MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

Visasili (Visa-asili)

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Visasili (Visa-asili)
#1
Visasili ni ngano za kihistoria zinazoeleza chimbuko /asili ya jamii/kabila fulani; tamaduni mbali mbali katika jamii ile na namna jamii hiyo ilivyofika katika eneo lake la sasa. Visasili husaidia kuelezea asili ya mambo yasiyoelezekakama vile mauti, jando, tohara, ndoa na tamaduni/imani nyinginezo.
Tanbihi: Tofauti kati ya visasili na usuli(visaviini) ni kwamba visasili huhusisha jamii fulani, mila, imani na matukio ya kiada kama vile kifo, tohara n.k ilhali ngano za usuli huelezea kwa nini mambo fulani hufanyika bila kuhusisha jamii au imani.

Sifa za Visasili
  1. Huelezea chimbuko la jamii fulani
  2. Matokeo yake hufanyika mwanzoni (k.v mwanzo wa dunia)
  3. Aghalabu huhusisha miungu, malaika n.k
  4. Kuburudisha
Umuhimu wa Visasili
  1. Kutafuta jibu kwa maswali yanayotatiza
  2. Kuhifadhi historia na imani ya jamii
  3. Kuunganisha jamii
  4. Kuwasilisha mila na desturi za jamii

Mifano
  1. Asili ya jamii ya Wamaasai
  2. Asili ya Wagikuyu
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)