08-31-2021, 07:16 AM
MASWALI NA MAJIBU-7: DARASA LA 3 & 4
SEHEMU A: Chagua jibu sahihi
SEHEMU B: Chagua muundo sahihi kukamilisha sentensi.
ORODHA A ORODHA B
Sijali hakuwa mwangalifu wa maisha yake, siku moja alichomwa na mwiba mguuni. Majirani zake walimwambia aende hospitalini lakini hakujali. Mwishowe mguu ulivimba na kidonda chake kuoza na kutoa harufu. Hali ilipokuwa mbaya alitafuta msaada na kwenda hospitali. Maskini Sijali mguu wake ulikuwa umeoza na dawa pekee ilikuwa ni kuukata. Ama kweli mdharau mwiba mguu huota tende.
Jaza nafasi zilizoachwa wazi.
SEHEMU A: Chagua jibu sahihi
- Haraka haraka haina……………………
- Fikiri kabla ya ………………..
- Mbwa ni …………..wa nyumba yetu
- Juma alimuua mbwa wake kwa………………
- Wezi walishindwa kuiba nyumbani kwa Juma kwa sababu ya………..wa fensi yake.
- Mtu anaposema vijana wale ni chanda na pete maana yake ni………………
- Kinyume cha nahau vunjika moyo ni………………………….
SEHEMU B: Chagua muundo sahihi kukamilisha sentensi.
Quote:kabla ya, baada ya, kwa ajili ya, bila shaka, huna budi, mara kwa mara
- Wingu jeusi limetanda angani kote…………….mvua itanyesha sasa hivi.
- Ukitaka kufaulu ……………kusoma kwa bidii.
- ………………kumsubiri muda mrefu, hatimaye mgeni aliwasili.
- ………………kuanza kujibu swali lolote lile ni vizuri kulisoma tena na tena.
- Anafaulu kwa sababu hupitia masomo yake…………..
- Wageni wote tayari wameshawasili……….mkutano.
ORODHA A ORODHA B
- Kushirikiana ( ) Kuweka vitu tayari
- Ndugu ( ) Watu waliozaliwa pamoja
- Shabaha ( ) kufanya pamoja
- Kuandaa ( ) kusudi, lengo
- Kuogopa ( ) kukamata kitu
- Kutundika mtini ( ) kuwa na hofu
- Shika ( ) kuning’iniza juu ya mti
Sijali hakuwa mwangalifu wa maisha yake, siku moja alichomwa na mwiba mguuni. Majirani zake walimwambia aende hospitalini lakini hakujali. Mwishowe mguu ulivimba na kidonda chake kuoza na kutoa harufu. Hali ilipokuwa mbaya alitafuta msaada na kwenda hospitali. Maskini Sijali mguu wake ulikuwa umeoza na dawa pekee ilikuwa ni kuukata. Ama kweli mdharau mwiba mguu huota tende.
Jaza nafasi zilizoachwa wazi.
- Sijali hakuwa………………….wa maisha yake.
- Kina nani walimwambia Sijali aende hospitali?…………….
- Kutokana na kisa cha Sijali andika maana ya methali mdharau mwiba mguu huota tende………………..
- Mguu wa Sijali ulikuwa umekwisha……………na ukatakiwa……………
- Umejifunza nini kutokana na habari hii uliyosoma?………………
- B
- A
- C
- C
- B
- B
- C
- Bilashaka
- Huna budi
- Baada ya
- Kabla ya
- Mara kwa mara
- Kwa ajili ya
- C
- B
- D
- A
- F
- G
- E
- Mwangalifu
- Majirani
- Anayedharau tatizo mwishowe hujuta
- Oza na kukatwa
- Mdharau mwiba mguu huota tende
Mwl Maeda