SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” *SEHEMU YA 06** - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” *SEHEMU YA 06** (/showthread.php?tid=957) |
SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” *SEHEMU YA 06** - MwlMaeda - 08-20-2021 SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU “ *SEHEMU YA 06**
Msitu wa majini;
Viumbe hatari wa msituni ghafla
wanasikia kishindo katika moja ya mitego waliyokuwa wametega, hali hii inawafanya wagundue kuwa tayali adui yao alikuwa ameshaingia msituni, kwani hawakuweza kumuona katika ramani zao, na hata walipotumia uwezo wao wa kijini, walishindwa kumuona adui yao, mala baada ya Njoshi kujifunga kiunoni kitambaa cheusi alichopewa na mama yake. “Jamani tayali adui alishaingia msituni, fanyeni kila njia mumkamate akiwa hai au amekufa “,jini mweupe, kiongozi wa askari wa msituni, alitoa amli ya kuanza kumtafuta adui, baada ya kufika katika eneo ambalo kishindo kikubwa kilisikika, na sehemu ambayo walitega mtego wao, na kukuta kamba ya mtego ikiwa inaning’inia baada ya kukatwa huku adui akiwa ameshatoweka. “Nazani mnaisikia
harufu ya binadamu, hayuko mbali, mtafuteni haraka sana ” ,jini mweupe alizidi kuongea na kuliamlisha jeshi lake la msituni, kumtafuta adui baada ya kuhisi harufu yake katika eneo lile la mtego, eneo ambalo lilizungukwa na vichaka pamoja na miti mirefu. ********
Baada ya Njoshi kuponea
chupuchupu kutoka katika mtego, haraka sana anaingia ndani ya kichaka chenye majani marefu, kwani alitambua kuwa majini wa msituni lazima wafike katika eneo lile muda sio mrefu baada ya kusikia kishindo kile kikubwa, hivyo asingeweza kukimbia na kufika umbali mrefu bila kukamatwa. Lakini ukistaajabu ya
Musa, utayaona ya firauni, Njoshi alishangaa sana baada ya kuliona kundi kubwa la majini, likifika eneo lile haraka sana huku akiwa hata hajajificha vizuri kwenye majani. Kwani viumbe wale walikuwa na uwezo wa kupotea na kufika eneo lolote walilolitaka wao, ndani ya sekunde tu, kwani hawakuwa binadamu bali majini, tena majini hatari wa msituni, msitu ambao ulikuwa maarufu katika nchi ya Mwamutapa, pamoja na ulimwengu mzima, kutokana na utajiri wake. “Mungu wangu,
mbona hawanioni “,Njoshi alistaajabu sana kwani kiongozi wa askari wale, jini mweupe alisimama karibu sana na kichaka kile, na ilikuwa imebakia kidogo amkanyage Njoshi kwani alikuwa hata hajajificha vizuri katika kichaka, eneo ambalo mtego ulikuwepo. Njoshi ujasiri ukiwa
umetoweka, alianza kutetemeka kwa woga kwani majini wale walitisha sana kwa kuwatazama, wengine walikuwa na mguu mmoja huku wakiwa na vichwa vingi sana, pamoja na mikono zaidi ya miwili. Njoshi akiwa anatetemeka aliamua kufumba kinywa chake asiweze kupiga kelele, kwani jini mweupe, aliyekuwa na kichwa cha nyoka aina ya koboko, huku akiwa na mwili mweupe tena wa binadamu, alitoa amli ya kumsaka Njoshi katika kichaka kile, kwani waliweza kuhisi harufu yake. “Asante mizimu ya
mababu, sionekani, leo nilikuwa nimekwisha “,Njoshi akiwa amejifumba mdomo wake kwa kutumia viganja vya mikono, aliishukuru mizimu, kwani majini waliokuwa wanatisha sana walipita karibu yake bila kumwona, jambo ambalo lilimshangaza sana kwani sehemu kubwa ya mwili wake ilikuwa wazi na hakufunikwa vizuri na majani, bila kutambua kuwa mkanda ule wa kitambaa cheusi aliouvaa kiunoni, ndiyo uliyosababisha majini wasiweze kumuona. “Msitu huu niliuskia
tu, leo nimejionea mwenyewe “,Njoshi aliongea moyoni huku akiwa anamshangaa askari mmoja wa msituni,mwili wake ukiwa umebakia mifupa tu,huku akiwa ameshika mshale, na kusonga mbele, lakini Njoshi alishindwa kutumia hata panga lake kuwaangamiza majini wale kwani hakutambua matumizi yake, huku yeye akiwa anashangaa muonekano wa majini wale na kuzidi kumuongezea woga. Mwamutapa
Asubuhi mida kama ya saa moja, kijana
Ngesha aliamka kutoka usingizini, na kunawa uso ili aelekee nyumbani kwa rafiki yake, ili asikute wameshaondoka kwenda shambani. “Mwanangu mbona
haraka sana asubuhi hii, unaenda wapi ” ,ilikuwa ni sauti ya mama yake Ngesha, mama ambaye alibaki mjane baada ya mume wake kuitwa na mfalme,na alipokwenda huko hakuweza kurudi.Kwani alipofika ikulu kwa mfalme,alikuta kundi kubwa la wanaume wakiwa huko wanasaga unga wa mahindi kwa kutwanga kwenye vinu,lakini baada ya kumaliza kazi hiyo na kudai malipo yao ,kundi lote lilitupwa kwenye bwawa la mamba bila huruma ,amli iliyotoka kwa mtoto mkubwa wa kiume wa mfalme. Lakini mama Ngesha kila
alipojaribu kuulizia kwa mfalme kuhusu mumewe ,hakuweza kupatiwa jibu sahii zaidi ya vitisho.Kitendo kilichomfanya mama Ngesha pamoja na mwanae kuweka msiba nyumbani kwani tayali waliamini mzee wao aliyejulikana kwa jina la Mugina,alikuwa ameuawa,jambo ambalo lilikuwa kweli. “Naenda kumsalimia
rafiki yangu Njoshi,mara moja,” Ngesha alimjibu mama yake na kisha kutokomea huku akikimbia ili kumuwahi Njoshi,kwani ilikuwa ndio mida ya Njoshi na mama yake kwenda shambani. Ikulu kwa mfalme;
Asubuhi na mapema siku ya jumanne,siku
ambayo usiku uliopita kijana Njoshi alitoweka ikulu kuelekea katika msitu wa majini,kwenda kuchukua jeneza la ajabu kwa ajili ya kumzikia mfalme atakapokufa ,na kisha kufufuka ndani ya wiki moja. Vilio vinatawala katika
ngome yote ya mfalme,huku familia nzima ya mfalme pamoja na wafanyakazi wote wakilia kwa kwikwi,ama kweli mkuki kwa ngurue kwa binadamu mchungu,leo hii maneno haya yalijidhirisha waziwazi.Walizoea kuona wengine wakilia,lakini leo ilikuwa ni zamu ya familia ya mfalme kulia. “Baba rudi,baba
rudi baba yangu nakupenda”,msichana Grace alilia kwa huzuni,huku akitamka maneno ambayo yaliongeza uchungu katika familia nzima ya mfalme.Walitamani sana Njoshi afanikiwe kurudi na jeneza salama,ili mfalme afufuke ndani ya wiki moja na kuishi milele,lakini hawakuamini kama kweli Njoshi atafanikiwa kurudi salama,kwani huko msituni alikoenda ni hatari sana. Nyumbani kwa kina
Njoshi; Mama yake Njoshi,akiwa ameshika jembe
kama kawaida yake tayali kuelekea shambani,huku kichwani akiwa na mawazo mengi juu ya hatma ya mwanae. Akiwa anatoka nje ya
uzio wake wa nyumba,uzio ambao ulitengenezwa kwa nyasi,Kwa mbali alishangaa kumuona kijana akija uelekeo wa nyumba yake huku akikimbia.Kitendo hicho kilimfanya aweze kuweka jembe lake chini,pamoja na kikapu kilichokuwa na maji ya kunywa pamoja na chakula kwa matumizi ya shambani siku nzima. “Aiweee…mama
,Njoshi ni memkuta…aiweeh”,Ngesha alimsalimia mama yake Njoshi na kumuulza kuhusu rafiki yake,huku mama akipumua baada ya kumtambua kijana aliyekuja nyumbani kwake,na pia hakuweza kuleta taarifa mbaya. “Aiweeeh
Kifo chamwanangu,rafiki yako aliitwa na mfalme tangu jana asubuhi,mpaka sasa sina taarifa yoyote,aiweeeh”,mama Njoshi alimjibu rafiki yake mwanae,na kumtia hofu sana,kitendo ambacho kilimfanya Ngesha kutoweka bila hata kuaga kuelekea ikulu,kwani alitambua kuwa rafiki yake lazima atakua hatarini kama kweli alienda ikulu tangu siku iliyopita na hajarudi mpaka wakati ule. mfalme,haitakiwi wananchi wa Mwamutapa wafahamu,zaidi ya familia ya mfalme na mtu aliyelifuata jeneza msituni,lakini Ngesha kaelekea ikulu kwenda kujua nini kinaendelea kwa rafiki yake Njoshi.… |