MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'SHEHE'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'SHEHE'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'SHEHE'

Neno *shehe* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: a-/-wa, wingi: mashehe*] yenye maana zifuatazo:

1. Mtu mwenye kiwango cha juu cha mafunzo ya dini ya Kiislamu ambaye pia huwa na jukumu la kuwafundisha wengine.

2. Mtu mzima aghalabu mzee ambaye jamii inampa heshima kubwa kutokana na hekima na busara zake.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *shehe*( *soma: shaykhun/shaykhan/shaykhin شيخ )* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Mtu mzima aliyefikia umri wa zaidi ya miaka 50.

2. Mtaalamu wa dini kwa Waislamu

3. Mwanazuoni wa taaluma yoyote ile.

4. Mwalimu anayewafundisha wengine.

5. Mkuu wa ukoo au kabila.

6.  Mtu yeyote mwenye cheo au hadhi mahali fulani.

7. Likiongezwa neno Al-Aqlun (akili) Shaykhul Aqli شيخ العقل kiongozi mkuu wa dini/Madhehebu ya Ad-Duruuz.

8. Likiongezwa neno Az-Zawjat (mke) Shaykhuz Zawjat  شيخ الزوجة mume wa mtu.

9. Likiongezwa neno An-Naaru (moto) Shaykhun Naar شيخ النار ibilisi, Shetani.

Ingawa neno shehe ndilo lililosanifiwa na kusajiliwa kamusini, Waswahili wa mwambao wa Afrika Mashariki wanalitamka shekhe, sheikh na shaikh.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *shehe* ( *soma: shaykhun/shaykhan/,shaykhin شيخ )* lilipoingia katika  Kiswahili lilichukua maana ya mtu aliyeelimika katika dini ya Kiislamu ambaye huwafundisha wengine, ikabuniwa maana mpya ya Mtu mzima aghalabu mzee ambaye jamii inampa heshima kubwa kutokana na hekima na busara zake na kuziacha maana zingine zilizo katika lugha yake ya asili - Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)