MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BAATHI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'BAATHI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BAATHI' (/showthread.php?tid=2600)

ETIMOLOJIA YA NENO 'BAATHI' - MwlMaeda - 06-15-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAATHI'

Neno *baathi* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Bath.i* [Kitenzi elekezi] chenye maana ya 'rejesha uhai wa mtu au kiumbe aliyekuwa amekufa; fufua.

*Kisawe* : huisha.

*Minyambuliko:*
baathia, baathika, baathiwa, baathisha.

2. *Bath.i* [Kitenzi elekezi] chenye maana ya -pa mtu uwezo na mamlaka ya kwenda kufanya kazi au jambo kwa niaba ya mtu mwengine.

3. *Nomino [Ngeli:-a/-wa]* yenye maana ya kiongozi wa dini; mtume. 

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *baathi* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'ba-aath*( *soma: ba-athun/ba-athan/ba-athin بعث )* ambalo ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Kufufua, kufufuliwa, kuhuisha *yawmul ba-athi يوم البعث* siku ya Kiyama.

2. Mtume, mitume.

3. Kumuamsha mtu toka usingizini.

4. Kikundi cha askari wapiganaji; jeshi.

5. Mtu asiyeweza kupata usingizi kutokana mazonge aliyokuwa nayo.

6. Furaha, utulivu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'ba-athun بعث* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *baathi* lilichukua baadhi ya maana kutoka Kiarabu na kuziacha zingine.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*