Unominishaji kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2007) wanasema ni hali ya kuunda nomino kutoka katika kategoria nyingine ya neno. Kategoria hizi zaweza kuwa kitenzi, kivumishi au hata nomino yenyewe.
Ø Kwa hiyo vinominishi (o, i) vinaweza kunominisha vitenzi vya Kiswahili katika mazingira yafuatayo: Tukianza na kinominishi (o); kinominishi “o” huweza kunominisha vitenzi vya kibantu vinavyoishia na kiambishi tamati “a”.
Kwa mfano: tenda→ tend-o
Andika → andik-o
Piga → pig-o
Pata → pat-o
Jenga → jeng-o
Fundisha → fundish-o
Ona → on-o
Pamba → pamb-o
Ø Hata hivyo kuna baadhi ya vitenzi vya kibantu vinavyoishia na kiambishi tamati “a”ambavyo havinominishwi na kinominishi “o” mfano wa vitenzi hivyo ni kama lowa, tembea nk.
Ø Pia kinominishi “o” huweza kunominisha vitenzi kwa kuambatana na vinyambulishi (-i-) au (-li-) katika baadhi ya vitenzi.
Kwa mfano: kaanga→ kaang-i–o
Chuja→ chuj-i–o
Pamba → pamb-i–o
Fua → fu-li–o
Kaa → ka-li–o
Ø Mazingira mengine ambamo kinyambulishi nominishi “o” huweza kunominisha kitenzi ni pale ambapo huambatana na mofimu (-e-)
Mfano: Chekecha → chekech-e–o
Fyeka → fyek-e–o
Zoa → zol-e–o
Ø Vilevile kinominishi “o” huweza kunominisha kitenzi kwa kushirikiana na viambishi awali vinominishi.
Mfano: Lima → ki-lim-o
Soma → ki-som-o
Kula → m-l-o
Lia → ki-li-o, m-li-o
Penda → u-pend-o
Cheza → m-chez-o
Ø Pia baadhi ya vitenzi huweza kuondolewa irabu ya mwisho na kubakiwa na kinyambulishi “o” kama kinominishi.
Mfano: toboa→ tobo
Ø Vilevile unominishaji huweza kufanyika katika vitenzi vya utendewa na utendeshwa kwa kuondoa mofimu (-w-a).
Mfano: somwa → som-o
Pigwa →pig-o
Lishwa → lish-o
Tendwa →tend-o
Ø Kwa upande wa kinominishi “i” pia huweza kunominisha kitenzi katika mazingira tofautitofauti kama ilivyoonyeshwa hapa chini.
Kinominishi “i” huweza kunominisha kitenzi kwa kusaidiana na viambishi awali vinominishi.
Mfano: soma → m-som-i
Soma → u-som-i
Chunguza → u-chunguz-i
Chokoza → u-chokoz-i
Ø Kinominishi “i” huweza kuchukua nafasi ya kiambishi tamati “a” katika kitenzi na kunominisha kitenzi hicho.
Mfano: Sema → sem-i
Ø Vilevile kinominishi “i” huweza kuambatana na vinyambulishi vingine ili kunominisha kitenzi.
Mfano: Chuja → chuj-i–o
Pita → pit-i–o
Habwe na Karanja (2007:45) wanasema kinominishi “i” kinapotumika kunominisha mizizi inayoishia na konsonanti, mfano; (pik) na (jeng). Mofimu “i” inapopachikwa kwenye mizizi hubadili na kuifanya kuwa nomino.
Mfano:
Kitenzi
Unominishaji
Nomino
Pika
mu+pik+i
mpishi
Jenga
mu+jeng+i
mjenzi
Iba
mu+ib+i
mwizi
Ø Vilevile kinominishi “i” huweza kunominisha shina la kitenzi cha mnyambuliko.
Mfano: tembeza→ m-tembez-i
Kimbiza → m-kimbiz-i
Tapisha → ma-tapish-i
· Kivumishi cha sifa kikiongezwa irabu “u” mwanzoni mwa kivumishi husika huunda nomino zalika: mfano: baya ubaya, zuri uzuri, vivu uvivu
· Nomino zinazotokana na kuongeza kiambishi “ki” mwazoni na “o”mwishoni mwa kitenzi. Mfano: soma – kisomo, apa – kiapo, piga –kipigo, ziba – kizibo, lia – kilio.
· Nomino zinazotokana na kuongezwa kwa kiambishi “m” mwanzoni mwa silabi na “ji” mwishoni mwa kitenzi. Mfano: chora – mchoraji, cheza – mchezaji, baka – mbakaji, kamua – mkamuaji, fagia –mfagiaji.
· Nomino zinazotokana kwa kuongeza viambishi awali “m” na “u”mwanzoni mwa kitenzi au kiambishi tamati “vu” au “zi” mfano: legeza – ulegevu (hali), mlegevu (mtu), teleza – utelezi (hali),mtetezi (mtu), kakamaa – ukakamavu (hali), mkakamavu (mtu).
· Kwa kuambatanisha maneno mawili. Mfano: uambatanishaji wa jina kwa jina: askarikanzu, batamzinga, afisakilimo,
· Jina na kivumishi: mjamzito.
· Kitenzi na jina: chemshabongo, changamoto.
Jina tegemezi na jina huru: jinategemezi hutokana na kitenzi na linahitaji jina huru ili maana ikamilike. Mfano: mpigambizi, kitindamimba,kifunguakinywa, kifunguamimba, nk.