MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ARAFA' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'ARAFA' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ARAFA' (/showthread.php?tid=2410)

ETIMOLOJIA YA NENO 'ARAFA' - MwlMaeda - 02-27-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARAFA'

Neno *arafa* katika lugha Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino [Ngeli: i-/i-]* siku ya tisa ya mwezi Dhulhija (Mfungo Tatu) katika Kalenda ya Kiislamu - Hijiriyyah.

2. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* ujumbe mfupi wa maandishi unaotumwa na kupokewa katika simu ya mkononi.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *arafa*( *soma: arafatu/arafata عرفة)*  ni nomino ya Kiarabu, wingi wake ni *arafaat عرفات* yenye maana zifuatazo:

1. Mahali penye mchanga paliponyanyuka.

2. Kizuizi kati ya vitu viwili.

3. Tendo-jina la Kitenzi cha Kiarabu *arafa/ya-arifu  عرف/يعرف* chenye maana ya : -metafuta habari, -meuliza.

4. Siku ya tisa ya mwezi Dhul-Hijjah (Mfungo Tatu) katika Kalenda ya Kiislamu - Hijiriyyah.

5. Jina la mlima maarufu karibu na mji wa Makkah, nchini Saudi Arabia.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *arafatu/arafata/عرفة)*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno  *arafa* lilichukua kutoka lugha ya asili - Kiarabu maana ya *siku ya tisa ya mwezi Dhul-Hijjah (Mfungo Tatu)* na kubeba maana mpya: *ujumbe mfupi wa maandishi inaotumwa na kupokewa katika simu ya mkononi.*

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*