ETIMOLOJIA YA NENO ' ADIA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO ' ADIA (/showthread.php?tid=1897) |
ETIMOLOJIA YA NENO ' ADIA - MwlMaeda - 12-29-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' ADIA' Neno *adia*[ *Ngeli: i-/zi-]* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana ya: fedha au mali unayompa mtu kwa lengo la kumthamini au kuonesha upendo wako kwake. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *adia* (soma: *hadiyyatun/hadiyyatan/hadiyyatin هدية)* ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Harusi. 2. Zawadi. 3. Upande wa uelekeo. 4. Njia; mwenendo wa maisha. Kinachodhihiri ni kuwa neno *adia* ( *soma: hadiyyatun/hadiyyatan/hadiyyatin هدية*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *Adia* lilijifunga na ile maana ya 'fedha au mali unayompa mtu kwa lengo la kumthamini au kuonesha upendo wako kwake; zawadi, na kuziacha maana zingine za neno hili katika lugha ya Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |