SHAIRI: YUPO BINTI ANIGHURI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: YUPO BINTI ANIGHURI (/showthread.php?tid=1946) |
SHAIRI: YUPO BINTI ANIGHURI - MwlMaeda - 01-03-2022 SHAIRI: YUPO BINTI ANIGHURI ********* Ninahisi vungevunge, miye mwana Mnyarwanda, lakini wacha nitunge, beti zifikie kenda. ***** Jama nawafahamisha, yupo binti anighuli, hili limenighumisha, nakosa hata kauli. ***** Kimwana aso na tenge, uno badii jamali, tenzi hili nilitunge, liwe tuzo la kimwali. ***** Uzuri we mdawari, kidege Mtanzania, kwake nimedadahari, ni aje ‘tanifikia? ***** Ipo siku alikuja, anapaa ja tuyuri, kumpokea nikaja, akamficha khantwiri. ***** Ni Purinsezi makini, msanii mshairi, ni mtunzi na aghani, anikosha ninakiri. ***** Nti yetu iko powa, naja mwa hini qamari, siyo kwa kuogopewa, nikute uko tayari. ***** Yeo ‘wache kupulika, longo wanakuambia, kwetu Rwanda ukifika, uwe wangu Malikia. ***** Beti kenda ni’shafika, n’kushukuru Rahmani, n’najisikia kuchoka, kalamu natuwa chini. ******* Rwaka rwa Kagarama Mshairi Mnyarwanda. |