08-20-2021, 02:36 PM
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO
*SEHEMU YA 08**
Dar es salaam;
Nyumbani kwa mzee Jastin kulikuwa na hekaheka, japokuwa nilikuwa sina miguu lakini niliweza kushuka kwenye sofa ambalo nilikuwa nimeketi na kisha kutambaa kuelekea chumbani kwa Juliet. Sekunde chache tu, nilikuwa uvunguni mwa kitanda. Huku nikipumua kwa kasi sana, upumuaji ambao ulikuwa mithili ya mgonjwa mahututi wa Pumu.
Kitendo cha mimi kutoweka sebuleni kwa mwendo wa ajabu, mwendo ambao niliufananisha na spidi ya magari yaendayo mikoani. Ndicho ambacho kilinifanya mimi kupumua kwa kasi, kwani pumzi iliniishia kabisa.
“Leo ni leo, nimepatikana, mzee huyu akibahatika kuiona sura yangu, lazima aniue “,nilizungumza peke yangu bila kujali kama kuna mtu yeyote aliweza kuisikia sauti yangu au laa!. Niliendelea kutambaa na kujivuta polepole kwa mwendo wa taratibu mithili ya kinyonga, na kuketi katikati uvunguni mwa kitanda. Sehemu ambayo mtu yeyote ambaye angechungulia kwa macho ya kawaida asingeniona, kwani giza totoro lilikuwa uvunguni mule, na lazima yeyote ambaye angetaka kuona kilichokuwa uvunguni, lazima atumie vifaa kama tochi bila hivyo asingeweza kuniona.
********
Mzee Jastin alipiga honi ya gari lake kwa muda mrefu sana, lakini hakuna mtu yeyote aliyeweza kwenda kumfungulia geti. Akiwa na hasira sana, alitoka ndani ya gari na kisha kuisogelea batani moja iliyokuwa ukutani na kisha kuibonyeza. Rose akiwa sebuleni, aliendelea kusimama kama sanamu kwani hakujua nini afanye kwa wakati ule, jambo pekee ambalo lilimfanya apigwe na butwaa. Ujio wa baba yake nyumbani ghafla, na tena bila taarifa ndio sababu iliyomfanya Rose kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu kichwani mwake.
“Au kuna mamluki kampatia taarifa baba, kuwa Robert yuko nyumbani !,siko tayali kumuona baba akimuua, moyo wangu sitakuwa nimeutendea haki”,Rose aliongea kwa sauti ya juu bila kujitambua, sauti ambayo hata mimi niliweza kusikia kila kitu alichokiongea nikiwa uvunguni mwa kitanda, ndani ya chumba chake.
“Griiiiiii, griiiiiiiii, griiiii ……” mlio wa kengele ulisikika katika masikio ya Rose, na kumfanya akurupuke kutoka katika mawazo aliyokuwa akiwaza. Bila shaka alitambua hasira ambayo baba yake alikuwa nayo, hasa baada ya kuamua kubonyeza kitufe cha kengele, alipoona honi ya gari haijazaa matunda na geti kufunguliwa.
“Shikamoo baba! “, Rose aliongea kwa upole sana na kumsalimia baba yake, baba ambaye alikuwa na sura iliyokunjamana utazani alikuwa amekula chumvi nyingi kumbe sivyo!, hasira aliyokuwa nayo ndiyo iliyosababisha kukunja sura yake, sura ambayo Rose aliweza kuogopa kumsogelea kwani pengine angeambulia kofi au mateke kwani siku zote baba yake ndicho kitendo alichokuwa akimfanya Rose akiwa amemkosea.
“Hebu fungua geti mwanaharamu wewe! Na utaniambia kilichokufanya unikalishe hapa nje nusu saa nzima bila sababu “,mzee Jastin akiwa na hasira, alitamka maneno ambayo yalimshangaza sana Rose. Hakuamini kama kweli baba yake ndiye aliyeweza kumtamkia maneno makali kiasi kile, tena binti yake pekee wa kumzaa.
“Baba hivi kweli wewe ni baba yangu, unaniita mwanaharamu!!! Kweli baba! Kweliiii “,Rose alijikuta akisahau kama ndani alikuwa amemwacha mtu ambaye hapendwi na baba yake, alisahau kila kitu kuhusu kulipiza kisasi na kuniua, kwani aliniona kuwa chanzo cha yeye kumkosa Peter. Jambo ambalo lilikuwa kichwani mwake, ni kuhusu mahusiano yake yeye na baba yake mzee Jastin.
“Hivi baba yako wa kukuzaa anaweza kukaa siku tano bila kukupigia simu na hujui kaenda wapi!, baba yako wa kukuzaa anaweza kukuficha ndugu zako! baba yako wa kukuzaa anaweza kukuacha uishi peke yako nyumbani bila hata mlinzi au mfanyakazi wa ndani!,baba yako mzazi anaweza kukupangia kuolewa na mtu anayemtaka yeye ili kuendeleza biashara zake! na pia isitoshe anakuita mwanaharamu kwelii!
“Noo, noo, no! This is not my dady! aim sure hundred percent! But where is my real parents? ” (Hapanaa, hapanaa, hapana! Huyu sio baba yangu !nina uhakika asilimia mia moja !Lakini wako wapi wazazi wangu halisi?)
Rose akiwa ameegemea geti kubwa baada ya kumfungulia baba yake mzee Jastin, alijiuliza maswali mengi na hatimaye kupata jibu lake. Jibu ambalo lilimfanya atokwe na machozi mengi sana, kwani aliamini mzee Jastin hakuwa baba yake mzazi.
********
Mzee Jastin aliingia ndani na kubamiza mlango kwa fujo, aliamini kabisa Rodgers atakuwa tayali amekamtwa na polisi, kwani muda ulikuwa umepita mrefu sana! Hivyo basi ingekuwa vigumu kumtorosha uwanja wa ndege wa Mombasa akiwa salama.
“Shitiii! hizi ndizo hasara za kuishi na watoto wa kuokota! Mitoto haina akili kabisaa! And this bastard president, aim sure! Kafanikiwa kumkamata kijana wangu”,jambazi la kutisha nchini Tanzania, mzee aliyetumia kivuli cha biashara kuficha makucha yake. Mzee aliyejulikana kwa jina la Jastin, mmoja wa wafanyabiashara ambao walikuwa na sauti kubwa katika serikali ya Tanzania, aliongea maneno bila kutambua kuwa kuna mtu aliweza kuyasikia. Adui ambaye siku zote aliweza kumchukia, na kujalibu kumuua mala nyingi bila mafanikio ,kijana Robert ndiyo aliyeweza kusikia maneno yake ambayo yalimfanya kujiuliza maswali mengi.
“Rose kasema hataki kumuona baba yake akiniua, anataka autendee haki moyo wake yeye mwenyewe! Kuna nini hapa katikati? “,
“Mzee Jastin anasema Rose kamuokota!!, ndio maana anamfanyia mambo ya ajabu “,nilijiuliza maswali moyoni mwangu, na kuapa kumweleza Rose kila kitu nilichokisikia kama nitafanikiwa kutoka salama uvunguni mwa kitanda nilipokuwa nimejificha.
“Kijana imefika salama Mombasa! ile kijana imafia kabisa, imetoroka polisi yote uwanja kwa ndege bila kukamatwa “,ilikuwa ni sauti ya simu, sauti ambayo bila shaka iliwekwa roud speaker !.Ilikuwa ni sauti ya mtu aliyeonekana kutokuwa mtanzania kutokana na kiswahili chake alichokuwa akiongea, niliposikia neno Mombasa likitajwa! Bila shaka niliamini mtoa taarifa alikuwa raia wa Kenya.
“Waaaoh! Aim happy now! Good work Rodgers ……!”,(waaoh, nina furaha sasa, kazi nzuri Rodgers …” ,)nilisikia sauti ya mzee Jastin, mzee aliyeongea huku akiwa amechomeka simu chaji bila kujali hatari yoyote ambayo ingeweza kumkuta kwa kufanya mawasiliano huku simu ikiwa inachajiwa.Niliamini asilimia mia moja kuwa alikuwa akiongea na mtu aliyemtaja katika maongezi, mtu aliyejulikana kwa jina la Rodgers kumbe sikuwa sahihi.
“Hapa ngoja niende kambini, kwenye kambi yetu ya Mbezi, sasa hivi hapa nyumbani sio salama mimi kuishi “,mzee Jastin alichomoa simu yake chaji, lengo lake la Rodgers kusafiri bila kukamatwa liliweza kutimia, hivyo hakuwa na budi kutoweka nyumbani kwake.Alimpita Rose akiwa kibarazani na mawazo mengi sana, kwani baada ya Rose kuchoka kuegemea geti aliamua kwenda barazani na kupunga upepo huku akitafakali namna ya kuanzia kutambua siri iliyofichika kuhusu ukweli wa maisha yake.
“Wewe mpuuzi usisahau kufunga geti! mimi naondoka zangu “,mzee Jastin kweli alibadirika!,Alikuwa tofauti na zamani alipokuwa akionyesha mapenzi ya kuigiza kwa mwanae Rose, sasa hivi alimuonyesha chuki ya waziwazi kabisa. Mzee huyu aliongea huku akisindikiza mitusi kwa msichana mrembo Rose, na kisha kuondosha gari lake eneo lile na kuacha geti likiwa wazi.
“Yes i have got the way! his computer can aswer me every thing ……” (Ndio nimepata njia! Kompyuta yake inaweza kunijibu kila kitu),hatimaye Rose aliweza kutabasamu, fikra zake hazikwenda bure! aliamini komyuta ya baba yake iliyomfanya kutambua kazi halisi ya baba yake na lengo la kumlazimisha kuolewa na mtoto wa raisi aliyeitwa Jacob, ingeweza kumpatia majibu pia kuhusu historia ya maisha yake.
Rose alitabasamu kwa mbali huku akifuta machozi yake yaliyokuwa yakimtiririka usoni na kisha kwenda kufunga geti haraka sana, geti ambalo liliachwa wazi na baba yake alipolifungua na kutoweka nyumbani na gari yake. Hakuwa na sababu ya kuchelewa! Lengo lake ilikuwa ni kwenda kuchezea kompyuta ya baba yake, kompyuta ambayo mzee Jastin aliamini Rose alikuwa hafahamu namba zake za siri kuifungua.
********
Raisi wa Tanzania hakuamini taarifa aliyokuwa ameambiwa, aliamini kabisa camera za uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere zilizonesha Rodgers kusafiri usiku ule, na pia aliamini taarifa aliyopewa mwanzoni kabisa na mtoa ticketi za ndege aliyeitwa Juma, kijana aliyemsariti rafiki yake mzee Jastin na kumpatia taarifa raisi kuwa muuaji wa mwanae alikuwa akisafiri kutoweka Tanzania. Baada ya raisi kupokea taarifa kutoka kwa Juma, aliamuru ndege isiweze kuruka mpaka askari wake aliyemwamini sana atakapofika na kusafiri katika ndege hiyo huku akiifanyia ukaguzi na kumsaka mtuhumiwa.
Lakini bila kutegemea! ndege ilifika Mombasa bila Rodgers kukamatwa, askari wa Kenya walipojaribu kukagua camera za uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mombasa (MOI),nao pia walishangaa, sura ya Rodgers haikuonekana kufika uwanjani hapo usiku huo.
Jambo hilo lilimtatiza sana raisi, raisi aliamini Rodgers alikuwa mtu hatari sana na kazi ya ziada ilihitajika na pengine hata kuomba msaada wa askari wapelelezi wa kimataifa. kuja kumtafuta mtuhumiwa huyu aliyeonekana kuwa moto wa kuotea mbali.
“Unajua sielewi! Uwanja wa ndege anaonekana akipanda ndege, lakini Kenya hajaonekana! Insipekta Chacha amekagua ndege hajamuona! Hapa inatakiwa mtumie akili za kuzaliwa bila hivyo tutakufa sisi kabla yake “,raisi akiwa amekasirika, aliongea maneno ya kuoneshwa kushangazwa sana na taarifa aliyopatiwa na askari wake, tena askari aliokuwa akiwaamini sana katika kazi zao.
Mwl Maeda