MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MATUMIZI YA WIMBO NA NYOMBO

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MATUMIZI YA WIMBO NA NYOMBO
#1
Abdilatif Abdalla: Kwa ruhusa ya rafiki yangu, Prof. Abdulaziz Lodhi, hapa chini nawaletea maoni yake aliyoniandikia baada ya mimi kumpelekea yale maelezo yangu niliyoyaleta kwenye ukumbi wetu huu kuhusu matumizi ya maneno "wimbo" na "nyimbo." Natumai maoni yake hayo aliyoniandikia, pamoja na jawabu zangu, yatasaidia kuuendeleza mjadala huo.?

Abdilatif Abdalla: Ustaadh 'Atifu, Nakutakieni nyote Mwaka Mpya Mwema!

Shukran kwa maelezo yako ya kitaaluma kuhusu "wimbo/nyimbo" n.k..
Katika matumizi ya Kiswahili chetu cha Kijiweni (kilahaja cha Kimjini, cha Kiunguja Mjini) twasema k.m. "nyimbo nzuri moja yake" na "nyimbo nzuri mbili zake" (Nomino za Ngeli za 9/10. Hoyo ni Kifasaha. Ndivyo nimelelewa nacho Kiswahili cha kwetu. Na hata jamaa zetu wa Mwambao walikuwa wanasema hivyo.
Lakini skuli tulifundishwa "wimbo mzuri mmoja wake/nyimbo nzuri mbili zake"  n.k. (Nomino  za Ngeli za 11/10). Hiyo ni Kisanifu.
Pili, watu wengi, hata baadhi ya wasemaji wa jaddi wa Kiswahili, hawatafautishi baina ya vitenzi vya "ku-kua" na "Ku-wa". Badala ya kuandika k.m.  "Alikuwa amelala."  wanaandika "Alikua amelala."
Yako na makosa mengineyo (kama "rekebisha" badala ya  "rakibisha" na "hutuba" badala ya "hutuba" ambayo nitayaeleza kesho au kesho kutwa.
Wasalaam!
Abdulaziz Lodhi
Uppsala, Uswidi.

Abdilatif Abdalla: Assalaamu alaykum. Ahsanta (ahsante) sana, Prof. Abdulaziz Lodhi, kwa salamu za mwaka mpya wa 2022. Allah Aujaaliye uwe na kheri nasi kuliko ulivyokuwa mwaka uliopita.

Nimefurahi mno kupata maoni yako kuhusu niliyoyaandika jana. Hii ni hishima kubwa kwangu: kwamba uliziweka kando  shughuli zako muhimu
na kuniandikia. Nakushukuru mno.

Nakubaliana nawe kwamba wako wasemao "nyimbo" kwa hali ya umoja na kwa wingi pia - kama nilivyoeleza katika hayo maoni yangu ya jana. Na nakubaliana nawe pia kwamba wako hata baadhi ya "jamaa zetu wa Mwambao" walitumiao neno hilo hivyo. Bali kwa jinsi idadi ya walitumiao neno "nyimbo" kwa umoja na kwa wingi inavyoongezeka sana, huenda baada ya miaka michache hilo "wimbo" likapotea kabisa! Hata hivyo, kwa hivi sasa hatufai kulinyima haki yake, maadamu wako walitumiao - wangawa wachache.

Naona kama nakukosea adabu (na nakuomba uniwie radhi) nisemapo kwamba, kama  ujuavyo, kuna tafauti za matumizi, matamshi na  maana, za baadhi ya maneno hayo hayo ya Kiswahili  fasaha - hata miongoni mwa "jamaa zetu wa Mwambao". Kwa vile wewe ni msomi wa miaka mingi mno na ni mwanataaluma mbobezi wa isimu na lugha ya Kiswahili(kinyume na mimi ambaye si mwanataaluma wala si msomi, bali nimeokotezaokoteza kichache tu barabarani) huhitaji kuelezwa nami tafauti hizo. Lakini kwa madhumuni ya kujirahisishia mimi mwenyewe haya maelezo yangu, kwa mifano michache ya haraka haraka, kuna "jamaa zetu wa Mwambao" ambao katika Kiswahili chao fasaha husema nipa, amkua (ambalo kwa wengine "amkua" lina maana ya ita); inua, ufuo, embe hili, (maembe haya); ilhali wengine wa Mwambao husema nipe, amkia, nyanyua (neno ambalo kwa hao wa mwanzo  lina maana ya kuchana au kurarua), ufukwe au ufuko (neno ambalo kwa hao wa mwanzo lina maana ya sehemu inayochimbwa ndani ya nyumba, chini ya kitanda cha kuoshea maiti, ili maji anayooshewa maiti yaingie humo); na embe hii (embe hizi).

Kwa hivyo, hilo neno "nyimbo" kutumiwa na baadhi ya watu kwa umoja na kwa wingi pia, laweza kutiwa kwenye mkumbo wa  tafauti kama hizo za Kiswahili fasaha kitumiwacho na "jamaa zetu wa  Mwambao".

Umenieleza katika hayo maoni yako kwamba neno "wimbo" kuwa ni umoja wa "nyimbo" ulifundishwa skuli; kwa hivyo, kwa maoni yako, ni athari ya Kiswahili Sanifu. Mimi nami tangu nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa nikilisikia  neno "wimbo" likitumiwa nyumbani kwetu na wazazi na wazee wangu wengine, kuwa ni umoja wa "nyimbo. Na wao  hawakupata kusoma  skuli. Kwa hivyo, hawakuwa wakilitumia hivyo kutokana na athari za skuli au Kiswahili Sanifu. Hata ile misemo miwili niliyolitolea ushahidi neno "wimbo" (yaani "Wimbo hutokea ngomani" na "Wimbo muwi hauongolewi mwana") ni misemo ya kale sana ya Kiswahili, ambayo ikitumika kabla ya kubuniwa hicho Kiswahili Sanifu mwaka 1930.

Kwa mara nyengine tena, nakushukuru sana ndugu yangu kwa kuniandikia na kunipa maoni yako.
Wassalaamu alaykum.

-Abdilatif Abdalla,
2.1.2022,
London
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)