MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO "MUDIRI" "NA MUDIRIA"

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO "MUDIRI" "NA MUDIRIA"
#1
Neno mudiri katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mkuu wa idara au kitengo katika taasisi.

2. Kiongozi anayetawala eneo la nchi kama vile wilaya; Afisa Tawala wa Wilaya.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili mudiri (mudiirun/mudiiran/muddirin مدير) lina maana zifuatazo:

1.  Msimamizi wa shughuli na maamuzi katika eneo la kazi; Mkurugenzi, Mkuu wa Shule/Chuo, Mkuu wa Idara/Kitengo.

2. Mahali paliposakafiwa udongo (kivumishi).

3. Jina la mtendaji wa kitenzi cha Kiarabu adaara أدار ameongoza/ameendesha; mwongozaji/mwendeshaji.

Katika Lugha ya Kiarabu neno hili *mudiir* linatumika kwa jinsia zote (nadra kwa maneno mengi ya Kiarabu) na wingi wake ni mudaraau/mudaraa'a  مدراء .

Na neno mudiria katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Eneo la kiutawala la nchi ambalo mkuu wake ni Mudiri.

2. Wilaya au jimbo.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili mudiria (mudiiriyyatu/mudiiriyyatan/mudiiriyyatin (soma: مديرية) lina maana zifuatazo:

1. Eneo au taasisi ambayo mkuu wake ni Mudiir (Neno hili limesanifiwa na si neno asili la lugha ya Kiarabu.)

2. Ni eneo la utawala la kiserikali.

Ni dhahiri kuwa maneno haya yalipoingia katika Kiswahili maana zake katika lugha yake ya asili - Kiarabu hazikubadilika.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)