MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JE, KISWAHILI NI KIARABU?

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
JE, KISWAHILI NI KIARABU?
#1
Kuna hoja kuu tatu ambazo baadhi ya wananadharia hii huzitumia kutetea nadharia hii kuwa Kiswahili asili yake ni Kiarabu.
  1. Inadaiwa kuwa maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kama Pijini ya Kiarabu.
  2. Inahusu neno lenyewe Kiswahili ambalo asili yake ni Kiarabu. Neno Kiswahili linatokana na neno “sahili” (umoja) na “swahil” (wingi) lina maana ya pwani.
  3. Inadaiwa kwamba kwa kuwa Kiswahili kilianza pwani, kwa kuwa idadi kubwa sana ya wenyeji wa pwani ni waislamu, na kwa kuwa uisilamu uliletwa na Waarabu, basi Kiswahili nacho kililetwa na Waarabu.
   Kiswahili si Kiarabu
Madai kwamba Kiswahili si Kiarabu yanathibitishwa na hoja kinzani zifuatazo:
Tukianza na dai la kwanza ‘kwamba maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kama pijini ya Kiarabu’ tunaona wazi kwamba madai haya hayana mashiko. Lugha ya Kiswahili imetokea kuwa na maneno yenye asili ya Kiarabu (na kwa hakika yapo yenye asili ya Kiajemi, Kireno, Kihindi, Kijerumani, Kiingereza nk.) kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na mawasiliano ya karne na karne baina ya wenyeji wa pwani na wafanyabiashara wa Kiarabu. Wasemaji wa lugha mbili tofauti wanapokutana hawaachi kuathiriana kilugha. Kwa hiyo lugha kuwa na maneno mengi ya kigeni kutoka lugha nyingine, haifanyi lugha hiyo isemekane kuwa imetokana na hiyo lugha nyingine.
Pili wataalamu hawa wanadai kwamba neno lenyewe Kiswahili lina maana ya Kiarabu.
Kwani linatokana na neno “sahili” (umoja) na “swahil” (wingi) lina maana ya pwani. Hapa ingetupasa tuelewe kwamba kila mtu binafsi au jamii binafsi aghalabu hajiiti mwenyewe jina lake, yeye huitwa kwa hilo jina alilopewa na wengine: Jamii yake au wageni waliomtembelea kwake. Na hivi ndivyo ilivyojitokeza kwa upande wa jamii ya watu wa pwani ya Afrika mashariki, yaani Waswahili,  walipotembelewa na Waarabu na kuitwa As-Sahilyy au As-Sawahiliyy, na nchi yao kuitwa sahil (wingi wake Sawahil), yaani pwani (upwa), ufuo. Kwa mantiki hii, dai hili halina mashiko !
Kigezo cha dini nacho hakikubaliki lugha haiwi lugha kwa sababu ya imani. Hata hivyo lugha ya Kiarabu yenyewe ilikuwepo karne nyingi kabla ya kufunuliwa dini ya Uislamu. Hali kadhalika, lugha nyingine za Kimagharibi zilikuwepo karne nyingi kabla ya kufunuliwa imani ya ukristo. Kama ilivyo kwamba Kiingereza au Kijerumani si ukristo, basi ndivyo vivi hivyo ilivyo kwamba Kiswahili hakiwezi kuwa dini ya uislamu, aslan! Wala Kiarabu nacho si uislamu. Tunachoweza kufanya ni kuitumia lugha kuifasili dini, lakini hatuwezi kuitumia dini kuifasili lugha.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)