MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AJABU'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'AJABU'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AJABU'

Neno *ajabu* katika lugha Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino [Ngeli: i-/ya- wingi: maajavu]* kitu, kiumbe au jambo linaloshangaza.

2. *Nomino [Ngeli: i-/ya- wingi: maajabu]* kitu au jambo lisilomithilika wala kuaminika.

3. *Kivumushi* . (i) -a pekee, -iso kawaida, -a kioja, -a kigeni (ii) -isomithilika wala kuaminika, -a kimiujiza.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ajabu*( *soma: ajabun/ajaban/ahabin عجب)*  ni nomino ya Kiarabu  yenye maana zifuatazo:

1. Mshangao, kukishangaa kitu kutokana na kutokuwa na mazoea nacho.

2. Mapenzi, hali ya kukipenda kitu kisichostahili kupendwa, moyo kuvutwa na kukiona kibaya kuwa kizuri.

3. (Kutoka kwa Mwenyeezi Mungu) ridhaa.

Kinachodhihiri ni kuwa neno ya Kiarabu *ajabun/ajaban/ajabin عجب)*  likipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno  *ajabu* lilichukua kutoka lugha ya asili -  Kiarabu maana inayohusu mshangao, upekee na kupendeza na kuacha maana ya kiibada inayohusu ridhaa ya Mwenyeezi  Mungu kwa waja wake.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)