MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'HEKIMA' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'HEKIMA' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'HEKIMA' (/showthread.php?tid=1748)

ETIMOLOJIA YA NENO 'HEKIMA' - MwlMaeda - 12-15-2021

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' HEKIMA'

Neno *hekima* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Maarifa, uwezo wa akili alionao mtu unaomuwezesha kufikiri kwa kina na kutoa uamuzi unaokubalika; busara.

2. Uwezo wa akili katika kutoa maamuzi kutokana na tajiriba na uzoefu wa muda mrefu.

3.  Akili inayomuwezesha mtu kufikiri na kuweza kutoa uamuzi unaofaa.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *hekima* ( soma: *hikmatun/hikmatan/hikmatin* *حكمة* ) lina maana zifuatazo:

1. Uamuzi, *masdar* *مصدر* *tendo-jina* kutokana na *kitenzi* cha Kiarabu *hakama* *حكم* (ameamua/ametoa uamuzi).

2. Maarifa ya kujua kilicho bora zaidi kwa kutumia njia bora za kielimu; falsafa.

3. Taaluma ya kujua uhalisia wa mambo.

4. Uwezo wa kudhibiti nafsi na mihemko wakati wa kupandwa na ghadhabu/hasira.

5. Haki, uadilifu.

6. Sababu ya kutokea jambo fulani.

7. Maneno machache yenye maana kubwa na pana.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *hikmatun* *حكمة*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *hekima* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika ingawa imejifunga katika uwezo wa akili wa kufikiri na kutoa uamuzi unaofaa.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*