MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO ' AFWAJI' NA 'UMMA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO ' AFWAJI' NA 'UMMA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' AFWAJI' NA 'UMMA'

Neno afwaji[ Ngeli: li-/ya-/wingi: maafwaji] katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Kundi la watu lililokusanyika pamoja kwa lengo fulani; mkusanyiko wa watu kadhaa.

2. Kikundi cha askari jeshi wakiwa na silaha.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili afwaji (soma: afwaajun/afwaajan/afwaajin افواج) ni wingi wa neno la Kiarabu fawju ( soma: fawjun/fawjan/fawjin فوج kundi ) lenye maana zifuatazo:

1. Kundi la watu.

2. Kundi la wanajeshi.

Neno umma[ Ngeli: u-/u-] katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana ya jumla ya watu wote katika nchi.

Kadhalika hutumika kuonesha jambo la wote (sio jambo la mtu/watu binafsi) kama vile:

1. Mali ya umma ni mali ya wananchi wote kwa pamoja iliyo  mikononi mwa serikali.

2. Jeshi la umma ni jeshi la wananchi kwa faida ya nchi nzima.

Katika lugha ya Kiarabu neno 'umma' ( soma: ummatun/ummatan/ummatin امة) lina maana zifuatazo:

1. Kundi la watu wanaounganishwa na mambo shirikishi ya kihistoria. Mambo hayo yanaweza kuwa lugha, Dini au uchumi. Watu hao huwa na malengo ya pamoja kiitikadi, kisiasa au kiuchumi, mfano Al-Ummatu Al-Ifriqiyyat الامة الإفريقية umma wa Kiafrika.

2. Mfano mwema. Sura ya 16 (Surat An-Nahli), Aya ya 120 katika Qur'aan Tukufu, Mwenyeezi Mungu Amesema: "Hakika Ibrahim alikuwa ummatan (mfano mwema), mnyenyekevu kwa Mwenyeezi Mungu, mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina."

3. Kundi la watu wanaoishi nchi moja.

4.  Kila aina kutokana na wanyama.

5. Mzazi wa kike (mama).

6. Dini.

7. Kizazi (Generation).

8. Njia, barabara.

9. Muda, wakati, kitambo.

10. Kimo.

Kinachodhihiri ni kuwa wakati neno afwaji ( soma: afwaajun/afwaajan/afwaajin  افواج) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno afwaji maana zake katika lugha yake ya asili - Kiarabu haikubadilika, neno ' umma ' ( soma: ummatun/ummatan/ummatin أمة)  lilichukua maana ya jumla ya watu wanaoishi katika nchi na kuziacha maana zingine za neno umma katika Kiarabu.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)