Alimpenda mno mke wake, alijitahidi kumpa mkewe kila kitu kilochopo ndani ya uwezo wake, lakini mke wake hakuwa akiridhika na ku appriciate. Ingawa hakuwa tajiri lakini alijitahidi mno ku share kile alichonacho.
Kila alipomnunulia nguo mkewe, jibu pekee alilolipata lilikuwa ni kwamba alikuwa akikamilisha jukumu lake kama mume. Mkewe hakuwahi kutoa shukrani hata mara moja.
Mwanaume angemnunulia nguo mkewe lakini mkewe alikuwa akimjibu kwamba nguo ni ya bei ya chini na quality yake ni ndogo. Mume angetabasamu na kumwambia mkewe kwamba “siku moja nitakapokuwa tajiri nitakununulia vitu vyote vya gharama unavyovitaka” kwa sasa naomba nivumilie tu mke wangu!
Mke hakuwa akimpigia simu mume wake labda tu pale alipokuwa akihitaji kitu au pesa kutoka kwa mumewe, na kama asipokamilishiwa ombi lake ilikuwa ni ugomvi kwa siku kadhaa.
Jioni moja, mume alirudi kutoka kazini, alileta nyumbani kilogramu moja ya nyama, kwa furaha tele alitegemea kumsuprise mkewe. Alifika nyumbani na kumuona mkewe na akamuonyesha ile kilo ya nyama! Mkewe kwa dharau akamwambia ” eh na ndio unajiita mwanaume? Unafikiri kurudi nyumbani na kilo moja ya nyama bila viungo, mafuta ya kupikia wala mbogamboga ndio kutakufanya uonekane kidume? Bora ungeacha tu! Huna msaada wowote hapa.
Kisha akaenda kuitupa ile nyama jalalani, mume alijisikia vibaya sana lakini hakuchoka kuendelea kumpenda mkewe. Aliendelea kufanyiwa vituko mbalimbali lakini hakuteteleka juu ya mapenzi kwa mkewe na familia yake.
Siku moja mume alipatwa na maumivu ya mguu wa kushoto, baadae uvimbe ukatokea katika mguu na ukawa ukikua siku baada ya siku.
Alienda hospitalini na akakutwa alikuwa na kansa, hakuwa na pesa za kutosha za matibabu ya kansa. Japo alikuwa mgonjwa ila alijitahidi kuhudumia familia yake.
Miaka miwili baadae hali ilizidi kuwa mbaya, mpaka akapelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Alifanyiwa operation na mguu ukaondolewa baada ya kuwa umeathiriwa vibaya na kansa. Lakini kwa bahati mbaya walikuwa wamechelewa, ugonjwa ulikua umesha athiri na maeneo mengine mengi ya mwili.
Alimwita mkewe na kumwambia “NITUNZIE WANANGU” najihisi mwili udhaifu, roho inataka kunichomoka, maumivu hayaniishi, nafikiri siwezi kuishi tena! Siku zote nitakuwa na wewe kiroho! Mwenyezi Mungu akubariki na ninakupenda sana mke wangu!
Alivuta pumzi yake ya mwisho na kufariki. Mkewe na watoto wake pamoja na ndugu na marafiki waliomboleza msiba ule na wakazika!
Miezi mitatu baadae mkewe alikuwa ameinamia kaburi la mumewe akitamka maneno haya kwa uchungu mwingi!
“Mume wangu mpenzi! Ulifanya kila uwezalo kunihudumia, ulinijali vema na kunipa kile kilichokuwa ndani ya uwezo wako. Ila mimi nilichokulipa ni migogoro na ugomvi usiokwisha. Sikutambua umuhimu wako! Nimeuona sasa hivi ulivyoondoka na kuniachia watoto!
Sasa nimekua mimi ndio wa kuwatafutia chakula watoto, kuwalipia ada, mavazi na kila kitu! Sio siri ulikuwa wa muhimu sana
Nakumbuka siku ile nilivyotupa jalalani ile kilo ya nyama, lakini sasa sijui hata kilo moja ya nyama naipata wapi.
Wema hufa mapema! Najuta mume wangu, mume ambae kila nilipokuudhi hukuonesha kukasirika bali ulitabasamu. Najua unanisikiliza nakuomba sana unisamehe. Wote tumekumbuka uwepo wako. Mwanao Diana kila siku anauliza utarudi lini?
Hautatutoka akilin mwetu mpaka pale tutakapoungana na wewe huko uliko. Mwenyezi Mungu akulaze mahala pema peponi.
MUHIMU:
*Siku zote kubali kile ulichopewa bila kujalisha ni kidogo ama kikubwa.
*Mapenzi sio ni nini tulicho nacho, au ni utajiri gani tulionao ila mapenz ni ku share kile kidogo tulicho nacho
*Ushawahi kuchukua muda wako na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kile alichokubariki nacho? Kama hujawahi kufanya hivyo ni bora ufanye sasa!
Shukuru Mungu kwa alichokupa, kitunze kidumu. usije ukajikuta ukipoteza almasi wakati upo busy ukikusanya mawe.