11-17-2021, 08:19 PM
Kwa taarifa zaidi ni kwamba leo, pendekezo na azimio lililowasilishwa na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya kuwa na Siku ya Kiswahili Duniani itakayosherehekewa kila tarehe 7 Julai ya kila mwaka, imepitiswa na Kamisheni ya Masuala ya Utawala, Fedha na Mahusiano ya Kimataifa (The APX Commission). Hivyo, tunasubiri ipitishwe katika Plenary ya Mkutano Mkuu mwezi huu mwishoni ambayo itatoa Azimio.
Habari za kutia moyo. Leo UNESCO imepitisha tarehe 7 Julai kuwa ni siku ya Kiswahili Duniani.
Ni mwanzo mzuri kwa Kiswahili Kimataifa. Baadaye tunaweza kupata wakalimani kwenye vikao vya kimataifa nasi kuwasilisha masuala Kwa Kiswahili!!!

Mwl Maeda