MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ASKOFU'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'ASKOFU'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ASKOFU'

Neno *askofu*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* yenye maana zifuatazo:

1. Kasisi au mchungaji mkuu wa madhehebu ya Kikristo.

2. Kiongozi mkuu wa dini ya Kikristo katika jimbo au dayosisi.

3. Msimamizi wa mambo ya kiroho katika eneo maalumu.

Neno *askofu* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *asqufun/asqufan/asqufin اسقف* lenye maana zifuatazo:

1. Mchungaji (padri) mwenye cheo cha juu ya kasisi na chini ya matrani مطران (metropolitan).

2. Mtu mrefu.

3. Mifupa mizito.

4. Ngamia mwenye manyoa mengi.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *asqufun اسقف* lilipoingia  katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *askofu*  maana yake katika lugha asili - Kiarabu inayomuhusu kiongozi wa Dini ya Kikristo haikubadilika na maana zake zingine katika lugha ya Kiarabu ziliachwa.

*TANBIHI:*
Ingawa baadhi ya makamusi yamesajili etimolojia ya neno askofu kuwa Kiarabu, kauli yenye nguvu ni kuwa etimolojia ya neno askofu ni *Kiyunani* kutokana na neno *ἐπίσκοπος (ebisokobos)* lenye maana ya anayeangalia akiwa juu ( *msimamizi* ).

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)