11-27-2021, 06:56 PM
TANGULIZI.
Maana ya unyambulishaji
Massamba (2009:105), unyambulishaji ni utaratibu wa kupachika viambishi kwenye mizizi ili kuunda maneno mapya.
Unyambulishaji ni mbinu ya uundaji wa maneno,hivi kwamba viambishi mbalimbali huambikwa kwenye mzizi husika na kuunda neno jipya.(Matinde,2012:119).
Unyambulishaji ni utaratibu katika lugha wa kupachika au kuongeza viambishi kwenye mzizi wa neno ili kuunda maneno mapya. Kwa mfano, kuunda nomino kutokana na vitenzi kwa kutumia viambishi. Maneno mapya yanayoundwa hapa huwa ya kategoria nyingine (Masebo,2012:127).
Hivyo basi tunaweza kusema kwamba unyambulishaji ni aina ya uambishaji unaosababisha neno kutoka katika kategoria moja hadi nyingine.
Unyambulishaji wa nomino
Habwe na Kalanje (2004),wanadai kuwa unyambulishaji wa nomino ni hali ya kuunda nomino kutoka kuwa kategoria nyingine za maneno huitwa unominishaji. Nomino za Kiswahili zinaweza kuundwa kutokana na vitenzi, vivumishi na hata kutokana na nomino moja hadi nyingine.
Hivyo basi, unyambulishaji wa nomino ni hali ya kuweka viambishi vinyambulishi kwenye mzizi wa neno ambao hupelekea neno hilo kuhama kutoka kategoria moja kwenda kategoria nyingine ambayo ni nomino.
Nomino.
Ni neno linalotaja kitu, kiumbe, hali, dhana au tendo kama kiti,ndege na furaha. (Massamba, 2009:68).
Unyambulishaji wa nomino hufanyika kama ifuatavyo;
Kinominishi {o} kinaweza kunominisha vitenzi vya Kiswahili katika mazingira yafuatayo;
Kwa mfano vitenzi vya kibantu vinavyoishia na kiambishi tamati {-a}
{Mzizi} + {-o}
Mfano,
Kitenzi mzizi nomino
Tenda tend +o tendo
Andika andik + o andiko
Jenga jeng + o jengo
Pamba pamb + o pambo
Hata hivyo, kuna baadhi ya vitenzi vya kibantu ambavyo huishia na kiambishi tamati {-a} ambavyo vikiambikwa viambishi tamati {-o} haviwezi kubadilika na kuwa nomino. Kwa mfano kitenzi ;Lowa,tembea.
Pia kiambishi cha unyambulishi {-o} huweza kunyambulisha nomino kwa kuambatana na kinyambulishi {-i} au {-li}.
kwa mfano; {mzizi} + {-i/-li-} + {-o}
Kitenzi mzizi nomino
Kaanga kaang + i + o kaangio
Chuja chuj + i + o chujio
Kaa ka + li + o kalio
Mazingira mengine kiambishi kinyambulishi {o} huweza kunominisha kitenzi pale ambapo huambatana na mofimu {e}.
{mzizi} + {-e-} + {-o}
Kwa mfano;
Kitenzi mzizi nomino
Fyeka fyek + e + o fyekeo
Chekecha chekech + e + o chekecheo
Pia unyambulishaji wa nomino huweza kutokea kwa kuambika kiambishi {M-/Mw-} mwanzoni kabla ya shina la kitenzi na kiambishi cha unyambulishi {-ji} baada ya mzizi wa neno. Kiambishi tamati {-ji} cha unominishaji ambacho huonesha mtu anayetenda kitendo kama kazi yake ya kila siku.
{M/Mw-}+{shina-T}+{-ji}
Mfano
kitenzishinanomino
Baka m + baka + ji mbakaji
Chezam + cheza + ji mchezaji
Imba mw+imba+ji mwimbaji
Omba mw +omba + jimwombaji
Nomino zenye mofolojia yenye kiambishi awali {ku}, ambacho hutumiwa kuunda nomino. Kiambishi hiki {ku} huwekwa mbele ya shina la kitenzi na hubadili kitenzi kuwa nomino.
{Ku-} + {shina-T}
Mfano,
Kitenzi shina nomino
imba ku + imba kuimba
Cheza ku + cheza kucheza
Lia ku + lia kulia
Piga ku + piga kupiga
Nomino zenye mofolojia yenye kiambishi awali {u} cha unominishaji , mzizi wa kitenzi na kiambishi tamati {vu/fu} cha unominishaji. Huonyesha mtu au watu walio katika hali fulani.
{u} + {MZIZI} + {vu/fu}
Mfano:-
Kitenzi Mzizi Nomino
Tulia u + tuli + vu Utulivu
Vumilia u + vumili + vu Uvumilivu
legea u + lege + vu Ulegevu
Nomino zenye mofolojia yenye kiambishi awali {ki} cha unominishaji katika umoja au {vi} katika umoja , mzizi wa kitenzi na kiambishi tamati {o} kiambishi hiki huweza kuleta dhana ya kitu/ kifaa kinachotumika kutenda kitendo.
{Ki/ Vi} + {MZIZI} + {o}
Mfano:-
Kitenzi Mzizi Nomino
Funika ki + funik + o kifuniko/vifuniko
Pima ki + pim + o kipimo/vipimo
Tua ki + tu + o kituo/vipimo
Kiambishi kinyambulishi {-a}
Ikiwa kitenzi huishia kwa irabu i au u irabu hizo hubadilika na mahali pake huchukuliwa na kiambishi tamati {a} hivyo husababisha kitenzi kubadili kategoria yake na kuwa nomino.
Yaani, {mzizi} + {a}
Mfano,
Kitenzi mzizi nomino
Hoji hoj + a hoja
Faidi faid + a faida
Heshimu heshim + a heshima
Unyambulishaji katika vitenzi
Rubanza Y.I (1996), unyambulishaji wa vitenzi ni upachikaji wa mofimu fuatishi katika vitenzi.
Kitenzi ni neno ambalo huarifu tendo linalofanyika. TUKI (2012).
Mgullu (2012),anadai kuwa katika lugha ya Kiswahili vitenzi vinaweza kuundwa kutokana na vivumishi.
Kwa mfano;
Refu refusha
Fupi fupisha
Bora boresha
Safi safisha
Pia mara chache sana nomino zikinyambuliwa huunda vitenzi, Masebo (2012:134).
Kwa mfano;
Nomino Kitenzi
Taifa taifisha
Sulubu sulubisha
Ratiba ratibu
Hata hivyo kuna idadi ndogo ya vielezi vikinyambuliwa vinaweza kutumikakatika kuunda vitenzi. Kwa mfano;
Kielezi Kitenzi
Haraka harakisha, harakishwa,
HITIMISHO.
Unyambulishaji wa maneno katika lugha ni muhimu sana katika ukuaji wa lugha kwani hupelekea kuongezeka kwa misamiati katika lugha.
MAREJELEO.
Habwe na Karanja, (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Foenix Publishers.
Massebo (2012). Nadharia ya Lugha Kiswahili 1,kidato cha 5&6.Dar Es salaam: Nyambari
Matinde, S. (2012), Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia, kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo
Mgullu, (2012), Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers. Nyangwine Publishers.
TUKI (2012). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar Es salaam: Oxford University Press.
Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers.

Mwl Maeda