Nafasi ya Sanaa Katika Uchumi
Jani la kunywea maji
2. Kufinyanga Mitungi
Hashim A. Nakanoga
Sanaa na uchumi vimekuwa vikiishi pamoja toka karne nyingi ama tuseme toka binadamu alipoanza kuishi wakati ambao tunaamini sanaa nayo ilianza. Ilitangulia sanaa uchumi ukafuata, Uchumi hutua mahalipopotepenyethamani, nasanaa inathamani.
Sanaa ina matawi makubwa mawili, hisi na zana. Kwenye matawi haya mawili kuna mgawanyiko wa kazi nyingi kwa kila tawi mojawapo.
Mifano mizuri ya sanaa za hisi ni sanamu za kuchongwa, picha za kuchorwa. Sanaa hizi hutengenezwa kwa madhumuni ya kufichua, kudhihirisha na kutafsiri hali halisi ya uhai, ama kuchokozafikra.
Katika sanaa ya hisi kuna hisia na mawazo ya msanii. Msanii akiwa mwenye mpango mzuri na mtulivu ama mwenye fujo na vurugu huonekana katika kazi yake ya sanaa. Sanaa ya hisi humueleza mengi sana mtazamaji. Mwonaji anaweza kufahamu mazingira ya msanii yalivyo na kiasi cha maendeleo ambacho jamii ya msanii huyapendelea sana katika maisha yake na yale ambayo huyachu kia.
Zaidi ya hivyo, mwonaji anaweza kugundua fikra za msanij, maisha na matatizo yake. Sanaa ya hisi pia huweza kukumbusha jambo lililotokea muda mrefu uliopita ama kuelezea tukio muhimu linalotokea sehemu fulani na pia kutabiria jambo kubwa litakalotokea baadaye sana kitaifa au kiulimwengu. Vile vile sanaa huweza kuchochea hisia za waonaji katika ukiwa ama sherehe, mahaba ama chuki, furaha au huzuni, joto na baridi, mchangamko ama mzizimo.
Sanaa za zana ni vifaa vinavyotengenezwa kisanii vikiwa vimekamilika katika mikono ya msanii ama kiwandani. Kama vina usanii na vimetengenezwa kwa ajili ya matumizi tunaziita sanaa za zana. Kwa mfano, chanuo, viti, mikeka, kanga, viatu, marimba, migono, vinu, mitungi, nyumba, pete, heleni, vidani navingine vingi ambavyo hatutaweza kuviorodhesha katika sura hii. Sanaa za hisi na za zana zlna nafasi maalum katika uchumi. Nafasi hii itaonyeshwa katika sehemu tatu, yaani sanaa na uchumi, sanaa viwandahi na sanaa za msanii binafsi.
SANAA NA UCHUMI HAPO ZAMANI
Sanaa imedumu toka binadamu ameanza kuishi kwasababu msanii huzaliwa. Msanii huzaliwa nabaada ya hapo ndipo mazingira yake yanapoingia moja kwa moja katika kumlea na kumwongoza, kumtajirisha kifikra na inapowezekana kumwendeleza. Hivyo basi, tuelewe kwamba kila penyejamii ya watu panawasanii wa fani mbalimbali. Kuna waimbaji, watunzi wa hadithi, washairi, wacheza ngoma, wachongaji na wachoraji.
Mwanzo wa sanaa ni hisia za msanii. Kutokana na msukumo wa hisia, msanii huanza kuunda sanaa zake. Ndipo anapofahamika kwamba yeye ni msanii na hapo huanza hali ya kutegemewa katika kazi zinazohusiana na sanaa kama ile ambayo msanii amekwisha ionyesha. Bila shaka wengi wetu tunafahamu namna ambavyo wakale wetu wa mwanzo kabisa walivyoanza kuishi na jinsi hatua zao za maendeleo zilivyokuwa zikibadilika mpaka kufikia hali tuliyonayo hivi sasa. Kuna wakati ilibid, watumie mawe kama silaha ama vifaa vya kukatia Mawe haya waliyachonga wenyewe. Ingawa pengine kila mtu alishiriki katika uchongaji huo ilifika wakati, wenyewe kwa pamoja walijigundua kwamba mmoja kati yao aliweza kuchonga vizuri zaidi ya wengine. Huo ukawa mwanzo wa kumtegemea kwa utengenezaji wa vifaa hivyo.
Kumtegemea msanii kwa namna kama hii hakukuwa kumeishia hapo tu kwa sababu bingwa huyo alikuwa akichonga silaha zake pamoja na silaha za wengine. Hivyo basi muda mwingi aliutumia kwa kazi hiyo kiasi ambacho haikuwa rahisi kwake kufanya mambo mengine ambayo vile vile ni muhimu kwa maisha yake, kama vile kuwinda. Kutokana na hali hiyo wenzie walilazimika kumpa sehemu.ya mawindo yao kufidia muda ambao binawa huyo aliutumia kuwatengenezea vifaa walivyohitaji. Kubadiliishana kwa namna hii’kuliendelea kudumu sio katika silahaza mawe na mawindo tu, bali ulikuwa kufuatana na mahitaji yalivyoongezeka.
Hali iliendelea kuwa hivyo mwaka hata mwaka na mpaka kufikia wakati ambao wazazi wetu hao walianza kutumia vyungu kwa kupikia, kukalia vigoda na kuvaa nguoza magomeya miti.
Uchumi ulijihusisha na sanaa kwa sababu sanaa toka mwanzo na daima inatawala sehemu kubwa sana karibu asilimia tisini na tisa ya mahitaji ya binadamu. Kadri wazazi wetu walivyokuwa wakipiga hatua za maendeleo ndivyo mahitaji yalivyozidi kuongezeka. Mahitaji haya yalitofautiana katika sehemu tatu muhimu; nyenzo, bidhaa na hisia. Sehemu kubwa ya mahitaji na ambayo tunaamini ndiyo waliyoanza nayo mababu zetu wa awali ni nyenzo. Baadae walihitaji vyombo kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani. Ndipo yalipofuata mahitaji mengine yanayohusiana na hisia. Tutazame basi uhusiano ulivyokuwa kati ya uchumi na sanaakatikavipengele hivi vitatu vya nyenzo, bidhaa na hisia.
Tunapotaja neno nyenzo kwa karne ya sasa ambayo imepiga hatua kubwa katika taaluma ya ufundi maana ya nyenzo inabaki palepale lakini inaeleweka kimapana zaidi. Hatahivyovitu vinavyohesabiwakatika fungu la nyenzo ni vingi mno na vinazidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda mbele. Nyakati hizo za mababu zetu sanaa za zana walizotengeneza ni zile zilizosaidia katika kuleta uchumi wa kumuwezesha kuishi. Nyenzo yakwanzakabisa iliyotumiwa ilikuwa ni mawe. Wakati mwinginewaliweza kuchukuaainafulani ya miti migumu na kuichonga mfano wa mikuki. Mawe na miti waliyochonga waliitumia kwa kuwindia na kukatia nyama ama kukatia baadhi ya matunda makubwa waliyofanikiwa kuyapata. Baadaye walilazimika kuacha nyenzo ya mawe kwa kuwindia na kukatia, wakavumbua nyenzo zilizo borazaidi kamavile visu, nyengo, mikuki na majembe. Hali hii ilifikiwa walipogurdua maisha ya kuishi pamoja. Walitumia majembej kwa kulimia na kujipatia mzazo zaidi. Mikuki ilitumiwa kwa kuwindia. Wakati mwingine kutokana na migongano baina ya vikundi au familia na familia, ama kushambuliwa na wanyama, walitumia mikuki hiyo kwa kujilinda.
Uvumbuzi wa nyenzo mbalimbali za uchumi uliendelea na zana nyingi tofauti zilitengenezwa kutokana na maendeleo yalivyohitaji. Ndivyo tulivyoanza kupata mashoka, mapanga, migono na bunduki aina ya gobole. Baadhi ya zana hizo zilitumiwa kwa kuwindia na nyingine kuzalishia mazao zaidi. Ili aliyekuwa na mazao aweze kupata mawindo na aliyekuwa na mawindo apate mazao va chakula, na kwa kuwa hakukuwa na mfumo wa fedha, ilibidi wateja haowabadilishanemali zao.
Walipoanza kutumia vyakula vya mashambani, waligundua kuwa walihitaji vifaa maalum kwa matayarisho mbalimbali ya mazao yao. Baadhi yavifaa hivyo ni pamoja na vyombo vya kusagia nafaka, vya kuwekea chakula wakati wa kula, kunywea maji, kukaliana mavazi.
Wakati wa kula waliweka vyakula vyao juu ya majani mapana ama majani ya migomba. Hata maji walikunywa kwa kutumia majani waliyoyakunja kiufundi sana kiasi cha kuweza kuhifadhi maji. Kidogo kidogo walianza kutumia nyungo ndogo (vitunga) kwa kuwekea vyakula na kunywea maji wakati wa kula. Siku zilivyoendelea waligundua kutengeneza sahani na mabakuli ya miti kwa ajili ya chakula na kata za miti amamatunda magumu kwa kunywea na kutekeamaji.
Jani la kunywea maji
Kimavazi, mababu zetu walianza kwa kujifunga majani kuhifadhi sehemu muhimu. Waliendeleakidogo kidogo wakafikia kutunga vijiti vingi walivyovivaa aidha kuzunguka kiuno kizima ama kuficha sehemu kidogo. Baadae kati yao wakatokea wasanii wa kutengeneza vazi la magamba ya miti Kutokana na kukaa pamoja, walifikiwa na hali ya kuzingatia usafi. Hivyo waliamua kukalia majani na mara nyingi kwa kuwa kiongozi wa familia au kikundi, nyakati za mahakama zao, mikutano ama ulaji walitaka aonekane tofauti walimtengenezea kigoda akalie. Siku zilivyoendelea, kigoda walikichukua kama kikalio cha kawaida kwa mtu yeyote kwa hiyo kiongozi wao walimtengenezea kigoda cha ainayapekee, tofauti kabisa na vigodavingine. Badala yakukalia majani walitengeneza majamvi na mikeka.
Vyakula walivyokula nyakati hizo walipoanza kutumia mazao ya mashambani ni vile vilivyohitajika kupikwa. Hivyo ilibidi watengeneze vyungu vya udongo kwa kupikia na walifinyanga mitungi kwa kuhifadhia maji. Baadae walitengeneza miundo tofauti ya vifaa hivyo vya udongo kwa matumizi ya aina mbalimbali katika mapishi, hifadhi ya maji ama hifadhi ya vyakula vyao.
Vifaa hivi, vinu, sahani, na mabakuli ya miti, kata, vazi la magamba ya miti, vigoda, mikeka, vyungu, na mitungi ya udongo tunavihesabu katika fungu la sanaa za zana kama bidhaa. Lugha ya biashara iliyokuwa ikisimama kati ya sanaa hizi za zana, mazao ya kilimo na mawindo ni kubadilishana. Ilibidi watu wawili waelewane na kukubaliana kwa thamani ya bidhaa walizotaka kubadilishana. Kama mkulima alitaka kupata kinu ilibidi aongee na mchongaji afahamu mchongaji huyo alitamani nini kati ya mpunga, mtama au mahindi. Pengine kama mchongaji alitamani mpunga walifikia uamuzi katika kukisia kwa kinu kimoja wangepimiana vitunga vitatu, vinne au hata sita, kufuatana na kinu kilivyothaminiwa na mpunga ulivyothaminiwakwa nyakati hizo.
2. Kufinyanga Mitungi
Tukiacha nyenzo na bidhaa kama vitu vya kuzalishia mali na vyombo vya matumizi ya nyumbani jamii yeyote ile huwa na nyakati za furaha na huzuni.
Nyakati za furaha hasa kama baada ya mavuno maadhimisho ya harusi ama ilipofikia kijana wa kike au wa kiume kutolewa kutoka katika jando na unyago, jamii iliyohusika ilifanya sherehe. Katika sherehe mambo mengi yalihitajika. Kwa mfano mavazi au mapambo maalum yaliyohusiana na tukio ama vifaa muhimu vilivyohitajika kuandamana na sherehe. Ilihitajika mitungi, mikeka, vyungu, vinu michi na nyungo kumsindikizia biharusi kwenye ndoa, au kumkabidhi kijana wa kiume mkuki, sime, kisu ama mshalena upindebaadayajando.
Sanaa hizi walizinunua au kuzipata kutoka kwa wasanii katika hali ileya kubadilishana. Mbali nasanaa hizi za zana kutumika katika sherehe, kuna sanaa maalum ambazo zilitengenezwa na kununuliwa kwa madhumuni ya kuhifadhiwa kutokana na uzuri wake.
Katika kuishi pamoja, jamii hizo za mababu zetu zilikua na kuendelea. Kukua huko kwa jamii kulisababisha utawala uingie. Mara nyingi mtawala alipenda kuwa na vitu vyenye thamani au vizuri zaidi ya vile walivyokuwa navyo watu aliowatawala. Watawala hao waliteua wasanii hodari ili wasanii hao wawaundie sanaazapekee.
Sanaa zilitumiwa hata katika ibada. Imani katika dini ilikuwapo tangu enzi ya mababu zetu, ili imani ile iwe na nguvu kwao ijenge sawa sawa ilibidi kiongozi wa kizazi hicho ashughulikie uumbaji wa sanamu ya mkale wao. Hata hivyo hawakusita kutaka ushauri wa msanii. Kwa njia hii wasanii waliheshimiwa kwa kazi zao nzuri na hivyo walitunukiwa zawadi katika kufikiriwa kwamba walikuwa na uwezo wa kuunda sanamu.
Sanaa Viwandani.
Kuna mabadiliko mengi yaliyotokea katika utengenezaji wa sanaa. Baadhi ya sanaa za zana zinaendelea kutengenezwa na kumalizika mikononi mwa msanii mwenyewe. Sehemu nyingine ya sanaa za zana huchukuliwa mawazo ya msanii yakiwa katika mchoro, ramani au pambo yakaendelezwa na kuzalisha sanaakatika mashine.
Pamoja na kuwa na hali ya namna hii sanaa sasa hufanywa hata viwandani. Kwa hiyo tunao uchumi unaoletwa na sanaa kutoka viwandani, uchumi unaoletwa na sanaa kutoka kwa vikundi vidogo vidogo vilivyojiunga na uchumi unaoletwa na sanaa kutoka kwawasanii binafsi.
Kwa muda mrefu tulikuwa tukinunua kutoka Ulaya sanaazazanazinazozalishwaviwandani. Lichayakuwa utengenezaji wake ulitegemea mali ghafi kutoka huku kwetu, kama vile pamba na ngozi. Sanaa hizi zilitugharimu pesa nyingi sana za kigeni. Hivyo ununuaji wake ulidhoofisha uchumi wetu.
Ndipo nchi yetu ilipochukua hatua ya kujenga viwanda vya kutengeneza sanaa za zana zilizo muhimu kwa uchumi wa taifa na kwa mahitaji ya wananchi. Vilijengwa kwanza viwanda vinavyotumia mali ghafi inayopatikana humu humu nchini. Kati ya viwanda hivi nivilevinavyotengenezanguo, viatu navitabu.
Tunavyo pia viwanda vingine kama Kibo kiwanda cha kutengeneza karatasi, kitichopo Chang’ombe, Dar es Salaam, ambacho mbali na utengenezaji wa karatasi, uchumi wake mkubwa unapatikana katika uchapaji wa picha za vielelezo zinazowekwa kwenye makopo kama yale ya kahawa na makasha ya madawa ya aina mbalimbali ama sabuni. Kiwanda kingine ni kiwanda cha Kauri kilichoko Chang’ombe Dar es Salaamchakutengenezavikombe, sahani nabakuli.
Uchumi unaoletwa na utengenezaji wa nguo hlvi sasa ni mzuri sana. Tuna viwanda vya nguo kwa mfano Urafiki, Mwatex, Kiltex, Sunguratex, Mablanketi na vingine vinavyojengwa Mbeya, Morogoro, Musoma na Ubungo. Viwanda hivi vinazalisha nguo za kutosheleza mahitaji ya wananchi na kiasi kuuza nchi za nje. Sehemu ya nguo zetu zinauzwa huko Ulaya na soko lingine kubwa zaidi ni majirani zetu katika ukandawa Afrikaya Mashariki.
Pamba ambayo tulikuwa tukilima na kuuza nje kwa bei hafifu, baadaye kununua kwa bei ghali nguo zilizotengenezwa kutokana na pamba yetu sasa, tunahakjkisha tunaishughulikia wenyewe mpaka kuuza nguo kamili. Nguo zinazozalishwa katikaviwandayyetu ni haki, jinja, bafta, shuka na mablanketi. Uchumi mkubwa unaletwa na uzalishaji wa kanga, vitenge, vitambaa vya magauni na mapazia. Mara nyingi zao lolote linalohusisha mkono wa msanii thamani yake huongezeka.
Kwenye viwanda hivi kuna wasanii wanaobuni mapambo ya nguo. Michoro yao inatumika katika kuchapa kanga, vitenge, vitambaa vya magauni, mapazia nasehemu nyingine hutumika kuchapashuka. Ndipo bidhaa hizi zikazidi thamani.
Kazi ya msanii katika sehemu hii ya uchumi wa viwandani ni nzuri sana. Mfano wa hali halisi ilivyo tunaweza kuuona katika takwimu ya mazao ya viwanda vyote vya nguo vilivyo chini ya Texco kwa mwaka 1977 namwaka 1978.
MAZAO YA NGUO KATIKA METARI
MWAKA 1977 1978
AINAYAMAZAO
METARI METARI
Khanga 12,251,000 10,609,000
Kitenge 13,808,000 14,119,000
Gauni 3,605,000 3,241,000
Pazia 58,000 36,000
29,722,000 28,005,00
Marekani 4,699,000 4,094,000
Lineni 9,328,000 15,344,000
Palini 788,000 725,000
Kaki 3,675,000 9,648,000
Sufi 1,793,000 2,710,000
Twili 2,980,000 1,480,000
Kitambaa
chashati 1,698,000 1,811,000
Shuka 4,762,000 3,567,000
Jinja 568,000 656,000
Bed Sheeting 2,289,000 1,513,000
Mulmul 1,888,000 1,559,000
Polyster 1,413,000 –
Mengineyo 429,000 439,00066,
131,000
71,652,000
Takwimu zinatuonyesha kuwa katika miaka miwili hii, aina ya bidhaa zilizozalishwa kwenye viwanda vya nguo vya Taifa ni kumi na nane. Katika aina hizi zote, bidhaa nne, Khanga, Kitenge, Vitambaa vya gauni na mapazia ambazo ukilinganisha zinachukua nafasi ya asilimia 22 tu.ya aina zote, zimeweza kuzalishwa kwa wingi mno kufikia asilimia 41.8 va wingi wa mazao yote. Hii inadhihirisha kwamba bidhaa hizi, khanga, na kitenge zinapendwa sana na hivyo hutolewa zaidi. Kupendwa huku kunatokana na kazi za usanii ambazo zimehusishwa katikakuzalisha bidhaa hizi nakuzipatia umaarufu. Pengine msomaji atashangaa kuona kuwa kuna bldhaa mbili nyingine za lineni na kazi zimechukua nafasi nzuri vile vile. Hii ni kwa sababu ya umuhimu wa vazi la kaki kwa kazi na lineni kwa hali ya hewa hapa nchini. Wakati huo huo viwanda vya nguo vimeipatia nchi fedha za kigeni kiasi cha shilingi 15,000,000 kwa kipindi cha miaka miwili 1977 na 1978. Katika mauzo hayo ya nchi za nje kiasi kikubwa kilitokana na Khangana Vitenge.
Tuchukue mfano mwingine wa kiwanda cha viatu cha Bora kilichoko Barabara ya Pugu, Dar es Salaam. Kwa muda mrefu bidhaa hii ilikuwa ikiagizwa kutoka nje nakuigharimu nchi yetu kiasi kikubwachafedhaza kigeni. Hali hii iliongeza tatizo la kudhoofisha nchi kiuchumi. Hivi sasa viatu vinatengenezwa katika kiwanda cha hapa hapa nchini na tunao wasanii katika kiwanda hiki cha viatu ambao kazi yao ni kubuni mapambo mbalimbali yanayotumiwa katika kutengenezea viatu vya miundo tofauti, kama vile wachoraji wa mapambo ya khanga wanavyobuni michoro itumikayo katika nguo.
Sanaa na Msanii Binafsi
Hapa itatubidi kwanza tuangalie kuna wasanii wa aina ngapi. Kiitikadi wasanii wote ni sawa. Msanii ni msanii awe wa fani yoyote ile lakini ni msanii. Tofauti yao kubwa iko katika lugha na ala wanazotumia wanapotaka kuutengeneza usanii wao.
Wasanii wana fani nyingi za sanaa kama kuchonga, kuchora, kufinyanga, kusuka na nyingine nyingi zote zikitafsiri sanaa za hisi au sanaa za zana. Kilamsanii hutengenezasanaa ambayo imemchepukia zaidi. Mwingine hutokea kuchepukiwa na fani nyingi, mwingine akawa katika fani moja tu. Itakuwa vizuri tukiwaweka kila mmoja na fani yake ili tuwe na picha iliyokamili.
Kwa mfano, mchongaji, hutumia mpingo ama pembe za ndovu kama nyenzo. Vifaa kama tezo, patasi, tupa na msasa ni zana. Msanii huyu ili afanikiwe na kazi yake inambidi awe na mtaji wa kutosha kununulia pembeza ndovu au mpingo. Labda tofauti iliyopo ni bei kati ya mpingo na pembe. Kwa hiyo ikiwa mchongaji huyo anataka kujiimarisha na kazi yake na awe na mtaji, itambidi aanze kwa kuchonga sanamu ndogo ndogo, mpaka atakapokuwa na mtaji wa kutosha kununua miti mikubwa au pembe.
Kutokana na hali hii, mchongaji, anapotaka kuipangia bei sanamu aliyoichonga, huangalia gharama aliyotumia kununulia nyenzo, kazi aliyoifanya, muda alioutumia kuifanya kazi hiyo, zana alizotumia na muundo aliodhamiria kuuchonga ikiwa amefikia hatua aliyoikusudia.
Soko kubwa kwa wachongaji ni nchi za nje, watalii na wakati mwingine Shirika la Uuzaji wa Sanaa hununua sanamu hizo na kuzisafirisha nje ama kuuza katika maduka yake yaliyomo humu humu nchini. Ili mchoraji afanye kazi yake, huhitaji kitambaa cha marekani, turubai ama bodi gumu kama uwanja wa kuzungumzia, rangi, mafuta ya kulainishia rangi, mafutaya kuoshea rangi nabrashi kamazana. Rangi za mafuta si rahisi kupata hapa nchini. Mradi rangi hizo zimeadimika basi inakuwa ghali mara dufu. Hivyo mchoraji akizipata anahakikisha atakapoitumia siyo penyemazungumzo madogo madogo.
Msanii huyu inambidi awe na uwezo wa kuzipata hizo rangi kwanza pamoja na kuwa na mtaji. Wengi wao wanaweza kuwa na mtaji wakashindwa kuzipata hizo rangi. Uchoraji uko wa namna nyingi. Uko uchoraji wa kutumia rangi za maji, penseli tupu, wino na mkaa kwenyekaratasi.
Hapa inategemea mchoraji alichagua kutumia zana ipi na uwanja upi wa kuundia sanaa yake. Gharama ya vifaa vya kazi, usanii wake, muda alioutumla katika usanii, dhana na hadhi ya msanii, ndio msingi wa bei ya sanaa. Wakati mwingine msanii anaweza kuajiriwa achore picha kubwa ya ukutani, hivyo bei itategemea msingi huo.
Masoko ya picha hizi za kuchora hutegemea mchoraji na vifaa alivyotumia katika kuchora. Mara nyingi picha zilizochorwa kwa rangi za mafuta ndizo zenye bei kubwa, lakini hata hivyo thamani ya picha inategemea msingi huo huo.
Msanii wa kufinyanga huhitaji shaba, chuma cha kumimina au saruji na mchanga, chokaa, udongo wa tope na maji kama nyenzo. Kazi hii huwa nzitb kutegemea na sanaa inayotakiwa kutengenezwa. Kutokana na gharamaya nyenzo, mtaji ni kitu muhimu. Kazi kama hii ikifanywa kwa maagizo maalum ni rahisi kupata nyenzo kutoka kwa mwajiri.
Msanii mwingine ni wa sanaa za kusuka. Huyu husuka vikapu, mikeka, nyungo, migono na majamvi. Kwa msukaji inategemea anataka kusuka kitu gani. Kama ni kikapu na majamvi, atahitaji milala kama nyenzo. Ikiwa anataka kusuka migono au nyungo atahitaji mianzi.
Chanzo >>>>>>>>
Mwl Maeda