08-19-2021, 04:11 PM
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU
SEHEMU YA 26
mimi siyo mtumwa kwa hapa Bali nilikuwa kama mchumba wa Tito.
Ila Sasa ndiyo nakwambia kwamba Yaani hapo Ndiyo umejipaka uji wa moto usoni kabisaaaaaaa.
Ili nini Sasa?.
Utaelewa tu.
Sasa nitaelewa nini?.
Sijui.ila utaelewa tu.
Haya Bana. Glady muage bibi yako mwambie sisi ndiyo tunaenda Hivyo japokuwa hataki.
Mda wote huo wa majibishano Kati ya Mama Tito na Zamda Kwakweli Jeni alikuwa akimsikiliza tu mama Tito mama Yake. Lakini Jeni hakuongea hata Kidogo kutokana na kurushiana kule maneno.
Kwahiyo basi Baada ya mda kidogo Jeni alimsaidia Zamda Mizigo yake ambayo alikuwa nayo pale ili waweze kuelekea stendi.
Basi siku nazo zilichachama kweli kweli. Siku hiyo Ndiyo ilikuwa Siku maalumu ya kuweza kutangazwa kwa mshindi wa mashindano yale ya uandishi wa hadithi za kufikirika na zisizo za kufikirika. Ambapo mchujo huo ulikiwa ni mchujo wa Mara ya pili.Ambapo katika mchujo huo Ndipo patapatikana mshindi wa kwanza hadi wa tatu.
Basi ikiwa ni mishale ya saa mbili za Usiku watu wakiwa kwenye Runinga wakiwa wanasubiria taarifa ya habari.Hapo nyumbani kwa mama Tito Walikuwa wanaangalia taarifa ya habari kupitia Runinga ya Taifa iliyokuwa ikiitwa R.K.Hapo sebuleni wako Mama Tito, Jeni na wa Watoto wake kasoro Bite tu .Ulisomwa mhutasari wa habar kwanza. Mhutasari huo wa habari Ulikuwa ukisikika hivi.
Kijana Mwenye umri wa miaka ishirini na moja kutoka Kinani ashinda tunzo ya dunia ya uandishi wa hadithi za kufikirika na zisizo za kufikirika.
Kwakweli mhutasari ulivyosoma tayari Jeni alianza kufurahi kweli kweli akiwa anajua kabisa dhahiri dhahiri mshindi Huyo ni zaidu.
Basi baada ya mihutasari yote kusomwa na mwandishi wa habari yule tayari akaanza kusoma taarifa Sasa kwa ujumla. Ilikuwa hivi.
Wanaje hali ndugu mtazamaji na msikilizaji wa R.K.Ni Mimi mwandishi wako Siraji Hamadi Kutoka R.K.tupanze habari kama ifuatavyo.
Kijana Mwenye umri wa miaka ishirini na moja kutoka nchini Kinani aitwaye Zaidu Sudaysi Zaidu amepatiwa tunzo kwakushika nafasi ya kwanza kidunia katika mashindano ya uandishi wa hadithi za kufikirika na zisizo za kufikirika.Ambapo shindano hilo lilifanyika nchini Denmark na Marekani. Kwa taarifa zaidi tumsikilize ripota wetu kutoka R.K ambaye kwasasa yuko huko Marekani akitupatia taarifa kamili.
Mda huo kweli ripota huyo anaonekana Hapo akiwa yuko na Kijana Zaidu Sudaysi Zaidu.Mwandishi huyo alikuwa akisema Hivi.
Aaaaaa tukiwa hapa katika ukumbi ambao Ndiyo mashindano ya uandishi wa hadithi za kufikirika na zisizo za kufikirika, ambao ulifanyika kwa kuwashindanisha washindi Kumi kutoka katika awamu ya Kwanza ambaye ilifanyikia huko Denmark. Basi aliyechukua taji Hilo la dunia ni Kijana Kutoka nchini Kinani kati ya mataifa yote yaliyoshiriki katika mashindano haya.Basi huyu hapa ndiyo mshindi wa mashindano haya. Embu aongee kidogo kwa namna alivyoupokea Ushindi huu."Nakweli anaonekana Zaidu akiwa amevaa suti nyeusi. Alikuwa akisema Hivi ".
Aaaaa namshukru sana mungu kwakuweza kushinda katika mashindano ya uandishi wa hadithi za kufikirika na zisizo za kufikirika kati ya mataifa yote ambayo yameshiriki.Pia nawashukuruni sana wote ambao mlikuwa mkiniombea Popote mlipo Natumai dua zenu zimekubaliwa.Inshaallah.
" Baada ya kumaliza kuongea kisha mwandishi akawa amemuuliza swali mheshimiwa waziri wa habari michezo sanaa na utamaduni Ambaye kwa mda huo alikuwa pembeni na Zaidu. Mwandishi yule Alimuuliza hivi.".Mheshimiwa waziri Ushindi huu umeuchukuliaje?.
Aaaa Kwakweli Ushindi huu ni Ushindi ambao Yaani sijui nisemeje tu.Ila juzi juzi tu nilivyoenda Kinani niliwaambia kabisa Zaidu Sudaysi Zaidu lazima achukue tunzo hii. Kwakweli tunawashukuru sana kwa watu waliotuombea dua hadi tukaweza kufanikisha. Aaaaa tutapumzika kwa siku ya Kesho ili siku inayofuatia tutakuwa tunasafari ya kurudi huko Kinani. Kwahiyo wana Kinani wajiandae tu hapo Mapokezi uwanja wa ndege kuja kumpokea mshindi wetu. Shukrani sana.
Ikiwa ni siku nyingine Hivi. Siku hiyo ilikuwa ni Siku ya jumapili. Kwa siku hiyo Jeni hakwenda kutembea kama kawaida yake ya kwenda Au kutoka na mwanaume fulani.
Kwaujumla Jeni ni mwanamke ambaye kwakweli kati ya wanaume mia moja waliyowahi kumhonga Lakini anayesex naye yaani kujamiiana naye ni mmoja tu.Wote hao ni huwa anawachukulia tu Fedha zao yaani anawachuna tu.Jeni amejaaliwa kwelikweli mdomo wa kuongea kwa mwanaume hadi mwanaume huyo anashawishika na kujikuta huyo mwanaume anatoa Hela tu.
Basi kwa siku hiyo nyumbani hapo ambapo kipindi hicho hata Tito amesharudi kutoka kwenye ile Safari yake ya kikazi ambayo ilikuwa. Hapo nyumbani kwa Mda huo wako Jeni na Tito. Wengine Walikuwa wametoka kutokana na Kwamba Siku ya jumapili ni siku yao ya kwenda kutembea maeneo mbalimbali ya starehe.
Basi kumbe Tito naye alikuwa akimmezea mate Jeni siku nyingi tu ila ndiyo hivyo alikuwa anashindwa kwamba ataanzaje anzaje pale.Kwahiyo kwa siku hiyo kwa pale nyumbani wako wawili tu ila kila mtu alikuwa chumbani kwake. Basi Baada ya mda Tito akashindwa kuvumilia na kuamua kwenda kwa Jeni. Pale mlangoni kwa Jeni akawa anagonga akisema.
Hodiiiiiiii.
"Jeni akiwa kitandani alikuwa akiburudika zake na simu Alisema hivi".Karibu.
Basi nakweli Tito akawa amefungua mlango na kumkuta namna tu Jeni alivyolala na nguo aliyovaa Kwakweli hapo Ndiyo Kama alizidi kuchanganyikiwa na Jeni. Kwasababu naye Jeni si wa mchezo mchezo tu.Baada ya Jeni kuona kwamba ni Tito ndiyo kaingia akawa ameshajua kabisa malengo ya Tito kuingia ndani pale kwa mda ule ni nini.kisha Jeni akamuambia hivi.
Tito karibu kiti Hicho hapo.
Sawa.
Au Unataka uje ukae hapa kitandani?.
Ukiniruhusu sawa.
Basi sawa njoo ukae hapa.
Siyo tulale kabisaaa.
Ikiwezekana kabisa tunaweza hata Kulala.
" Nakweli Tito akawa ameenda kukaa kitandani pembeni kabisa alikokuwa amelala Jeni. Kisha akasema "Hivi Unajua Jeni Mimi sijawahi kabisaaa kuingia kwenye hiki chumba chako Tangu ujage Hapa.
Kwanini sas?.
Huwa naogopa tu.
Mbona leo umeingia.
Aaaaaaa....hata sielewi.
Huelewi kivipi Sasa.
Aaaaaa....leo hamna watu bana ndiyo maana nikasema embu nikamsalimie Jeni chumbani kwake.
Karibu Sana."Mda huo Jeni akawa anajifunua shuka alilokuwa amejifunika na kumumfanya Tito abaki kuangalia mapaja meupeee ya Jeni yalivyo.Yote Hiyo ni Kwasababu tu Jeni anajua kabisaaaaaaa kilichomleta Tito pale ndani ninini.Basi Mda huo akawa anasema Hivi".
Hivi Jeni Unajua sijawahi kabisaaaaaaa kumuona Shem kabisaaaaaaa hapa nyumbani.
Yuko mbona.
Ila sijawahi kumuona hapa.
Yuko mbali sana.
Duuuuuuuuuuuu mbali Sana.
Ndiyo.
Sasa unavumiliaje mda wotee huo.
Mbona kawaida tu.ila siku si chache naondoka.
Aaaaaaa Jeni unaondoka kuelekea wapi.
Huko kwa jamaa yangu.
Kwanini Sasa.
Aaaaaa hapa kodi Yangu imebaki kama siku kadhaa tu hivi iishie. Alafu kwasasa sina Hela kabisaaaaaaa.
Aaaaaaaaaaaaaaa Jeni Yaani hicho ndicho kitu kinachokufanya wewe uhame hapa?.
Ndiyo maana yake.
Aaaaaaa baki tu hapa Bana.
Sasa nikibaki nani atanilipia kodi.Si bora niende zangu huko tu.
Aaaaaa tatizo hukusema.
Kwanani.
Kwani mimi sifai kukulipia kodi?.
Eeeeeeee naogopa weeeee.
Unaogopa nini Sasa.
Namuogopa Zamda.
Ana nini?.
Akijua.
Kwamba nakulipia kodi siyo?.
Ndiyo.
Hawezijua.Kwanza kwasasa siamesafiri Kwahiyo niko huru Kidogo.
Kwahiyo unaniambiaje.
Usihofu ntakulipia kodi.
Lakini Huwa nalipa kwa miezi sitasita.
Ahaaaaa haina shida. Kwani ni shilingi ngapi.
Huwa nampa mother laki moja na elfu themanini tasilimu kwa miezi sita hiyo.
Ahaaaaa Mbona simple tu hiyo.
Kwahiyo vipi Unataka kunilipia Nini?.
Usihofu ntakupatia Lakini mbili na nusu kwa ajili ya matumizi mengine pia.
Daaaaaaa Shukrani Sana."mda huo Tito akawa ameinuka na kukaa kitako karibu na Tito. Jeni akawa anasema Hivi "Daaaaa utakuwa umenisaidia sana.Sasa ntakurudishia lini?.
Wala usihofu, haina shida Jeni kuwa huru. Warembo kama nyiye kwanini Sasa muishi kwa mateso Bana.
Haya Bana.
Ila daaaa Jeni.
Nini.
Kwasasa kwangu usiku unakuwa mfupi kweli kweli.
Kwanini?.
Sina mtu wa pembeni alafu na hiki kipindi cha baridi Noma sana.
Unataka nije tulale.
Itakuwa vizuri pia.
Ayaaaa.
Nini Sasa.
Vipi kuhusiana na Zamda.
Wala usimuwazie yule Bana.
Kweli Tito.
Ndiyo maana yake.Hivi Unajua nilikuwa nikitamani hata Siku moja tu.
Kwahiyo utanipa lini hiyo hela?.
Ntakupatia nikitoka hapa.
Sawa.
Basi mda huo Tito akawa anataka aanze kumtomasa Jeni. Kweli Jeni akawa anakubali tu kutomaswa na Tito. Baada ya mda kidogo hivi Tito akawa anajua Jeni atampatia mautamu.Tito akasema Hivi.
Vipi Sasa.
Niko kwenye siku zangu Tito. Samahani.Labda siku nyingine.
Mwl Maeda