Tulipolinganisha maneno {mtu} na {watu} hapo juu tulisema kuwa kwa kujua uhusiano kati ya maneno hayo mawili, ni wazi kuwa kila moja limeundwa na vipashio zaidi ya kimoja. Kwa kuzingatia sehemu isiyobadilika ya maneno hayo, ni dhahiri kuwa kila moja limeundwa na vipashio viwili: /m-tu/ na /wa-tu/. Tunafahamu pia, kimatumizi, kuwa tofauti kati ya maneno hayo ni kuwa moja {mtu}linaonyesha ‘umoja’, na lingine {watu} linaonyesha ‘wingi’. Kwa vile kipashio /-tu/ kinajirudia katika maneno yote mawili, tunajua kuwa tofauti hiyo inaletwa na kuwepo kwa viumbo /m-/ na /wa-/, hivyo tukaweza kuhitimisha kuwa viumbo hivi vinasimamia ymoja na wingi, na kiumbo /-tu/ ni mzizi au kiini cha maneno yote mawili. Vipashio, vinavyojenga maneno hayo mawili haviwezi kuvunjwavunjwa zaidi na vikaendelea kuwa na kazi hizo hizo katika sarufi ya Kiswahili.
Vipashio vidogo sana vya msingi kama hivyo hapo juu vinavyotumika katika kuunda maneno ya lugha vinaitwa mofimu. Neno hili asili yake ni lugha ya Kigiriki, na maana yake ni “umbo”. Mofimu ni vipashio vinavyoonyesha uhusiano uliopo kati ya sauti-msingi za lugha (yaani fonimu) na maana maalumu katika sarufi ya lugha. Hivyo tunaweza kusema kuwa mofimu ya umoja katika neno {mtu} imeundwa na fonimu /m/ ambayo ni king’ong’o cha mdomo; na mofimu ya wingi imeundwa na fonimu mbili /w,a/ ambazo ni kiyeyusho na irabu chini. Sasa bila shaka unaweza kuona uhusiano uliopo kati ya vipashio vya kifonolojia tulivyojadili katika sura ilyotangulia, na uundaji wa mofimu za lugha.
Kila neno katika lugha limejengwa na mofimu moja au zaidi. Neno linalojengwa na mofimu moja tu linaitwa neno sahili, na lile linalojengwa na mofimu zaidi ya moja linaitwa neno changamano. Hivyo, katika Kiswahili, tunaweza kusema kuwa {chungwa} ni neno sahili kwa vile haliwezi kukatwakatwa katika vipashio vidogo zaidi, kama tukilinganisha {chungwa: machungwa}.
Maneno yaliyo mengi katika lugha kama ya Kiswahili ni changamano kama itakavyodhihirika katika mifano. Hata maneno mafupi kama {wa, ya, vya} ya sentensi za (4) hapo juu, ni changamano. Kila moja lina mofimu mbili, moja ambayo inasimamia upatanisho na nomino, na /-a/ ambayo haibadiliki, na katika sarufi ya Kiswahili tunaiita {-a} mofimu ya ‘uhusiano’. Lugha nyingine zinayo maneno sahili mengi zaidi ya Kiswahili. Katika lugha ya Kiingereza, kwa mfano, nomino nyingi katika umoja ni manerio sahili: {boy, girl, book} etc. Lakini, katika wingi, nomino nyingi za Kiingereza ni maneno changamano {boy-s, girl-s, book-s} etc. Hata vitenzi vya Kiswahili si maneno sahili hata kama hayajaambikwa vipashio vingine. Kwa mfano neno {sema}:
Quote:
8 a) Juma amesema wageni wamekuja
b) Juma hasemi uwongo.
Kipashio /sem-/ katika sentensi hizo ni mzizi wa kitenzi {sema}, kwa sababu ndiyo sehemu ambayo haibadiliki, na hivyo tunaona kuwa fonimu /a/ ya {sema} si sebemu ya mzizi wa kitenzi hicho kwa sababu inaweza kudondoshwa na nafasi yake ikacbukuliwa na kinashio kingine kama hapo juu. Hata hivyo tunaweza kupata maneno zaidi ya Kiswahili ambayo ni sahili, kama vile maneno ya sifa: {safi, kubwa, dogo, fupi; zuri} n.k. (mfamo:{chungwa safi, kubwa, zuri} n.k.
Neno changamano linaundwa na aina mbili za mofimu: mzizi na kiambishi (au viambishi); ambapo neno sahili linaundwa na mzizi peke yake. Viambishi viko vya aina tatu: viambishi-tangulizi, vinavyoambikwa kabla ya mzizi wa neno; viambishi-fuatishi, vinavyoambikwa baada ya mzizi; na viambishi-kati, ambavyo vinaingizwa katika mzizi, na hivyo kuukata katika sehemu. /m/ na /wa/ katika maneno {m-tu} na {wa-tu} ni viambishi-tangulizi, ambapo /-i-/ na /-ish-/ katika maneno {kat-i-a} na {kat-ish-a) ni viambishi-fuatishi. Viambishi kati havitokei katika Kiswahili, lakini vipo katika lugha nyingine. Kwa mfano katika maneno yafuatayo ya lugba ya Kiebrania, mzizi ni /zkr/ ambao unakatwa na viambishi kwa njia tofauti katika kila neno:
Ni dhahiri kuwa viambishi vya aina zaidi ya moja vinaweza kutokea katika neno lnlo hilo mbja kama tulivyoona katika mfano wa bapo juu, na pia katika neno lifuatalo la Kiswahili:
Quote:
10 a) mkutano : {m-kut-an-o} (mzizi ni {kut-}.
Katika neno hili, kuna kiambishi-tangulizi {m-}, na viambishi-fuatishi {-an-, o}. Neno hili linaweza kulinganishwa na maneno:
Quote:
10 b) kuta: kutana.
Katika uchambuzi wa mofimu kuna istilahi nyingine ambazo ni muhimu kuzijua. Mofimu zinaweza kuwa huru, au tegemezi. Zile mofimu ambazo hazina haja ya kuchukua viambishi vyovyote na hivyo kuweza kusimama peke yake kama maneno ni mofimu huru. Hivyo maneno sahili ni mofimu huru pia. Mofimu tegemezi ni zile ambazo haziwezi kusimama peke yake katika neno bila kuambatana na mofimu nyingine, yaani zikiwa peke yake haziwezi kuunda neno katika lugha. Kwa mfano, neno {m-tu} limeundwa na mofimu tegemezi mbili, ambapo neno {ma-chungwa} limeundwa na mofimu tegemezi moja na mofimu huru moja. Vivyo hivyo, neno la Kiingereza {girl} limeundwa na mofimu huru moja, ambapo {girl-s} lina mofimu huru moja na mofimu tegemezi moja. Mofimu za mzizi zinaweza kuwa huru, (kama nomino na vitenzi vingi vya Kiingereza), au tegemezi (kama nomino nyingi na vitenzi vingi katika Kiswahili). Lakini mofimu za viambishi, kwa kawaida ni tegemezi.
Tukiweka pamoja hayo tuliyoyasema mpaka sasa tunaweza kuonyesha uhusiano uliopo kati ya vipashio tulivyoainisha katika uchambuzi wa mofimu za lugha: vipashio vya msingi vinavyounda maneno ya lugha ni mofimu. Neno linalojengwa na mofimu moja tu, ni neno sahili. Ikiwa linajengwa na mofimu zaidi ya moja ni neno-changamano. Mofimu ziko za aina mbili: mizizi na viambishi, na kila neno lina mzizi. Ikiwa neno limeundwa na mzizi peke yake bila viambishi, mzizi huo ni mofimu huru. Mofimu ambayo haiwezi kusimama peke yake bila kuwa na mofimu nyingine katika neno ni mofimu tegemezi. Hivyo neno-sahili ni mofimu-huru na ni mzizi.