MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Kamusi]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ 2024-04-28T10:01:30Z MyBB MwlMaeda]]> 2022-01-06T04:26:10Z 2022-01-06T04:26:10Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2037 <![CDATA[ISTILAHI ZA UTAFITI TATAKI -APRILI 2019]]>
.pdf   ISTILAHI ZA UTAFITI TATAKI -APRILI 2019.pdf (Size: 332.75 KB / Downloads: 10) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-11T16:41:00Z 2021-12-11T16:41:00Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1705 <![CDATA[KAMUSI YA KINGONI]]> 1: Kusakulila/Kung'olea
2: Mang'ova/Mahame
3: Fulesi/Mvi za Nywele
4: Madakali/Matope
5: Chijomela/Kisonjo
6: Mfuleni/Mto
7: Kumfuleni/Mtoni
8: Manyahi/Nyasi
9: Suwuwu/Mbu
10: Uhembe/Unga
11: Mcheche/Nne
12: Mhanu/Tano
13: Shuli/Shule
14: Njila/Barabara
15: Uleyi/Ulezi
16: Malombi/Mahindi
17: Mayau/Mihogo
18: Ngundi/Kunde
19: Msopi/Mweupe
20: Yidung'u/Nyekundu
21: Yititu/Nyeusi
22: Nyosi/Kamba
23: Kifundu/Kifundo/Siri
24: Bwelayi/Njoo
25: Hambayi/Nenda
26: Kiliukayi/Urudi
27: Jumbayi/Kimbia
28: Tilayi/Kimbia/Toroka
29: Matoki/Ndizi
30: Kuwanana/Kufanana
31: Manjwemba/Ndevu
32: Chitanda/Kitanda
33: Mpasa/Mkeka
34: Nyula/Nguo
35: Mpundi/Mwiko wa Kusongea ugali
36: Chijiku/Kijiko
37: Chihimwisi/Zezeta
38: Mandyoli/Kushoto
39: Kuhwela/Kushinda
40: Pipipi/Kutwa
41: Kudyolesa/Kulemba
42: Kuhusa/Kutoa
43: Kushuli/Shuleni
44: Shuli/Shule
45: Kuvemba/Kulia
46: Njila/Njia
47: M,betu/Umande
48: Mene/Mbuzi
49: Liguluvi/Nguruwe
50: Limbelele/Kondoo
51: Lidelele/Mlenda
52: Pitiku/Mboga ya Maboga Isiyoungwa
53: Chisamvu/Kisamvu
54: Likolo/Mboga
55: Liyoka/Nyoka
56: Lihimba/Simba
57: Linu/Jitu
58: Linyoto/Chura
59: Chibudula/Kaptura
60: Kudorola/Kuharisha
61: Tilya/Tunakula
62: Ilya/Anakula
63: Mkila/Mkia
64: Mau/Mama
65: Tata/Baba
66: Gogo/Babu
67: Bambu/Mzee
68: Kukiliwusha/KURUDISHWA
69: Chindendemesi/Kutetemeka tetemeka hususani Ukishika Kitu.
70: Kudigidala/Kutetemeka Wakati wa Baridi au Ukitoka kuoga Maji ya Baridi
71: Makisira/Mkaa
72: Kuvemba/Kulia
73: Chivembu/Msiba
74: Kulwala/Kuugua/Kuumwa
75: Kundendema/Kutetemeka
76: Libwa/Mbwa
77: Pusi/Paka
78: Ng'ombi/Ng'ombe
79: Chitita/Giza
80: Kilu/Usiku
81: kuhoma/Kuchoma
82: Kulwala/Kuugua
83: Kuhelela/Kuteremka
84: Kukwela/Kupanda Mlima au Mti
85: Kuhika/Kufika
86: Kutama/Kukaa
87: Kuyimba/Kuimba
88: Kutereka/Kupika
89: Kuhova/Kupotea
90: Kusivigana/Kuchanganya Mada kwa Kukusudia/Kumchanganya Mtu ili asitambue Siri au Diri Lako.@⁨Mwl Mama B⁩]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-10-31T06:42:10Z 2021-10-31T06:44:57Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1409 <![CDATA[KAMUSI YA TUKI NA BAKITA]]> MobiTUKI Englisha-Swahili Dictionary


3. KAMUSI KUU YA KISWAHILI (BAKITA) &t&t&t&t&t https://play.google.com/store/apps/detai...musi&hl=en]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T18:14:21Z 2021-06-29T18:23:52Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=363 <![CDATA[USANIFU WA VIDAHIZO VYA KAMUSI YA KISWAHILI SANIFU]]> Utangulizi
Makala haya yanakusudia kujadili usanifu wa vidahizo vya Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS). Ili kuweza kuikabili mada hii ipasavyo, itafaa kwanza kujadili kwa muhtasari suala la usanifishaji. Tunafanya hivyo kwa sababu mbili: Kwanza mada yenyewe ni juu ya usanifu wa vidahizo vya Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Pili, kwa kawaid a dhana ya Kamusi imehusishwa na vidahizo sanifu, ijapokuwa kwa fasiri inachukuliwa tu kuwa kitabu chenye orodha ya maneno yaliyopangwa kialfabeti pamoja na kategoria, maana, etimolojia, matamshi, n.k. ya kila neno. Baada ya kuelezea usanifishaji tutachambua suala la usanifu wa vidahizo vya Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Matarajio yetu ni kutoa mchango utakaohamasisha juhudi za kukuza na kuendeleza taaluma muhimu ya leksikografia. Hatimaye makala yatahitimishwa kwa kutaja mafanikio yaliyopatikana na matatizo yaliyokabiliwa yakiwapo.
Suala la Usanifishaji
Usanifishaji umejadiliwa na wanaisimu na wanalugha wengi wanaotajika (Allerton. 1982, Crystal. (ed.) 1980, Haas, (ed.) 1982. Kitsao, 1983, 1991, Lyons. 1977, Vachek, 1982. Zgusta 1971 miongoni mwa wengineo). Hivyo basi makala haya hayawajibiki kulishughulikia kwa undani suala hili bali kulirejelea kimapisi tu kwajinsi linavyokuwa daraja la kufikisha kwenye mahusiko hasa. Kusanifisha ni kuanzisha kifani au utaratibu unaonuiwa kusawazisha jambo. Ni kuweka kigezo kinachokubalika na kuzingatiwa kiujumla.
Usanifishaji wa lugha ni maratibu unaopuuza tofauti zote za lu gha zinazotokaua na lahaja na kuhusiana na jinsia. umri, hadhi ya kaz i, n.k. Lugha sanifu ni matokeo ya juhudi ya jamii kulazimisha lahaja moja kuwa lugha sanifu. Usanifishaji wa lugha ni uanzishaji wa aina fulani ya utaratibu jumuishi unaokuwa msingi wa maneno na miundo ambayo wengi wa waongeaji wa lugha husika wangeukubali na kuuchukulia kuwa horomo kwa kiasi kikubwa kutokana na jinsi usivyotia maanani tofauti ndogondogo zinazotokana na lahaja.
Usanifishaji hushughulikia lugha, ukizingatia hasa matamshi. tahajia semantiki na sarufi. Maneno hudhihirika katika tahajia au grafimu inapowakilishwa kimaandishi. Hivyo basi matamshi na tahajia huwa na uhusiano mkuruba kiasi kwamba makala haya yanazungumziu kipamoja.
Kuna lugha nyingi ulimwenguni, ambazo matamshi ya maneno hayaoani na maandishi yake. Hizi ni lugha zenye matamshi hijai, totau ti na hijai matamshi, ambapo hijai za neno hazioani na matamshi kwa upande mmoja. na hijai za neno kukubaliana na rnatamshi kwa upande mwingine. Kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazodhihirika kihijai matamshi. Hii ina maana kwamba kwa jumla maneno au leksimu za Kiswahili hutamkwa jinsi zinavyoonekana kimaandishi. Kuna jambo moja tu la kuzingatia – matamshi ya Kiswahili hutiliwa mkazo kwenye silabi moja kabla ya ile ya mwisho. Hivyu basi tuna haki ya kusema kuwa suala la matamshi katika lugha ya Kiswahili si bina. Tatizo hasa ni kwenye hijai kama tutakavyoonyesha baadaye. Semantiki ni tawi kuu la isimu linaloshughulikia uchunguzi wa maana za maneno. Semantiki ina misingi yake katika suala la lugha kuwa imeasisiwa kimaana. Bila lugha kuasisiwa jinsi hiyo, hapangekuwa na mawasiliano miongoni m wa jamii ya waongeaji. Hii ndio sababu iliyofanya Kamati ya Lugha (Kiswahili) ya Afrika Mashariki (1930) kukubaliana matumizi ya maneno au msamiati uliopo na mpya.
Usanifu wa Vidahizo vya KKS
Vidahizo ni yale maneno yanayoingizwa na kuelezwa katika kamusi. Tatizo linalojidhihirisha katika vidahizo vya KKS ni tahajia.
Tahajia na Usanifishaji
Tahajia ni kaida zinazozingatiwa wakati maneno yakiwa katik a umbo la matamshi yanapowakilishwa kimaandishi. Kwa kawaida lug ha yoyote ile ina lahaja mbalimbali zinazotumiwa na wazungumzaji wake. Lugha ya Kiswahili, ina takribani lahaja kumi na sita. Lahaja zote hizi zina tofauti za kimatamshi. Usanifishaji wa Kiswahili ulifanywa il i kurahisisha ufundishaji wake pamoja na kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji wake. Kazi hii ilifanywa na Kamati ya Lugha ya Kiswahili ya Afrika Mashariki iliyoundwa 1930. Kabla ya h apo kulikuwa na Kongamano la Elimu (1925), ambalo liliteua lugha ya kutumiwa kama lugha ya mawasiliano katika shule nyingi iwezekanavyo kote Afrika Mashariki.
Madhumuni makuu ya kamati za lugha (Kiswahili) ya Afrika Mashariki yalikuwa kusanifisha Kiswahili na kuendeleza usanifishaji n a ukuzaji wa lugha hii. hasa kwa upande wa msamiati. Kuhusu hasa usanifishaji wa tahajia. kamati ilipendekeza kufanywe makubaliano ya pamoja ya kuwa na tahajia moja kwa maneno yenye tahajia zaidi ya moja.
Maneno ya lahaja
Lahaja ni lugha za eneo au jamii fulani ya wazungumzaji wa lugha moja inayojidhirisha katika maumbo au matamshi ya maneno pamoja na miundo maalumu ya kisarufi. Ugawikaji wa lugha kilahaja ni tukio la kawaida katika lugha yoyote ile yenye idadi kubwa ya wazungumzaji. hasa pakiwa na mipaka ya kijografia au ya kijamii inayotenganisha watu. Kwa mfano neno mchele lina tahajia tofauti kati ka lahaja za Kiswahili kama .ifuatavyo: ‘mtee’ (Kiamu), ‘mtele’ (Kimvita). ‘mchele’ (Kiunguja). Kwa kuwa Kiswahili sanifu kinatokana na lahaja ya Kiunguja tahajia ya kiunguja ndiyo sanifu, na ‘mtee’ na ‘mtele ni tahajia za kutumika katika lahaja zinazohusika.
Usanifishaji katika kiwango cha tahajia huhitaji uteuzi wa tahajia moja itakayokuwa sanifu na nyingine kuwa za kilahaja na ambazo zitatumika katika muktadha wa Jahaja inayohusika. Uteuzi wa vidahizo vya KKS haukuzingatia usanifu wa msamiati, bali tahajia za lahaja mbalimbali za Kiswahili: ‘aghalabu’ na pia aghlabu’, ‘elimu’ na ‘ilimu’ihitilafu’ na ‘hitilafu’, ‘ikitisadi’ na ‘iktisadi’. ‘zaituni’ na ‘zeituni’, ‘ziaka’ na ‘riaka’, n.k. Kwa bahati mbaya. KKS haionekani kuwa na msimamo kuhusu haya kwani haionyeshi tahajia iliyo sanifu na ile isiyo sanifu na mazingira ambapo vibadala vilivyoingizwa hutumika. Kwa mfano, kati ya baasiri na bawasiri, lipi ni sanifu. Iwapo ulikuwapo umuhimu wa kuonyesha kibadala cha tahajia sanifu ni muhimu kuonyesha kibadala hicho hutumiwa na wazungumzaji gani. Vivyo hivyo kwa dada na dade, fadhaika na fazaika, mwida na muda n.k.
Kamusi ya lugha sanifu kama ilivyo KKS haikustahili kuingiza tahajia za kilahaja za maneno. Uingizaji wa vidahizo vikiwa katika tahajia tofuati waelekea kuwa umefanywa kwa lengo la kuikuza KKS iwe kub wa kwa kuingiza vidahizo vingi isivyostahili au kujaribu kuwaridhisha watunzi wa kamusi hii ambao ni waongeaji wa lahaja tofauti waliotaka tahajia za lahaja zao nazo ziingizwe katika KKS. Hali hii ndiyo iliyoifanya KKS iwe na vidahizo pamoja na vibadala vyake kama ifuatavyo ‘asubuhi’ sambamba na ‘asubuhi’, ‘usubuhi’, ‘baleghe’ sambamba na ‘balehe’; ‘chakleti’ sambamba na ‘chakeleti’, ‘chakuleti’ , na ‘chokoleti’, na ‘muale’ sambamba na ‘muali’ sabini. sambamba n a ‘sabiini’; ‘ahsante’, ‘sambamba’ na ‘asante’ n.k. Tofauti hizi za tahajia zinazotokana na tofauti za matamshi ya neno miongoni mwa wazungumzaji wa lugha hazikustahili kuonyeshwa kwani haiwezekani kuridhisha kila mmoja. Watunzi wa KKS walipaswa kusanifisha tahajia moja.
Kwa kuwa tofauti za kilahaja zinatokana na matamshi tu, kusanifu tahajia kusingeathiri mawasiliano kama Allerton (op. cit. 59) anavyosisitiza. Kwanza kabisa, nyingi ya tofauti tuzisikiazo kati ya waongeaji hazina misingi na hutokana tu na hali za kifisiolojia za watu binafsi. Tofauti kama vile thamani ya sauti. kiwango cha unazali, kwa mfano, hutumiwa kutambulisha mwongeaji siyo yale anayosema. Tofauti nyingine huwa kiushi ndogo za kilafudhi kutoka kwenye kaida za kifonemiki ambazo kwake msikilizaji anaweza kujirekebishia. Tofauti za kifonetiki ambazo kweli ni muhimu kwa mtengenezaji wa alfabeti ni zile zinazoathiri idadi ya ubainishi wa kifonemiki ambazo huhusiana na maneno hasa, hivyo basi akatumia kila moja ya fonimu zake. Thamani sahihi ya kifonetiki anayoipa fonimu zake (au, vizuri zaidi, alofoni zake) katika kila mmoja ya miktadha mingi ya kutukia kwake ina umuhimu kidogo tu.
Kushindwa kusanifisha Kiswahili kwa kuzingatia mapendekezo ya usanifishaji yaliyoasisiwa katika miaka ya 1930 ndiko kulikosababisha kuzuka aina ya lugha iliyomfanya mjumbe mmoja wa Idara ya Elimu y a Kenya alalamike kama ifuatavyo katika memoranda yake:
Quote:
Tumesanifisha Kiswahili na kutika utaratibu huo Kiswahili kimekuja kuonekana kuwa lugha mpya. Ambapo bila shaka, sote tuko tayari kukiri kuwa Kiswahili, kama lugha nyingine yoyoce hakina budi kukua na kupanuka katika umbo, ndumo na msamiati, kutokana na athari ya staarabu za jamii hamizi, lakini kwa hakika ukuaji ni lazima utokane na moyo wa Waswahili, siyo kubandikwa kwao kutoka nje. Lakini hivyo hasa ndivyo ambavyo tumejaribu, na bado tumajaribu kuganya, matokeo yakiwa kwamba tumo katika ile hali isokubalika, ya kuchekesha – ya kuwafundisha Waswahili lugha yao wenyewe kupitia vyombo vya vitabu ambavyo vingi si vya Kiswahili katika umbo au yaliyomo, na ambavyo lugha yake inafanana kidogo sana na lugha ongezi. Labda tuna pupa ya kutufanya tusione ukweli hwamba Waswahili wenyewe hawana tu uwezo wu kurekebisha lugha yao kulingana na mahitaji ya kisusa bali pia wanafanya hivyo kwa kasi inayostaajabisha. (Whiteley, 1959:85).
Maoni haya yalizusha hoja kadhaa zilizoyapa umuhimu wa kuyafanya yajadiliwe kwa muda wa miaka ishirini iliyotuatia kwani yanaunga mkono madai kwamba usanifishaji haukueleweka na kutumiwa kwa utaratibu ufaao.
Leksimu Unganishi
Dhana ya ‘leksimu’ hapa inatumiwa kama inavyoeleweka na wanaisimu, ikirejelea kisehemu kidogo bainishi katika utaratibu wa kisemantiki wa lugha fulani. Inachukuliwa kulingana na madhumuni yake ya awali, yaani kupunguza utata wa dhana ya neno, ambayo ilihusiana na viwango vya kiorthografia/kifonolojia, kisarufi na kileksika, na kubuni dhana mwafaka zaidi kwa matumizi katika muktadha wa kujadili msamiati wa lugha. Hivyo basi leksimu inapendelewa kwa kufaa kwake katika kusimamia seti za miundo ya ki.sarun inayodhihirika kama vile kwa uradidi wa ‘piga’ -&t ‘pigapiga’, maneno ambatano k.m. ‘mwanadamu’ na ‘ngombedume’, pamoja na viambatani kama vile katika ‘yoyote’. ‘vivihivi’, n.k. Hivi ni kusema kwamba leksimu ni visehemu maneno vinavyotamkwa kama neno mojamoja lakini ambavyo huorodheshwa kama kwamba ni visehemu huru katika kamusi kama Lyons (1977:534-5) anavyofafanua: “Leksimu unganishi ni neno ambalo shina lake huundwa kwa kuunganisha mashina2 mawili au zaidi (na au bila marekebisho ya kimofolojia)” ufafanuzi huu unakuwa muhimu hasa kwa sababu ubainishi unaweza kufanywa katika lugha maalumu. kati ya miundo-maneno na miunganisho za miundo maneno.
Katika Kiswahili, uwakilishi wa miunganisho kama vile ‘pigapiga’ na ‘ng’ombedume’ kama vidahizo katika kamusi si bina. Yanayotuhumu ni madhihiriko kama vile ‘yeyote’, ‘vivihivi’. ‘mmojammoja’, ‘mbalimbali’. ‘kutekote’, n.k. Kigezo kikuu cha kubainishia leksimu katika Kiswahili ni kile cha msisitizo. Kwa jumla, kila leksimu katika Kiswahili huwa na msisitizo mmoja wa kimsingi, mahali pake pakiwa silabi moja kabla ya ile ya mwisho. Msisitizo kwenye silahi ya pili katika ‘barabara’. tofauti na msisitizo wa kawaida katika ‘harabara’ ni muhimu kwa madhumuni tu ya kubainisha maana. Kwa kutia maanani kwamba mifano ya uradidi pamoja na miunganisho kama vile ‘kiamshakinywa’ na ‘kiguu-na-njia’ huchukuliwa kuwa leksimu moja hata kama huunganishwa kwa vistari katika lugha maandishi, na kwa kuona kuwa leksimu katika Kiswahili zina misisitizo wazi kwenye silabi moja kabla ya mwisho, tunapendekeza kwamba miundo kama vile mmojammoja’. ‘yeyote’. ‘vivihivi’. ‘tofautitofauti’, n.k. ambayo msisitizo mmoja ni leksimu moja na yafaa kuainishwa na kuwakilishwa hivyo.
Maneno ya Kigeni
Kwa mujibu wa Crystal (1980) maneno ya kigeni “ni faridi ya kiisimu. (kwa kawaida faridi ya kileksika) ambayo imekuja kutumiwa katika lugha au lahaja. mhali na kule kwenye asili yake”. Maneno mkopo yanaweza knchukuliwa na lugha pokezi bila mofimu zake ngeni kubadilishwa au angalau kurekebishwa kidogo. Hali namna hii inaweza kutolewa mfano wa ‘hwana’ (mkopo katika kamusi ya CHAMBERS TWENTIETH CENTURY DICTIONARY. kutokana na Kiswahili) na propaganda kutokana na Kiingereza katika KKS).
Lakini wakati mwingine, sehemu ya neno, hasa likiwa unganishi, hupisha mofimu. au, hasa katika Kiswahili, fonimu nyenza ya lugha pokezi. Katika Kiswahili, leksimu hukopwa kifonetiki (jinsi zinavyosikika kimatamshi) au kifonemiki,( namna zinavyodhihirika kimaandishi) katika lugha kopeshaji. Hivi ni kusema kwamba ukopaji hufanywa kama leksimu katika lugha kopeshaji hudhihirika kitahajia matamshi au kimatamshi tahajia. Leksimu inayopokewa kifonetiki katika Kiswahili kama lugha kopaji ni kama vile ‘ajenda’, ‘baiskeli’, ‘namba’, ‘edita’. ‘pensheni’. na ‘taksi’, kama zinavyopatikana katika KKS. Kamusi hii haikustahili iingize pia tahajia vibadala kwa leksimu zilezile: ‘agenda’, ‘baiskili’, ‘nambari’, ‘editori’, ‘pencheni’. ‘teksi’. Uingizaji wa vibadala vya tahajia ya maneno ya mkopo unapotosha dhana ya kusanifisha lugha.
‘Agenda’ na ‘pencheni’ kama vibadala vya ‘ajenda’ na ‘pensheni’, hata kama dhana ya usanifishaji ingepuuzwa au hata kama maneno haya yangewakilishwa kifonemiki bila shaka ni kosa kutojua. Ukweli ni kwamba, herufi inayoshikwa na jicho kama g kwa upande wa ‘agenda’ au kusikika sikioni kama ch kwenye ‘pension’ si g wala ch kifonetiki. Kwa mfano neno ‘geography’ hukopwa kama ‘jografia’. siyo kama ‘gografia’.
KKS haiwezi kutetea editori kama kibadala cha edita kwani hii inamaanisha kwamba ni mkopo kutokana na ‘editory’ ambayo haipatikani katika lugha kopeshaji. Ni kweli Kiswahili kimepokea ‘nambari’ kwa matumizi ya kila siku kiasi kwamba neno hili halihisiki kutokubalika. Lakini halina msingi wa kiisimu. Si ‘numbery’ bali ‘number’ katika lugha kopeshaji. Uwakilishi wa moja kwa moja wa ukopaji kifonetiki ungekaribisha maneno mageni kama vile ‘fenomena’, ‘kafeteria’. ‘logo’ ‘parafanelia’. n.k. Hivi ndivyo ambavyo Kiswahili kimekopa maneno kama vile ‘penalti‘, ‘digrii‘, ‘bucha’ na ‘buchari’.
Mbali na utohozi wa moja kwa moja wa faridi za kileksia kama zilivyojadiliwa hapojuu, uwakilishi kifonetiki wa manenomkopo unaweza kufafanuliwa ili kusahilisha matamshi katika lugha pokeaji. Ukopaji wa istilahi za taaluma umekuwa na msingi imara wa kutegemea, uliojengwa na leksimu tangulizi kama vile katika ‘filosofia’, na biolojia hata ijapokuwa maneno haya huenda yalikopwa kimajaribio hapo awali. Matokeo ni kwamba hivi leo tuko huru kuwa na ‘bibliografia’, ‘leksikografia’. ‘orthografia’, n.k. katika kundi moja; ‘methodolojia’, ‘etimolojia’, n.k. katika jingine. Utaratibu unaoonekana kuzingatiwa ni kuwa fonimu /phy/ na /gy/ za lugha kopeshaji zirekebishwe na kukaribishwa kama /fia/ na /jia/ katika lugha pokeaji.
Kuhusiana na /ry/, /cs/, /x/ na /sis/ kama vile kalika ‘history’. ‘physics’, ‘syntax’, na ‘hypothesis’, kama vile katika ‘historia’, ‘fizikia’, ‘sintaksia’, na ‘haipothesia’. Katika muktadha wa ruwaza hizi leksimu ‘kemia’ badala ya ‘kemistria’ (kutokana na ‘chemistry’), na paradigmatiki na semantiki badala ya ‘paradigmatikia’ na ‘semantikia’) (kutoakana na ‘paradigmatics’ na ‘semantics’ zaweza kusemekana kuwa ziliteleza. Huenda waliozisanifu walizichukua hivyo ili kusahilisha matamshi kwa kujaribu kuzipunguza urefu.
Hitimisho
Makala haya yamejadili haja ya kutazama upya usanifu wa vidahizo vya KKS. Katika mjadala huu tumeunyesha upungufu wa KKS katika kikishughulikia Kiswahili sanifu. Kamusi imeshindwa kuorodhesha masaniati sanifu. Kuwa hivyo ipo haja ya wanaoidurusu KKS kuvipembua vidahizo vilivyomo na kuorodhesha vile tu vilivyo katika tahajia inayokubalika. Leksikografia, haiwezi kujitenga na usanifishaji wa lugha, Kwa hivyo inahitaji kutekelezwa kwa uvumilivu, kujitolea na ujuzi japokuwa ni kazi ngumu na yenye kuchosha. Mwanaleksikogratia hana budi kutamhua kuwa kamusi ni rejeo muhimu amhalo watumiaji wa lugha huirejelea ili kupata majibu ya maswali mengi yanayoihusu lugha.
Upungufu mwingine wa KKS ni kukosekana kwa minyambuliko na maneno ya kawaida kama vile ‘nyama’ na ‘kama’ ya ‘masharti’ k.m. ‘kama utakuja, sema’. Kasoro zilizo katika KKS zinahitaji kufanyiwa utafiti. Ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika KKS inafaa wanaleksikografia kufanya juhudi ya dhati ya kuyabaini matatizo yaliyomo na kuyasahihisha ipasavyo kwa kuzingatia nadharia za isimu na kanuni za utungaji wa kamusi.
Maelezo
1. Neno hili linatumika Kenya kwa maana ya tahajia.
2 Yaonekana Lyons anatumia dhana ya shina kwa maana maalumu kurejelea neno kama linavyoeleweka kikawaida. Ingawaje katika Kiswahili, dhana hii hutumiwa bila utata kurejelea msingi au mzizi wa neno unaoweza kuongezwa viambishi. Kimatumizi ‘yeyote’ hudhihirika kama ye yote, ‘vivihivi’ kama ‘vivi hivi’ ‘mmojamoja’, kama ‘mmoja mmoja’, ‘mbali mbali’, kama ‘mbalimbali’, na ‘kote kote’ kama ‘kotekote’. Kwa jumla miunganisho hii haipatikani katika kamusi (za Kiswahili).
MAREJELEO
Allerton, D.J. 1982 “Orthography and dialect”. katika Haas, W. (ed.)
Antilia, R. 1972. An Introduction to Historical and Comparative Linguistics New York: MacMillan Publishing Co., Inc.
Broomfield, G.W. “The Development of the Swahili Language,” in AFRICA Vol. 3.1930.
Cartford, J.L. 1966. ALinguistic Theory of Translation London: O.U.P.
Cary, E.A. & Jumplet, R.W (eds.) 1950. Quality in Translation. London: Pergamon Press Ltd.. The International Federation of Translators.
Crystal, D (ed.) 1980 A First Dictionary of Linguistics and Phonetics. London: Andre Deutsch Ltd.
Fullas, H. “Problems of Terminology”. in Whiteley, W.H. 1971. Language Use and Social change. London: OUP.
Gower, R.H. “Swahili Borrowings From English” katika Africa Vol. 22, 1952.
Gurr, A.” Literary Translation, Impure But Anticolonial“. in Gorman, T. (ed.) Journal of Language Association of Eastern africa Vol.2. University of Nairobi, Nairobi 1971.
Guenthner, F. & Guenther 1978 M. Meaning and Translation: (eds.) Philosophical and Linguistic Approaches. London: Duckworth & Co. Ltd.
Haas, W. (ed.). 1982 Standard Languages: Spoken and Written. Manchester: Manchester University Press.
Hyder, M. “Swahili in a Technical Age”, in Africa Contemporary Monographs, No. 4 East African Publishing House. 1966.
Johnson, F. 1939. A Standard Swahili-English Dictionary. Nairobi O.U.P. Kirkpatrick, E.M. (ed.) 1983. Chambers 20th Century Dictionary Great Britain: W & R Chambers Ltd.
Kitsao, J. Ukubalifu wa msamiati/ Istilahi. Mifano kutoka Kenya. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu.
Kitsao, J. Usainfitshaji wa Istilahi za Kiswahili. DSM: TUKI. 1989
Kitsao, J. Standardisation of Kiswahili: A Review with Special Reference to Othography: makala yaliyowasilishwa katika 22nd Annual Conference on African Linguistics (ACAL) Chuo Kikuu cha Nairobi, Nairobi, Kenya. 1991.
Krapf, J.L. 1882. A Dictionary of the Swaluli Language. London.
Lyons, J. 1977. Semantics 2 London, NewYork: Cambridge University Press.
Madan, A.C. 1894. English-Swahili-Dictionary. London.
Madan, A.C. Swahili-English Dictionary. London.
Nida, E.A. 1961. Bible Translation. London: United Bible Society. Towards a Science of translating. Printed in Netherlands. 1975
Exploring Semantic Features. Munchen: Fink.
Pyles, P. & Algeo, J. 1993. The Origin and Development of the English Language. Fourth Edition. Harcourt Bracc Juvanovich College Publishers.
Snoxall, R.A 1958 A Concise English-Swahili Dictionary. Nairobi, DSM:OUP.
Steere, E.1870 A Handbook of the Swahili Language as Spoken at Zanzibar London.
TUKI Lugha ya Kiswahili. UDSM. 1990.
TUKI Usanifishaji wa Istilahi za Kiswahili UDSM. 1990
TUKI Kamusi Sanifu va Biolojia. Fizikia na Kemia. UDSM. 1990
Ullmann, S.1951. Word and their use. London: Muller, Series, Man and Society,
United Bible Sucieties. 1952. The Holy Bible in kiswahili. Union Version.
Vachek, J. English Orthography, in Haas, (ed.) ambayo imerejelewa.
Wajiyewardene, G.E.T. 1959. SWAHILI CONCEPTS OF HEALTH AND DISEASES. Kampala: E.A. Insitute of Social Research. Makerere College.
Whiteley, W. 1969. SWAHILI: The Rise of a national Language. London: Methuen & Co. Ltd.
Zgusta. L. 1971. MANUAL OF LEXICOGRAPHY Paris: Mouton.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T17:56:24Z 2021-06-29T18:09:50Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=362 <![CDATA[MATUMIZI YA KAMUSI]]>
Kamusi ni kitabu cha marejeleo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani, na kupangwa kwa utaratibu maalumu, kasha kufafanuliwa kwa namna ambayo msomaji huweza kuelewa.
Ufafanuzi wa msamiati unaoingizwa kwenye kamusi ni fasili na maelezo mengine kulingana na lengo la kamusi husika.
Msamiati unaoingizwa katika kamusi waweza kuwekwa katika makundi makuu mawili: (a) maneno yote ya lugha au fani fulani (b) orodha ya maneno yaliyochaguliwa kutoka katika lugha ya kawaida au lugha ya fani fulani na kupewa maelezo mafupi ya maana za maneno hayo.
Mtunga kamusi huteua msamiati fulani anapotunga kamusi na kuacha mwingine. Uteuzi wa maneno yanayoingizwa katika kamusi huongozwa na vigezo vifuatavyo:
(i) Umbo la neno
(ii) Maana ya neno
(iii) Historia ya neno
(iv) Matumizi ya neno
Kwa nini kamusi ilitungwa?
Utungaji wa kamusi ulianza katika jamii zilizojua kusoma na kuandika. Kamusi ilihitajika ili imsaidie mtumiaji kufahamu maana za maneno aliyoyasoma. Maneno haya yalipatikana katika matini mbalimbali kama vile vitabu na magazeti. Kwa sababu hii ni  wazi kuwa, kamusi zilianza kutungwa ili kukidhi haja ya kupata maana ambazo hazikujulikana.
Jamii isiyojua kusoma na kuandika, hususani ile ambayo haikuingiliana na watu wa jamii nyingine yenye utamaduni tofauti haikuhitaji kamusi, hii ni kwa sababu kila mwanajamii alifahamu msamiati wote uliohitajika kwa mawasiliano.
Kwa hali hii ni dhahiri haja ya kamusi ilichochewa na kuongezeka kwa msamiati kutokana na kupanuka kwa matumizi ya lugha. Matumizi ya lugha yalipanuka ili kutosheleza haja ya kueleza na kufafanua dhanna mpya zilizotokana na kukua na kubuniwa kwa maarifa mapya yaliyojidhihirisha katika Nyanja mbalimbali za sayansi na teknolojia.
Muundo wa Kamusi
Kamusi imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni: Utangulizi, matini ya kamusi na Sherehe ya kamusi.

Utangulizi wa kamusi
Hii ni sehemu ya mwanzo ya kamusi ambayo hutangulia matini yenyewe ya kamusi. Utangulizi hujumuisha muhtasari wa sarufi ya lugha yenyewe pamoja na maelezo ya namna ya kuitumia kamusi. Utangulizi huonesha pia vifupisho vilivyotumika ndani ya kamusi na maana zake.

Matini ya kamusi
hii ni sehemu yenye vidahizo vyote vya kamusi husika kuanzia herufi ya alfabeti “A” hadi “Z”. Vidahizo vyote huorodheshwa hapa na kufafanuliwa. Taarifa mbalimbali za kiisimu huingizwa hapa. Taarifa hizo huhusu aina ya neno, maana (fasili) ya neno, vifupisho vya maneno, matumizi ya alama na vituo mbalimbali, matamshi, matumizi ya misemo, nahau, methali, n.k.
  • Kidahizo ni neno lolote linaloingizwa kwenye kamusi na kutolewa fasili yake.
Sherehe ya kamusi
Sehemu hii ya Kamusi huingiza baadhi ya taarifa za ziada zenye msaada kwa mtumiaji wa kamusi. Taarifa zinazoingizwa sehemu hii ni kama vile:
  • Majina ya nchi mbalimbali

  • Vyeo vya kijeshi

  • Vipimo mbalimbali vya urefu, ujazo, ukubwa, n.k.
Mpangilio wa maneno katika kamusi
Maneno yanayoingizwa katika kamusi nyingi hupangwa kwa utaratibu wa alfabeti. Maneno yanayoanza na herufi A, yote huwekwa chini ya herufi A. Vivyo hivyo kwa maneno yanayoanza na herufi b, ch, d hadi z. maneno yanayoanza na herufi fulani nayo hupangwa katika utaratibu wa alfabeti kwa kuzingatia herufi ya pili, ya tatu, nne au tano ya neno kama mfano unavyoonesha hapa chini:
Mfano: jabali, jabiri, jadhibika, jadi.
Maneno yote yanaanza na herufi [j]. Herufi ya pili kwa maneno yote ni [a]. Herufi ya tatu ni . Kwa kuwa  hutangulia [d] katika mpangilio wa alfabeti, maneno yenye  huorodheshwa kwanza kabla yay ale yenye [d]. Kwa vile maneno yenye  ni mawili itabidi tutazame herufi ya nne ya maneno hayo ili kuchagua neno litakaloorodheshwa mwanzo. Neno jabali litaorodheshwa kabla ya jabiri kwa kuwa [a] (herufi ya nne kwenye jabali hutangulia [i] ya jabiri ambayo pia ni herufi ya nne. Kasha tunatazama maneno yenye [d] kama herufi ya tatu. Hapa tunaangalia pia herufi ya nne ili kubaini neno litakaloandikwa mwanzo kati ya jadhibika na jadi. Kwa kuwa [h] hutangulia [i] basi jadhibika litaorodheshwa mwanzo na kufuatiwa na jadi.
Taarifa za Kikamusi
Kamusi za siku hizi huwa na taarifa zaidi ya maana. Miongozi mwa taarifa ambazo kamusi huwa nazo ni:

Kidahizo
Kidahizo ni neno linaloorodheshwa katika kamusi ili litolewe maana zake pamoja na taarifa nyinginezo. Katika kamusi, vidahizo vinaorodheshwa ki- alfabeti na huandikwa katika chapa iliyokolezwa wino.
Mfano
Ardhi nm 1. nchi kavu udongo

dunia
Fuska nm: tabia mbaya, hasa ya uasherati.

Vibadala
Kibadala ni kimoja kati ya maneno au zaidi yanayotofautiana kidogo kimaandishi na kimatamshi lakini yenye maana sawa. Maumbo au matamshi hayo tofauti hutumiwa na watu wa maeneo tofauti au wa lahaja tofauti za Kiswahili. Kwa mfano, neno benki hutumiwa zaidi Tanzania na banki hutumiwa zaidi Kenya. Kama vibadala viwili vitabainika vyote ni sanifu au vina matumizi mapana, maumbo yote mawili yanaingizwa katika kamusi kama vile “alimradi na ilimradi” nm, aminifu – Amini, amwali – amuali, amin – amini, n.k.

Misemo (ms), methali (mt) na nahau (nh)
Taarifa nyingine zinazoingizwa katika kamusi ni misemo, methali na nahau. Taarifa hizi zinawekwa baada ya fasihi au mifano ya matumizi katika chapa ya italiki. Semi hizi hutengwa na taarifa zilizotangulia kwa nukta mkato (Wink na kutanguliwa na alama (ms) kwa misemo, (mt) kwa methali na (nh) kwa nahau.
Mfano
Adimika kt [sie]: patikana kwa uchache au kwa nadra; ghibu; (ms) ume – kama wali wa daku.

Kitomeo
Kitomeo ni neno linaloingizwa katika kamusi kama kidahizo pamoja na taarifa zake zote kama vile kategoria, idadi, sinonimu, n.k.

Michoro
Kamusi huingiza michoro ya vitu mbalimbali. Lengo la michoro hiyo ni kusaidia fasili kuelezea maana ambazo hazieleweki kwa urahisi.

Orodha ya nchi na utaifa
Taarifa nyingine zinazoingizwa katika kamusi ni orodha ya nchi na utaifa. Lengo la orodha hiyo ni kuwasaidia wazungumzaji na watumiaji wa lugha kuwa na namna moja ya kutaja majina ya nchi na utaifa. Orodha hii inawekwa mwishoni kabisa mwa kamusi.

Tahajia ya neno
Tahajia ni uwasilishaji wa sauti kwa herufi katika maandishi kufuatana na mwendelezo wa maneno uliokubaliwa. Maneno katika kamusi yanaandikwa kufuatana na tahajia sanifu. Kwa yale maneno yenye tahajia zaidi ya moja, basi lahaja zote zinaoneshwa.

Matamshi ya Maneno
Kamusi huonesha namna ya kutamka maneno yanayoingizwa katika kamusi ili kumwelekeza mtumiaji wa kamusi jinsi yanavyotamkwa. Matamshi ya maneno huoneshwa kwa kutumia alama za kifonolojia ambazo huonesha herufi zinazounda neno.
Maneno ya Kiswahili yanaandikwa kama yanavyotamkwa kwa hiyo hayahitaji alama za kuonesha namna ya kuyatamka. Isitoshe haja ya kuwa na maelekezo ya matamshi ya maneno ni muhimu kwa wanafunzi wa Kiswahili, hususan wageni ambao hawakuzoea sauti fulani ambazo hazipo katika lugha zao. Kwa mfano, Kiingereza hakina sauti inayowakilishwa na umbo /ng/ kama inavyodhihirika katika neno /ngoma/ japokuwa wanalo umbo kama hilo ambalo hutamkwa kama /ng’/ ya neno /ng’ombe/ na /th/ za Kiswahili huwakilishwa na umbo moja tu katika Kiingereza.
Kwa hali hii ni dhahiri kuwa, maelezo ya namna ya kutamka maneno ya Kiswahili siyo muhimu kwa kamusi iliyolenga wenyeji wa Kiswahili kama ilivyo Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Kamusi inayotungwa mahususi kwa wageni haina budi kuonesha namna ya kutamka kwa usahihi yale maneno ambayo ni magumu kutamka. Maneno yasiyokuwa na shida kutamka ambayo kwa hakika ni mengi katika Kiswahili yasiyooneshwa, kwani itakuwa kujaza nafasi bure.

Sarufi ya lugha
Sarufi ya lugha kama inavyojitokeza katika kila neno kama vile maumbo ya wingi wa nomino, vinyambuo vya maneno kama vile lima, limia, limika, limisha, limwa, n.k. ambayo hutokana na kitenzi “Lima”

Maana za maneno
Kamusi huonesha maana za maneno. Maana hizi zinaelezwa kwa kutoa fasili (maelezo) pamoja na maneno mengine yenye maana sawa au zinazokaribiana, yaani sinonimu. Kimpangilio, fasili hutangulia na sinonimu hufuata.
Kidahizo chenye maana zaidi ya moja huoneshwa maana zake kuu kwa kutumia tarakimu 1,2,3, n.k. Pale ambapo maana kuu ina maana nyingine ndogondogo, maana hizo zinaoneshwa kwa kuwekewa alama (a), (b), ©, (d), n.k. au tarakimu.
Mfano
Fungo1 nm (ma) (a) muda wa kujinyima kwa hiyari chakula, maji na vinginevyo; muda wa kufunga. (b) namna ya kufunga © dhamana
Fungo2  nm dawa inayotengenezwa kwa mizizi ya ndago ambayo husaidia meno ya mtoto kuota yakiwa imara.
Fungo3 nm mnyama kama paka mwitu na mdogo kuliko ngawa.

Etimolojia ya neno
Kamusi huonesha etimolojia ya neno, yaani asili ya neno, mfano neno fulani asili yake ni kutoka nchi gani au lahaja gani.

Matumizi ya maneno
Kamusi huonesha matumizi mbalimbali ya maneno. Kwa kawaida, maneno mengi ya lugha hutumiwa katika nyanja mbalimbali. Hata hivyo, kuna baadhi ya maneno hutumika zaidi katika maeneo fulani maalumu, kama vile dini, fizikia, baiyolojia, ushairi au sarufi. Maneno kama haya hupewa alama maalumu kuonesha maneno yanamotumika zaidi.
Mfano:
Kwaresima nm (kd) siku arubaini za mfungo wa wakristo kabla ya sikukuu ya pasaka.
Yambiwa nm (sarufi) kipashio cha sentensi kinachodokeza mtendewa.
AINA ZA KAMUSI
Kwa kutumia kigezo cha dhima au lengo la kamusi kuna aina zifuatazo za kamusi:

Kamusi wahidiya
Hii ni kamusi inayoandikwa katika lugha moja tu, na inalengwa kwa wazungumzaji wazawa wa lugha hiyo. Wakati mwingine huwafaa wanaojifunza lugha hiyo kama lugha ya pili au ya kigeni. Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba, vidahizo vya kamusi wahidiya na maelezo ya maana ya vidahizo hivyo huwa katika lugha moja. Mfano wa kamusi wahidiya ni Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI iliyochapishwa mwaka 1981 na ile ya Oxford Advanced Learners Dictionary.

Kamusi thaniya
Hii ni kamusi iliyoandikwa kwa lugha mbili. Vidahizo huandikwa katika lugha moja (lugha chanzi) na maelezo ya maana ambayo aghalabu huwa neno moja, yaani visawe, huandikwa katika lugha ingine (lugha lengwa). Lengo la kamusi thaniya ni kumsaidia mtu anayefahamu lugha moja kati ya zilizotumiwa kujifunza lugha ingine, kuelewa matini anazosoma ambazo zimeandikwa katika lugha ya vidahizo vya kamusi na kumsaidia kujieleza vizuri hasa anapoandika katika lugha lengwa. Mifano ya kamusi thaniya ni kamusi za TUKI za mwaka 1996: Englisha – Swahili Dictionary,  Kamusi ya Kiswahili – Kiingereza, Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha (1990) na Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia

Kamusi mahuluti
Hii ni kamusi yenye lugha zaidi ya mbili. Ni kamusi iliyoandikwa kwa lugha nyingi. Vidahizo vya kamusi mahuluti hupatiwa visawe katika lugha mbili au zaidi.
Mfano
Kiswahili             Kiingereza           Kijerumani
nyumba nm             house                    haus
  mtoto nm                child                    kind
 kitabu nm                 book                    buch
  tembea kt                  walk                   laufen

Kamusi za kitaaluma
Hizi ni kamusi zinazoandikwa na wasomi ili zitumike katika uwanja fulani wa kitaaluma kama vile fizikia, kemia, biolojia, isimu, fasihi, n.k. Kamusi za aina hii huwa na maneno ya kitaaluma. Mfano wa kamusi za kitaaluma ni Kamusi Awali ya Sayansi na Teknolojia (1995), Kamusi ya Isimu na Lugha (1996), Kamusi ya Biolojia, Fizikia na Kemia (1996) Dictionary of Archaeology (1972).

Kamusi za semi
Kamusi za aina hii huwa na mkusanyiko wa semi kama vile nahau, methali, misemo, n.k. Kamusi hizi hueleza maana za semi mbalimbali na matumizi yake. Mfano wa kamusi za semi ni Kamusi ya Misemo na Nahau (2000) na Kamusi ya Methali (2001)

Kamusi za watoto
Hizi ni kamusi wanazotungiwa watoto, hasa katika madarasa ya chini. Sifa kubwa ya kamusi hizi ni wepesi wa maelezo na matumizi mengi ya picha. Mfano wa kamusi za watoto ni Kamusi ya Kwanza ya Kiswahili – Kiingereza

Kamusi za visawe
Hizi ni kamusi zenye kueleza maana za maneno kwa kutumia visawe vyake. Katika kamusi ya aina hii, neno kama vile ghilba huelezwa kwa visawe vyake kama vile uongo, ulaghai, hadaa, n.k.
Dhima ya kamusi
Kamusi ina umuhimu kwa mtumiaji yeyote wa lugha kwa sababu zifuatazo:
(a)  Kamusi huonesha tahajia (spellings) sahihi za maneno
(b) Kamusi hueleza maana (fasili) mbalimbali za maneno
©  Kamusi huonesha matamshi sahihi ya maneno
(d) Kamusi hubainisha aina (kategoria) ya neno
(e)  Kamusi huonesha misemo, semi, misimu na methali mbalimbali
(f)   Kamusi huonesha asili ya neno
(g)  Kamusi huonesha alama na vifupisho mbalimbali vya lugha
(h) Kamusi huongeza maarifa zaidi kuhusu lugha ya mzungumzaji
(i)    Kamusi husaidia kujifunza lugha za kigeni.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T17:28:12Z 2021-06-29T17:38:25Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=360 <![CDATA[TOLEO LA KWANZA LA KAMUSI YA KISWAHILI-KIINGEREZA]]> DIBAJI YA TOLEO LA KWANZA LA KAMUSI YA KISWAHILI-KIINGEREZA
Kamusi hii ya Kiswahili-Kiingereza ina historia ndefu. Wazo la kutunga kamusi hii ilianzishwa mwaka 1964 na Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili (ambacho kuanzia mwaka 1972 kilijulikana kama Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili). Wazo hili lilibuniwa wakati wa enzi ya Profesa Wilfred H.Whitely, ambaye wakati huo alikuwa ndiye Mkurugenzi wa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili, ikiwa ni miaka 25 baada ya kuchapishwa kwa kamusi ya Johnson ijulikanayo kama Standard Swahili-English Dictionary (1939). Kazi ya utunzi wa kamusi mpya ilianza baada ya shirika lijulikanalo kama Calouste Gulbenkian Foundation kutoa msaada wa pesa kwa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 1964 hadi Octoba 1967 ili kukiwezesha chuo kumwajiri mchunguzi atakayeweza kuifanya kazi hiyo.
Katika kutekeleza azma hiyo, Chuo kilimwazima Bwana J.A.Tejani kutoka Wizara ya Elimu Zanzibar na kumwajiri kama Mchunguzi. Bwana Tejani wakati huo alikuwa na shahada ya B.A. katika lugha za Kiarabu na Kiajemi ya Chuo Kikuu cha London, na alikuwa pia na ujuzi katika lugha za Kigujarati, Kiurdu na Kiswahili. Ilipangwa kuwa Mchunguzi Tejani angekuwa anasaidiwa na Mchunguzi Msaidizi na angeshauriwa na Miss M.A. Bryan wa School of Oriental and African Studies (SOAS), London Profesa E. Dammann wa Marbury na Profesa D.A. Olderogge wa Leningrad.
Bwana Tejani alipokuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili kati ya mwaka 1968 na 1969, aliendelea kuifanya kazi hii hadi mwaka 1970 alipoikabidhi kwa Mkurugenzi mpya wa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili, Bwana George Mhina. Mwaka 1967, kabla ya kuteuliwa kwa Mkurugenzi mpya, Baraza la Kiswahili la Taifa lilikielekeza Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili kuwa kamusi inayopaswa kuandaliwa mwanzo iwe kamusi ya Kiswahili-Kiswahili na wala sio kamusi ya Kiswahili-Kiingereza. Kwa hiyo mwaka 1970 kazi ya kwanza ya Mkurugenzi mpya, Bwana George Mhina, ilikuwa ni kuhakikisha kuwa vitomeo vyote vilivyomo katika kamusi ya Kiswahili-Kiingereza iliyoanzishwa na Tejani vinatafsiriwa upya katika Kiswahili. Mswada wa kamusi ya Kiswahili-Kiswahili ulikamilika Juni 4, 1978 na kamusi ikatoka mwaka 1981.
Mwaka 1972, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ilimpata mtaalamu wa kamusi kutoka Poland, Profesa Rajmund Ohly. Kwa kuanzia profesa huyu alipewa kazi ya kutunga kamusi ya Kiingereza-Kiswahili. Hata hivyo, mwaka 1975, Taasisi ilipounda jopo la wataalamu wa kamusi ili kukamilisha kazi ya kutunga kamusi ya Kiswahili-Kiswahili, Profesa Ohly alisitisha kazi ya kutunga kamusi ya Kiingereza-Kiswahili na kujiunga na jopo la kamusi ya Kiswahili-Kiswahili.
Baada ya kazi ya kutunga kamusi ya Kiswahili-Kiswahili kukamilika mwaka 1978, wachunguzi katika Sehemu ya Kamusi walirejelea kazi ya kutunga kamusi ya Kiingereza-Kiswahili aliyokuwa ameianza Profesa Ohly. Kamusi hiyo ilikamilika na kuchapishwa Desemba , 1996.
Baada ya utunzi wa kamusi za Kiswahili-Kiswahili na Kiingereza-Kiswahili kukamilika na miswada kuchapishwa, Sehemu ya Kamusi ya TUKI ilipata nafasi ya kuurejelea tena mradi wa Kiswahili-Kiingereza uliokuwa umeahirishwa tangu mwaka 1967. Kazi ya kuandaa mswada wa Kamusi hii ilianza rasmi Januari 1997 na jopo la kwanza lililopitia herufi A na B liliketi Machi 1997. Katika kuandaa kamusi ya Kiswahili-Kiingereza, wataalamu wa Sehemu ya Kamusi hawakutegemea kadi za maneno zilizotayarishwa na Bwana Tejani kama msingi wa kupatia vidahizo, bali walitegemea mswada wa toleo la pili la Kamusi ya Kiswahili Sanifu ambao wakati wa udurusu wake uliongezewa maneno mapya kutoka Kenya na Tanzania.
Utayarishaji wa mswada wa kamusi hii ulipitia hatua mbalimbali na kufanyiwa vikao vya jopo na vya uhariri nje ya kituo cha kazi ili kuharakisha ukamilishaji wake. Vikao hivyo vilifanyika huko Kibaha (1997), Moshi (Agosti, 1999), Morogoro (Juni, 2000), Tanga (Septemba, 2000) na Dar-es-Salaam (Desemba, 2000). Wanajopo walioshiriki katika utayarishaji wa muswada na kushiriki katika vikao vya jopo ni Profesa James S. Mdee, Profesa Hermus J. Mwansoko, Dkt. Albina R. Chuwa, Dkt. Eliezer K.F. Chiduo, Dkt. John G. Kiango na Dkt. Zubeida N. Tumbo-Masabo. Tunapenda pia kumtaja Dkt. George Mrikaria, kwa mchango alioutoa katika kazi ya uhariri wa mwisho wa kazi hii, na Bi Eiko Kimura wa ubalozi wa Japani kwa kutuunganisha na wanataaluma wa Chama cha Japan cha Taaluma za Kiafrika ambao wamechangia katika mradi huu.
Wakati wa harakati za utayarishaji wa kamusi hii, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili iliweza pia kuwashirikisha wazawa wa lugha ya Kiingereza katika hatua mbalimbali za uhariri. Tunapenda kutambua ushirikiano na mchango mzuri katika uhariri
uliofanywa na Mabwana Richard Mabala na Christopher Elkington. Tunapenda kutambua ushirikianao na mchango tulioupata kutoka kwa watu na makundi mbalimbali. Kwa kuwa hatuwezi kuwataja wote kwa majina, tunapenda kutoa
shukrani zetu za dhati kwa wote waliohusika. Hata hivyo, hatuna budi kutoa shukrani za pekee kwa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, hususan kwa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, Profesa Matthew L. Luhanga, ambaye pamoja na timu yake ya utawala wa Chuo, alihakikisha kuwa hatukwami katika utekelezaji wa kazi hii. Tunapenda pia kuwashukuru wanafanyakazi wote wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ambao wameshiriki kwa namna mbalimbali katika kukamilisha kazi hii.
Mwisho hatuna budi kumtaja Mkurugenzi Mstaafu wa TUKI, Profesa S.A.K.Mlacha, kwa kufanikisha utungaji wa kamusi hii. Yeye ndiye aliyekuwa msimamizi mkuu wa mradi huu tangu mwaka 1997. Taasisi inampongeza kwa jitihada zake alizozifanya katika kuhakikisha kamusi hii inachukua muda mfupi kukamilika. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili inapenda pia kuwashukuru wafadhili wetu waliotusaidia katika kuikamilisha kazi hii. Kwanza tunapenda kushukuru Shirika la Canadian Organization for Development in Education (CODE) East Africa, kwa kutupatia msaada wa karatasi. Pili, The Norwegian Council for Higher Education’s Programme for Development Research and Education (NUFU), kwa kutupatia kompyuta na kufadhili gharama za vikao vya jopo la kamusi. Tatu, Profesa Hino Shungya pamoja na wanataaluma na maprofesa wenzake wa Chama cha Japan cha Taaluma za Kiafrika na Kampuni ya uchapishaji ya Kijapan Kodansha Ltd, kwa michango yao waliyoitoa kwa moyo mkunjufu kwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ili kufanikisha uchapishaji wa kamusi hii. Michango yao imesaidia sana siyo tu katika kuikamilisha kamusi hii, bali pia katika kukienzi na kukiendeleza Kiswahili, na pia kuendeleza urafiki uliopo baina ya Tanzania na Japan. Kuchapishwa kwa kamusi hii kunakamilisha seti ya kamusi za Kiswahili. Kwa sasa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili imechapisha Kamusi ya Kiswahili Sanifu (1981), Kamusi ya Kiingereza-Kiswahili (1996) na Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza(2001). Ni matumaini yetu kuwa kamusi zote tatu zitawanufaisha wasomaji wetu, na kuwa zitakuwa hazina bora ya lugha ya Kiswahili.
Profesa M.M. MulokoziMachi, 2001 Mkurugenzi
 BOFYA HAPA KUINGIA KWENYE KAMUZI &t&t&t&t&t&t&t]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T17:12:22Z 2021-06-29T17:12:22Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=359 <![CDATA[KAMUSI NA URAFIKI WAKE KWA MTUMIAJI]]> Usuli wa Wa mada. Lengo la makala haya ni kuangazia maana, aina na sababu zinzojenga urafiki wa msomaji na kamusi husika.
Masogora wa lugha hukubaliana kuwa Kamusi ni kitabu chenye mkusanyiko na mpangilio sahihi wa msamiati wa lugha uliofasiliwa maana zake kwa ufasaha kwa ajili ya kuwasaidia watumia lugha husika kuwasiliana kila leo. BAKIZA (2010)TUKI, (2013) Mdee ( 2011) Massamba (2013)
Kihistoria utengenezaji wa kamusi ulianza siku nyingi yasemekana miaka ya 1600 huko Ulaya hasa katika nchi ya Mesopotamia (sasa Iraq).
Utunzi huo wa kamusi ulianza kwa mtindo wa faharasa (orodha ya maneno magumu katika lugha na maana zake) ambapo mwingiliano wa kiiraq na kilatini pamoja na ligha zingine za huko ulaya ulisababisha wanajamii wa Mesopotamia waanze kuichambua misamiati yote ya kilatini na kutafutia maana zake.
Harakati hizo za kutengeza faharasa zilimea si tu katika Mesopotamia bali hata katika jamii nyingine za ulaya uingereza ikiwemo huku zikisaidia kujifunza lugha za kigeni kwa wanajamii.
Kfikia karne ya kumi na saba sura ya faharasa ilianza kubadilika na kuwa katika mfumo wa maneno mchanganuiko yaani maneno magumu na yale ya kawaida hasa misimu.
Kamusi ya kwanza kujumuisha msamiati wa mtaani na ule mgumu iliandikwa na bw. Johnson (1755), Kessy (1702) na wanaleksigrafia wengine wa kiingereza walifuatia hasa kwa kuziba mapengo ya kamusi hizo za awali kuandikwa.
AINA ZA KAMUSI
Katika kuainisha Kamusi wanaisimu leksikografia hutumia vigezo mbali mbali kama ionekanavyo hapo chini;

Kigezo cha lugha zilizotumika kuunda kamusi husika. Hapa zipo kamusi za lugha moja na huitwa Wahidiya, za lugha mbili huitwa tathirita mfano Kiswahilo- Kingereza na zile za lugha zaidi ya mbili huitwa kamusi Mahuluti.
Kigezo cha ukubwa zipo kamusi au makundi matatu ya kamusi yaani Kamusi ndogo huwa na maneno yasiyozidi 100000. Kamusi ya kati huwa na vidahizo si zaidi ya 25000 na Kamusi kubwa ni ile yenye vidahizo zaidi ya 50000.
Kwa hakika vigezo ni vingi kv uwanja wa taaluma, walengwa na wakati ilipotungwa.
SABABU ZINAZOIFANYA KAMUSI IWE NA WASOMAJI WENGI.
1. Uwepo wa taarifa muhimu zinazokidhi haja ya Wasomaji.
2. Fasili za vidahizo kutokuwa za mzunguko kiasi cha kumchosha msomaji.
3. Uwepo wa vielelezo k.v picha , grafu na ramani zinazojazia maelezo ya vidaizo katika kamusi ua lugha husika.
4. Kamusi kuandaliwa na wanasayansi wa lugha wakishirikiana na wadau mbali mbali k.v wanajamii na wahariri nguli wa lugha.
5. Kamusi kuwa na aina na makundi tofauti tofauti ya vidahizo okiwemo maneno ya mtaani.
Hata hivyo pamoja na sifa hizo bora za kamusi bado ipo changamoto kubwa hasa kwa waandoshi wa kamusi ambao huandika kwa lengo la kuhifadhi lugha lskini pia kwa ajili ya kujipatia mkate hivyo kutokana na jamii kutokuwa na utamaduni wa kusoma mssndiko hasa vitabu na kamusi waandishii hukata tamaa na hivyo kuacha kuunda kamusi. Halii hii hufisha lugha na utamaduni kwa ujumla.
MAREJEO:
BAKIZA 2010

KAMUSI YA KISWAHILI SANIFU 2012 TUKI
Mdee, J.S, 2011. Nadharia ya lekskografia
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T11:54:07Z 2021-06-29T11:54:07Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=358 <![CDATA[TUJIFUNZE KISWAHILI MAANA KINAKUA KWA KASI]]> 1. Charger – kimemeshi
2. Remote – kitenzambali
3. Password – nywila
4. Akala (bladder shoes) – kirikiri
5. Passion fruit – karakara
6. Kangaroo – bukunyika
7. Fridge – jokofu
8. Juice – sharubati
9. Chips – vibanzi
10. PHD – uzamivu
11. Masters degree – uzamili
12. Degree – shahada
13. Diploma – Stashahada
14. Certificate – Cheti
15. Keyboard – kicharazio/baobonye
16. Scanner – mdaki
17. Flash disk – diski mweko
18. Mouse (for a computer) – kiteuzi
19. Floppy disk – diski tepetevu
20. Computer virus – mtaliga
21. Distillation – ukenekaji
22. Evaporation – mvukizo
23. Synthesis – uoanishaji
24. Oesophagus – umio
25. Greenhouse – kivungulio
26. Femur – fupaja
27. Germ cell – selizazi
28. Humus – mboji
29. Nector – mbochi/ntwe
30. Nutrients – virutubisho
31. Crystal – fuwele
32. Appetizers – vihamuzi
33. ATM – kiotomotela
34. Business card – kadikazi
35. Scratch card – kadi hela
36. Simcard – kadiwia/mkamimo
37. Memory card – kadi sakima
38. Microwave – tanuri ya miale
39. Mobile phone – rununu/rukono
40. Stapler – kibanizi
41. Laptop – kipakatalishi
42. Power saw – msumeno oto
43. Duplicating machine – kirudufu
44. Photocopier – kinukuzi
45. Cocktail party – tafrija mchapulo
46. Air conditioner – kiyoyozi
47. Calculator – kikokotozi
48. Lift – kambarau
49. Reaction-radiamali
50. Toothpick-kimbaka

51. Browser – Kisakuzi

]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T11:45:22Z 2021-06-29T11:45:22Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=357 <![CDATA[MAANA ZA NENO KOJA]]>

NOMINO wingi makoja
  • 1
    mtungo mrefu wa maua avishwao mtu kama zawadi au pambo.

Ufafanuzi msingi wa koja katika Kiswahili
koja2


NOMINO wingi makoja
  • 1
    aina ya sufuria ya bati.

Matamshi
koja
/kOʄa/]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T11:36:06Z 2021-06-29T11:36:06Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=356 <![CDATA[Vidahizo vya Fani ya Sayansi]]>
Aa
alijebra ji algebra: hesabu zinazotumia tarakimu na herufi.
alikoholi ji alcohol: kioevu safi kisicho na rangi kwenye vinywaji visivyolevya. Mfano: bia, mvinyo, n.k., ambavyo hutokana na mkeneko wa matunda, mboga, n.k.
anatomia ji anatomy: elimu ya muundo wa seli na viungo mbalimbali katika miili ya viumbe.
antiseptiki ji antiseptic: aina ya kemikali inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha, ngozi, n.k., sabuni za kaboli.
atomu ji atom: sehemu ndogo kuliko zote ya elementi ambayo bado inaonyesha tabia za kikemikali za elementi hiyo.
Bb
badiliko kikemikali ji chemical change: badiliko linalotokea katika dutu kwa kubadilisha muundo wa kemikali kwa njia ya kuongeza, kupunguza au kupanga upya atomu katika molekuli za dutu hiyo.
badiliko la kiumbo ji physical change: badiliko katika kitu ambalo ni la umbo tu na sio la kikemikali, k.m., kuganda kwa maji na kuwa barafu.
bakteria ji bacteria: viumbe hai vidogo sana visivyoonekana kwa macho ila kwa hadubini ambavyo baadhi yake husababisha magonjwa kwa wanyama na mimea na baadhi yake husaidia kurutubusha ardhi.
bakteriolojia ji bacteriology: elimu ya sayansi ya bakteria, yaani, viumbe hai vidogo sana visivyoonekana kwa macho ila kwa hadubihi ambavyo baadhi yake husababisha magonjwa kwa wanyama na mimea na baadhi husaidia kurutubisha ardhi.
barometa ji barometer: chombo cha kupimia kanieneo ya angahewa.
barometa
biolojia ji biology: elimu ya asili na miundo yote ya viumbe hai.
botania ji botany: elimu ya sayansi ya mimea.
brasi ji brass: mchanganyiko wa shaba na zinki.
bronzi ji bronze: metali ngumu ambayo ni mchanganyiko wa shaba na bati.
Dd
duaradufu ji ellipse: umbo linalofanana na yai.
duara katipande ji eccentric circles: duara zenye kitovu zaidi ya kimoja.
duara katipande
Ee
elementi kemikali ji chemical element: elementi yoyote yenye tabia ya kikemikali.
erio kv aerial: -a hewani, k.m., mizizi hewa (aerial roots), yaani, mizizi inayoota kutoka sehemu za mmea zilizo hewani.
Ff
famasia ji pharmacy: elimu tanzu ya tiba inayohusika na mafunzo au uchunguzi unaohusiana na utayarishaji na utoaji wa madawa na vitibiaji.
fiziolojia ji physiology: elimu inayochunguza jinsi miili ya viumbe inavyofanya kazi.
fokasi ji focus: nukta ambapo mionzi sambamba ya nuru hukutana.
fomula ji formula: njia ya kuandika maelezo ya kihisabati, n.k., kwa kutumia herufi, namba, na alama.
fumbatio ji abdomen: sehemu ya mwili wa kiumbe iliyoko chini ya kifua, ambayo hujumuisha vitu kama utumbo, figo, ini na tumbo.
fyonza ji absorb: nyonya kitu chenye maji.
Gg
giligili ji fluid: kioevu au gesi ya aina yoyote yenye uwezo wa kutiririka.
gimba ji body: umbo la kitu au mtu lionyeshalo mjengo, unene, au ukubwa.
glukosi ji glucose: aina ya sukari isiyokuwa na rangi na hupatikana kwenye asali na matunda matamu.
Hh
hidragiri ji mercury: metali pekee ambayo ni kioevu katika halijoto ya kawaida.
Ii
isometali kv non-metallic: isiyo na tabia ya kimetali.
Kk
kaboni ji carbon: elementi yenye namba atomu 6.
kiashirio ji indicator: dutu inayoonyesha kuwepo kwa asidi au alikali.
kimumunyishaji ji solvent: kitu, aghalabu kioevu, chenye uwezo wa kumumunyisha vitu vingine ndani yake.
kiuavijasumu ji antibiotic: kemikali iundwayo na vijiumbe kama kuvu na bakteria ambayo yaweza kuangamiza backteria au virusi, au kuzuia ukuaji wake, k.m., penisilini, tetrasaiklini, kloramfenikoli.
kizio ji unit: namba ambayo kwayo namba nyingi huhesabiwa.
kupri ji copper: metali yenye rangi kama dhahabu inayotumika zaidi katika kutengeneza nyaya za umeme.
kipukusi ji disinfectant: kemikali inayotumika kuzuia au kuua viini vya maradhi, k.m. deta.
kutomea tumba kt budding: kuunganisha mmea kutoka kwenye mmea wa mti wa jamii moja hadi nyingine, k.m., mchungwa na mdimu.
Ll
lenzi ji lens: kipande cha glasi au dutu nyingine yenye uso pinde inayopitisha mwanga.
Mm
madini ji mineral: kitu kinachochimbwa ardhini kama vile shaba, risasi, mafuta, chumvi, n.k.
maji laini ji soft water: maji yanayotoa povu mara moja kwa sabuni.
maji mkeneko ji distilled water: maji yaliyopatikana na kupoza mvuke maji.
mangisha kt solidify: badilisha hali ya uoevu na kuingiza hali ya umango.
masi ji mass: kiasi cha kitu bila umbo maalumu.
maunzi ji material: chochote ambacho kutokana nacho kitu kingine hutengenezwa.
metali ji metal: dutu, aghalabu mango, kama vile chuma, bati, shaba, dhahabu, zebaki, alumini, n.k.
mfumo meta ji metric system: mfumo wa vipimo unaotumia vizio msingi vya meta, kilogramu na sekunde.
mmumunyo ji solution: tokeo la kuchanganya kimumunyishwaji na kimumunyishaji.
mnato ji viscosity: muelekeo wa mmiminiko kunata au kukataa kujimiminisha au kumwagika taratibu sana.
mnyeso ji secretion: hali ya kutoa utomvu au kioevu au umajimaji kama kimiminiko kutoka kwenye tishu au tezi, k.m., kutoa mate, machozi, maziwa, utomvu, n.k.
mnyweo ji contraction: hali ya kupungua hasa kutokana na mshuko wa halijoto.
molekuli ji molecule: chembe ndogo sana ya msombo inayoweza kushiriki katika mbadiliko kikemikali.
mvukizo ji evaporation: mgeuzo wa kioevu kuwa mvuke bila kulazimika kufikia kiwango mchemko.
mvutano ji gravity: hali ya vitu kuvutana kiasili, k.m., kati ya dunia na jua. Kani inayovuta vitu chini na kuvileta kwenye uso wa dunia.
mzingo ji circumference: mzungumo wa nje wa duara.
mzio ji allergy: hali ya kudhuriwa kwa baadhi ya watu wanapokula vyakula fulani au wanapogusa au kunusa vitu fulani kama vile chavua.
Oo
oksijeni ji oxygen: gesi safi inayotumiwa na viumbe hai. Alama yake ni O1; fomula yake ni O2.
Pp
patholojia ji pathology: elimu ambayo inachunguza asili na matokeo ya magonjwa ya wanyama na mimea.
Ss
sanjari ji series: aina ya mpangilio ambapo vitu vinapangwa kwa kufuatana kimoja nyuma ya kingine.
saruji magnesia ji magnesia cement: aina ya saruji inayotumika katika tiba, kwa mfano, kufunga kuhara; na katika viwanda.
saruji meno ji dental cement: aina ya saruji inayotumika kwa matibabu ya meno.
sayansi ji science: elimu inayotokana na uchunguzi, majaribio, vipimo na kuthibitishwa kwa muda uliopo.
sayari ji planet: magimba makubwa yenye umbo mduara yanayolizunguka jua na ambayo yenyewe hayatoi nuru bali huonekana tu kwa kuakisi nuru ya jua.
seli ji cell: chanzo cha asili ya umbile la kiumbe na shughuli zote za kifiziolojia katika kila kiumbe hai.
selulosi ji cellulose: aina ya kabohidrati itokanayo na sukari ya glukosi ambayo hupatikana katika kuta za seli za mimea.
silika ji silica: muungano wa oksijeni na silikoni upakatikanao kiasili kama mchanga na hutumika kutengenezea kioo.
silikoni ji silicon: elementi kijivu isiyo metali inayofanana na kaboni hasa hupatikana katika hali ya msombo.
sumaku ji magnet: nguvu inayoweza kuvuta vyuma au vitu vyenye asili ya chuma.
Tt
teknolojia ji teknology: utumiaji wa maarifa tupatayo kutokana na sayansi ili kutengeneza vitu viwandani, kujenga vitu, n.k.
tishu ji tissue: kundi la seli za aina moja zinazofanya kazi maalumu mwilini.
tohoa kt adapt: badilisha matamshi au maendelezo ya neno la lugha ya kigeni ili lilingane na matamshi au maendeleo ya lugha ya kienyeji, k.m., shirt (Kiingereza) kuwa shati (Kiswahili).
Uu
ukenekaji ji distillation: tendo la kugeuza kioevu kiwe mvuke, kisha kuutonesha huo mvuke uwe kioevu na kukusanya kioevu hicho.
ukifishwaji ji saturation: kuwepo kwa kitu, aghalabu kimumunyishwaji katika ukolezi wa juu kabisa kiasi kwamba uongezapo kimumunyishwaji zaidi hakimumunyiki tena.
Vv
vena ji vein: mshipa unaorudisha damu chafu kwenye moyo kutoka sehemu mbalimbali za mwili.
virusi ji virus: vijiumbe hai ambavyo kimaumbile havijafikia hata ngazi ya seli bali vipo katika ngazi za molekuli kubwa za protini, ambavyo huweza kuzaana tu vikiwa vinaishi kwenye seli za viumbe wenye uhai.
Zz
zindiko ji antibody: aina ya protini inayotengenezwa mwilini ili kukinga mwili na mashambulizi ya viini vya maradhi.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T11:15:21Z 2021-06-29T11:15:21Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=355 <![CDATA[Vidahizo vya Fani ya Sayansi Kimu]]> Vidahizo vya Fani ya Sayansi Kimu
Aa
asidi jani ji folic acid: aina ya vitamini B ipatikanayo katika majani inayotumika kutibu upungufu wa damu (anemia)
asidi nikotini ji nicotinic acid: asidi inayosaidia usanisi na uyeyushaji wa sukari. Hupatikana katika nyama, samaki na karanga.
Bb
beriberi ji beriberi: ugonjwa unaotokana na ukosefu wa vitamini B1 ambapo neva husika hazifanyi kazi, hasa miguuni, na mtu hushindwa kutembea.
biokemia ji biochemistry: kemia inayohusu viumbehai.
bwana/bibi shamba ji extension worker: mshauri wa kilimo anayetoa ushauri kwa wakulima kitaalamu.
Cc
choo sanifu ji improved pit latrine: aina ya choo cha shimo chenye fursa ya bomba la kutolea harufu.
chuma ji iron: 1. madini ambayo ni muhimu mwilini kwa ajili ya kutengeneza damu. Hupatikana katika maini, figo, nyama, samaki, karanga, matembele, n.k. 2. metali ngumu inayotumiwa kuunda vitu, k.m., mashine, ngao, nondo, pao, injini, n.k.
Dd
daktari wa akili ji psychiatrist: mganga wa magonjwa ya kuharibikiwa na akili.
dawachanjo ji vaccination: dawa ya kuchanja, mara nyingi ni sumu au vimelea vilivyotenguliwa nguvu. Dawa hii hutengeneza kinga kwa magonjwa kama vile ya ndui, polio, pepopunda, kifaduro, n.k.
Ee
elimuafya ji health education: mchakato wa kupatiwa mafunzo ili kuendeleza na kustawisha siha.
elimulishe ji nutrition education: mchakato wa kupatiwa mafunzo ili kuendeleza lishe (chakula bora).
elimusiha ji hygiene: sayansi inayohusika na usafi wa mwili na makazi.
Ff
florini ji fluorine: madini yaliyo kundi moja na klorini, nayo ni sumu kali yenye rangi njanokijani. Husaidia kutakasa meno na kuyakinga na uozaji. Ziada ya madini haya majini husababisha meno kuwa na rangi ya kutu (meno mshuku)
fotoksini ji photoxin: sumu ya kufukiza inayotumiwa katika maghala yasiyopitisha hewa ili kuua wadudu.
fukusi ji weevil: aina ya wadudu wadogo ambao hushambulia nafaka na kundekunde.

fukuzi
Gg
ghalabanda ji corn maize crib: aina ya ghala inayojengwa kama banda ili kuhifadhi nafaka.

ghalabanda
Hh
hadubini ji microscope: chombo chenye lenzi inayofanya vitu vidogo sana vionekane vikubwa.

hadubini
haiba ji personality: hali ya umbo na matendo ambayo mtu humtambulisha na kumpambanua na wengine.
hamira ji yeast: dutu inayofanya unga uliokandwa uumke (chachu).
Ii
idadi ya watu ji population: makisio ya jumla ya watu katika eneo au nchi.
iodini ji iodine: madini yanayosaidia tezi za koromeo kufanya kazi yake ya kurekebisha mataboli mwilini.
Jj
jikosanifu ji sandard cooker: jiko lililotengenezwa kwa bati, udongo wa mfmyanzi na mchanga; nalo hupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

jikosanifu
jungu ji big pot: chombo cha kuhifadhia nafaka, nacho hutengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi.

jungu
Kk
kabohidrati ji carbohydrate: kirutubisho cha kuleta joto na kutia nguvu mwilini kinachopatikana katika uwanga, sukari, selulosi, n.k.
kadhiasabababishi ji causal factors: jambo linaloleta mchakato wenye athari (matokeo) fulani. Kwa mfano, ukosefu wa vitamini, protini, kabohidrati ni kadhiasababishi za utapiamlo.
kadi ya afya ji health card: kadi maalumu ya kliniki inayotumika kuonyesha maendeleo ya afya ya mtoto.
kalisiamu ji calicium: madini laini nyeupe yenye alama Ca. Madini hii husaidia kujenga meno na mifupa, na hupatikana kwa uwingi katika maziwa.
kano ji ligament: nyuzi zenye nguvu zilizo katika minofu ya mwili.
karantini ji quarantine: hali ya kuzuiliwa kwa watu, mifugo, au mimea ili kuepukana na ugonjwa wa kuambukiza.
kansa ji cancer: ugonjwa unaotambulika kama kitu cha sumu kinachoota kwa ndani katika sehemu ya mwili, kama vile mguuni, katika ziwa la mwanamke, tumboni n.k.
kemia ji chemistry: sayansi inayohusu muundo wa vitu na jinsi vinavyoathiriana.
kemia lishe ji food chemistry: kemia inayotathmini vimtubisho vya chakula.
kemia tiba ji clinical chemistry: kemia inayohusiana na utengenezaji dawa za kutibu magonjwa.
kifukuzi ji repellant: dawa inayowafanya wanyama, hasa wadudu, wakimbie kutoka mahali ilipofukizwa.
kibenge ji aina ya ghala ya mviringo iliyojengwa kwa miti na kuzibwa kwa fito au kwa kusuka mianzi au nyasi.
kibenge
kijongozi ji seamer: chombo au mashine inayoshona vipande vya ngozi, nguo au plastiki.
kilimo ji agriculture: shughuli za kutayarisha ardhi, kustawisha mimea, na ufugaji.
kilimo cha kisasa ji modern agriculture: kilimo cha kutumia mashine na pembejeo.
kilimo cha umwagiliaji ji irrigation farming: kilimo cha kutumia maji ya mifereji na mabomba.
kilimojadi ji traditional farming: kilimo cha kutumia zana za mikono.
kilindo ji chombo cha kuhifadhia nafaka mfano wa pipa ambalo hutengenezwa kwa kutumia magamba ya miti.
kinga ji immunity: hali ya asili ya kiumbe ambayo humwezesha kujikinga na maradhi hasa ya kuambukiza.
kirutubisho ji nutrient: kemikali au kiini chakula kinachosaidia kuimarisha mwili. Virutubisho hujenga mwili, huupatia nguvu na joto, na kuulinda.
kiseyeye ji scurvy: ugonjwa wa fizi au meno unaotokana na ukosefu wa vitanuni C.
kitamizi ji incubator: mashine ya kutia fukuto mayai mpaka kutotoa vifaranga.
kituo cha afya ji health centre: mahali ambako watu huenda kwa madhumuni ya kupata matibabu; kuchunguzwa afya zao; na kupatiwa ushauri wa matibabu na waganga.
kituo cha kutunzia watoto ji day care centre: mahali pa kuwaweka watoto wadogo wakati wa mchana, wazazi wao wakiwa kazini.
kiuamchwa ji chlorodame: sumu ya kuulia mchwa. Sumu nyingine ni aldrin na dieldrin.
kiuapanya ji rodenticide: sumu ya kuulia panya.
kiua wadudu ji insecticide: kitu kitumikacho kuulia wadudu. Viuawadudu vipo vya aina kubwa tatu: vya tumboni, vya kugusana, na vya kufukiza.
kliniki ji clinic: kituo cha wagonjwa wa nje kitumikacho kwa ajili ya kufanyia uchunguzi na matibabu maalumu.
Ll
laza kt admit: pokea na weka mgonjwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
lishe ji nutrition: sayansi inayohusu chakula na tathmini ya virutubisho mwilini.
Mm
maabara ji laboratory: chumba au jengo la kufanya uchunguzi na majaribio ya kisayansi.
madini ji minerals: virutubisho ambavyo husaidia mwili kutengeneza damu na kujenga mifupa, meno, na kucha.
mafuta madini ji mineral oil: mafuta yanayotokana na madini. Ni tofauti na yale yanayotokana na mimea au wanyama.
maji madini ji mineral water: maji ya chemchemi yenye madini mbalimbali.
malathioni ji malathion: aina ya sumu ya unga inayotumika kuhifadhi mtama ulioputwa.
matege ji rickets: ugonjwa wa kupinda miguu unaowapata watoto wadogo kutokana na ukosefu wa vitamuni D.
mazao ji crops: mavuno yanayotokana na mimea iliyopandwa.
mazao ya biashara ji cash crops: mavuno yanayouzwa ili kujipatia fedha, kama vile, pamba, kahawa, mkonge, korosho, n.k.
mazao ya chakula ji food crops: mavuno yanayotumika kwa chakula, kama vile mahindi, muhogo, mpunga, n.k.
mazao ya ukame ji drought resistant crops: mimea isiyohitaji maji mengi ili kukua, kama vile, mtama, uwele, ulezi na mihogo.
mbawakawa ji beetle: mmojawapo ya aina nyingi za wadudu wenye mbawa ngumu.

mbawakawa
mboji ji humus: mbolea yenye rangi nyeusi ambayo imetokana na kuoza kwa viumbe, (k.m., majani, wadudu, wanyama, n.k.).
mbolea asilia ji natural fertilizer: aina ya rutuba ya udongo inayotokana na samadi au mboji.
mbolea kemikali ji chemical fertilizer: aina ya rutuba ya udongo inayotengenezwa kiwandani.
mchachuko ji fermentation: mbadiliko wa kikemikali unaotokea kwenye dutu za kikaboni kwa kutendana na viumbe hai kama chachu, bakteria, n.k., kwa utendano uliosababishwa na vimeng’enya vyake.
meno awali ji milk teeth: seti ya mwanzo ya meno ya wanyama wa ngeli mamalia ambayo baadaye hung’oka yote na yakaota meno ya kudumu.
metaboli ji metabolism: hali ya jumla inayohusika na ujenzi na uvunjajivunjaji wa kemikali mwilini.
mjamzito ji expectant mother: mwanamke mwenye mimba.
mkunga wa jadi ji traditional midwife: mama anayezalisha wajawazito, hususan vijijini.
mlo kamili ji balanced diet: chakula chenye aina zote za virutubisho.
msaada wa kwanza ji first aid: huduma ya awali anayopata mtu aliyefikwa na matatizo ya ghafla ya afya kabla hajapelekwa hospitalini.
msuli ji muscle: mkusanyiko wa nyuzi za kano au kono za nyama ndani ya mwili wa baadhi ya viumbe.
Nn
nafaka ji cereal: vyakula vya punjepunje kama vile mtama, mpunga, mahindi, mawele, ngano, n.k.
neva ji nerve: mshipa wa fahamu ambao hupokea na kupeleka habari kati ya ubongo na sehemu nyingine za mwili.
njiti ji premature baby: mtoto aliyezaliwa kabla ya miezi tisa.
nyongea ji marasmus: maradhi yanayowakabili watoto wenye umri chini ya miaka mitano yanayotokana na ukosefu wa virutubisho vya kutia nguvu mwilini, hasa mafuta na uwanga.
nyonyochupa ji formula feeding: utaratibu wa kumnyonyesha mtoto maziwa ya unga yaliyokorogwa au maziwa mabichi yaliyochemshwa ya ng’ombe, mbuzi, n.k.
nyonyotiti ji breast feeding: utaratibu wa kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama yake.
Oo
opoa ji resuscitate: rejeshea mtu fahamu zake.
Pp
pareto ji pyrethrum: aina ya maua yanayotumika kutengeneza sumu itumikayo kunyunyizwa kwenye maharagwe ua mazao mengine ili kuua wadudu.
pelagra ji pellagra: ugonjwa unaotokana na ukosefu wa vitamini B7, na husababisha ngozi ya mwili kubabuka.
pembejeo za kilimo ji agricultural inputs: mahitaji muhimu katika kufanikisha kilimo ikiwa ni pamoja na zana za kilimo; mbolea, sumu za kuulia wadudu, maji na utaalamu.
protini ji protein: kirutubisho cha kujenga mwili kinachopatikana katika nyama, ute wa yai, samaki, n.k. ambacho ni mchanganyiko wa kaboni, hidrojeni, oksijeni, chuma, n.k.
protini mimea ji plant protein: virutubisho vyenye kujenga mwili vinavyopatikana kutokana na mimea ambavyo kwa kawaida sio kamili.
protini nyama ji animal protein: virutubisho vyenye kujenga mwili vinavyopatikana kutokana na kula vyakula vya nyama mbalimbali.
Rr
riboflavini B2 ji riboflavin B2: vitamini ambayo husaidia kuzipa seli za mwili nguvu, nayo hupatikana kwenye maharagwe, nyama, samaki, maziwa na mboga.
rovu ji goitre: ugonjwa wa kuvimba tezi la shingo unaosababishwa na ukosefu wa iodini.
Ss
sayanslmelea ji parasitology: sayansi ya uchunguzi wa vimelea.
shigiti ji storage bin for shelled maize: ghala linalotengenezwa kwa matete yaliyosukwa na kuinuliwa kutoka chini ya ardhi kwa mihimili mifupi.

shigiti
supu ji soup: chakula cha majimaji kinachotayarishwa kwa kuchemsha nyama, samaki, mboga, n.k.
Tt
tezi ji gland: sehemu ya mwili inayotengenezwa na kuhifadhi kemikali ambayo huchukuliwa na damu, na kuleta mabadiliko fulanifulani mwilini.
thiamini B1 ji thiamine B1: vitamini inayozuia beriberi; nayo hupatikana katika maharagwe, samaki, nafaka, n.k.
tibalishe ji nutritionai rehabilitation: marekebisho ya afya za watoto walioathiriwa na utapiamlo.
Uu
uachishaji ji weaning: utaratibu wa kumzoesha mtoto chakula cha ziada mbali ya maziwa ya mama.
uchambuzi ji analysis: upembuzi au upambanuzi.
uchanja ji mahali pa juu palipojengwa kwa miti kwa ajili ya kuwekea vitu aghalabu vyombo au chakula.
uchuzaji ji observation: udadisi wajambo kwa makini makubwa ili kujua undani wake.
udumavu ji growth retardation: hali ya kuvia kwa mwili na akili.
ulajimimea ji phytophagy: tabia ya viumbe kuishi kwa kula mimea.
ukame ji drought: hali ya jua kali na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu hadi husababisha mazao, watu na wanyama kufa kwa njaa. Baadhi ya mazao, kama vile, mtama, uwele na mhogo yanahimili ukame.
umeng’enyaji ji digestion: uvunjaji wa chakula mwilini kwa kutumia kimeng’enya maalum.
unga wa kuokea ji baking powder: unga ambao ukipashwa moto au ukilowanishwa huunda viputo vya hewa (k.m., katika unga wa ngano) ili kuufanya uumke.
unyafuzi ji kwashiokor: ugonjwa wa watoto walio chini ya umri wa miaka minne unaotokana na ukosefu wa virutubisho vya aina ya protini katika mlo.
upofu usiku ji night blindness: ugonjwa utokanao na ukosefu wa vitamini A ambao humsababisha mtu kushindwa kuona vizuri usiku au kwenye gizagiza.
usafi mazingira ji environmental sanitation: uwekaji wa mazingira katika hali safi ili kuepuka madhara mbalimbali.
ushauri ji counselling: utaratibu wa kumpa mtu rai au nasaha kuhusu jambo linalomtatiza ili apate muelekeo wa kufana katika kuamua hatua ya kuchukua.
utapiamlo ji malnutrition: ukosefu wa lishe bora usababishao mwili kushindwa kuhimili magonjwa.
uvutishaji hewa ji artificial respiration: kitendo cha kumsaidia mtu aweze kupumua tena kwa kumpulizia hewa mapafuni kupitia puani na mdomoni.
uwanga ji starch: kabohidrati inayoupatia mwili joto na nguvu. Vyakula vya uwanga ni mhogo, viazi, mkate, ugali, wali, keki, n.k.
uzazi wa mpango ji family planning: utaratibu wa kuzaa watoto kwa kuacha muda wa kutosha kati ya mtoto mmoja na mwingine.
Vv
vitamini ji vitamin: virutubisho mbalimbali vya kulinda mwili dhidi ya magonjwa na kuusaidia ukue. Vitamini huitwa kwa alfabeti A, B, C, D, E, G, H, K, n.k.
vitamini A ji vitamin A: aina ya vitamini inayosaidia macho kuona vizuri, huratibu misuli ya moyo, na huifanya ngozi kuwa laini. Hupatikana kwa wingi katika vyakula vya asili ya maziwa, maini, matunda na mboga.
vitamini bandia ji artificial vitamin: vitamini zilizotengenezwa ambazo si asilia.
vitamini C ji vitamin C/assorbic acid: aina ya vitamini inayosaidia kuponyesha vidonda; na kupatikana katika matunda na mboga.
vitamini D ji vitamin D: vitamini inayosaidia kukuza mifupa; na hupatikana katika vyakula vya asili ya maziwa na mwanga wa jua.
Zz
zingizi ji placenta: kondo ya nyuma: kinachotoka tumboni mwa mzazi baada ya mtoto kuzaliwa.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T10:57:01Z 2021-06-29T10:57:01Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=354 <![CDATA[Vidahizo vya Fani ya Ufinyanzinakshi, Mkonge, Mianzi na Vibuyu]]> Vidahizo vya Fani ya Ufinyanzinakshi, Mkonge, Mianzi na Vibuyu
Aa
ageti ji agate: aina ya mawe magumu ya silika yanayotumika kutengeneza vitu vya kutwangia na kusagia vitu vigumu.
Bb
bombwe (ruwaza) ji pattern: mpangilio wa vitu katika utaratibu maalumu.
bitana ji lining: sehemu laini ya ndani ya vyombo vya ufinyanzinakshi.
bomba ji pipe: taz. bomba: UFUNDI.
buluu ji blue: rangi ya samawati. Dawa ambayo hutumiwa kung’arisha nguo nyeupe zinapofuliwa.
Cc
chenezo ji tapemeasure: chombo cha kupima urefu chenye kutumia vigao vya kumikumi.
chokaamawe ji limestone: aina ya mwamba ambao hutumika kujengea; nao ni kaboni ya kalisi.
Dd
dai ji dye: taz. dai: KARATASI, MATOFALI NA VIGAE.
digali ji flue: bomba au mrija wa kupitisha joto, moshi au hewa ya joto.
digavu ji ashtray: kisahani au kijisinia au kijibakuli kwa ajili ya kuwekea majivu ya sigara, kiko, n.k.
dohani ji chimney: taz: dohani: KARATASI, MATOFALI NA VIGAE.
Ee
enameli ji enamel: dutu aina ya kioo inayotumika kutengenezea bitana.
Gg
gurudumufinyanzi ji potter’s wheel: gurudumu linalotumika katika kutengeneza umbo la kitu kinachofinyangwa.

gurudumufinyanzi
Il
itale ji granite: mwamba mgumu sana wenye rangi ya kijivu.
Jj
jiwebwimbwi ji feldspar: aina ya jiwe jeupe au la rangi ya kidaka linalochanguka kwa urahisi.
jiwesabuni ji soap stone: aina ya ulanga mzito unaotumika kutengenezea uso wa meza, joko, mapambo, n.k.
Kk
kalibu ji mould: taz. kalibu: KARATASI, MATOFALI NA VIGAE.
kaolini ji kaolin: udongo mwororo mweupe unaotumika kutengenezea vikombe, sahani, n.k. Pengine hutumika pia kutengeneza dawa.
kauri ji porcelain: udongo mweupe sana nao hutengenezwa kwa kuchoma mchanganyiko wa kaolin, udongo mfinyanzi, na vitu vingine.
kichubuzi ji abrasive: dutu, kama vile mchanga, inayotumika kung’arisha au kusugulia vitu, kama vile safuria, sahani, n.k.
kidoto ji nest-shaped dish, bowl, plate: sahani au sinia au bakuli inayotengenezwa kwa chane za miyaa, mianzi, minazi, n.k.
kikekameza ji table mat: kipande cha maunzi ya pamba, katani, mkonge, n.k., ambacho juu yake huwekwa chombo kilicho na chakula cha moto.
koleo ji pliers: kifaa cha kushikia, kukatia au kung’olea vitu kama waya, misumari, meno, n.k.
Mm
makaamawe ji coal: taz. makaamawe: KARATASI, MATOFALI NA VIGAE.
mfinyanzi ji potter: taz. mfinyanzi: KARATASI, MATOFALI NA VIGAE.
mhenzirani ji: aina ya mti ambao ukipindwa hauvunjiki kwa urahisi, na kamba zake hutumika kutengeneza vyombo na samani mbalimbali.
Nn
nachingwea ji: kikapu kidogo cha mianzi chenye pembe nne, aghalabu hutumika kanisani kuwekea sadaka.
Rr
rangi ji colour: taz. rangi: KARATASI, MATOFALI NA VIGAE.
Pp
pozolana ji pozzolana: aina ya chokaa inayotumika katika ufinyanzinakshi.
Ss
shondo ji guartz: jiwe gumu jeupe linalong’aa.
Tt
tanuri ji kiln: taz. tanuri: KARATASI, MATOFALI NA VIGAE.
tembwe mgomba ji banana fibre: nyuzinyuzi zinazotokana na magome ya mgomba.
tindikali ji flux: dutu inayotumika kusafishia metali.
trei ji tray: taz. trei: KARATASI, MATOFALI NA VIGAE.
Uu
unakisishaji ji reduction: uondoshaji wa oksijeni au elektroni au uongezaji wa hidrojeni katika dutu.
utengenezaji chokaa ji calcination: uchomaji mawe kwa nia ya kutengeneza chokaa.
Ww
wakala ji reducing agent: kitu kinachoondosha oksijeni au kuongeza hidrojeni au elektroni kwenye kitu kingine.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T10:37:44Z 2021-06-29T10:37:44Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=353 <![CDATA[VISAWE NA MAANA ZAKE]]> BOFYA HAPA CHINI KUFUNGUA &t&t&t&t&t


.pdf   VISAWE-NA-MAANA.pdf (Size: 190.42 KB / Downloads: 20) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T10:03:13Z 2021-06-29T10:05:53Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=352 <![CDATA[Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu]]> Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu
Bb
bikariolezi ji wing dividers: bikari itumiwayo na mafundi, k.m., seremala, fundi viatu, n.k., kutengeneza violezo.

bikariolezi
Kk
kichopeko ji shoe horn: kifaa maalum kinachosaidia kuingiza mguu kwenye kiatu wakati wa kukivaa.

kichopeko
kidira ji cutting nipper: Kifaa cha kukata na kung’oa misumari.

kidira
kisuwembe ji rampat edger: kifaa mfano wa wembe ambacho hutumiwa kwa ajili ya kukatia ngozi.

kisuwembe
Mm
maleti mpira ji rubber mallet: nyundo kubwa ambayo kichwa chake ni mpira.

maleti mpira
mwega feleji ji iron rest: pande la chuma ambalo juu yake huwekwa kiatu wakati wa kugongwa misumari.

mwega feleji
Nn
ngoeko ji hook: kifaa cha kukamatia au kutolea ubaowayo kwenye kiatu.

ngoeko
Pp
panchi gezamguu ji wooden hole punch: ubao uliochongwa kulingana na nambari tofauti za miguu ya watu.

panchi gezamguu
panchi mzunguko ji revolving punch: chuma chenye meno ya kutobolea matundu kwenye ngozi.

panchi mzunguko
Rr
riveti ji eyelet: metali zenye vitobo zinazowekwa kwenye vitundu katika viatu, nguo, n.k.

riveti
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-29T09:44:54Z 2021-06-29T09:44:54Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=351 <![CDATA[Vidahizo vya Fani ya Usindikaji Mafuta na Matunda, na Utengenezaji wa Sabuni]]> Bb
besi ji base: kemikali ambayo ikitendana na asidi hutoa chumvi na maji, na hubadili litimasi kuwa buluu.
Cc

chachuka kt ferment: kubadilika kikemikali kwa vitu vya kikaboni kwa kutendana na viumbe hai kama bakteria, n.k.
Ff
fua kt dehydrate: ondoa maji yote yaliyomo ndani ya kitu.
Hh
hasi kt sterilize: 1. ua vijidudu na viumbe vinavyosababisha maradhi. 2. fanya kiumbe kisiwe na uwezo wa kuzaa.
hatimiliki ji patent: kibali anachopewa mtu na serikali cha kumruhusu kutengeneza, kuuza kitu kwa muda maalum.
Kk
kabohidrati ji carbohydrate: msombo wa kaboni, hidrojeni na oksijeni, kama vile uwanga, sukari na selulosi.
kakamaza kt stabilize: fanya kitu tepetepe kuwa kigiumu kwa kutulizana.
kichochezi ji catalyst: dutu inayozidisha kasi ya mmenyuko.
kihawilijoto ji heat exchanger: kitumi cha kuhamisha joto la kioevu kimoja kwenda kwenye kioevu kingine bila ya kuchanganyika pamoja.
kihifadhi ji preservative: kitu kinachozuia uharibikaji au udhurikaji wa dutu.
kimeng’enya ji enzime: kichochezi ambacho kwa kawaida ni protini kinachotengenezwa na selihai.
kimeng’enywa ji substrate: dutu inayosahilishwa kwa ajili ya matumizi ya kujenga, kulinda na kutia joto mwilini.
kindaoksidishi ji antioxidant: kemikali inayozuia athari za ubabuzi wa metali, k.m., kupata kutu kwa chuma.
kinu ji mill: mashine itumikayo kuponda au kusaga mbegu za mafuta au nafaka.
kioevu ji liguid: kitu kama maji, maziwa, mafuta, au soda kinachoweza kumiminwa.
kioevu babuzi ji caustic lye: kioevu kinachotumika kutengeneza sabuni, nacho huunguza au huharibu kwa amali ya kemikali.
kiolwa ji object: kitu kinachoweza kuonekana, kusikika, kuhisika au kuguswa.
kitako ji base: sehemu ya chini kabisa ya kitu, hasa ile sehemu ambayo kitu husimamia.
kitako
kitambulisho ji label: kipande cha karatasi au maunzi kinachoambatishwa ili kukijulisha kitu fulani ni nini, cha nani au wapi kinatoka au kinapelekwa.
kiwangomchemko ji boiling point: halijoto ya kioevu kinapoanza kuchemka. Hali hii hutofautiana kutegemea kanieneo ya angahewa ya mazingira.
kiwangomyeyuko ji melting point: halijoto ambapo dutu hubadilika kutoka mango kuwa kioevu.
koleza kt concentrate: fanya kioevu kuwa thabiti kwa kuongeza kumumunyishwaji au kwa kupunguza kiasi fulani cha maji.
Mm
mafutaghafi ji crude oil: mafuta ambayo hayajapitia mchakato wowote wa usafishaji.
mafuta haradali ji mustard oil: mafuta yaliyokamuliwa kutokana na mbegu za haradali.
mafuta laini ji soft oil: mafuta ambayo yamesafishwa sana.
mafuta mahindi ji corn oil: mafuta yaliyotengenezwa kutokana na kukamua mahindi.
mafuta mimea ji vegetable oil: mafuta yanayotokana na usindikaji wa mbegu za mimea, k.m., alizeti, n.k.
mafutauto ji oil: mafuta ya majimaji yasiyoganda kwenye baridi.
magadi ji soda ash: kemikali inayounguza; inayochoma; inayomomonyoa mwili na vitu vingine. Fomula NaCh.
magadi babuzi ji sodium hydroxide: aina ya kemikali inayounguza, inayochoma, inayomomonyoa mwili au vitu vingine.
majinyongo ji brine: maji yenye madini mengi ya chumvi.
mango ji solid: kitu kisichokuwa kioevu au gesi.
maunzi ji material: chochote ambacho kutokana nacho kitu chaweza kutengenezwa.
menyu kv pure: isiyo na uchafu au mchanganyiko wa dutu yoyote nyingine.
midia ji medium: dutu inayoingilia kati ambayo inabidi kani au athari fulani ipite ndani yake, mathalani, hewa maji, metali, n.k.
mikrobiolojia ji microbiology: mtaala wa kisayansi wa viumbehai vidogovidogo sana kama vile bakteria, virusi, protozoa, kuvu, n.k.
mituamo ji statics: elimu ya jinsi ya vitu vinavyokaa katika hali tuli na kani za msawazisho.
mjao ji volume: kipimo cha nafasi kinachokaliwa na kitu.
msibiko ji contamination: hali ya kuwa chafu kutokana na kuguswa au kuingiwa na kitu.
mtovu kv centripetal: -enye kuelekea kwenye nukta.
mumunyisha kt disssolve: fanya kioevu kwa kutia ndani ya kioevu.
mvuke ji vapour: hali mojawapo ya mata ambapo dutu inakuwa katika hali ya gesi.
mvukemaji ji steam: maji katika hali ya gesi inayotokana na kuchemka.
myuko ji convection: msogeo ndani ya gesi au kioevu unaosababishwa na kioevu au gesi fukuto inayopanda juu na gesi au kioevu baridi kinachoshuka chini.
Nn
neli ji tube: mrija mwembamba
nishati ji energy: nguvu, na uwezo wa kufanya kazi.
nururisha kt radiate: piga kiolwa kwa miali ya nuru, joto, n.k.
Oo
ombwe ji vacuum: nafasi bila ya hewa au gesi ndani yake.
Pp
pimamchepuko ji refractometer: chombo cha kupimia kiasi cha mchepuko na kipeomchapuko.
pimamchepuko
pepetaka ji foreign matters: takataka ambazo huvunwa pamoja na mbegu zinazotoa mafuta; nazo hutolewa kabla ya ubanguaji.
Rr
regesha kt recycle: rudisha katika hali ya kwanza ili kitumike tena.
Ss
sabuni ya kimetali ji metallic soap: chumvi isiyomumunyika iundwayo na metali pamoja na asidi shahamu. Hutumika kuvifanya vitambaa visipenyeke na maji kwa urahisi na pia kama kikaushio cha rangi.
safisha kt refine: toa uchafu, k.m., kutoka kwenye sukari, metali, na mafuta.
shahamu ji fats: mafuta yanayotokana na wanyama, aghalabu ya kuganda.
Tt
themometa ji thermometer: ala ya kupimia halijoto.
themometa
Uu
uchepukaji ji refraction: badiliko la uelekeo wa mnururisho wakati wa kupita, kutoka na kuingia midia nyingine kutokana na mnururisho kuwa na kasi tofauti katika midia hizo.
ujazo ji capacity: nafasi inayopimwa kwa kuzidisha urefu kwa upana kwa kina.
ukebeshaji ji canning: hifadhi ya chakula katika makopo.
uoksidishaji ji oxidation: utaratibu au kitendo cha kuongeza oksijeni, kupunguza hirojeni au kupunguza eleletroni kwenye kemikali yoyote.
upasterizaji ji pasteurilization: kuua bakteria katika maziwa kwa kuchemsha hadi kufikia halijoto ya 60°C.
usindikaji ji milling: ukamuaji wa mbegu au tunda ili kutoa umajimaji uliomo.
utokaji ji emission: kutoka kwa kitu katika kitu kingine.
uvukizaji ji evaporation: ubadilishaji wa kioevu kuwa mvuke.
uzito wiani ji relative desinty: uwiano kati ya masi ya mata katika mjao fulani na masi ya maji yenye mjao sawa.
Vv
vitamini bandia ji artificial vitamin: taz. vitamini: SAYANSI KIMU.
]]>
false