MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO ' AGHALABU/AGHLABU' NA 'NADRA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO ' AGHALABU/AGHLABU' NA 'NADRA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' AGHALABU/AGHLABU' NA 'NADRA'

Neno aghalabu/aghlabu katika lugha ya Kiswahili ni kielezi chenye maana ya mara nyingi, kwa kawaida, mara kwa mara.

Mifano:
1. Nyota nyingi aghalabu/aghlabu huonekana usiku.

2. Watu wanaofanya mazoezi, aghalabu/aghlabu huwa na afya njema.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili aghalabu/aghlabu (soma: aghlabu/aghlaba اغلب) ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mtu mwenye shingo nene.

2. Mnyama simba.

3. Mwenye nguvu.

4. Mara nyingi.

Neno nadra katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino: [Ngeli: i-/zi-] uchache wa vitu au mambo kwa nadra mara chache sana.

Mfano : Tunaonana kwa nadra siku hizi.

Methali: Heri huenda mara kwa mara kwa wajasiri, nadra huenda kwa walegevu.

2. Kivumishi : -a uchache, haba, kidogo sana, -siyopatikana kwa urahisi.

Mfano : Siku hizi asali ni nadra sana kupatikana.

Katika lugha ya Kiarabu neno ' nadra ' ( soma: naadiratu/naadiratan/naadiratin نادرة/ nadiratun ندرة) lina maana zifuatazo:

1. Kinachopatikana kwa uchache sana, mfano: kitaabun naadirun.

2. Kitu kulichoadimika.

3. Jambo au kitu kinachotokea mara moja moja.

Kinachodhihiri ni kuwa neno aghalabu/aghlabu ( soma: aghlabu/aghlaba  اغلب) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno aghalabu lilichukua maana ya ' mara nyingi' na kuziacha maana zingine, kama ambavyo neno ' nadra ' ( soma: naadiratun/naadiratan/naadiratin نادرة/nadiratun/nadiratan/nadiratin ندرة) lilipoingia katika Kiswahili lilichukua maana ya ' mara chache' na kuziacha maana zingine.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)