MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

USAWIRI WA WAHUSIKA WA KIKE KATIKA KAZI ZA ZAINABU BURHANI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
USAWIRI WA WAHUSIKA WA KIKE KATIKA KAZI ZA ZAINABU BURHANI
#1
Usawiri wa wahusika wa kike katika kazi za zainabu Burhani
Utafiti huu umeshughulikia usawiri wa wahusika wa kike katika kazi za Zainabu Burhani. Mtafiti amehakiki riwaya tatu zake mwandishi huyu. Kazi zilizochanganuliwa ni Mali ya Masikini (1981), Mwisho wa Kosa (1987) na Kipimo cha Mizani (2004).

Burhani katika kuwasawiri wanawake anapiga vita mfumo wa kuumeni ijapokuwa haepuki athari zake kabisa. Hii yatokana na malezi na pia dini yake ya Kfslamu.

Amejitokeza na vizazi tofauti vya wanawake; He kichanga kina shime ya kupambana ili kiweze kujikomboa. Kwa upande mwingine kizazi kikongwe kimekubah hali ilivyo.

Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha mtazamo-kike ambayo ni nadharia ya unisai wa Kiafrika. Nadharia hii huj aribu kueleza matatizo yanayowakabili wanawake wa Kiafrika, kinachoyasababisha na jinsi wanavyoweza kujiepusha nayo.

Kupitia hii nadharia ni dhahiri kuwa wanawake wa Burhani wamesawiriwa kwa mtazamo hasi na j amii na pia kuwekwa katika nafasi ya pili. Haya yote yanasababishwa na itikadi ya mfumo wa kuumeni inayowafanya hawa wanawake lcuikubali half yao. Hata hivyo kuna matumaini kupitia kizazi kichanga cha wanawake ambao wanajitahidi kuikata hii minyororo. Tasnifu hii imegawanywa katika sura saba.

Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambapo mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada pamoja na upeo wa utafiti huu zimeshughulikiwa. Aidha yaliyoandikwa kuhusu mada hii pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti huu zimej adiliwa.

Sura ya pili inashughulikia swala la itikadi na sura zake mbalimbali. Tumechunguza ni vipi itikadi hizi zinavyomwathiri mwandishi ambaye ni mzaliwa wa jamii anayoishughulikia. Katika sura ya tatu uhalisi wa mwanamke wa kiafrika umesawiriwa. Nayo sura ya nne imeshughulikia jinsi mwanamke wa Kiafrika alivyo na uwezo wa kujitegemea. Sura ya tano imemsawiri mwanamke wa Kiafrika anavyojitokeza kuwa shujaa na hata mtawala katika j amii.

Sura ya sita imeshughulikia jinsi mwanamke kama mwanamume, alivyo na nafasi katika uj enzi wa j amii.

Sura ya saba ni hitimisho linalotoa muhtasari na matokeo ya utafiti huu, pamoja na mapendekezo ya mtafiti. Mwisho kabisa kuna marej eleo ya utafiti huu.

Jambo linalojitokeza kupitia usawiri wa wahusika wa kike wa mwandishi Burhani ambaye ni mwanamke ni kuwa, katika uandishi mwandishi awe ni wa kiume au kike huathiriwa pakubwa na itikadi ya jamii yake. Hii ni kwa sababu malighafi yake hutokana na mazingira anamoishi. Asasi za kidini na kitamaduni, kwa mfano zina athari kubwa kwa mtazamo wa Zainabu Burhani. Chanzo>>>>>>
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)