NADHARIA YA UHUSIANO: DHANA YA PROPOSISHENI (2) - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Nadharia mbalimbali (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=14) +--- Thread: NADHARIA YA UHUSIANO: DHANA YA PROPOSISHENI (2) (/showthread.php?tid=618) |
NADHARIA YA UHUSIANO: DHANA YA PROPOSISHENI (2) - MwlMaeda - 07-23-2021 DHANA YA PROPOSISHENI Katie Wales (2001),
anasema kuwa proposisheni ni neno lililoazimwa kutoka kwa elimu ya falsafa. Maana kiproposisheni katika kauli au sentensi ndio ya kimsingi akilini na wakati huohuo maana katika proposisheni ni ya kidhahania ambayo huhusisha kiima na kiarifu. Proposisheni hufanana na vitendo usemi vya kauli. Hulingana kisarufi na sentensi arifu ambayo huwa na kiima na kiarifu. Hata hivyo, kuna tofauti baina ya viwango tofauti vya sarufi na maana. Kama vile, sentensi katika kauli tendaji na katika kauli tendwa zaweza kueleza proposisheni ambayo yaonekana kuwa moja hata kama zina kiima na kiarifu tofauti. Kwa mfano:
Mpira
ulichezwa na watoto. Watoto
waliucheza mpira. Vilevile, proposisheni
yaweza kuwa na maana zaidi ya moja, kama ina utata. Kwa mfano: Joy
amepigia Judy mpira. Maelezo katika mfano , yana maana kuwa labda Joy alimpiga Judy kwa sababu ya Mpira au pengine
alimpigia mpira ili wacheze pamoja, vilevile huenda ikawa Joy aliupiga mpira kwa niaba ya Judy. Hivyo basi, proposisheni katika sentensi hii tabainika kama msemaji ataeleza bayana maana aliyoikusudia katika kutamka kauli hii. Kulingana na Halliday
(1985), proposisheni hukubaliwa au kukataliwa. Hii ina maana kuwa kama ni ya ukweli ambao unaweza kuthibitika, basi itabidi washiriki katika mazungumzo kuikubali na kuamini jambo lililomo katika proposisheni hiyo. Kwingineko, kama itakuwa haina ukweli ambao unaweza kuthibiti, basi washiriki katika mazungumzo wataikataa na kutoiamini kuwa ya kweli. Hivyo basi, ni lazima proposisheni ithibitiwe katika misingi ya kweli au uongo. Kwa mfano: ‘Nchi ya
Kenya ni huru.’ Proposisheni katika
kauli hii itakubalika kwa sababu ni jambo lililo wazi na kila mtu anafahamu kuwa ni nchi yetu ilijinyakulia uhuru na kujikomboa kutoka kwa utawala wa wakoloni Larson (1984:89 -197),
anasema kuwa proposisheni ni mkusanyiko wa dhana katika kundi la watu ambalo huwasiliana. Hivi anamaanisha kuwa Proposisheni hutegemea uhusiano uliopo baina ya dhana zilizomo. Kwa mfano: John,
Peter, alimpiga. Kama John ndiye
aliyetenda kitendo cha kumpiga Peter, basi proposisheni itakuwa: John alimpiga Peter. Vivyo hivyo, Kama Peter ndiye aliyetenda kitendo cha kumpiga John, basi proposisheni itakuwa: Peter alimpiga John. Muundo wa semantiki katika proposisheni waweza kuonyeshwa kwa njia zifuatazo tunazoziangazia hapa chini. Kwa mfano: Proposisheni
katika 1) Mtenda -.John … kitendo : kumpiga… mwathiriwa :
Peter 2) Mtenda : Peter … kitendo : kumpiga … mwathiriwa :
Joh M fuatano wa maneno
katika sarufi utabainisha ni nani aliyempiga mwingine. Proposisheni yaweza kuzua maana kadha. Kwa mfano:
1) John aiimpiga Peter.
2) Peter alipigwa na
John. 3) Kupigwa kwa Peter
kulifanywa na John. 4) Peter ndiye alipigwa
na John. 5) John ambaye aiimpiga
Peter. Kuna proposisheni za
matukio ambazo hubainishwa kwa dhana ambazo huwakilishwa na maneno tofauti. Kama vile: Sentensi hiyo hapo juu
kwanza itachanganuliwa kwa kutambua dhana ambazo huwakilishwa na maneno tofauti. Kisha, sentensi hii ya kisarufi kuelezwa kama proposisheni ambapo matukio yatakuwa msingi wa proposisheni hizo. Hivyo basi, matukio hayo yatakuwa; kuharibu na kupanga. Proposisheni zitakuwa: Mtu aliharibu mji
Mtu
alipanga vyema. Proposisheni huelezwa
kwa kujumlisha wahusika. Nomino Mtu imetumika katika proposisheni hizi kuwakilisha mtenda ambaye alitenda kitendo. Kwa mfano: “John
alikataa ahadi ya Peter.’ Matukio basi ni kukataa na ahadi kisha Wahusika ni John
na Peter. Hivyo basi, John
alikataa naye Peter alikuwa ameahidi kufanya kitu fulani na Peter aliahidi kabla ya John kukataa. Hatimaye tunafahamu kuwa tukio la kuahidi lilifanyika kabla ya tukio la kukataa. Proposisheni ndicho
kitengo kidogo zaidi katika mawasiliano. Dhana moja hutokea pamoja na dhana zingine ili kuwepo na mawasiliano yenye maana. Kila tukio huwakilisha proposisheni. Kwa mfano: “Joy aliruka ukuta, alikimbia na kutumbukia ndani ya ziwa’. Sentensi hizi zina
proposisheni tatu ambazo ni: 1) Joy aliruka ukuta.
2)
Joy alikimbia. 3)
Joy alitumbukia ziwani. Matini chanzi katika
lugha yoyote yaweza kuwa proposisheni. Kwa mfano: 1) Lugha chanzi: Kutotii husababisha kuteseka sana.
Proposisheni: Mtu hukosa kutii.
Mtu huteseka.
2) Lugha chanzi: Sifa hiyo ilipokelewa vyema na Maria.
Proposisheni: Mtu alimsifu Maria.
Maria aliitikia vyema.
3) Lugha chanzi: Watu wanaofikiria kuwania kiti cha Urais,
wataanzisha kampeni zao hivi karibuni.
Proposisheni: Kuna watu wanaolifikiria tendo.
Wanataka kuwa Rais.
Watafanya kampeni hivi karibuni.
Tukio laweza kuwa; tendo, tajriba au mfanyiko.
Kwa mfano: Tendo:
Wavulana walikimbia. Paul alikula.
Tajriba: Maria
alisikiaJilimbi. John aliona ng ‘ombe.
Mfanyiko: Barafu iliyeyuka.
Paka alikufa.
Kuna proposisheni za
hali ambazo kitu au matokeo ndio msingi wake. Proposisheni ya hali huwa na sehemu mbili kuu: Sehemu hizo ni mada na maoni. Tukianza na mada, hii ni dhana itakayozungumziwa, ilhali maoni yahusu kitu au matokeo katika kueleza mada na uhusiano katika hali yake. Kwa mfano: ‘Kitabu
ni cha Peter.’ Mada ni kitabu na chahusishwa na dhana Peter kwa uhusiano wa kuwa Peter anakimiliki kitabu kile. Kwa mintarafu hii Peter ndiye mwenye kitabu.
Proposisheni za hali huelezwa
kwa kitenzi cha kuwa ni. Kama vile: Proposisheni ya hali;
Maelezo; Gari …umiliki…
mimi gari ni langu. Mbwa
…jin a … fido Jina la mbwa ni fido. Msimamizi
…kitambulisho… Bwana John Msimamizi ni Bwana John. John
…mahali …nyumba John yumo nyumbani. John
.. maelezo…mkubwa John ndiye mkubwa. Maana ya proposisheni
yaweza kuwa katika matumizi. Mzungumzaji anaweza kuuliza swali, kutoa arifa au kuamrisha. Proposisheni huwa ni moja lakini matumizi tofauti. Kwa mfano:
Maana
clekezi: John … mtenda … aliupiga .. mwathiriwa…mpira Arifa:
John alipiga mpira. Swali: Je, John alipiga
mpira?. Amri: John, piga mpira!
Maana elekezi
haibadiliki lakini matumizi huwa ni tofauti katika kila proposisheni. Matumizi hayo yapo katika proposisheni za matukio na vilevile katika proposisheni za hali, ambayo hujulikana kama misukumo ya kiilokusheni katika proposisheni. Sentensi sahihi, mfuatano wa maneno na uakifishaji ni mambo ambayo huonyesha msukumo wa kiilokusheni katika proposisheni. Mara nyingi kiimbo huonyesha msukumo wa kiilokusheni katika mazungumzo. Kwa mfano: 1) Proposisheni ya hali
ambayo inaamrisha: Uwe hapa karibu! 2) Proposisheni ya hali
ambayo yauliza: Je, Maria ni dadake? 3) Proposisheni ya hali
ambayo yaarifu: Mbwa yumo katika chumba chake. 4) Proposisheni ya
tukio ambayo yauliza swali katika kufanyika: Je, maziwa yaliganda? 5) Proposisheni ya
tukio ambayo yaonyesha tendo la kuamrisha: Wewe, kimbia haraka! 6) Proposisheni ya
tukio ambayo yatoa arifa katika tajriba: Tulisikia sauti. Msukumo wa kiilokusheni
waweza kuoneshwa kwa mfuatano wa maneno, viambishi au maneno na huibuka hasa kupitia kwa dhamira. Matumizi ya proposisheni ni muhimu katika kuleta maana kwa sababu mtu huenda asifahamu maana iliyokusudiwa na msemaji. Kwa mfano:
Tukio
– kula, mtenda – chui, mwathiriwa – msafiri. Katika mfano; maana
haiwezi kueleweka ila msemaji afafanue lile jambo analolitamka kuwa sentensi yenyewe ni Arifa: Kama vile; Kauli: ”Chui alimla msafiri’ au ni sentensi ya kutaka kuhakikishiwa jambo: Kama vile; Swali: ‘Je, chui alimla msafiri. Jinsi msemaji anavyosema jambo huchangia katika kuelewa maana. Kuna wakati ambapo msemaji hutaja msukumo wa kiilokushcni. Kwa mfano: Nenda
– Nakuamrisha uende!…Amri. Alikwenda – Nasema kuwa
alikwenda: Arifa. Kwa nini alikwenda? –Nauliza
ni kwa nini alikwenda?: Swali. Arifa hukusudia kumpa
msikilizaji ujumbe. Swali hukusudia kumpa msikilizaji ujumbe kutoka kwa msemaji, ilhali amri hukusudia kutoa sheria itakayofuatwa na msikilizaji. Kama vile: Nakuamrisha, nasema na nauliza ni proposisheni tendaji kwa sababu huonesha kitendo kinachofanyika, yaani ni maana iliyopo katika proposisheni, ili mawasiliano yaweze kufaulu. Maana ya proposisheini
hujumlisha maana kadiri ya vitendo katika kishazi. Kwa mfano: : “Jengo refu ambalo ni adhimu lilianguka”.
Yadhihirisha proposisheni kuwa: 1) Jengo ni refu.
2)
Jengo ni adhimu. 3)
Jengo lilianguka. Katika Kiswahili, kila
mojawapo ya kauli hizi zifuatazo ni proposisheni. Kwa mfano:
‘Alex alikula ndizi.’
‘Ndizi ililiwa na Alex.’
‘Je, Alex, alikula ndizi?’
Matamshi yaliyo katika
mfano hapo juu, yaweza kuchanganuliwa kuwa na kiarifu kinachotaja kundi au hali na mijadala kadha na wahusika katika tukio au hali fulani. Shughuli ni ya kula. Mtenda ni Alex. Mtcndwa ni ndizi Proposisheni ya
uhusiano huzua maana ya umaanisho kati ya proposisheni mbili au makundi ya proposisheni ambayo yahusiana katika mwingiliano wa kiproposisheni ulipo katika kauli. Huleta uamuzi na mshikamano mkubwa kuhusu yaliyozugumzwa. Kwa mfano: “Nina njaa. Twende Westlands”. Kauli hii
ina proposisheni kuwa: 1) Msemaji anahisi njaa.
2)
Msemaji anaonelea wacnde Westlands wapate chakula. Uhuasiano wa
proposisheni hizi mbili ni kuwa kuna suluhisho la njaa na jinsi ya kusuluhisha. ‘Kwenda kwetu Westlands‘ ni sehemu ya suluhisho la tatizo langu kuwa ‘naona njaa’ Leech (1974:18-23),
anasema kuwa hisia za mtu binafsi huwepo kama zinazomhusu mtu anayepokea ujumbe au kuhusu kitu fulani zitabainika wazi. Maana hisivu yaweza kuibushwa na proposisheni. Kwa mfano:: “Samahani kwa kuwakatiza mazungumzo yenu
lakini, ni vyema kama mngepunguza sauti zenu“. Msemaji wa kauli hii
alikuwa ana hasira kwa sababu ya kelele kutoka kwao, kisha alijaribu kuwa mpole katika kuwaambia kuwa sauti zao za juu hazimfurahishi kamwe. Vilevile, proposisheni yaweza kuzua maana katika dhamira. Jinsi mzungumzaji anavyoupanga ujumbe wake katika mpangilio wake wa maneno na kusisitiza jambo. Kwa mfano: 2 .19: (A)
1) ‘Bi Smith ali/adhili
tuzo la kwanza 2) ‘Tuzo la kwanza
lilifadhiliwa na Bi. Smith’ Sentensi ya kwanza ni
katika kauli tendi ilhali sentensi ya pili ni katika kauli tendwa. Kwa mfano: 2.20: (B)
1)
‘Ndugu yangu amemiliki duka lililo kubwa zaidi mjini Nairobi’ 2)
Maana ni tofauti‘Duka lililo kubwa zaidi katika mji wa Nairobi limemilikiwa na ndugu yangu’ kulingana na kauli zilizotumika, kulingana na mpangilio wa maneno na msisitizo. Mfano; (A), sentensi ya kwanza ina proposisheni kuwa Bi.Smith ni mtu mabaye ni muhimu sana ili ufadhili wa tuzo la kwanza uwepo, sentensi ya pili ina proposisheni kuwa tuzo la kwanza ni lenye umuhimu na sio lazima lifadhiliwe na Bi. Smith, mbali pia mtu mwingine yeyote anaweza kufadhili. Mfano; (B), sentensi ya kwanza ina proposisheni kuwa ni ndugu yangu aliye na uwezo wa kumiliki lile duka kubwa zaidi mjini Nairobi, ilhali katika sentensi ya pili mtu mwingine yeyote isipokuwa ndugu yangu hana uwezo wa kumiliki duka kubwa zaidi mjini Nairobi. MAREJELEO Abraham, S. (1996). A Theory o f Structural Semantics’. Mouton and Company Publishers. Akmajian, A. na Wenzake. (2004) Linguistics. An lntrodution to Language and Communication. Fifth Edition: MIT Press, Cambridge. Atichi, A.R. (2004) The Semantic Distinctiveness of Kenyan English: UON. Unpublished MA Thesis. Atoh, F.O. (2001) Semantics Analysis of Dholuo Nowns: The Semantics Field Approach. UON. Unpublished MA Thesis. Blass, R. (1990) Relevance Relations in Discource. A Study in Special Reference to Sissala: Cambidge University Press. Brown, G. na Yule, G. (1983) Discource Analysis: Cambridge University Press. Bussman, H. (1996) Route ledge Dictionary o f Language and Linguistics: International Thompson Publishing Company. Cambridge (2008) Cambridge Advanced Learners Dictionary. Cambridge University. Carston, R. (2002) Thoughts and Utterances. The Pragmatics of Explicit Communication. MA: Blackwell Publishers Ltd. Comford, F. M. (1957) Platos Theory o f Knowledge: Routeledge and Kegan Paul Ltd. Crystal, D. (2003) A Dictionary o f Linguistics and Phonetics. Fifth Edition. Oxford: Blackwell Publishers. Falsod, R. W. (2002) An lntrodution to Language and Linguistics. Cambridge University Press. Fleming, (1998) Google Search. Powered by The Ultimate Programming Weblog. Sil lntematinal: http:// worldnet Princeton. Edu/Pert/Webwn. Fodor, J. D. (1997) Semantics: Theories o f Meaning in Generative in Generative Grammar: Harper and Row , Publishers. Fretheim, A. (2000) Pragmatic Markers and Propositional Attitude: John Benjamin Publishing Company. Green, G. M (1996) Pragmatics and Natural Language Understanding. Second Edition: Lawrence Erlbaum Associates Publishers. Greenbaum, S. na Wenzake. (1985) A comprehensive Grammar o f English Language: Longman Group UK Ltd. Griffin, E. M (1991) A First look at Communication Theory. Wheaton College: Me Graw- Hill, Inc. Company. Hofmann, T. R. (1993) Realms o f Meaning: An Introduction to Semantics: Longman Group UK Ltd. Ifantidou, E. (2001) Evidentials and Relevance. Volume 86: John Benjamin Publishing Company. Kamau, S. K. (2008) An Analysis o f Truth Conditions in Pragmatics: Relevance Theory A p p r o a c h . UON. Unpublished MA Thesis. Kasher, A. (1998) Pragmatics. Critical Concepts. Volume V: Communication, Interaction and Discourse: Routeledge Publishers. Katie, W. (2001) A Dictionary o f Stylistics: Longman Group UK Ltd. Katz, J.J. (1977) Propositional Structure and Illocutionary Force. A Study of the contribution of Sentence meaning and Speech Acts: The Harvest Press. Kempson, R. M. (1975) Pressuposition and The Delimination o f Semantics: Cambridge University Press. Larson, M. L. (1984) Meaning-Based Translation: A Guide to Cross-Language Eqivalence: University Press of America, Inc. Leech, G. (1974) Semantics: Penguin Books Limited. Leech, G. N. (1971) Towards a Semantic Description o f English: Longman Group Ltd. Linsky, L. (1952) Semantics and the Philosophy o f Language: University of Illinois Press. Longmans (1968) Longmans English Larousse: Longmans, Green and Co. Ltd. Munga, C. M. (2009) Sence Relations in Gikuyu: A Lexical Pragmatics Approach. UON Unpublished MA Thesis. Ndug’u, M. N. (2009) Mada na Fokasi katika Kiswahili: Mtazamo wa Muundo wa Taarifa. UON. Unpublished MA Thesis. Ogola, C. A. (2006) A Pragmatic Analysis of Intercultural Communication Failures. UON, Unpublished MA Thesis. Palmer, F. R. (2006) An Introduction to Language and Linguistics: Cambridge University Press. Rouchota, V, na Jucker, H. (1998) Current Issues in Relevance Theory: John Benjamin Publishing Company. Saeed, J. L. (2003) Semantics. Second Edition: Blackwell Publishing Ltd. Schroeder, H. (2005) Do we Speak the same Language? A cognitive Pragmatic Explanation of Cultural Misunderstanding. In Across Borders: Benefiting from Cultural Differences. Conference Proceedings. 17^-18th March: 2005. Sperber, D na Wilson, D. (1995) Communication and Cognition, 2nd Edition: Blackwell Publishers. Sperber, D na Wilson, D. (2004) A Handout on Relevance Theory (1985-2002): Blackwell Publishers. Tuki (1990). Kamusi ya Isimu na Lugha. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Educational Publishers and Distributors Ltd. Tuki (2006) English-Swahili Dictionary. Third Edition: Book Printing Services Ltd. Chanzo>>>>>>>> |