MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'MBUZI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'MBUZI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'MBUZI'

Neno mbuzi katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/wa-] yenye maana zifuatazo:

1. Mnyama wa kufugwa mfano wa swala mwenye pembe za ncha zinazoelekea nyuma ambaye hufugwa kwa ajili ya maziwa, nyama na ngozi, mnyama mwenye miguu minne aina ya mamalia ambaye huzaa na kunyonyesha.

2. Kibao mithili ya kigoda chenye panda mbili ambacho upande mmoja huwekewa chuma bapa chenye meno kinachotumika  kukunia nazi, kifaa ambacho kinatumika kukunia nazi na pia huweza kutumika kama kiti kidogo.

3. Jina mbadala kwa kundinyota la jadi (Capricornus).

Etimolojia ya neno hili mbuzi ni lugha za Kibantu likiwa na maana ya mnyama aliyetajwa na kifaa cha kukunia nazi ambacho huitwa pia kibao cha mbuzi.

Wazulu wa Afrika ya Kusini wanatumia neno ' imbuzi' wakati Waajemi wa Irani wanatumia neno ' boz' (بز) na Waarabu wanatumia neno ' maaiz' (ماعز).

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)