MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

MAJINA YA UKOO/NASABA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MAJINA YA UKOO/NASABA
#1
1. Mama/nina: Mzazi wa kike.
2. Baba: Mzazi wa kiume.
3. Kaka: Ndugu wa kiume.
4. Dada: Ndugu wa kike.
5. Nyanya/Bibi: Mama wa baba au mama.
6. Babu: Baba wa mama au baba.
7. Mjukuu: Mtoto wa mwana.
8. Kitukuu: Mwana wa mjukuu.
9. Kilembwe: Mwana wa kitukuu.
10. Kilembwekeza/kining’ina: Mwana wa kilembwe.
11. Ami/amu: Kaka wa baba.
12. Shangazi/mbiomba amati: Dada wa baba.
13. Mjomba/hau: Kaka wa mama.
14. Halati/hale: Dada wa mama bila kubagua kama ndiye mdogo au mkubwa kwa mama yako mzazi. Pia huitwa hale.
15. Mkazahau: Mke wa mjomba.
16. Mkazamwana: Mke wa mwana au mke wa mtoto wako.
17. Mavyaa: Mzazi wa kike wa mume.
18. Bavyaa: Mzazi wa kiume wa mume wako.
19. Mamamkwe: Mama wa mke/Mume.
20. Babamkwe: Baba wa mke/Mume.
21. Mcheja: Mzazi wa mke au mume (mkwe).
22. Kivyere : Jina la wazazi wa mume na wazazi wa mke hutumia kuitana.
23. Mpwa: Mtoto wa dada wa mtu mwanamume; jina analotumia mjomba kumwita mtoto wa dadake.
24. Mkoi: Mtoto wa shangazi, mjomba, halati.
25. Binamu: Mwana wa kiume wa ami.
26. Bintiamu: Mwana wa kike wa ami.
27. Shemeji: Ndugu wa mke au ndugu wa mume.
28. Mama wa kambo: Mama asiyekuzaa lakini anakulea.
29. Baba wa kambo: Baba asiyekuzaa
30. Umbu: Jina waitanalo kaka na dada. Ni jinsi kaka anavyomwita dada naye dada anavyomwita kaka wakiwa wamezaliwa na mzazi mmoja.
31. Ndugu mlungizi: Ndugu anayekufuata
32. Ndugu mlungizi: Ndugu anayekufuata nyuma.
33. Wifi: (a) Mke wa kaka. Iwapo wewe ni msichana, mke wa kaka yako utamwita wifi. (b) Dada wa mume: Iwapo msichana ameolewa dada wa mumewe atamwita wifi.
34. Mwamu/mlamu: a) Kaka wa mke. Mwanamume akioa, kaka wa mkewe atamwita mlamu. b) Mume wa dada: mvulana au mwanamume atamwita mume wa dadaye – mlamu.
35. Mwanyumba: Ni mwanaume mwenzako aliyeoa kutoka boma moja ulikooa wewe. Ni mume wa dada wa mke wako.
36. Mkemwenza/mitara: Jina wanalotumia wanawake walioolewa na mwanamume mmoja.
37. Kifungamimba/ kitindamimba/ mziwanda: Mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia.
38. Mwanambee/kifunguamimba/kichinjamimba: Mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia.
39. Nyanyamkuu: Mama wa nyanya.
40. Babamkuu: Baba wa babu.
41. Maharimu: Mtu usiyeweza kumwoa au kuolewa naye kwa sababu ya uhusiano wa nasaba.
42. Mnuna: Ndugu anayenifuata ndugu mdogo.
43. Baba mkubwa – Ndugu wa kiume, mkubwa wa baba yako.
44. Baba mdogo – Ndugu wa kiume, mdogo wa baba yako.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)