuwa anapatikana ndani ya msikiti kwa muda huo.
Matumizi haya ndiyo matumizi sanifu ya Kiswahili ingawa Waswahili wenyewe wamekuwa wakitumia viambishi/ vipashio hivi kwa kuvibadili. Hata hivyo, wenyewe huwa wanaelewana.
Aidha, matumizi mingine ya viambishi hivi ni haya yafuatayo:
Mosi, – ko hutumika kuulizia swali. Kwa mfano : Choo ki- ko =
: Vyoo, vi- ko =
( a) choo kiko wapi? Mtu huyu hafahamu pahala maalum kilipo choo. Kadhalika Vyoo.
( b) Hodi! Mama yuko wapi? ( Bado muuliza swali hajui aliko mamaye.
( c) IST iko wapi ? ( Hiyo iliyohongwa).
Pili, – po , wakati mwingine – po hutumika kwa tashtiti. Kwa mfano, unaweza kuwa unaongea na mtu kisha ukamuukiza ‘ upo’?
Indhari:
Watumiaji kwa kadri wanavyotumia lugha hasa viambishi vilivyobainishwa hapo juu , ni muhimu kutochanganya na aghalabu huwa hawachanganyi kiambishi – mo, ( kiambishi kinachodokeza ndani ya…) na vile vingine vya – po na – ko.
Mifano zaidi :
( a) Nimo ndani
Tumo kwenye gari
Mmo hotelini?
Maji yamo kwenye ndoo.
(Sentensi zote hizo zinadokeza undani ).
( b). Tembo wako wapi ? ( Swali)
( c) Tembo wapo Mikumi
( Wapo katika mbuga maalum ya Mikumi.)
………….. …Mwisho…………
Asanteni sana. Endelea kutufuatilia.
Usithubutu kupitwa na KAMUSI.
KAMUSI imeletwa kwenu kwa hisani ya Utu- Tanzania, Culture Link Africa Ltd na Kamusi Pevu ya Kiswahili.
Tuandikie : majidkiswahili@gmail.com Au +255 715 838480
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)