12-28-2021, 09:35 AM
Taswira ni picha inayojengeka akilini mwa msomaji. Kuna aina tofauti tofauti za taswira. Kama vile
Taswira uoni –inajitokeza unapopewa picha ya mtu (umbile)
Taswira sikivu- unapewa picha akilini lakini inayopitia masikio
-(Kana kwamba unaskia sauti masikioni)
-(Kana kwamba unaskia sauti masikioni)
Mfano katika wimbo aliomtungia mamake Kongowea kuhusu kifo chake
Taswira mwonjo – mfano Musa na Maksuudi wameandaliwa chakula na Kazija – (unasikia kana kwamba kuna harufu na wanakula chakula kwa maelezo)
Taswira mnuso – ni pale ambapo mwandishi anakupa maelezo
yanayokufanya unuse harufu. Mfano: Kongowea anapoinusa harufu ya Kazi-Kwisha alipofika kwake siku ya mwisho kutambua ni
yanayokufanya unuse harufu. Mfano: Kongowea anapoinusa harufu ya Kazi-Kwisha alipofika kwake siku ya mwisho kutambua ni
babake
Taswira hisi – wakati msomaji anaelezewa kuhusu kitendo kinachotoa hisia mfano wakati mhusika katika Utengano (Tamima) anachapwa na Maksuudi.
Taswira Mguso – msomaji anapohisi yuaguswa anaposoma wakati Vumilia anamshika Kongowea Mswahili akimsihi aende kulala.
Mwl Maeda