MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO 'AJILA' NA 'AJILANI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA MANENO 'AJILA' NA 'AJILANI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'AJILA' NA 'AJILANI' (/showthread.php?tid=2389)

ETIMOLOJIA YA MANENO 'AJILA' NA 'AJILANI' - MwlMaeda - 02-05-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'AJILA' NA 'AJILANI'

Neno *ajila* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* hali ya kufanya kitu kwa haraka; fanya jambo himahima.

2. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* utendaji jambo bila kukawia.

3. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* umuhimu.

Katika lugha ya Kiarabu, neno *ajila* limekopwa kutoka nomino ya Kiarabu  *aajilun/aajilan/aajilin عاجل*  yenye maana zifuatazo:

1. Mwenye kufanya haraka.

2. Hali ya kutokea jambo kwa haraka.

3. Jina lingine la dunia; mahali pa kupita kwa haraka.

Neno *ajilani* katika lugha ya Kiswahili ni kielezi chenye maana ya bila kukawia, mara moja, hivi sasa.

Katika lugha ya Kiarabu, neno *ajilani* limekopwa kutoka nomino ya Kiarabu  *ajlaanu/ajlaana  عجلان*  yenye maana zifuatazo:

1. Mwenye kufanya mambo yake haraka haraka.

2. Mwenye kutembea kwa haraka kuwahi shughuli zake.

Kinachodhihiri ni kuwa maneno *ajila* na *ajilani* yalipokopwa kutoka Kiarabu hayakuacha maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu isipokuwa Waswahili waliliweka neno *ajilani*  katika kategori mpya - *kielezi*  na kulipa neno *ajila* maana mpya - umuhimu

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*