MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA NGOSWE - PENZI KITOVU CHA UZEMBE

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA NGOSWE - PENZI KITOVU CHA UZEMBE
#1
UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA NGOSWE - PENZI KITOVU CHA UZEMBE
MTUNZI: EDWINI SEMZABA
MCHAPISHAJI:THE GENERAL BOOKSELLERS LTD
CHAPA YA 1-1988
UTANGULIZI
Ngoswe-penzi Kitvu cha Uzembe  inaonyesha namna jamii inapaswa kushiriki mipango mbalimbali ikiwepo ya kisiasa kiuchumi na kiutamaduni.Mafanikio ya mipango hiyo inategemea na kujulikana kwa idadi ya watu utayari,uelewa wa watu hao kuhusu mipango husika
Tamthiliya hii inaonyeshakazi ya kuhesabu watu ilivyokwama kijijini kwa mzee mitomingi ngengemkeni kutokana na uzembe wa afisa wa kuhesabu sensa Ngoswe.
DHAMIRA
  1.   MAPENZI
Mwandishi Edwin semzabaameonyesha jinsi mapenzi yalivyo kitovu cha uzembe,wahusika Ngoswe na Mazoea wametumiwa na mwandishi kufafanua dhamira hii
Ngoswe baada ya kufika kwa mzee Mitomingi anashindwa kuitawala nafsi yake mara anapomuona Mazoea,Ngoswe aliamua kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Mazoea hali iliyomfanya ashindwe kuimudu kazi yake na mapenzi kwa wakati mmoja.
Ngoswe anamtorosha Mazoea kitendo hiki kinamuudhi balozi Mitomingi Ngengemkeni (baba mzazi wa mazoea)na kuamua kuchoma moto karatasi muhimu za serikali.Ngoswe anaonekani ni mzembe kwa kuwa alishindwa kutofautisha kazi na mapenzi kama msomi (afisa wa sensa )alitakiwa ajue umuhimu wa kazi iliyompeleka kijijini.
  1.  ULEVI NA ADHARI ZAKE
Katika tamthiliya ya ngoswe penzi kitovu cha uzembe mwandishi  anaonyesha namna ulevi ulivyoleta madhara,mfano kuchelewesha kazi.Wahusika Mitomingi na Ngoswe wanashindwa kukamilisha kazi kwa vile wahusika (wahesabiwa)wapo kwenye Pombe kama maneno haya yanavyothibitisha;
Mitomingi:Haya ni matatizo yote hii shauri ya pombe nadhani yupo kilabuni
Ngoswe :hawezi kwenda kuitwa?
Mitomongi:haitosaidia mkewe tu hana habari ya kuhesabiwa sembuse hao wengine kwa leo haitowezekana
Licha ya kuchelewesha kazi ulevi huaribu kazi.Mfano:ngoswe anaunguza karatasi za sensa baada ya kulewa pombe ya mnazi.
  1.   ELIMU
Elimu ni chombo cha ukombozi kama itatumiwa vizuri ipaswavyo,mwandishi wa tamthiliya hii amemuonyesha kijana Ngoswe (msanii)alivyoshindwa kutumia elimu yake hususani katika kujua namna ambavyo  maisha ya mjini yanavyotofautiana na maisha ya kijijini,Ngoswe anajikuta akiharibu kazi yake kwa kukosa maarifa.
Mwandishi ameonyesha elimu katika familia ya mito mingi haikupewa thamani yoyote ile wananchi wengi hawakuwa na elimu kwa kisingizio cha shule kuwa mbali,ukosefu wa elimu ulichangia ukosekanaji wa huduma muhimu kama vile hospitali ,miundo mbinu na maji ili kupata maendeleo,suala la elimu lazima litiliwe maanani watu wakieleweshwa wataweza kujua wajibu wao :-
Mfano:kujali kazi na kuacha ulevi “kutumia vema hospitali badala ya kutegemea mitishamba
  1.  UCHAWI NA USHIRIKINA
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha jinsi watu wengi ndani ya jamii walivyo na imani juu ya uchawi,wanajamii hawa wameweka vikwazo kuhusu sensa wakiamini kuwa mtu anayewahesabu wenzake ni mchawi
Mfano:mama anasema mchawi ndiyo huhesabu watoto wa wenzake ili awaroge sasa wewe ni mchawi?hata kama si mchawi siwezi kukubali unihesabu maana sijui nia yako kama ni mbaya au nzuri.Imani hizo ni za kishirikina zinachangia kukwama kwa zoezi la sensa pia maendeleo kwa ujumla kuwachini,watu wakiugua hawapelekwi hospitali badala yake wanapelekwa kwa mganga wa kienyeji wakidhani kuwa amerogwa.
  1. NAFASI YA MWANAMKE
  Katika tamthiliya hii mwanamke ametazamwa katika mitizamo tofauti kama ifuatavyo;
  Ø  Mwanamke amechorwa kama chombo cha starehe,mwandishiamemuonyesha mzee mitomingi kuwa na wake wengi (mitala)bila kuoyesha bayana kazi zao.
  Ø  Mwanamke amechorwa kama mtu asiye na sauti
mfano:Mazoea na mama yake hawakushirikishwa katikamipango ya kutaka kuolewa mazoea kwa vile walionekana hawana mchango wowote katika maamuzi hayo
  Ø  Mwanamke amechorwa kama mlezi,
katika tamthiliya hii inamchora mwanamke kama mtu mwenye majukumu ya malezi ya watoto,baada ya Mazoea kuwa na mahusiano na Ngoswe mzee Mitomingi anamlaumu mama yake Mazoea kuwa hakuona dalili ya mahusiano ya kimapenzi kwa kuwa ni jukumu la mama kumwangalia binti yake.
  1.  NDOA NA MALEZI
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha suala la ndoa ni sualala hiyari na si kufuata matakwa ya wazazi,Mazoea alichaguliwa mchumba na wazazi wake (baba yake)hali iliyomfanya kutoroka na ngoswe
Hali kadhalika katika tamthiliya hii wanaume wengi wana mke zaidi ya mmoja hali hii inapelekea familia kuwa kubwa na kushindwa kuzitunza.
Mfano:Mzee Mitomingi ana wake wawili ambao ni mama Mazoea na mama Mainda,wazazi hawa wanatofautiana katika malezi hasa kwa Mazoea hali iliyopelekea kuwa na tabia mbaya.
 Kwa upande mwingine ndoa zenye mke zaidi ya mmoja haziwi na upendo ndani ya familia hivyo kuwa kikwazo kwenye malezi.
7.UVIVU NA ATHARI ZAKE
Wanakijiji wa Ngengemkeni mitomingi wengi ni wavivu muda mwingi wanautumia kwenye ulevi na uvuvi,unawafanya wakose huduma muhimu kama shule,barabara na hospitali huduma hizi zingepatikana kama wananchi wenyewe wanajitolea.
Siku zote wavivu wanatafuta visingizio,vifo vingine vinatokea sababu ya uzembe na uvivu kisha sababu hutafutwa.
Mfano:wanawake wawili walidai mume wao amerogwa ili hali wenyewe hawakumpeleka hospitali
 MIGOGORO
Ni hali ya kutoelewana baina ya pande mbili zenye mitazamo tofauti Katika tamthilia yaNgoswe penzi kitovu cha uzembe kuna migogoro mingi ambayo imeweza kujitokeza kama ilivyoonyeshwa na mwandishi
  Mgogoro kati ya Ngoswe na wazazi wa Mazoea chanzo cha  mgogoro huu umetokana na Ngoswe kumtorosha Mazoea,suluhisho wazazi kumfukuza Ngoswe na Mazoea kuchoma karatasi na kumwadhibu Mazoea
  •   Mgogoro kati ya Mazoea na wazazi wake,chanzo cha mgogoro huu ni baada ya Mazoea kutoroka na Ngoswe ili hali Mazoea tayari ana mchumba wake,suluhisho ni mitomingi kumchapa mazoea na kuchoma karatasi za sensa.
  • Mgogoro kati ya Ngoswe na serikali,chanzo cha mgogoro huu ni Ngoswe kuharibu kazi ya sensa na hivyo kusababishia serikali ishindwe kupanga mipango ya maendeleo,suluhisho halijapatikana hadi mwisho.
UJUMBE
  •   Si jambo zuri kuchanganya suala la kazi na starehe au mapenzi,wakati wa kazi uwe wa kazi na wakati wa starehe uwe wa starehe.
  • Wavulana wanaovuruga wasichana siku moja watakamatwa na wasichana wenyewe wanapewa tahadhali wasiwe na maamuzi bila kufikilia.
  • Elimu ni kitu cha muhimu sana katika jamii na jamii isipokuwa na watu walioelimika hawawezi kuwa na maendeleo maana ili tuwe na maendeleo tunatakiwa tutupilie mbali ulevi na uvivu katika jamii yoyote
  • Uchawi na ushirikina ni kikwazo kikubwa katika maendeleo
FALSAFA
Mwandishi anaamini kuwa ni rahisi jamii kuingia kwenye matatizo kama itachanganya mambo mengi kwa wakati mmoja hivyo ikumbukwe kuwa kila jambo na wakati wake.
FANI
Vipengele vya fani katika kazi ya fasihi ni muundo, mtindo, madhari, wahusika na matumizi ya lugha
MUUNDO
Muundo uliotumika katika tamthiliya ni wamuundo wa moja kwa moja ambapo kazi nzima ipo katika sehemu tano ambazo mwandishi amezipa majina ya kitwasira kulingana na ukubwa wa tatizo linalozungumziwa ,yaani ameonyesha kuingia kwa Ngoswe kijijini mazingira yanayoashiria hali ngumu ya maisha(kijito)
Ø  Sehemu ya pili inaonyesha kazi ya kuhesabu watu imeanza na watu hawana utayari na uelewa juu ya sensa (vijito)
Ø  Sehemu ya tatu inaonyesha Ngoswe ameanza kujihusisha na mapenzi na ulevi,ambavyo ni viashiria vya kuharibu kazi yake (mto)
Ø  Sehemu ya nne inaonyesha kazi aliyopewa Ngoswe tayari imekosa mwelekeo,Ngoswe amebobea kwenye mapenzi na ulevi, karatasi zinachomwa moto baada ya kumtorosha Mazoea (jito)
Ø  Sehemu ya tano inaonyesha serikali ikimuhukumu Ngoswe juu ya takwimu zilizoungua moto na Ngoswe asingizia kuwa kijijini kuna shida ya kuhesabu kwani nyumba zimejitenga na watu wenyewe kutoelewa (baharini)
MTINDO
Mtindo uliotumika ni wa kidayalojia ambapo wahusika wake wanazungumza kwa kujibizana
Pia kuna matumizi ya nafsi zote tatu na nafsi hizo zimetumika katika sehemu mbalimbali.Mfano sehemu ya tano kwa matumizi ya nafsi ya kwanza pale Ngoswe anapoulizwa na serikali kuhusu takwimu akajibu “usemi sinao”
MANDHARI
Kitabu hiki kimejengwa katika mandhari ya kijijini,hii inadhihirishwa na ukosefu wa huduma muhimu kama vile shule hospitali na miundo mbinu
Tabia za wahusika pia zinaonyesha mandhari ya kijijini mfano,ulevi wa pombe za mnazi,watu kutojali elimu,kun’gan’gania mila zilizopitwa na wakati
MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi ametumia lugha nyepesi na yenye kueleweka pia mwandishi ametumia tamathali za semi,misemo na mbinu nyingi za kisanaa.
Tamathali za semi
Hizi ni semi au kauli zitumiwazo na mwandishi katika kazi ya fasihi ili kuongeza ladha katika kazi husika
Tashibiha
Ni  tamathali ilinganishayo vitu viwili au zaidi kwa kutumia viunganishi kama mithili ya ,kama,mfano wa
Mfano,Ngoswe anaposhangaa ardhi ya kijijini kwa balozi Mitomingi anasema
  • Udongo mwekundu kama ugoro wa sabiani
  • Tazama suruali yake kama kengele ya bomani
  • Nikitoka hapa najitupa kitandani kama gogo
Tafsida
Ni tamathali itumiwayo kupunguza ukali wa maneno
mfano Mainda anasema labda anajisaidia(Uk 21)
Takriri
ni tamathali inayorudiarudia neno ili kuweka mkazo juu ya kile kinachosemwa
Mfano; karibu,karibu(pale Ngoswe alipokuwa akikaribishwa)
Mdokezo
Ni tamathali ambayo hueleza jambo kwa kukatakata maelezo
Mfano Mazoea anasema sijui......sijui......siwezi namwogopa baba (Uk 22)
Tanakali za sauti
Ni tamathali inayoiga mlio wa vitu
mfano Ngoswe alishindwa kujizuia akacheka ha ha ha ha
Methali
  • Ngoswe anamwambia Mazoea
  •  “Penye nia pana njia” (uk 22)
Misemo
  •   Hebu keti tutupe mawe pangoni
  •   Kupeleka chakula ndio unafanya makambi
Taswira/Jazanda
Taswira mbalimbali zimetumiwa na mwandishi katika tamthiliya hii. Msanii ametumia taswira ya mtu kwa kuhusisha na matukio ya wahusika. Mwandishi analinganisha mwanzo wa mchezo na kijito ambacho ni mto mdogo sana hivyo maelezo ya sehemu hii yanategemewa kuwa madogo sana.
  1. Sehemu inayofuata ya vijito,sehemu ya vijito inaonyesha kuwa masuala yanashughulikiwa na kujadiliwa hapa yanaongeza uzito ingawa sio mazito sana
  2. Sehemu  ya mto inaonyesha ukubwa wa shughuli ya Ngoswe yuko kazini (yuko m toni)tayari yupo ndani ya jukwaa bila shaka maji ya mto ni mengi (matatizo mengi)na hivyo yeyote atakayeingia mtoni yampasa awe mwangalifu
  3. Sehemu ya jito inaashiria kuna hatari, kuna matatizo mengi, katika jito kulivika si kazi rahisi hatimaye tunaonyeshwa Ngoswe amezama baharini ambapo kuzama kwa Ngoswe ni baada ya makaratasi kuchomwa moto.
  4. Sehemu ya mwisho ni bahari kama ishara ya kuzama kwa Ngoswe kutokana na wingi wa maji.
WAHUSIKA
Wahusika ni watu walioshiriki katika mchezo au tamthiliya husika.
Mwandishi amegawa wahusika katika makundi mawili yaani mhusika mkuu na wahusika wasaidizi
MHUSIKA MKUU
NGOSWE
Ni msomi anayependa kazi ya kuhesabu watu lakini kutokana na tamaa ya mwili wake anaharibu kazi baada ya takwimu zote kuchomwa moto na Mitomingi kutokana na kitendo cha kujaribu kumtorosha mazoea .
WAHUSIKA WADOGO
Mazoea
  1.  Msichana mwenye umri wa miaka 18-20
  2.  Ni mtoto wa balozi (Mitimingi)
  3.  Anawakilisha wanawake wasio na msimamo katika mapenzi
Ngengemkeni mitomingi
  v  Huyu ni balozi
  v  Baba yake Mazoea
  v  Anachoma karatasi za takwimu kutokana na Ngoswe kutaka kumtorosha Mazoea
  v  Ni mzee aliyeshikilia ukale na anapenda ndoa za mitara
JINA LA KITABU
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe jina hilo la kitabu linasadifu yaliyomo ndani ya kitabu ,kwani msanii kwa kiasi kikubwa amejaribu kujadili na kuonyesha matatizo yanayoikumba jamii katika shughuli za kijamii,matatizo hayo ni kama uchawi ulevi uzembe na dhana nyingine potofu
KUFAULU NA KUTOFAULU KWA MWANDISHI
Mwandishi katika tamthiliya hii amefeli kwa kuwa ameonyesha matatizo yaliyomo katika jamii bila kuonyesha mbinu mbadala ya kuyatatua.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)