MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'MAKALA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'MAKALA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'MAKALA'

Neno *makala* katika lugha Kiswahili *Nomino [Ngeli: ya-/ya-, pia i-/zi-]*  yenye maana ya andiko kuhusu mada fulani ya kutolewa gazetini, katika jarida, kitabuni au kuwasilishwa kwenye mkutano, kongamano na kadhalika.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *makala*( *soma: maqaalatun/maqaalatan/maqaalatin مقالة)*  ni nomino ya Kiarabu  yenye maana zifuatazo:

1. Andiko (utafiti) kuhusu Sayansi, Fasihi, Siasa au jamii linalotolewa kwenye jarida au gazeti, yaani: *maqaalatun siyaasiyyatin مقالة سياسية* makala ya kisiasa, *maqaalatun ilmiyyatun مقالة علمية* makala ya kisayansi/kitaaluma.

2. Tendo-jina *masdar مصدر* ya kitenzi *qaala قال*  amesema; kauli.

3. Andiko kutoka kitabuni.

4. Msimamo wa kielimu/kitaaluma; *madhehebu* .

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *maqaalatun/maqaalatan/maqaalatin مقالة )* lilipoingia katika Kiswahili  na kutoholewa kuwa neno *makala* lilichukua kutoka lugha yake ya asili - Kiarabu maana ya andiko kuhusu mada fulani ya kutolewa gazetini, katika jarida, kitabuni au kuwasilishwa kwenye mkutano, kongamano na kadhalika na kuziacha maana za *kauli* na *msimamo wa kielimu/kitaaluma*.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)