MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AMIRI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'AMIRI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AMIRI' (/showthread.php?tid=2073)

ETIMOLOJIA YA NENO 'AMIRI' - MwlMaeda - 01-09-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AMIRI'

Neno amiri katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino: [Ngeli: a-/wa-, wingi: maamiri ] mtoto wa mfalme; mwana mfalme.

2. Nomino: [Ngeli: a-/wa-] kiongozi mwenye mamlaka ya kutoa amri.

Mfano: kiongozi mkuu, amiri jeshi mkuu: mtu mwenye cheo kikubwa kijeshi anayetoa mwongozo kwa wanajeshi wengine walio chini yake.

2. Kitenzi si elekezi:  amir.i anza kufanya jambo; anzisha ( Minyumbuliko : amiria, amirika, amirisha, amiriwa.)

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili amiri(soma: amiirun/amiiran/amiirin امير) ni nomino inayotokana na kitenzi cha Kiarabu amura أمر ameamrisha , lenye maana: mwenye kutoa amri.

Maana zingine za neno (amiri) katika Kiarabu ni:

1. Mfalme

2. Mtoto wa mfalme.

3. Mtawala.

4. Mshauri.

5. Jirani.

6. Lakabu ya kiongozi wa Waislamu, amiru al-Muuminiina (soma: Amirul Muuminiina Kiongozi Mkuu wa Waislamu امير المؤمنين ).

Kinachodhihiri ni kuwa neno amiiri (soma: amiirun/amiiran/amiirin امير ) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno amiri  lilichukua baadhi ya maana zake kutoka Kiarabu na kuziacha maana zingine.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.