SIMULIZI: JENEZA LA AJABU **SEHEMU YA 01* - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI: JENEZA LA AJABU **SEHEMU YA 01* (/showthread.php?tid=967) |
SIMULIZI: JENEZA LA AJABU **SEHEMU YA 01* - MwlMaeda - 08-21-2021 SIMULIZI: JENEZA LA AJABU Mtunzi: HAKIKA JONATHAN
**SEHEMU YA 01*
Ikulu kwa mfalme ;
“Siwezi kufa
kirahisi namna hii, dunia tamu bwanaaa weeeh, mali zangu hizi nitamuachia nani?? “,yalikuwa ni maneno ya kejeli kutoka kwa mfalme wa nchi ya Mwamutapa, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mganga wake wa kienyeji kuwa kashindwa kumtibu maradhi yaliyokuwa yakimsumbua, hivyo asubili kufa tu. Hali iliyopelekea mganga yule kujuta kauli yake kwani, mfalme aliamuru auawe kwa kukatwa kichwa chake, na kisha kiwiliwili chake kitupwe ndani ya bwawa la mamba waliofugwa na mfalme kwa ajili ya kula watu waliomchukiza na kumpinga katika uongozi wake. “Yani mimi nife, siwezi kufa mimi, labda utangulie mpuuzi wewe “,mfalme Mutapa, alijitamba kwa mala nyingine tena, huku akishuhudia kichwa cha mganga wake kikitenganishwa na kiwiliwili,kutokana na kushindwa kumtibu mfalme na kumwambia asubili kifo tu, jambo ambalo mfalme alilichukulia kama katukanwa na kudharauliwa. Mitaani katika nchi ya
Mwamutapa; Hali ngumu ya maisha inazikumba familia
nyingi katika ardhi ya Mwamutapa, huku lawama nyingi zikitupwa kwa mfalme, kwani wanaume wengi wenye nguvu na vichwa vya familia, walitumikishwa kwa nguvu katika mashamba ya mfalme na kisha kulipwa ujira mdogo,jambo ambalo lilimchukiza kila raia wa Mwamutapa. Kelele zao za mateso hasikusaidia chochote, kwani kila mtu aliyejifanya kupinga kunyanyaswa, alijikuta akiuawa kikatili, hali iliyowaogopesha wengine na kujikuta wakikubaliana na manyanyaso kutoka kwa mfalme, kwani waliogopa kifo. “Naamini ipo siku
yatakwisha, usilie mama yangu “,ilikua ni sauti kutoka kwa kijana mkakamavu Njoshi, akimunyamanzisha mama yake, baada ya kupokea taarifa za kifo cha mume wake kwani alishindwa kumtibu mfalme. “Mwanangu baba yako kaondoka, tumebaki wawili tu, nakuomba uachane na Grace, mfalme atakuua na wewe, tegemeo na faraja langu lililobakia “,mama Njoshi alizidi kulia kwa uchungu, huku akimusisitiza mwanae kuachana na Grace,msichana mrembo sana na mtoto pekee wa kike wa mfalme. Jambo ambalo kwake aliliona ni gumu sana na halitowezekana, kwani alimpenda sana Grace licha ya kupokea vitisho mala kadhaa kutoka kwa mfalme ili aachane na Grace. Na kila mala mfalme alipojaribu kumuua Njoshi alishindwa, kwani alifanikiwa kutegua mitego yote aliyotegewa ili aweze kufa, kwani alikua ni hodari sana na aliweza kulishinda jeshi la mfalme mala nyingi, moja ya sababu ambazo Grace zilimfanya ampende sana Njoshi, kwani alihitaji mwanaume atakaye muoa awe ni shujaa na si mwanaume suruali tu, asiyeweza kumlinda na hatari yoyote. “Usjali mama, mimi
nipo siku zote, nitakulinda, lakini naamini ipo siku Mwamutapa itakua huru, na mimi nitakuwa kiongozi wake “,kijana Njoshi aliongea kwa ujasiri na kujiamini kwani ziku zote alifanya mazoezi ya kila aina, ili tu siku moja afanye mapinduzi na kuokoa wananchi dhaifu kutoka kwenye utumwa na uongozi wa mabavu wa mfalme Mutapa, jambo ambalo mama yake aliliona kama ndoto ya mchana, ambayo Njoshi alikuwa akiota. “Mwanangu banaa
unanifurahisha, hebu toa upuuzi wako huko “,mama Njoshi aliongea huku akitabasamu kwa mbali kutokana na maneno aliyoambiwa na mwanae, na kumfanya asahau machungu ya kumpoteza mume, japokuwa alikuwa ameshazoea na kuona kama vifo ni jambo la kawaida katika familia yake, huku akikumbuka jinsi wanae watatu walivyopoteza maisha kutokana na njaa kali iliyotokea miaka kadhaa iliyopita, na kumuachia Njoshi pekee. “Nakuombea mwanangu, ndoto zako ziwe kweli “,mama alizungumza huku akimkumbatia mwanae, bila kutambua kuwa Njoshi alijawa na hasira, huzuni na machungu kwa kumpoteza baba yake na kuapa kulipiza kisasi, kwani hakutaka mama yake agundue huzuni hiyo na kuzidi kumpa machungu mama yake aliyempenda sana. Ikulu kwa Mfalme :
Mganga maarufu wa kienyeji aliyesifika
katika nchi ya Mwamuyeshi, nchi iliyopakana na Mwamutapa, na kuongozwa na mfalme Muyeshi ,anafika ikulu kumtibu mfalme maradhi yake, baada ya Muyeshi kupata taarifa za rafiki yake mpendwa kuugua kwa muda mrefu, hali iliyopelekea kumtafuta muganga katika ardhi yake ili amsaidie rafiki yake asiweze kupoteza maisha. “Karibu sana katika ardhi ya Mwamutapa,,, naamini rafiki yangu ndiyo kakutuma hapa “,mfalme Mutapa aliongea bila shida yoyote huku akitabasamu,huku akiwa amelala katika kitanda chake kwa takribani mwezi mmoja sasa bila kuamka kutoka kitandani, japo aliweza kuzungumza vizuri kama vile hakuwa mgonjwa. “Ndiye mimi mtukufu mfalme, mganga
kutoka katika ardhi ya rafiki yako Muyeshi, nimekuja kukusaidia “,mganga yule aliongea huku akijiamini, na kumfanya mfalme atabasamu kwani hakupenda kufa, na alitamani aishi milele jambo ambalo mganga yule alikua ameshalitambua. “Usjali mtukufu
“Sawa …sawa sa…wa ni…me…kusikiamfalme, mpaka sasa nimeshachelewa siwezi kukutibu, muda wowote kuanzia sasa utaweza kufa, lakini inatakiwa ukifa uzikwe ndani ya jeneza lililotengenezwa kutoka katika miti iliyo katikati ya msitu hatari wa Majini, msitu ambao uko katika ardhi yako ya Mwamutapa, ukizikwa ndani ya jeneza hilo, utaweza kufufuka baada ya wiki moja na kuishi milele “,mganga yule alizungumza maelezo marefu sana, huku jina la kijana Njoshi likijirudia rudia ndani ya kichwa cha mfalme, kwani ndiye kijana pekee aliyemuona anafaa kufanikisha swala hilo, na kutoka akiwa salama katika msitu hatari wa Majini, msitu ambao hakuna aliyewahi kuingia humo akitaka mali, watoto au ufalme kutoka kwa mizimu ya msitu huo na kutoka salama bila kupoteza maisha. “Na pia inatakiwa iwe siri, raia wako wasifahamu labda tu atakayekwenda huko msituni “,mganga alizidi kuzungumza huku mfalme mawazo yakiwa mbali sana, kwani mwanae Grace alishamuonya kuwa Njoshi siku akipata matatizo yaliyosababishwa na yeye, ataweza kujiua, jambo ambalo mfalme hakuwa tayali kumkosa mwanae wa kike pekee aliyenaye, kati ya watoto arobaini kutoka kwa wake watano alionao ,mtoto ambaye alizaliwa na mke wa tano baada ya wake zake wanne waliotangulia kushindwa kumzalia mtoto wa kike. “,mfalme alijibu bila kujitambua huku mawazo na maswali lukuki yakikisumbua kichwa chake . |