12-12-2021, 10:51 AM
- Kuchambua na kuweka wazi funzo litolewalo na kazi ya fasihi.
- Kuchambua na kufafanua taswira (picha za kisanii) zilizotumika katika kazi ya mwandishi.
- Kumshauri na kumtia moyo mwandishi ili afanye kazi bora zaidi (hivyo mhakiki pia ni mwalimu wa mwandishi)
- Kumwelekeza na kumchochea msomaji kusoma na kupata faida zaidi ya ambayo angeipata pasipo dira ya mhakiki (mhakiki ni mwalimu na daraja kati ya mwandishi na jamii)
- Kuhimiza na kushirikisha fikra za kihakiki katika kazi za fasihi.
- Kukuza kiwango cha utunzi na usomaji wa kazi za fasihi.
- Kutafuta na kuweka sawa nadharia za fasihi teule.
- Kuthamini na kuheshimu kazi za waandishi kwa kuzitendea haki
Mwl Maeda