MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIDHIO' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIDHIO' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIDHIO' (/showthread.php?tid=2455)



ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIDHIO' - MwlMaeda - 03-13-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIDHIO'

Neno *aridhio* katika lugha Kiswahili ni *Nomino* inayotokana na kitenzi elekezi *aridh.i* chenye maana zifuatazo:

1. Ingilia mtu katika jambo analolisimamia.

*Mnyumbuliko: aridhia, aridhika  aridhiwa, aridhiana, aridhisha.*

*Visawe: kera, sumbua, udhi, ghasi.*

2. Orodhesha vitu; weka vitu kwa mpangilio kuanzia kimoja hadi kingine.

3. Soma kwa kukariri bila ya kuangalia maandishi mbele ya mwalimu aghalabu Qur'aan Tukufu.

4. Kitenzi elekezi *aridhi.a* fafanua jambo fulani.

*Visawe: arifu, juvya, fahamisha, julisha.*

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *aridhi* linafanana na kitenzi cha Kiarabu  *aaridh عارض* kitenzi cha kuamrisha/kutaka tendo kutendeka, kinachotokana na kitenzi cha msingi cha Kiarabu *aaradhwa  عارض* chenye maana zifuatazo:

1.  Ingilia mtu kati kwa kuhoji au kupinga anachokisema.

2. Epuka jambo fulani.

3. Yapinge maandishi kwa kutoa maandishi dhidi yake.

4. Tembea pembezoni mwa njia.

5. Dhihirisha/weka wazi jambo/taarifa fulani; soma kwa kukariri bila ya kuangalia maandishi.

6. Onesha kitu fulani kwa wengine.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiswahili *aridhio* halina mfano wake katika Kiarabu na *si neno la Kiarabu* bali limebuniwa kutokana na kitenzi cha Kiarabu *aaridhi عارض* kinachotokana na kitenzi cha msingi cha Kiarabu *aaradha عارض* kilichofafanuliwa hapo juu.

Katika Kiarabu tendo-jina *masdar  مصدر* la kitenzi cha Kiarabu  *aaradha* ni *muaradha معارضة* lenye maana ya kuweka wazi taarifa; *onesho* .

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*