MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' BALAGHA'.

Neno Balagha katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Ufundi wa kutumia lugha kwa kutia chumvi maelezo na kuuliza hadhira maswali yasiyo na majibu kwa lengo la kuvutia hisia za msikilizaji.

2. Mtu ambaye ni stadi wa kutumia lugha kwa kutia chumvi kwa lengo la kuvutia hisia za msikilizaji.

3. Swali linaloulizwa kwa udadisi na lisilohitaji majibu.

4. Ufundi wa matumizi ya lugha kwa nia ya kumfanya msikilizaji ashawishike au afurahike.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *balagha* ( soma: balaaghatun/balaaghatan/balaaghatin بلاغة) lina maana zifuatazo:

1. Namna bora ya kutoa maelezo na nguvu ya kushawishi na kuathiri.

2. (Kwa Wanazuoni wa Taaluma ya Balaagha-Elimu ya Ufasaha wa kusema/kuandika) ufasaha wenye kubeba maneno yanayosadifu muktadha.

3. Ufasaha wa kutamka na kunyoosha maneno.

4. Balaagha ya Kiarabu: Taaluma ya ufasaha wa kusema na kutia madoido inayojumuisha fani tatu, nazo ni: ALBAYAAN (Rhetoric), ALMAAN (Semantic) na ALBADII'I (The Art of Figures of Speech/The Art of Metaphors and Stylistics/Good Style)

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *balaagha *(tun)* *بلاغة*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *balagha* , maana zake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - hazikubadilika bali imeongezeka maana ya mtu ambaye ni stadi wa kutumia lugha kwa kutia chumvi kwa lengo la kuvutia hisia za msikilizaji. Mtu mwenye sifa hizi kwa Kiarabu huitwa *baliigh* *بليغ* na sio *balagha* .

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)