07-21-2021, 08:41 PM
Makosa Yaliyozoeleka katika Kiswahili Sanifu
Sehemu ya Kumi na Mbili
Je, ni MAONYESHO au MAONESHO?
1.0 Usuli na tatizo
Maneno hayo tajwa, MAONESHO na MAONYESHO yamekuwa yakitumiwa katika muktadha mmoja. Mathalani, ni kawaida kuona gazeti A limeandika habari yake hivi "Maonyesho ya Sabasaba Yameanza"; huku gazeti B limeandika hivi "Maonesho ya Sabasaba Yameanza". Je, gazeti lipi liko sahihi?
2.0 Uchambuzi/Uchanganuzi
2.1 Mikabala ya Uchanganuzi/Uchambuzi wa Tatizo
Zipo shule mbili za mawazo juu ya kufikia muafaka wa matumizi ya neno fulani. Mkabala (shule ya mawazo) wa kwanza ni mkabala wa Kiufafanuzi wa Uchambuzi wa Lugha, kwa Kiingereza DESCRIPTIVE ANALYSIS OF LANGUAGE na wa pili ni mkabala wa Kielekezi wa Uchambuzi wa Lugha, kwa Kiingereza PRESCRIPTIVE ANALYSIS OF LANGUAGE. Mkabala wa kwanza unalenga kueleza na kufafanua jinsi watu wanavyoitumia lugha fulani kisha kutengeneza kanuni zinazoongoza lugha hiyo pamoja na kufanya maamuzi ya kurasimisha maneno ambayo yameshika kasi kimatumizi katika jamii. Kwa ufupi, huu ni uchambuzi na uchanganuzi wa lugha kadiri inavyotumiwa na watu.
Mkabala wa pili ni uwekaji wa kanuni za kiisimu katika lugha ili zifuatwe na watumiaji wa lugha husika. Hapa wataalamu wanazingatia misingi ya kiisimu ( ambayo ni ya kisayansi) kuweka utaratibu unaotakiwa ufuatwe katika matumizi ya lugha.
2.2 Uhusiano wa MAONYESHO na MAONESHO na Mikabala Iliyoelezwa
Kiufundi/kiisimu/kisayansi: neno ONESHO linatokana na kuona, tunapata pia maonesho; watu wanaoneshwa vitu mbalimbali.
Neno ONYESHA linatokana na ONYA. Mfano: Baba anampa onyo kali mtoto wake.
Huu ndio ufafanunuzi kwa misingi ya mkabala wa pili. Kwa hivyo, tukiamua kutumia mkabala huu kutoa hitimisho, tutasema kwamba neno sahihi ni MAONESHO na sio MAONYESHO.
Tukijikita katika mkabala wa kwanza, kimatumizi ya kawaida (na matumizi hayo yamelazimika kuingizwa katika kamusi baada ya kuona yametamalaki), neno MAONYESHO linachukuliwa sawa na MAONESHO.
Hii ni kutokana na neno hilo kutumiwa sana na watu katikati miktadha rasmi na isiyo rasmi. Wataalamu walilazimika kuliingiza neno hilo katika kamusi baada ya kuona matumizi yake yameshika kasi. Na hapo ndipo mkabala wa kwanza unapofanya kazi.
Tutazame sehemu hii kutoka Kamusi ya Kiswahili- Kiingereza ya TUKI yenye maana za maneno hayo:
"#on.a# kt [ele] 1 see: Kusikia si ku~ hearing is not the same as seeing. 2 feel: Na~ njaa I am feeling hungry. (tde) onea; (tdk) oneka; (tdn) onana; (tds) onesha; (tdw) onwa.
#ony.a# kt [ele] 1 warn, admonish. 2 forbid, prevent. (tde) onyea; (tdk) onyeka; (tdn) onyana; (tds) onyesha; (tdw) onywa.
#onyesh.a# kt [ele] show, exhibit.
#onyesho# nm ma- [li-/ya-] 1 scene (in a play).2 exhibition, show: Ma~ ya vitabu book exhibition/fair"
Kamusi hiyo inatambua kuwapo kwa maneno yote mawili (MAONYESHO na MAONESHO) katika muktadha mmoja.
3.0 Hitimisho
Licha ya utetezi wa matumizi ya maneno hayo yote mawili, hatutegemei mtaalamu wa lugha pamoja na mtu yeyote mwenye uweledi na matumizi ya lugha adhimu ya Kiswahili aseme MAONYESHO bali tunategemea aseme MAONESHO. Hata hivyo, hatutamshutumu wala kumlaumu yoyote atakayetumia neno MAONYESHO bali tutamtofautisha tu kiuweledi katika matumizi ya lugha ya Kiswahili.
Itaendelea....
Mwl. Issaya S Lupogo
0712-143909
lupogoissaya1@gmail.com
N.b
Issaya pia ni sehemu ya Lupogo Intellectual MCs

Mwl Maeda