MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI (/showthread.php?tid=1906)

ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI - MwlMaeda - 12-31-2021

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI'

Neno *afiriti*[ *Ngeli: a-/wa-]* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: ya:

1. Mtu anayechochea wenzake kufanya maovu.

2. Shetani aletaye madhara kwa watu, maluuni, jini, ibilisi.

3. Mtu mwenye tabia za ujanjaujanja, mdangayifu.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *afiriti* (soma: *ifriit عفريت)* ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mtu khabithi/habithi, muovu, mdaganyifu.

2. Mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu katika kutenda jambo fulani; mahiri.

3. Jini, shetani, pepo.

4. Kreni inayoinua magari na kadhalika.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *afiriti* ( *soma: ifriit  عفريت*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *afiriti* maana zake zinazohusu jini na mtu mjanjamjanja/mdanganyifu hazikubadilika isipokuwa limeacha maana zingine katika Kiarabu na kuchukua dhana ya mtu anayechochea wenzake kufanya maovu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*