MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
CHANGAMOTO AMBAZO ZINAZOKIKABILI KISWAHILI SHULENI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
CHANGAMOTO AMBAZO ZINAZOKIKABILI KISWAHILI SHULENI
#1
CHANGAMOTO AMBAZO ZINAZOKIKABILI KISWAHILI SHULENI
KUNA changamoto nyingi zinazoikabili lugha ya Kiswahili kama somo katika shule zetu humu nchini. La kutia moyo ni kwamba imebainika, ingawa si mapema sana, kuwa zipo njia za kukabiliana na changamoto hizo.
Kwanza, ni kukua, kusambaa ama kuenea kwa lugha za mitaani hasa Sheng. Shule zetu zimejaa vijana ambao wanapenda lugha za mitaani ambazo hazifungwi na kanuni za lugha. Lugha hizi hazizingatii mfumo wa ngeli tuujuao wala kujali istilahi (msamiati maalumu) za lugha zinazotakikana.
Katika shule zetu pia kumejaa wanafunzi wengi ambao hawaithamini lugha ya Kiswahili. Wengi wao wanaona kuwa ni kuwa lugha ya watu wenye kiwango duni cha elimu. Yaani ni watu ambao hawawezi kujieleza vyema katika Kiingereza.
Watu kama hawa zamani walikumbana na wakaguzi wa Kiswahili ambao siku hizi ni wachache na wamelemewa na kazi nyingi za kiofisi. Muda wao wa kwenda nyanjani haupo tena!
Tatu, ni kwamba baadhi ya wanafunzi wamejawa na kasumba ya kikoloni kiasi kuwa wanapenda Kiingereza na lugha nyingine za kigeni na kuendelea kukidunisha au kukidharau Kiswahili ambacho wanakiona kuwa lugha ya askari, vibarua na watu wa mitaani ambao hawajasoma sana.
Vyombo vya habari
Changamoto nyingine tuliyonayo ni ile ya vyombo vingi vya habari, si vyote, kupotosha Kiswahili. Vingi vya vyombo hivi; magazeti, radio na televisheni havitumii Kiswahili sanifu.
Mara kwa mara tunakumbana na Kiswahili kisicho sanifu kikiwa kimetumika katika vyombo hivi vya habari. Makosa katika vyombo hivi ni ya msamiati, maendelezo (tahajia) sarufi, semi, matumizi ya lugha na kadhalika.
Baadhi ya haya makosa hutokana na athari ya lugha ya kwanza ya mwandishi ama mtangazaji. Makosa kama haya yanaathiri lugha yetu sanifu kwa kiasi kikubwa sana.
Mbali na makosa haya ni yale mengi ya lugha kukosa sera. Hii inatokana na nchi kutokuwa na chombo mahususi cha kudhibiti matumizi na ukuaji wa lugha. Lugha inajikulia tu kiholela ambapo hatima yake kila mmoja wa watumizi wake anaweza kuibuka na msamiati wake, semi zake na hata kanuni zake za sarufi bila kupingwa na wenzake mradi tu aweze kujitetea vyema.
Changmoto nyingine tuliyonayo ni kwa shughuli nyingi zinazofanyika katika shule zetu huendeshwa kwa Kiingereza. Nafasi ya Kiswahili ni ndogo sana na nyakati nyingine haipo kabisa.  Hivyo, Kiswahili hakifanyiwi mazoezi yoyote.
Masomo kufundishwa kwa Kiingereza
Kulingana na mfumo wetu wa elimu masomo yote yanafundishwa kwa Kiingereza. Wanafunzi wetu hawaoni hata haja ya kujiimarisha katika lugha ya Kiswahili. Yenyewe ni somo moja tu na inakaribiana sana na lugha yao ya kwanza hasa kwa wale walio Wabantu.
Katika baadhi ya shule, taasisi na vyombo vingine muhimu vya lugha wale na wale wanakishughulikia Kiswahili si walimu waliofuzu. Mtu yeyote anayeweza kujieleza kwa Kiswahili huambiwa jaribu tu kwa muda ilhali tukisubiri kupata mwalimu. Akiweza kuwaridhisha wanafunzi wake basi huachiwa madarasa kadhaa kuyafundisha.
Kufikia sasa kuna baadhi ya shule hukumbwa na uhaba wa vitabu vya kufundishia Kiswahili va vile vya kujisomea kukuza msamiati, semi na miundo mingine ya sarufi. Kupanda kwa gharama ya maisha kumewafanya baadhi ya wazazi kushindwa kuwanunulia wana wao vitabu vya masomo yote. Vya Kiswahili vinakuwa ni vile vya kubambanya.
Tumekuwa tukilalamikia muda mfupia ambao umetengewa Kiswahili wa vipindi vitano ilhali Kiingereza kina vipindi vinane. Kile kinachowasumbua walimu wa Kiswahili ni kwamba kina mambo mengi ya kufunzwa kama Kiingereza tu; karatasi ya 1 – Insha, ya pili – Lugha; Ufahamu, Muhtasari, Matumizi ya lugha na Isimu jamii. Bila shaka ili mtahiniwa afanye vyema katika mitihani yake ya Darasa la Nane (KCPE) na Kidato cha Nne (KCSE) anahitaji wa kutosha wa kuandaliwa vyema.
Mbali na KCPE na KCSE katika vyuo pia kuna tatizo pia. Wanafunzi wanaosomea Kiswahili kwa shahada ya kwanza lazima wasome Kiswahili na somo jingine kama vile Jiografia, Historia, Dini na kadhalika ilhali wenzao wa Kiingereza wanasoma Kiingereza na Fasihi ya Kiingereza. Mbona wenzetu wa Kiswahili wasisome Kiswahili na Fasihi ya Kiswahili badala ya kuongezewa somo jingine?
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)