MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MOFOLOJIA YA KISWAHILI MUHADHARA WA KWANZA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MOFOLOJIA YA KISWAHILI MUHADHARA WA KWANZA
#1
MUHADHARA WA KWANZA
Mofolojia: ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha na mpangilio wake katika uundaji  wa maneno.
Mofolojia : ni utanzu mmojawapo katika tanzu za isimu
Tanzu hizo za isimu ni:
  1. Mofolojia
  2. Fonolojia
  3. Sintaksia
  4. Semantiki na
  5. Pragmatiki
Lugha ya Kiswahili ina vipashio anuai ambapo kipashio kidogo kabisa huitwa mofimu (mofu) na kikubwa kabisa ni sentensi.
Mofimu: Ni kipashio kidogo chenye maana ya kisarufi au ya kileksika. Kipashio hicho kinaweza kuwa neno zima au sehemu ya neno. Mofimu hugawanyika katika aina zake kwa vigezo vikuu viwili ambavyo ni
*   Kigezo cha kimaana
Kwa kigezo hiki tunapata aina mbili za mofimu ambazo ni:
  1. a)Mofimu zenye maana ya kileksika
  2. b)Mofimu zenye maana ya kisarufi
  3. i) Mofimu zenye maana ya kileksika.
Huwa ni maneno kamili yasiyogawanyika na yanayojitosheleza kimuundo na kitaarifa. Hizi ni mofimu ambazo maana yake inatabirika.
Mfano:
baba, maji, hewa, jua n.k
  1. ii) Mofimu zenye maana ya kisarufi
Huwa ni viambishi ambavyo hujiegemeza kwenye mzizi fulani wa neno ili kutoa taarifa. Maana ya mofimu hizi huwa haitabiriki bali hutegemeana na muktadha wa utokeaji wa mofimu husika.
Mfano:
– A-na-chez-a
– Tu-me-imb-a
– Wa-li-som-a
Mifano hiyo inadokeza mofimu zenye maana kisarufi na kila maana hiyo imetokea wapi na vipi ni kama inavyoonekana hapa chini.
  1. A-inadokeza nafsi ya 3-umoja
-uyakinishi
-ngeli ya kwanza (A-wa)
  1. i)Na-ni njeo iliyopo,hali ya kuendelea
  2. ii)me – hali timilifu
*   Kigezo cha kimofolojia
Kigezo hiki huchunguza mofimu kama umbo na uhuru wa umbo lenyewe. Hapa tunapata mofimu huru na mofimu tegemezi au funge
v  Mofimu huru.
Ni maneno kamili yanayojitosheleza kiumbo na kitaarifa
Mfano: baba, maji, hewa, Mungu, jua, mvua, n.k
  1. Mofimu za kileksika huwa ndizo mofimu huru.
(ii) Mofimu tegemezi / funge.
Huwa ni viambishi ambavyo hupachikwa kwenye mzizi wa neno ili kutoa taarifa fulani. Mofimu tegemezi huwa ndio mofimu zenye maana kisarufi.
Mfano
Tu-li-o-imb-a
a-li-ye-ni-on-a
m-na-vyo- wa-pig-a
Mofolojia hushughulikia mambo yafuatayo
v  Vipashio vya lugha ambavyo vimeitwa mofimu
v  Mpangilio unaokubalika wa mofimu ili kuunda maneno, mpangilio huo huitwa kanuni
MOFOLOJIA NA FONOLOJIA
Mofolojia ni nini?
Ni taaluma yenye uhusiano na taaluma ya fonolojia katika kuishughulikia lugha
Fonoloji ni Taaluma inayoshughulikia sauti za lugha ambazo hutumiwa  kuunda maneno. Vipashio vya  kifonolojia  vitumiwavyo  kuunda maneno huitwa fonimu
Uhusiano uliopo  kati ya mofolojia na fonolojia huweza kuelezwa  kwa namna mbili
v  uhusiano wa kisemantiki
Ambapo badiliko la umbo la neno kifonolojia huweza kuathiri maana ya neno zima au kuathiri mofolojia pekee.
Mfano
(a) mu+ana = mwana
(b) mu+anafunzi = mwanafunzi
© mu+alimu = mwalimu
(2) Uhusiano wa pili ni ule wa kileksika ambapo mofolojia huwa na
maneno yasiyogawanyika na yenye maaana ya wazi.
FONOLOJIA KWA UJUMLA
Uwanja wa fonolojia unahusu uhusiano uliopo baina ya lugha na sauti zinazoijenga lugha.Lugha inayozungumziwa  hapa ni lugha  ASILIA
Lugha hutumiwa na wanadamu katika mawasiliano yao kwa njia ya sauti zinazounda maneno. Lugha asilia hutofautishwa na mifumo mingine ya mawasiliano kama vile Ishara ambazo pamoja na kutumiwa katika mawasiliano ya binadamu  ishara hizo hazijaweza kutumia sauti.
Lugha ya kompyuta ambayo kimsingi  ni lugha unde (iliyoundwa kwa makusudi maalumu) imebaki kuwezesha mawasiliano baina ya mashine hizo pasipokutumia sauti kama ilivyo kwa binadamu.
SAUTI ZA LUGHA ASILIA
Wanaisimu wengi wanakubaliana kuwa lugha ya binadamu ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii fulani ya watu kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao.
Sauti nasibu: Ni zile ambazo uteuzi wake  haukufanywa kwa kufuata mantiki au vigezo fulani maalumu bali umetokana na makubaliano  ya kimazoea ya watumiaji wa lugha husika na hii ndiyo maana sauti za lugha mbalimbali zinaweza kufanana sana au kwa kiasi fulani tu na pia zinaweza kusigana sana au  kiasi fulani tu.
Utaratibu wa kuunganisha sauti ili kuunda maneno ni wa nasibu kama ambavyo sauti zenyewe ni za nasibu. Utaratibu huo huweza kutofautiana toka lugha moja hadi nyingine.
ALA SAUTI ZA LUGHA ASILI
Utoaji wa sauti zitumikazo katika kuunda maneno ya lugha za binadamu hufanyika kwa kutumia sehemu au viungo mbalimbali maalumu vya mwili wa mwanadamu. Katika taaluma ya isimu sehemu ya viungo vya mwili vitumikavyo katika utoaji wa sauti za lugha hujulikana kama ALASAUTI
Ala sauti hizo ni pamoja na mapafu, umio, koromeo, kaakaa laini na gumu, ufizi, meno, midomo, pua, n.k
Kwa kutumia ala hizo za sauti mwanadamu anao uwezo wa kutoa sauti nyingi sana ambazo hutumika katika lugha.
NB: Zipo sauti ambazo hazitumii alasauti maalumu na huwa hazina maana mahususi, sauti hizi hujulikana kama vidoko vya midomo na alama yake ni kidoti ndani ya duara mf. ʘ, sauti hizo ni kama mluzi, kubusu, kusonya, n.k
MOFOLOJIA NA SINTAKSIA
Mofolojia ina uhusiano mkubwa na sintaksia kama ilivyo kwa vitengo vingine. Ingawa sintaksia hujishughulisha na tungo, muundo, dhima na maana za sentensi, hutegemea sana vipashio vya kimofolojia ambavyo ni maneno ili kuyapangilia katika darajia za kisintaksia.
Mfano
(a) Vitabu vya watoto wa Juma vimeibwa
(b) Madirisha ya shule za miembeni yamevunjwa
© Wizi wa bunduki za jeshi  umeongezeka
(d) Nyumba za Mapadri wa kilakala zimeuzwa
Mifano hiyo inaonesha jinsi nomino zinavyotawala vipashio vingine kisintaksia yaani:
[Image: SAM_1500.JPG]
Kwa ujumla sintaskia hutawala mpangilio na mfuatano wa vipashio vya kimofolojia. Hii  ni kusema kuwa ili sintaksia ifanye kazi yake ni lazima mofolojia ishiriki kutoa vipashio  hivyo.
UPWEO WA MOFOLOJIA YA KISWAHILI
Mofolojia ya Kiswahili kama zilivyo mofolojia za lugha nyingine inahusu taaluma ya maumbo ya maneno ya lugha ya Kiswahili.  Kama mtaalamu wa mofolojia ya Kiswahili unapaswa kuzingatia mambo yafuatayo.
  1.  a) muundo wa maneno
  2. b) makundi na mahusiano ya maneno
  3. c) kanuni za uundaji wa maneno (njia au mbinu)
Kwa mfano:
Kila mtaalamu wa Kiswahili anaelewa kuwa neno –Anasoma-limeundwa kwa vipashio  A-na-som-a
Neno hilo-anasoma-linalingana na neno, Anasomesha.
Kwa msingi kwamba maneno yote yanaundwa kwa mzizi – som – sawa na maneno usomi, msomaji, kisomo, usomaji n.k
Katika taaluma ya Kiswahili inabidi kujua uhusiano na athari za maneno hayo.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)