MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO 'AKIDI' NA 'AKDI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO 'AKIDI' NA 'AKDI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'AKIDI' NA 'AKDI'

Neno akidi katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino: [Ngeli: i-/zi-] makubaliano rasmi ya watu kuishi pamoja wakiwa mume na mke.

2. Kitenzi elekezi chenye maana zifuatazo:

i) Fikia kiwango kinachohitajika; tosha.

ii) Hitimisha jambo au shughuli fulani; kamilisha jambo. (Kisawe: Maliza.)

Minyambuliko: akidia, akidiwa, akidika, akidiana, akidisha.

3. Kitenzi elekezi: akid.i nakili andiko la mtu au saini kwa lengo la kufanya udanganyifu; ghushi . ( Visawe: ghilibu, iga, zuga).

Minyambuliko: akidia, akidiwa, akidika, akidiana, akidisha.

1. Nomino: [Ngeli: i-/zi-] idadi maalumu ya wajumbe inayoruhusu mkutano kufanyika na uamuzi kuweza kutolewa katika vikao.

5 . Nomino: [Ngeli: i-/i-] uchache wa watu au vitu.

Neno akdi katika lugha ya Kiswahili Nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya makubaliano rasmi ya watu kuishi pamoja wakiwa mume na mke.

Katika lugha ya Kiarabu, maneno akidi na akdi ni nomino inayotokana na neno aqdun/aqdan/aqdin عقد)  lenye maana zifuatazo:

1. Ahadi; makubaliano ya kufunga ndoa au kufanya biashara.

2. Mkataba kama vile mkataba wa kufanya kazi kwa ujira fulani au kwa kujitolea.

3. Makumi: Hesabu inayojumuisha kumi, ishirini hadi tisini.

4. Suluhu; mapatano baina ya waliohasimiana.

5. Kifungu cha maneno kinachoashiria kukubaliana, kama vile kusema: Nimekuoza...., Nimenunua kutoka kwako.

Kinachodhihiri ni kuwa maneno akidi na akdi yanatokana na neno la Kiarabu aqdun/aqdan/aqdin عقد) na neno hili lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa akidi na akdi lilichukua kutoka Kiarabu maana ya makubaliano rasmi ya wawili kuishi pamoja wakiwa mume na mke na kubeba maana mpya.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)