MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Sanaa za maonesho]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ 2024-04-29T06:52:05Z MyBB MwlMaeda]]> 2022-01-27T07:48:37Z 2022-01-27T07:48:37Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2329 <![CDATA[Matambiko Katika Jamii yA Wasambaa]]>
.docx   Matambiko_Katika_Jamii_yA_Wasambaa (1).docx (Size: 68.9 KB / Downloads: 3) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-10T13:22:16Z 2021-09-10T13:22:16Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1231 <![CDATA[Michezo ya Watoto/Chekechea]]> Michezo ya Watoto/Chekechea
  • Michezo inayoigizwa na watoto katika shughuli zao.
Aina
  1. Mchezo wa baba na mama
  2. Kuruka kamba
  3. Kujificha na kutafutana
  4. Kukimbiza kibaramwezi dhidi ya upepo ili kizunguke
  5. Mchezo wa baba na mama
Sifa
  1. Waigizaji ni watoto.
  2. Huhusu shughuli za kiuchumi na kitamaduni k.v. arusi, siasa, ukulima.
  3. Huandamana na nyimbo za watoto.
  4. Huwa na miondoko mingi k.v. kujificha, kuruka.
  5. Huwa na matumizi mengi ya takriri.
  6. Huchezwa popote.
  7. Huwa na kanuni fulani.
  8. Hukoma watoto wakichoka au wakikiuka kanuni
Umuhimu
  1. Kufunza watoto majukumu yao ya utu uzima.
  2. Kuwatanguliza watoto katika sanaa ya uigizaji.
  3. Kukuza ubunifu wa watoto kadiri wanapoendelea kuigiza.
  4. Kudumisha utamaduni wa jamii.
  5. Kuburudisha watoto.
  6. Kukuza stadi ya uigizaji miongoni mwa watoto.
  7. Kukuza utangamano miongoni mwa watoto kwa kuwajumuisha pamoja.
  8. Kukashifu matendo hasi ya watu wazima kwa watoto.
  9. Kuwapa watoto ukakamavu na kujiamini wakiwa wachanga.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-08-22T10:01:08Z 2021-08-22T10:01:08Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=985 <![CDATA[MUUNDO WA MAJIGAMBO]]>
.pdf   MUUNDO-WA-MAJIGAMBO.pdf (Size: 176.89 KB / Downloads: 8) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-08-01T05:26:14Z 2021-08-02T02:18:46Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=691 <![CDATA[Halafu ya Sanaa za Ubunifu wa Kiafrika Mtanziko Rejeleshi wa Tawala za Kiafrika]]>
.pdf   Halafu ya Sanaa za Ubunifuwa Kiafrika Mtanziko Rejeleshi wa Tawala za Kiafrika.pdf (Size: 312.72 KB / Downloads: 0)


CHANZO &t&t&t&t&t&t]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-26T05:59:27Z 2021-07-26T05:59:27Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=647 <![CDATA[SANAA YA TAARAB NA BI. SHAKIRA – WIMBO moyo unalia macho yanacheka]]> BOFYA HAPA KUTAZAMA &t&t&t&t]]> false MwlMaeda]]> 2021-07-26T05:37:11Z 2021-07-26T05:37:11Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=646 <![CDATA[MITAZAMO (NADHARIA) MBALIMBALI JUU YA SANAA ZA MAONESHO]]>
Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa, umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisi zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye dhana maalum.  Kuna aina kuu tatu za sanaa. Kwanza ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake kuonyeshwa wakati wowote. Hizi ni sanaa za uonyesho. Nazo ni kama vile uchoraji, uchongaji, ufinyanzi, kutarizi n.k. sanaa amabazo hututolea vitu kama vile picha, vinyago, nguo zilizotariziwa, vyungu n.k.
Aina ya pili ya sanaa ni sanaa za ghibu. Hizi ni sanaa ambazo uzuri wake haujitokezi kwenye umbo linaloonekana kwa macho au kushikika bali katika umbo linalogusa hisia. Mifano ni kama vile usahiri, uimbaji, upigaji muziki n.k. uzuri wa sanaa hizi umo katika kuzisikia.
Aina ya tatu ya sanaa ni sanaa za vitendo. Uzuri wa sanaa za aina hii umo katika umbo la vitendo, na ili kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama vitendo vikifanyika. Umbo hili linalazimisha kuwepo kwa mwanasanaa na mtazamaji wa sanaa mahali pamoja kwa wakati mmoja ama sivyo sanaa haikamiliki. Hali hii ndiyo iliyosababisha sanaa hizi za vitendo kuitwa sanaa za maonyesho, kwa sababu lazima wakati zinapotendeka awepo mtu wa kuonyeshwa, maana uzuri wake umo katika vitendo vyenyewe.
[url=https://www.blogger.com/null][/url]
Kwa hiyo sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa nne ambazo ni:
            i.            Dhana inayotendeka
          ii.            Mtendaji
        iii.            Uwanja wa kutendea
        iv.            Watazamaji
Sasa baada ya kuagalia dhana ya sanaa za maonyesho, sasa tuangalie nadharia zinazojaribu kuelezea sanaa za maonyesho. Nadharia hizi zipo tatu ambazo ni:
       1. Sanaa za maonyesho ni michezo ya kuigiza, ama ni michezo inayoonyeshwa kwenye jukwaa lenye pazia na mataa mengi ya jadi au ni michezo ya Shakespeare. Huu ni mtazamo mmoja wapo ambapo baadhi ya wataalamu wanaamini hiyo, kwamba sanaa za maonesho lazima zichezwe jukwaani, kuwepo na pazia na mataa mengi.
Tukizingatia nadharia hii huenda tukaamini kuwa sanaa za maonyesho ni tamthilia tu. Kitu ambacho kinaleta mashaka kidogo.  Inafahamika kuwa tamthilia ni utanzu ulioletwa na wakoloni hapa Afrika Mashariki. Kwa hiyo, kuamini nadharia hii ni sawa na kusema kuwa hakuna sanaa za maonyesho zenye asili ya hapa Tanzania ama Afrika Mashariki. Au kwa upande mwingine ni sawa na kusema kuwa kabla ya mkoloni kutuletea tamthilia sisi tulikuwa hatuna sanaa za maonyesho zetu wenyewe. Wazo hili si kweli na ni wazo potofu.   (Taz. Mhando &Balisidya 1976).
Kimsingi mtazamo huu unatokana na fasili ya sanaa za maonyesho inayodai kuwa sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa za mchezo, mchezaji, uwanja wa kuchezea na watazamaji. Ingawaje ufafanuzi huu ni sawa lakini hata hivyo mtazamo huu ni dhaifu kwani ulitokana na watu waliokuwa wakifafanua sanaa za maonyesho wakiegemea zaidi kwa zile za utamaduni wa kizungu. Ufafanuzi huu haukuzifikiria sanaa za maonyesho zenye ya utamaduni wa Kitanzania.
Dosari kubwa katika ufafanuzi huu imo katika neno mchezo (play). Neno hili lina maana duni likilinganishwa na hali na umuhimu wa sanaa za maonyesho zenye asili ya Kitanzania/Kiafrika. Tukichukua kwa mfano unyago, jando, kusalia mizimu, au masimulizi ya hadithi, ambayo ni mifano ya sanaa za maonyesho zenye asili ya Kitanzania, tunakuta zile sifa zote nne zipo. Isipokuwa tunajua kuwa shughuli zote hizi siyo mchezo na umuhimu wao hauruhusu hata kidogo kuingiza neno mchezo. Shughuli hizi zina maana muhimu ambayo inahusu maisha ya binadamu katika jamii yake. Ni shughuli zinazobeba wazo maalum lenye lengo la kujenga utu wa mwanajamii. Basi vipi tuseme shughuli hizi zina sifa ya mchezo?  Wenzetu wazungu wanaridhika na neno hili kwa  sababu sanaa za maonyesho za utamaduni wao mara nyingi zinafanywa kwa masihara tu. Sanaa za maonyesho zao zaidi ni kwa madhumuni ya kujiburudisha au pengine kutafuta kipato. Lakini kila aina ya sanaa za maonyesho ya Kitanzania ina dhana fulani ndani yake, kwa mfano dhana kuhusu maana ya maisha, kuhusu utekelezaji wa madaraka ya kiutu uzima,  kuhusu ushujaa, mafunzo ya historia ya jamii n.k.
Kwa hiyo basi sanaa za maonyesho za Kiafrika ni dhana zilizo kwenye umbo linalotendeka na siyo mchezo. Kutokana na utamaduni wa Kiafrika tunaweza kusema kuwa: sanaa za maonyesho ni dhana inayotendeka. Na ili dhana hii itendeke anahitajika mtu wa kuitenda (mtendaji). Mtendaji huyu huhutaji uwanja wa kutendea hiyo dhana na wakati akiitenda wanakuwapo watazamaji.   
         2. Sanaa za maonyesho ni vichekeso au ni maigizo yanayochekesha.
Wazo hili linatokana na historia ya sanaa za Maonyesho hapa Tanzania. Wakati mkoloni alipotuletea sanaa ya Maonyesho ya kikwao sisi tulishiriki katika tamthilia za Shakespeare kama washiriki au watazamaji tu. Kwani tamthilia hizi hazikuwa na maana yoyote kwetu kutokana na kuwa zilibeba na ziliongelea utamaduni wa kizungu. Tulifurahishwa na vile vitendo vilivyofanywa kwenye jukwaa katika tamthilia hizi na hivyo vitendo hivi vilituchekesha tu. Basi jambo kubwa kwa Mwafrika ikawa ni vile vichekesho na hivyo kudhani kuwa jambo muhimu katika tamthilia ni kule kuchekesha kwake.
        3.      Sanaa za maonyesho ni maigizo.
Wazo hili limetokana na tafsiri mbovu ya neno play ambalo limetafsiriwa kuwa mchezo wa kuigiza. Inawezekana aliyetafsiri neno hili alifuata nadharia za zamani sana za drama, ambapo ilidhaniwa kuwa uigizaji (imitation) ndio kiini cha drama. Hata hivyo nadharia hii ilitupiliwa mbali kwa vile haikudhihirisha kiini hasa cha drama. Tafsiri hii ndiyo imeleta matatizo hapa Tanzania katika kufahamu sanaa za maonyesho. Wengi wamepotoshwa na wazo kuwa uigizaji ndio kiini cha sanaa za maonyesho kama vile neno michezo ya kuigiza linavyoonyesha. Hivyo, hata katika kutazama sanaa za maonyesho za asili wengi wamekuwa wakitazama iwapo kuna uigizaji. Na hapa wengi wanakwama kwani katika unyago, jando, kusalia miungu n.k hakuna uigizaji bali wanaoshiriki wanashika nafasi fulanifulani. Hivyo ni bora kutumia neno tamthilia pale tunaporejelea neno plays.
Kwa ujumla kuwepo kwa mitazamo hii huweza kuwa kumesababishwa na mambo yafuatayo:
  • Wakoloni kutokutambua ama kwa makusudi ama kwa kutokuelewa kuwa tulikuwa na sanaa za maonyesho za kwetu, hivyo akatuletea drama kama vile anatuletea sanaa mpya ambayo aina yake haikuwepo hapa kwetu. Hivyo, mkazo wa sanaa za maonyesho ulitiliwa katika drama tu.
  •  Mkoloni alitumia mbinu mbalimbali za kufuta vitendo vyote ambavyo hasa ndiyo sanaa zetu za maonyesho. Mfano alitumia dini ya Kikiristo kupiga vita vitendo kama vile unyago, jando, kusalia mizimu n.k ambavyo viliitwa vya kishenzi.
  • Tafsiri mbovu zinazofuata nadharia zilizopitwa na wakati kama ilivyoelezwa hapo awali.
Kwa hiyo, tukisema sanaa za maonyesho, tunarejelea vitendo maalum vyenye sifa zilizotajwa na kujadiliwa hapo awali. Hata hivyo tutambue kuwa sifa hizi ingawaje ziko sawa lakini kimsingi zinatofautiana katika uzito wake baina ya jamii moja na nyingine. Hatutazamii sanaa za maonyesho za Kihindi kuwa sawa kabisa na zile za Kijapani au za Kiafrika. Ingawa zote ni sanaa za maonyesho zina misingi tofauti kutokana na tofauti za utamaduni wa jamii husika.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-26T05:18:47Z 2021-07-26T05:20:09Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=645 <![CDATA[MUZIKI WA ZAMANI NI SANAA INAYOPASWA KUENZIWA]]> BOFYA HAPA KUTAZAMA &t&t&t]]> false MwlMaeda]]> 2021-07-26T03:57:41Z 2021-07-26T03:57:41Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=644 <![CDATA[SANAA YA MAJIGAMBO (VIDEO)]]> BOFYA HAPA KUTAZAMA &t&t&t&t



Miongoni mwa vipera vya sanaa za maonesho ni Majigambo ambayo kihistoria yanatoka katika jamii ya watu wa Kagera. Hapa nakuletea mfano wa sanaa hiyo ya majigambo.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-26T03:45:55Z 2021-07-26T03:50:11Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=643 <![CDATA[KORASI NA UHUSIANO WAKE NA SANAA ZA MAONYESHO]]> Kioo cha Lugha
Juzuu 1, Na. 2 (1995)
KORASI NA UHUSIANO WAKE NA SANAA ZA MAONYESHO
Uchambuzi wa Kidayakronia
Aldin Kai. Mutembei
Utangulizi
Makala haya yanachambua kipengele muhimu katika sanaa kiitwacho korasi. Uchambuzi huu umegawanyika katika sehemu kuu tatu: kwanza, tutaangalia maana mbalimbali zinazojaribu kuielezea korasi. Katika kufanya hivyo tutaangalia pia udhaifu au uyakinifu wa kila maana hizo. Sehemu ya pili itaangalia chimbuko la korasi. Katika sehemu hii mjadala utazingatia zaidi mabadiliko katika jamii na hasa jinsi ambavyo mabadiliko hayo yaliiathiri korasi. Mabadiliko katika jamii yalileta mabadiliko katika korasi, hivyo korasi ikawa na maudhui na fani tofauti tofauti kutegemeana na jamii ilivyobadilika. Katika sehemu ya tatu mjadala utaangalia japo kwa kifupi uhusiano wa korasi na sanaa za maonyesho. Hapa tutachambua dhima ya korasi katika sanaa za maonyesho na katika jamii kwa ujumla. Tutahitimisha uchambuzi wetu kwa kutoa muhtasari wa mjadala mzima na kuacha maswali yanayoweza kujibiwa katika makala nyingine na utafiti mwingine zaidi ya huu.
Makala haya yanachukua mkabala wa kidayakronia katika uhakiki wa kifasihi. Mkabala huu huichunguza dhana fulani tokea katika maalumu na kuangalia mabadiliko yake katika vipindi mbalimbali vya kihistoria. Mkabala wa kidayakronia utatusaidia kuielewa korasi ambayo imekuwa na mabadiliko ya msingi kifani na kimaudhui. Makala haya yanatoa mchango katika uwanja wa Fasihi ikionyesha kuwa baadhi ya vipengele havina budi kuangaliwa upya na kupewa umuhimu wake.
Maana ya korasi
Baadhi ya wanafasihi wameitumia dhana hii wakiwa na maana ya “kiitikio”. Maana hii ni finyu mno kwa kuwa imezingatia aina moja tu ya korasi. Aidha kwa kuifafanua hivyo maana hii inaonyesha kuwa kipengele hicho hakiwezi kutokea katika tanzu nyingine za Fasihi ambazo si ushairi. Wengine wameiita mkarara. Hawa nao kama wale wa mwanzo wameangalia zaidi fani. Wameiangalia dhana hii kwa ufinyu na kuiondolea matawi yake mapana yanayogusa zaidi masuala ya utamaduni mila na desturi katika jamii. Wakaiita dhana hii ‘mkarara’ kwa maana ya kukariri au kurudia rudia. Ingawa ni kweli kuwa hii ni aina mojawapo ya korasi lakini si maana yake. Ndani ya maana hizi mbili vipengele muhimu vinavyoiunda korasi havionekani. Hatuoni utamaduni, mila wala desturi. Hatuoni dhima ya korasi katika jamii wala hakuna suala la imani katika istilahi hizo mbili. Kwa hiyo maana hizi hazikidhi haja ya dhana tunayoielezea hapa kama korasi. Korasi ni dhana changamano. Ni kiini cha sanaa za maonyesho hasa tamthiliya za kimagharibi. Katika makala haya inapendekezwa kuwa istilahi inayoweza kukidhi dhana pana ya jambo tunalolizungumzia iwe ni korasi.
Neno korasi tunalitohoa kutoka kwenye Kiingereza chorus. Waingereza pia walilichukua kutoka kwa Kilatini chorus. Hali kadhalika Walatini walilitohoa kutoka kwa Kiyunani xopos (choros).
Simpson na Weiner wanaielezea korasi kuwa ni ‘Kikundi cha waimbaji na wachezaji katika sherehe za kidini na sanaa za maonyesho za Uyunani ya kale (Tafsiri yangu). Hapa msisitizo unawekwa katika uimbaji na uchezaji. Kwanini? Waandishi wa Kamusi ya Webster wanalifananisha neno hili korasi na neno la Kilithuania zaras lenye maana ya kisababishi (course). Ufafanuzi zaidi umetolewa na waandishi wa Encyclopaedia Americana ambao wanasema:
Kwa kuwa katika Uyunani ya kale uchezaji ulikuwa, karibu wakati wote, ukiendana na uimbaji, basi [korasi] ilikuja julikana kama kundi la waimbaji na wachezaji wa utungo fulani. (Tafsiri yangu).
Hawa, wanaona kuwa kutokana na neno la Kiyunani Xopos linalomaanisha mahali pa kuchezea, wahusika katika kundi hili ndio waliosababisha tukio zima. Walikuwa washiriki na wahusika. Hivyo wakatoa maana ya korasi kuwa ni ‘Kundi ambalo lilihusika katika mchezo au kutoa maelezo kuhusiana na tendo. Waandishi wengine wa kamusi ya Webster toleo la pili, hawashikilii uimbaji tu bali wanaongezea kipengele kingine muhimu, kipengele cha maongezi. Wanasema:
(korasi), ni kikundi cha waimbaji au waongeaji (chanters). Dhima yake ilibadilika badilika, ilikuwa ni ile ya wahusika katika kitendo na wafasiri wa kitendo (Tafsiri yangu)
Katika kuipanua dhana hii, korasi ilikuwa na kutokeza tanzia. Hapo korasi ilikuwa imepata dhana pana zaidi. Sasa ilikuwa ni:
Watazamaji wenye usikitivu kuhusiana na yale yawapatayo wahusika katika mchezo, huku wakionyesha kwa maneno au vitendo kuguswa kwao baina ya vitendo vya wahusika, kuhusiana na mambo ya kimaadili na kidini ambayo hutolewa au kuonyeshwa na vitendo katika mchezo (Tafsiri yangu).
Jambo tunaloliona hapa ni kuwa dhana ya korasi inaingiza pia suala la hisi za watu. Tunaona kuwa, kutoka kuwa jamii nzima, kisha wahusika kadhaa katika mchezo, korasi pia iliweza kuwa ni hadhira nzima. Browne anatupeleka hatua zaidi mbele anapoiangalia korasi ki-historia kuwa:
Kihistoria, korasi ilikuwepo kabla ya michezo ya kuigiza ambayo ilitokana nayo, na kwa hakika korasi inatakiwa ibakie kama ilivyokuwa mwanzoni yaani kundi lililoteuliwa kuisemea jamii nzima (Tafsiri yangu)
Huyu ameligusia suala la chimbuko la sanaa za maonyesho ambazo ni maigizo. Jambo ambalo uhusiano wake na korasi utaangaliwa katika sehemu ya tatu ya mjadala huu. Lakini jambo muhimu ni uwakilishwaji wa jamii uliofanywa na watu wachache wateuliwa.
Kutokana na tafsiri hizi zote, na kwa mujibu wa hatua mbalimbali za korasi, makala haya yanaifafanua korasi kuwa ni:
Matendo au maneno ya kisanaa ayatoayo mtu mmoja au zaidi katika kitendo cha kisanaa au kuhusiana na kitendo hicho cha kisanaa ambapo hadhira hushirikishwa au hufanywa ifikirie undani wa kitendo au maneno hayo jinsi ambavyo isingelifanya kama ingelikuwa vinginevyo. Maneno hayo hutolewa kwa njia ya uimbaji au nathari. Tena, matendo yaweza kuambatana na maneno au yakawa peke yake na hivyo kutokeza utendaji bubu (miming)
Historia ya korasi
Chimbuko la korasi
Hatuwezi kugusia historia ya korasi tukaacha kuzungumzia sanaa za maonyesho. Aidha haiyumkiniki kuongelea juu ya korasi bila kuongelea habari za Wayunani. Lakini inawezekana kabisa kuwa dhana hii ilipatikana pia katika mataifa mengine. Jambo la kuwepo kwa korasi katika mataifa mengine litabakia kuwa swali mwishoni mwa sehemu ya tatu.
Baadhi ya waandishi kama vile G. Thomson O.G. Brockett .W.P. Cambridge, Oates na O’neil, jr na wengineo wanashikilia kuwa korasi ilitoka kwa Wayunani. Hii ilikuwa zamani za karne ya nane hadi ya tano kabla ya Kristo. Korasi ilitokana na jamii na ilikuwa jamii. Kila mtu alikuwa ni sehemu ya korasi hapo mwanzoni. Ikumbukwe kuwa wakati wa ujima, umoja na ushirikiano katika kazi yalikuwa ni mambo ya lazima yaliyofanya jamii izidi kuwapo na istawi. Korasi kama kipengele kimojawapo muhimu cha kazi kiliwahusisha watu wote.
Mwanzoni korasi ilikuwemo katika shughuli pana iliyoitwa “dithirambu” (dithyramb)). Shughuli hii au tendo hili lilifanyika kwa njia ya uimbaji wa sauti moja, leng kuu likiwa ni kutambika na/au kutoa zaka kwa mungu wa Wayunani aliyeitwa Dionysus. Katika matambiko haya yaliyofanywa na watu wote, kundi la wanawake lilijitokeza na kuongoza uimbaji huu, wengine wakafuatia huku kutambika kukiendelea. Arion ndiye anayejulikana kuwa mtu wa kwanza hapo Korintho, kuifanya korasi ushairi utakaodumu. Wakati huu bado ilikuwa katika muundo uleule wa uimbaji. Aeschylus alifanya mabadiliko ya msingi katika shughuli ya utambikaji na kuipa korasi nguvu zaidi, kama tutakavyoona baadaye. Korasi ikawa pana na kuenea Uyunani nzima. Kwa hiyo, korasi ilianza kama kundi la waimbaji likisindikiza na kuhusika katika shughuli ya utambikaji. Shughuli hii ilifanywa na vikundi vya wanawake vilivyoitwa thiasos.
Mabadiliko katika korasi
Jamii ilizidi kukua. Maendeleo katika sayansi na teknolojia yalisababisha uwepo ubora wa vitendea kazi. Kutokea mgawanyiko wa kazi na uhusiano katika uzalishaji mali ukawa chanzo cha vijitabaka. Mabadiliko haya yaliuingilia umoja na ushirika wa kale. Nguvu ya mwanamke aliyokuwa nayo pale mwanzoni kutokana na dhima yake katika Dithirambu ikawa inafifia. Hadi yake ikashuka kwa kuwa sasa vifaa vilitumika kutoa milio kuita watu. Vikundi vya kinamama thiasos vikawa vinapungua na mahali pengine kufifia kabisa.
Dhima ya Dithirambu ikabadilika. Kutoka kuwa uimbaji uendao na shughuli ya matambiko, zikawa ni nyimbo kuhusu visa-asili. Ikachukua umbo la kisanaa zaidi na mwigo (imitation) ukachukua nafasi zaidi na zaidi. Katika kufanya hivi, kukatokea badiliko jingine ambapo Arion aliweka mazungumzo au maneno katikati ya nyimbo hizi. Hivyo korasi ikawa ina sehemu ya nyimbo, mazungumzo na uigizaji bubu. Hapa, bado watu wengi walihusika ingawa Dithirambu sasa ilikuwa imechukua sura mpya. Katika badiliko kuu la msingi kuhusiana na korasi, hatuwezi kukosa kumzungumzia Thespis. Huyu aliishi baada ya Arion. Na kwa kumwingiza mwigizaji mmoja katika korasi alipelekea mwanzo wa korasi ya kale kubadilika na kuwa sanaa ya maigizo pengine ikiitwa michezo ya kuigiza. Nagler anamsifu Thespis hivi:
Mtu mwenye akili nyingi aliyewezesha mabadiliko kutoka kwenye umbo la ki ‘ Dithirambu’ kwenda kwenye ‘drama’ alikuwa Thespis wa Icaria. Mwandishi wa michezo ya kuigiza, mwigizaji, Mkurugenzi jukwani na mtoaji michezo (producer). Yeye pia anasemekana kuihusisha korasi katika msuko wa matukio (Tafsiri yangu)
Mhusika aliyeingizwa na Thespis, aliigiza kama Mungu, akijibu maswali au kuuliza kuhusiana na yale yaliyosemwa na watu wengine kwenye onyesho. Huu kwa hakika ulikuwa mwanzo wa kupandwa mbegu ya sanaa za kitanzia. Kuhusiana na hili Aristotle anasema:
Sanaa ya kitanzia ilichomoza kutoka katika viongozi wa Dithirambu.
Kama utanzu wa Fasihi katika uchanga wake Dithirambu ilikuwa na watu mia tano, waliojigawa katika vikundi vya watu hamsini hamsini. Vikosi hivi ndivyo korasi kama ilivyokwisha elezwa. Katika makundi haya, mhusika mmoja (muigizaji) alijitokeza akiuliza jambo, akitoa ushuhuda fulani, akichokoza hoja au akipinga maamuzi ya tabaka tawala kwa njia ya kisanaa. Kwa kufanya hivi, vile vikosi vya korasi vilijibu hoja za mhusika kwa nyimbo na maelezo huku zumari na filimbi zikipigwa. Baada ya Thespis, Aeschylus (525-456 BC) aliongeza mhusika wa pili katika michezo yake. Baadaye Sophocles (497-406 BC) aliongeza mhusika wa tatu. Wahusika walikuwa wakiongezeka na kupungua kadri ya mahitaji ya sanaa ya jamii. Katika maendeleo haya, korasi ilikuwa imeathirika kuwili: kwanza umuhimu wake, kama shughuli ya kiibada ulikuwa umepungua sana. Sasa ilikuwa ni ‘mchezo wa kuigiza’ ingawa ndani ya igizo hili mambo muhimu yalitolewa kuifundisha jamii. Pili, idadi ya watendaji katika korasi ilipungua mno. Wale waigizaji watatu walitoa ujumbe na kuonyesha sanaa vizuri zaidi kuliko kundi kubwa. Hapa wahusika – waigizaji (actors) wakawa wanaongezeka huku watendaji (nyimbo au mazungumzo) wakipungua mno.
Uhusiano wa korasi na Sanaa za maonyesho – Tamthiliya
Korasi iliingizwa katika tamthiliya kama muundo, kama mtindo na baadaye kabisa kama mhusika. Sophocles katika tamthiliya zake kama vile Mfalme Edipode, Ajax na Antigone aliongeza namba ya wahusika (waigizaji) kufikia kumi na watano. Wahusika hawa walipunguza kabisa umuhimu wa korasi, kiasi kwamba korasi sasa ilikuwa ni vikundi vya watu wachache walioingia mchezoni mara chache chache. Hapa tunaiona korasi kama muundo. Waliingia mwanzoni au katikati au kila mwanzo wa onyesho; wala hapa haikuwa ni lazima. Nafasi ya korasi ilikuwa imebadilika kabisa! Freedley na Reeves wanasema:
Hadi kufikia wakati huo, korasi haikuwa na umuhimu mkubwa katika tendo la kisanaa. Kwa mtazamo wake haikuhusishwa moka kwa moja na maigizo, bali ilibakia kuwa ni mtu mmoja kitu cha kusaidia waigizaji walioko jukwaani.
Sophocles alianzisha majibizano baina ya wahusika wake katika tamthiliya, ambapo hapa na pale aliweka korasi ambayo sasa ilibeba dhima tofauti na umbo tofauti. Jambo muhimu pia ni kuwa idadi ya korasi ilipungua sana. Sasa haikuwa lazima liwe ni kundi kubwa. Aliweza kuwa ni mtu mmoja au zaidi akitoa maelezo kuhusu onyesho, akiiuliza hadhira kuhusiana na onyesho au akiunganisha onyesho moja na jingine wakati wahusika wanabadilisha mavazi nyuma ya jukwaa au penginepo.
Katika kuangalia pia uhusiano wa korasi na tamthiliya hatuna budi kugusia nadharia ya mfarakisho (alienation) iliyoendelezwa sana na Brecht. Hili lilikuwa ni badiliko la msingi katika korasi. Nadharia hii inawatenga kwa muda watazamaji (hadhira) na ile tamthiliya waitazamayo, huku ikiwaandaa kuwa watazamaji washiriki. Inawaondoa katika ule mtiririko wa maonyesho unaowazuga watazamaji, na inafanya hivi kwa lengo maalumu. Lengo hili linafanywa na korasi, pale mtu mmoja au zaidi anapoingia ghafla mahali fulani maalumu katika tamthiliya ili kuionyesha hadhira uhalisia na uyakinifu wa tendo linaloigizwa jukwaani kama mchezo tu. Lakini hadhira ione uhalisi zaidi kuliko maisha ya kawaida, kuliko jinsi ambavyo ingelifikiriwa. Na kama ni jambo nyeti, basi ionekane kama mchezo au mzaha tu korasi ilikuwa imepata mawanda mapana na dhima zake zilikuwa bayana katika tamthiliya. Dhima za korasi zimeorodheshwa na Brockett katika andiko lake kuhusu tamthiliya. Anasema:
  1. Alikuwa ni mhusika katika mchezo akitoa ushauri, akitoa maoni, akiuliza maswali na wakati mwingine akiwa kama mtendaji wa mara kwa mara katika mchezo. (Tafsiri hii na zinazofuata hapa chini ni zangu).
  2. Mara nyingi korasi ilikuwa muhimili wa matukio ya kijamii na kimaadili na iliweka vigezo ambavyo kwavyo mchezo uliweza kupimwa.
  3. Mara kwa mara korasi ilichukuwa nafasi ya mtazamaji kama wa mawazoni tu ambaye huibuka akaongea juu ya matukio au juu ya waigizaji kwa kadri msanii atazamiavyo hadhira itende.
  4. Korasi ilisaidia kuumba mazingira ya mchezo kwa ujumla na yale ya kila onyesho na hata kukuza athari za tamthiliya ionyeshwayo.
  5. Korasi huongeza miondoko, nyimbo, ngoma na ukubwa wa wahusika katika tendo na hivyo kuchangia sana katika ukamilifu wa tamthiliya.
  6. Hufanya kazi ya ridhimu ikitokeza mapumziko na utendaji wa pole pole wa matukio na katika kufanya hivi huipa nafasi hadhira ijitathmini ikiangalia yale yaliyotokea na kufikiria yajayo.
Katika dhima hizi sita, Brockett anatuonesha kuwa kwa hakika korasi ni pan asana. Inaweza kuangaliwa kama mhusika mmoja au wengi katika sanaa za maonyesho. Inaweza pia kuangaliwa kama tukio au matukio yanayojirudia rudia katika onyesho moja au zaidi. Tena korasi inaweza kuangaliwa kama wimbo au sauti tu inayotokea mara kwa mara ikimrudisha nyuma mtazamaji au ikimpeleka mbele ya tukio au hata ikimtolea ujumbe ambao haukuonyeshwa wala hautaonyeshwa na wafanyao maonyesho hayo. Dhima ya saba ya korasi imezungumziwa sana na Brecht ingawa kwa hakika sio yeye aliyeibuni. Dhima hii tumekwisha kuieleza hapa juu kuwa ni ile ifanyayo kazi ya ufarakisho au mtengo. Yaani matukio au mawazo fulani katika onyesho huwekwa na yakaonekana sio ya kawaida au hayakutazamiwa na hivyo kuutenga mchezo au onyesho kutoka katika mtiririko wake. Kujitenga huku hufanya mtazamaji makini afikirie zaidi maana ya onyesho kwa ujumla.
Kwa hakika korasi ni kiungo muhimu sana kati ya tamthiliya na hadhira. Ni kipengele kilichojitokeza kutokea katika ibada za Kiyunani na matambiko kwa miungu wao na hata kuwa suala la kisanaa. Inajitokeza kama mhusika, kama muundo lakini zaidi kama mtindo katika tamthiliya ambao hauwezi kuepukika. Dhana hii ya korasi imetumiwa pia na wasanii wa tamthiliya za Kiafrika hasa Ibrahim Hussein na Penina Muhando. Lakini je dhana hii ni ya Kiafrika?
Marejeleo
Brecht, B. Plays Vol. 1, (1960) Methuen and Co. Ltd London
Brockett, O.G. History of the theatre, sixth edition, (1991) Allyn and Bacon. Boston
Browne, E.M. The Making of  T.S. Eliot’s plays, (1969), Cambridge University Press. Cambridge.
Cambridge, A.W.P. The theatre of Dionysus in Athens, (1956) Oxford University Press, London.
Fredly, G. na Reeves, J. A. A history of the theatre (1968), Crown Publishers, Inc.N.Y.
Hartnoll, P. (mh) The Oxford Companion to the theatre, third edition,(1967), Oxford University Press, London.
Lihamba, A. Politics and theatre in Tanzania After Arusha Declaration 1967-1984, Unpublished Ph.D Thesis (1985) University of Leeds.
Muhando, P. Tanzanian traditional theatre as a pedagogical Institution: The Kaguru case study. Unpublished Ph.D thesis (1983) University of Dar es Salaam.
Muhando, P na Balisidya, N. Fasihi na Sanaa za Maonyesho, (1976), Tanzania Publishing House, Dar es Salaam.
Nagler, A.M. A source book in theatrical history, (1952) Dover Publishers, Inc. N.Y.
Oates W.J. na O’neill, E.jr. (Wah). The Complete greek drama Vol.1 (1938), Random House; N.Y.
Smith, C.H. T.S. Eliot’s dramatic theory and practice (1963), Princetown University Press, New Jersey.
Thomson, G. Aeschylus and Athens, (1973), Lawrence and Wishart, London.
Willet, J. (Mh). Brecht on theatre, (1977), Hill and Wang New York.
Weisstein, U. Comperative Literature and Literary theory (1973), Indiana University Press Bloomington.
Kamusi na insaiklopedia
Encyclopedia Americana, Intaernational edition, Vol 6 (1980) Grolier Incoporated, Connecticut.
Simpson J. A na Weiner E.S.C. The Oxford English Dictionary. Second edition Vol. 3 (1979) London.
Webster’s New International Dictionary, Second edition (1961), Merrian Webster Inc. Springfield.
Webster’s Third New International Dictionary, (1986), Merrian Webster Inc. Springfield.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-26T03:38:36Z 2021-07-26T03:38:36Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=642 <![CDATA[MITAZAMO (NADHARIA) MBALIMBALI JUU YA SANAA ZA MAONYESHO]]>
Kabla hatujaanza kujadili mitazamo hii ni vema tukajua kwanza dhana ya sanaa, kwamba tunaposema sanaa tunamaanisha nini.
Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa, umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisi zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye dhana maalum.  Kuna aina kuu tatu za sanaa. Kwanza ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake kuonyeshwa wakati wowote. Hizi ni sanaa za uonyesho. Nazo ni kama vile uchoraji, uchongaji, ufinyanzi, kutarizi n.k. sanaa amabazo hututolea vitu kama vile picha, vinyago, nguo zilizotariziwa, vyungu n.k.
Aina ya pili ya sanaa ni sanaa za ghibu. Hizi ni sanaa ambazo uzuri wake haujitokezi kwenye umbo linaloonekana kwa macho au kushikika bali katika umbo linalogusa hisia. Mifano ni kama vile usahiri, uimbaji, upigaji muziki n.k. uzuri wa sanaa hizi umo katika kuzisikia.
Aina ya tatu ya sanaa ni sanaa za vitendo. Uzuri wa sanaa za aina hii umo katika umbo la vitendo, na ili kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama vitendo vikifanyika. Umbo hili linalazimisha kuwepo kwa mwanasanaa na mtazamaji wa sanaa mahali pamoja kwa wakati mmoja ama sivyo sanaa haikamiliki. Hali hii ndiyo iliyosababisha sanaa hizi za vitendo kuitwa sanaa za maonyesho, kwa sababu lazima wakati zinapotendeka awepo mtu wa kuonyeshwa, maana uzuri wake umo katika vitendo vyenyewe.
Kwa hiyo sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa nne ambazo ni:
  1. Dhana inayotendeka
  2. Mtendaji
  3. Uwanja wa kutende
  4. Watazamaji
Sasa baada ya kuagalia dhana ya sanaa za maonyesho, sasa tuangalie nadharia zinazojaribu kuelezea sanaa za maonyesho. Nadharia hizi zipo tatu ambazo ni:
  1. Sanaa za maonyesho ni michezo ya kuigiza, ama ni michezo inayoonyeshwa kwenye jukwaa lenye pazia na mataa mengi ya jadi au ni michezo ya Shakespeare.Huu ni mtazamo mmoja wapo ambapo baadhi ya wataalamu wanaamini hiyo, kwamba sanaa za maonesho lazima zichezwe jukwaani, kuwepo na pazia na mataa mengi.
Tukizingatia nadharia hii huenda tukaamini kuwa sanaa za maonyesho ni tamthilia tu. Kitu ambacho kinaleta mashaka kidogo.  Inafahamika kuwa tamthilia ni utanzu ulioletwa na wakoloni hapa Afrika Mashariki. Kwa hiyo, kuamini nadharia hii ni sawa na kusema kuwa hakuna sanaa za maonyesho zenye asili ya hapa Tanzania ama Afrika Mashariki. Au kwa upande mwingine ni sawa na kusema kuwa kabla ya mkoloni kutuletea tamthilia sisi tulikuwa hatuna sanaa za maonyesho zetu wenyewe. Wazo hili si kweli na ni wazo potofu.   (Taz. Mhando &Balisidya 1976).
Kimsingi mtazamo huu unatokana na fasili ya sanaa za maonyesho inayodai kuwa sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa za mchezo, mchezaji, uwanja wa kuchezea na watazamaji. Ingawaje ufafanuzi huu ni sawa lakini hata hivyo mtazamo huu ni dhaifu kwani ulitokana na watu waliokuwa wakifafanua sanaa za maonyesho wakiegemea zaidi kwa zile za utamaduni wa kizungu. Ufafanuzi huu haukuzifikiria sanaa za maonyesho zenye ya utamaduni wa Kitanzania.
Dosari kubwa katika ufafanuzi huu imo katika neno mchezo (play). Neno hili lina maana duni likilinganishwa na hali na umuhimu wa sanaa za maonyesho zenye asili ya Kitanzania/Kiafrika. Tukichukua kwa mfano unyago, jando, kusalia mizimu, au masimulizi ya hadithi, ambayo ni mifano ya sanaa za maonyesho zenye asili ya Kitanzania, tunakuta zile sifa zote nne zipo. Isipokuwa tunajua kuwa shughuli zote hizi siyo mchezo na umuhimu wao hauruhusu hata kidogo kuingiza neno mchezo. Shughuli hizi zina maana muhimu ambayo inahusu maisha ya binadamu katika jamii yake. Ni shughuli zinazobeba wazo maalum lenye lengo la kujenga utu wa mwanajamii. Basi vipi tuseme shughuli hizi zina sifa ya mchezo?  Wenzetu wazungu wanaridhika na neno hili kwa  sababu sanaa za maonyesho za utamaduni wao mara nyingi zinafanywa kwa masihara tu. Sanaa za maonyesho zao zaidi ni kwa madhumuni ya kujiburudisha au pengine kutafuta kipato. Lakini kila aina ya sanaa za maonyesho ya Kitanzania ina dhana fulani ndani yake, kwa mfano dhana kuhusu maana ya maisha, kuhusu utekelezaji wa madaraka ya kiutu uzima,  kuhusu ushujaa, mafunzo ya historia ya jamii n.k.
Kwa hiyo basi sanaa za maonyesho za Kiafrika ni dhana zilizo kwenye umbo linalotendeka na siyo mchezo. Kutokana na utamaduni wa Kiafrika tunaweza kusema kuwa: sanaa za maonyesho ni dhana inayotendeka. Na ili dhana hii itendeke anahitajika mtu wa kuitenda (mtendaji). Mtendaji huyu huhutaji uwanja wa kutendea hiyo dhana na wakati akiitenda wanakuwapo watazamaji.   
         2. Sanaa za maonyesho ni vichekeso au ni maigizo yanayochekesha.
Wazo hili linatokana na historia ya sanaa za Maonyesho hapa Tanzania. Wakati mkoloni alipotuletea sanaa ya Maonyesho ya kikwao sisi tulishiriki katika tamthilia za Shakespeare kama washiriki au watazamaji tu. Kwani tamthilia hizi hazikuwa na maana yoyote kwetu kutokana na kuwa zilibeba na ziliongelea utamaduni wa kizungu. Tulifurahishwa na vile vitendo vilivyofanywa kwenye jukwaa katika tamthilia hizi na hivyo vitendo hivi vilituchekesha tu. Basi jambo kubwa kwa Mwafrika ikawa ni vile vichekesho na hivyo kudhani kuwa jambo muhimu katika tamthilia ni kule kuchekesha kwake.
  1.  Sanaa za maonyesho ni maigizo.
Wazo hili limetokana na tafsiri mbovu ya neno play ambalo limetafsiriwa kuwa mchezo wa kuigiza. Inawezekana aliyetafsiri neno hili alifuata nadharia za zamani sana za drama, ambapo ilidhaniwa kuwa uigizaji (imitation) ndio kiini cha drama. Hata hivyo nadharia hii ilitupiliwa mbali kwa vile haikudhihirisha kiini hasa cha drama. Tafsiri hii ndiyo imeleta matatizo hapa Tanzania katika kufahamu sanaa za maonyesho. Wengi wamepotoshwa na wazo kuwa uigizaji ndio kiini cha sanaa za maonyesho kama vile neno michezo ya kuigiza linavyoonyesha. Hivyo, hata katika kutazama sanaa za maonyesho za asili wengi wamekuwa wakitazama iwapo kuna uigizaji. Na hapa wengi wanakwama kwani katika unyago, jando, kusalia miungu n.k hakuna uigizaji bali wanaoshiriki wanashika nafasi fulanifulani. Hivyo ni bora kutumia neno tamthilia pale tunaporejelea neno plays.
Kwa ujumla kuwepo kwa mitazamo hii huweza kuwa kumesababishwa na mambo yafuatayo:
  • Wakoloni kutokutambua ama kwa makusudi ama kwa kutokuelewa kuwa tulikuwa na sanaa za maonyesho za kwetu, hivyo akatuletea drama kama vile anatuletea sanaa mpya ambayo aina yake haikuwepo hapa kwetu. Hivyo, mkazo wa sanaa za maonyesho ulitiliwa katika drama tu.
  •  Mkoloni alitumia mbinu mbalimbali za kufuta vitendo vyote ambavyo hasa ndiyo sanaa zetu za maonyesho. Mfano alitumia dini ya Kikiristo kupiga vita vitendo kama vile unyago, jando, kusalia mizimu n.k ambavyo viliitwa vya kishenzi.
  • Tafsiri mbovu zinazofuata nadharia zilizopitwa na wakati kama ilivyoelezwa hapo awali.
Kwa hiyo, tukisema sanaa za maonyesho, tunarejelea vitendo maalum vyenye sifa zilizotajwa na kujadiliwa hapo awali. Hata hivyo tutambue kuwa sifa hizi ingawaje ziko sawa lakini kimsingi zinatofautiana katika uzito wake baina ya jamii moja na nyingine. Hatutazamii sanaa za maonyesho za Kihindi kuwa sawa kabisa na zile za Kijapani au za Kiafrika. Ingawa zote ni sanaa za maonyesho zina misingi tofauti kutokana na tofauti za utamaduni wa jamii husika.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-26T03:28:31Z 2021-07-26T03:32:03Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=641 <![CDATA[NAFASI YA SANAA KATIKA UCHUMI]]> Nafasi ya Sanaa Katika Uchumi

Hashim A. Nakanoga
Sanaa na uchumi vimekuwa vikiishi pamoja toka karne nyingi ama tuseme toka binadamu alipoanza kuishi wakati ambao tunaamini sanaa nayo ilianza. Ilitangulia sanaa uchumi ukafuata, Uchumi hutua mahalipopotepenyethamani, nasanaa inathamani.
Sanaa ina matawi makubwa mawili, hisi na zana. Kwenye matawi haya mawili kuna mgawanyiko wa kazi nyingi kwa kila tawi mojawapo.
Mifano mizuri ya sanaa za hisi ni sanamu za kuchongwa, picha za kuchorwa. Sanaa hizi hutengenezwa kwa madhumuni ya kufichua, kudhihirisha na kutafsiri hali halisi ya uhai, ama kuchokozafikra.
Katika sanaa ya hisi kuna hisia na mawazo ya msanii. Msanii akiwa mwenye mpango mzuri na mtulivu ama mwenye fujo na vurugu huonekana katika kazi yake ya sanaa. Sanaa ya hisi humueleza mengi sana mtazamaji. Mwonaji anaweza kufahamu mazingira ya msanii yalivyo na kiasi cha maendeleo ambacho jamii ya msanii huyapendelea sana katika maisha yake na yale ambayo huyachu kia.
Zaidi ya hivyo, mwonaji anaweza kugundua fikra za msanij, maisha na matatizo yake. Sanaa ya hisi pia huweza kukumbusha jambo lililotokea muda mrefu uliopita ama kuelezea tukio muhimu linalotokea sehemu fulani na pia kutabiria jambo kubwa litakalotokea baadaye sana kitaifa au kiulimwengu. Vile vile sanaa huweza kuchochea hisia za waonaji katika ukiwa ama sherehe, mahaba ama chuki, furaha au huzuni, joto na baridi, mchangamko ama mzizimo.
Sanaa za zana ni vifaa vinavyotengenezwa kisanii vikiwa vimekamilika katika mikono ya msanii ama kiwandani. Kama vina usanii na vimetengenezwa kwa ajili ya matumizi tunaziita sanaa za zana. Kwa mfano, chanuo, viti, mikeka, kanga, viatu, marimba, migono, vinu, mitungi, nyumba, pete, heleni, vidani navingine vingi ambavyo hatutaweza kuviorodhesha katika sura hii. Sanaa za hisi na za zana zlna nafasi maalum katika uchumi. Nafasi hii itaonyeshwa katika sehemu tatu, yaani sanaa na uchumi, sanaa viwandahi na sanaa za msanii binafsi.
SANAA NA UCHUMI HAPO ZAMANI
Sanaa imedumu toka binadamu ameanza kuishi kwasababu msanii huzaliwa. Msanii huzaliwa nabaada ya hapo ndipo mazingira yake yanapoingia moja kwa moja katika kumlea na kumwongoza, kumtajirisha kifikra na inapowezekana kumwendeleza. Hivyo basi, tuelewe kwamba kila penyejamii ya watu panawasanii wa fani mbalimbali. Kuna waimbaji, watunzi wa hadithi, washairi, wacheza ngoma, wachongaji na wachoraji.
Mwanzo wa sanaa ni hisia za msanii. Kutokana na msukumo wa hisia, msanii huanza kuunda sanaa zake. Ndipo anapofahamika kwamba yeye ni msanii na hapo huanza hali ya kutegemewa katika kazi zinazohusiana na sanaa kama ile ambayo msanii amekwisha ionyesha. Bila shaka wengi wetu tunafahamu namna ambavyo wakale wetu wa mwanzo kabisa walivyoanza kuishi na jinsi hatua zao za maendeleo zilivyokuwa zikibadilika mpaka kufikia hali tuliyonayo hivi sasa. Kuna wakati ilibid, watumie mawe kama silaha ama vifaa vya kukatia Mawe haya waliyachonga wenyewe. Ingawa pengine kila mtu alishiriki katika uchongaji huo ilifika wakati, wenyewe kwa pamoja walijigundua kwamba mmoja kati yao aliweza kuchonga vizuri zaidi ya wengine. Huo ukawa mwanzo wa kumtegemea kwa utengenezaji wa vifaa hivyo.
Kumtegemea msanii kwa namna kama hii hakukuwa kumeishia hapo tu kwa sababu bingwa huyo alikuwa akichonga silaha zake pamoja na silaha za wengine. Hivyo basi muda mwingi aliutumia kwa kazi hiyo kiasi ambacho haikuwa rahisi kwake kufanya mambo mengine ambayo vile vile ni muhimu kwa maisha yake, kama vile kuwinda. Kutokana na hali hiyo wenzie walilazimika kumpa sehemu.ya mawindo yao kufidia muda ambao binawa huyo aliutumia kuwatengenezea vifaa walivyohitaji. Kubadiliishana kwa namna hii’kuliendelea kudumu sio katika silahaza mawe na mawindo tu, bali ulikuwa kufuatana na mahitaji yalivyoongezeka.
Hali iliendelea kuwa hivyo mwaka hata mwaka na mpaka kufikia wakati ambao wazazi wetu hao walianza kutumia vyungu kwa kupikia, kukalia vigoda na kuvaa nguoza magomeya miti.
Uchumi ulijihusisha na sanaa kwa sababu sanaa toka mwanzo na daima inatawala sehemu kubwa sana karibu asilimia tisini na tisa ya mahitaji ya binadamu. Kadri wazazi wetu walivyokuwa wakipiga hatua za maendeleo ndivyo mahitaji yalivyozidi kuongezeka. Mahitaji haya yalitofautiana katika sehemu tatu muhimu; nyenzo, bidhaa na hisia. Sehemu kubwa ya mahitaji na ambayo tunaamini ndiyo waliyoanza nayo mababu zetu wa awali ni nyenzo. Baadae walihitaji vyombo kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani. Ndipo yalipofuata mahitaji mengine yanayohusiana na hisia. Tutazame basi uhusiano ulivyokuwa kati ya uchumi na sanaakatikavipengele hivi vitatu vya nyenzo, bidhaa na hisia.
Tunapotaja neno nyenzo kwa karne ya sasa ambayo imepiga hatua kubwa katika taaluma ya ufundi maana ya nyenzo inabaki palepale lakini inaeleweka kimapana zaidi. Hatahivyovitu vinavyohesabiwakatika fungu la nyenzo ni vingi mno na vinazidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda mbele. Nyakati hizo za mababu zetu sanaa za zana walizotengeneza ni zile zilizosaidia katika kuleta uchumi wa kumuwezesha kuishi. Nyenzo yakwanzakabisa iliyotumiwa ilikuwa ni mawe. Wakati mwinginewaliweza kuchukuaainafulani ya miti migumu na kuichonga mfano wa mikuki. Mawe na miti waliyochonga waliitumia kwa kuwindia na kukatia nyama ama kukatia baadhi ya matunda makubwa waliyofanikiwa kuyapata. Baadaye walilazimika kuacha nyenzo ya mawe kwa kuwindia na kukatia, wakavumbua nyenzo zilizo borazaidi kamavile visu, nyengo, mikuki na majembe. Hali hii ilifikiwa walipogurdua maisha ya kuishi pamoja. Walitumia majembej kwa kulimia na kujipatia mzazo zaidi. Mikuki ilitumiwa kwa kuwindia. Wakati mwingine kutokana na migongano baina ya vikundi au familia na familia, ama kushambuliwa na wanyama, walitumia mikuki hiyo kwa kujilinda.
Uvumbuzi wa nyenzo mbalimbali za uchumi uliendelea na zana nyingi tofauti zilitengenezwa kutokana na maendeleo yalivyohitaji. Ndivyo tulivyoanza kupata mashoka, mapanga, migono na bunduki aina ya gobole. Baadhi ya zana hizo zilitumiwa kwa kuwindia na nyingine kuzalishia mazao zaidi. Ili aliyekuwa na mazao aweze kupata mawindo na aliyekuwa na mawindo apate mazao va chakula, na kwa kuwa hakukuwa na mfumo wa fedha, ilibidi wateja haowabadilishanemali zao.
Walipoanza kutumia vyakula vya mashambani, waligundua kuwa walihitaji vifaa maalum kwa matayarisho mbalimbali ya mazao yao. Baadhi yavifaa hivyo ni pamoja na vyombo vya kusagia nafaka, vya kuwekea chakula wakati wa kula, kunywea maji, kukaliana mavazi.
Wakati wa kula waliweka vyakula vyao juu ya majani mapana ama majani ya migomba. Hata maji walikunywa kwa kutumia majani waliyoyakunja kiufundi sana kiasi cha kuweza kuhifadhi maji. Kidogo kidogo walianza kutumia nyungo ndogo (vitunga) kwa kuwekea vyakula na kunywea maji wakati wa kula. Siku zilivyoendelea waligundua kutengeneza sahani na mabakuli ya miti kwa ajili ya chakula na kata za miti amamatunda magumu kwa kunywea na kutekeamaji.
[Image: p104.gif]
Jani la kunywea maji
Kimavazi, mababu zetu walianza kwa kujifunga majani kuhifadhi sehemu muhimu. Waliendeleakidogo kidogo wakafikia kutunga vijiti vingi walivyovivaa aidha kuzunguka kiuno kizima ama kuficha sehemu kidogo. Baadae kati yao wakatokea wasanii wa kutengeneza vazi la magamba ya miti Kutokana na kukaa pamoja, walifikiwa na hali ya kuzingatia usafi. Hivyo waliamua kukalia majani na mara nyingi kwa kuwa kiongozi wa familia au kikundi, nyakati za mahakama zao, mikutano ama ulaji walitaka aonekane tofauti walimtengenezea kigoda akalie. Siku zilivyoendelea, kigoda walikichukua kama kikalio cha kawaida kwa mtu yeyote kwa hiyo kiongozi wao walimtengenezea kigoda cha ainayapekee, tofauti kabisa na vigodavingine. Badala yakukalia majani walitengeneza majamvi na mikeka.
Vyakula walivyokula nyakati hizo walipoanza kutumia mazao ya mashambani ni vile vilivyohitajika kupikwa. Hivyo ilibidi watengeneze vyungu vya udongo kwa kupikia na walifinyanga mitungi kwa kuhifadhia maji. Baadae walitengeneza miundo tofauti ya vifaa hivyo vya udongo kwa matumizi ya aina mbalimbali katika mapishi, hifadhi ya maji ama hifadhi ya vyakula vyao.
Vifaa hivi, vinu, sahani, na mabakuli ya miti, kata, vazi la magamba ya miti, vigoda, mikeka, vyungu, na mitungi ya udongo tunavihesabu katika fungu la sanaa za zana kama bidhaa. Lugha ya biashara iliyokuwa ikisimama kati ya sanaa hizi za zana, mazao ya kilimo na mawindo ni kubadilishana. Ilibidi watu wawili waelewane na kukubaliana kwa thamani ya bidhaa walizotaka kubadilishana. Kama mkulima alitaka kupata kinu ilibidi aongee na mchongaji afahamu mchongaji huyo alitamani nini kati ya mpunga, mtama au mahindi. Pengine kama mchongaji alitamani mpunga walifikia uamuzi katika kukisia kwa kinu kimoja wangepimiana vitunga vitatu, vinne au hata sita, kufuatana na kinu kilivyothaminiwa na mpunga ulivyothaminiwakwa nyakati hizo.
[Image: p106.jpg]
2. Kufinyanga Mitungi
Tukiacha nyenzo na bidhaa kama vitu vya kuzalishia mali na vyombo vya matumizi ya nyumbani jamii yeyote ile huwa na nyakati za furaha na huzuni.
Nyakati za furaha hasa kama baada ya mavuno maadhimisho ya harusi ama ilipofikia kijana wa kike au wa kiume kutolewa kutoka katika jando na unyago, jamii iliyohusika ilifanya sherehe. Katika sherehe mambo mengi yalihitajika. Kwa mfano mavazi au mapambo maalum yaliyohusiana na tukio ama vifaa muhimu vilivyohitajika kuandamana na sherehe. Ilihitajika mitungi, mikeka, vyungu, vinu michi na nyungo kumsindikizia biharusi kwenye ndoa, au kumkabidhi kijana wa kiume mkuki, sime, kisu ama mshalena upindebaadayajando.
Sanaa hizi walizinunua au kuzipata kutoka kwa wasanii katika hali ileya kubadilishana. Mbali nasanaa hizi za zana kutumika katika sherehe, kuna sanaa maalum ambazo zilitengenezwa na kununuliwa kwa madhumuni ya kuhifadhiwa kutokana na uzuri wake.
Katika kuishi pamoja, jamii hizo za mababu zetu zilikua na kuendelea. Kukua huko kwa jamii kulisababisha utawala uingie. Mara nyingi mtawala alipenda kuwa na vitu vyenye thamani au vizuri zaidi ya vile walivyokuwa navyo watu aliowatawala. Watawala hao waliteua wasanii hodari ili wasanii hao wawaundie sanaazapekee.
Sanaa zilitumiwa hata katika ibada. Imani katika dini ilikuwapo tangu enzi ya mababu zetu, ili imani ile iwe na nguvu kwao ijenge sawa sawa ilibidi kiongozi wa kizazi hicho ashughulikie uumbaji wa sanamu ya mkale wao. Hata hivyo hawakusita kutaka ushauri wa msanii. Kwa njia hii wasanii waliheshimiwa kwa kazi zao nzuri na hivyo walitunukiwa zawadi katika kufikiriwa kwamba walikuwa na uwezo wa kuunda sanamu.
Sanaa Viwandani.
Kuna mabadiliko mengi yaliyotokea katika utengenezaji wa sanaa. Baadhi ya sanaa za zana zinaendelea kutengenezwa na kumalizika mikononi mwa msanii mwenyewe. Sehemu nyingine ya sanaa za zana huchukuliwa mawazo ya msanii yakiwa katika mchoro, ramani au pambo yakaendelezwa na kuzalisha sanaakatika mashine.
Pamoja na kuwa na hali ya namna hii sanaa sasa hufanywa hata viwandani. Kwa hiyo tunao uchumi unaoletwa na sanaa kutoka viwandani, uchumi unaoletwa na sanaa kutoka kwa vikundi vidogo vidogo vilivyojiunga na uchumi unaoletwa na sanaa kutoka kwawasanii binafsi.
Kwa muda mrefu tulikuwa tukinunua kutoka Ulaya sanaazazanazinazozalishwaviwandani. Lichayakuwa utengenezaji wake ulitegemea mali ghafi kutoka huku kwetu, kama vile pamba na ngozi. Sanaa hizi zilitugharimu pesa nyingi sana za kigeni. Hivyo ununuaji wake ulidhoofisha uchumi wetu.
Ndipo nchi yetu ilipochukua hatua ya kujenga viwanda vya kutengeneza sanaa za zana zilizo muhimu kwa uchumi wa taifa na kwa mahitaji ya wananchi. Vilijengwa kwanza viwanda vinavyotumia mali ghafi inayopatikana humu humu nchini. Kati ya viwanda hivi nivilevinavyotengenezanguo, viatu navitabu.
Tunavyo pia viwanda vingine kama Kibo kiwanda cha kutengeneza karatasi, kitichopo Chang’ombe, Dar es Salaam, ambacho mbali na utengenezaji wa karatasi, uchumi wake mkubwa unapatikana katika uchapaji wa picha za vielelezo zinazowekwa kwenye makopo kama yale ya kahawa na makasha ya madawa ya aina mbalimbali ama sabuni. Kiwanda kingine ni kiwanda cha Kauri kilichoko Chang’ombe Dar es Salaamchakutengenezavikombe, sahani nabakuli.
Uchumi unaoletwa na utengenezaji wa nguo hlvi sasa ni mzuri sana. Tuna viwanda vya nguo kwa mfano Urafiki, Mwatex, Kiltex, Sunguratex, Mablanketi na vingine vinavyojengwa Mbeya, Morogoro, Musoma na Ubungo. Viwanda hivi vinazalisha nguo za kutosheleza mahitaji ya wananchi na kiasi kuuza nchi za nje. Sehemu ya nguo zetu zinauzwa huko Ulaya na soko lingine kubwa zaidi ni majirani zetu katika ukandawa Afrikaya Mashariki.
Pamba ambayo tulikuwa tukilima na kuuza nje kwa bei hafifu, baadaye kununua kwa bei ghali nguo zilizotengenezwa kutokana na pamba yetu sasa, tunahakjkisha tunaishughulikia wenyewe mpaka kuuza nguo kamili. Nguo zinazozalishwa katikaviwandayyetu ni haki, jinja, bafta, shuka na mablanketi. Uchumi mkubwa unaletwa na uzalishaji wa kanga, vitenge, vitambaa vya magauni na mapazia. Mara nyingi zao lolote linalohusisha mkono wa msanii thamani yake huongezeka.
Kwenye viwanda hivi kuna wasanii wanaobuni mapambo ya nguo. Michoro yao inatumika katika kuchapa kanga, vitenge, vitambaa vya magauni, mapazia nasehemu nyingine hutumika kuchapashuka. Ndipo bidhaa hizi zikazidi thamani.
Kazi ya msanii katika sehemu hii ya uchumi wa viwandani ni nzuri sana. Mfano wa hali halisi ilivyo tunaweza kuuona katika takwimu ya mazao ya viwanda vyote vya nguo vilivyo chini ya Texco kwa mwaka 1977 namwaka 1978.
              MAZAO YA NGUO KATIKA METARI
                                                               MWAKA 1977                                         1978
AINAYAMAZAO
METARI                                                 METARI
Khanga                                                    12,251,000                                            10,609,000
Kitenge                                                    13,808,000                                            14,119,000
Gauni                                                       3,605,000                                              3,241,000
Pazia                                                         58,000                                                  36,000
                                                              29,722,000                                              28,005,00
Marekani                                                4,699,000                                                 4,094,000
Lineni                                                     9,328,000                                                15,344,000
Palini                                                       788,000                                                  725,000
Kaki                                                        3,675,000                                                 9,648,000
Sufi                                                         1,793,000                                                 2,710,000
Twili                                                        2,980,000                                               1,480,000
Kitambaa
chashati                                                  1,698,000                                               1,811,000
Shuka                                                     4,762,000                                               3,567,000
Jinja                                                        568,000                                                 656,000
Bed Sheeting                                           2,289,000                                               1,513,000
Mulmul                                                   1,888,000                                               1,559,000
Polyster                                                 1,413,000 –
Mengineyo                                             429,000                                                   439,00066,
                                                                                                                           131,000
                                                                                                                           71,652,000

Takwimu zinatuonyesha kuwa katika miaka miwili hii, aina ya bidhaa zilizozalishwa kwenye viwanda vya nguo vya Taifa ni kumi na nane. Katika aina hizi zote, bidhaa nne, Khanga, Kitenge, Vitambaa vya gauni na mapazia ambazo ukilinganisha zinachukua nafasi ya asilimia 22 tu.ya aina zote, zimeweza kuzalishwa kwa wingi mno kufikia asilimia 41.8 va wingi wa mazao yote. Hii inadhihirisha kwamba bidhaa hizi, khanga, na kitenge zinapendwa sana na hivyo hutolewa zaidi. Kupendwa huku kunatokana na kazi za usanii ambazo zimehusishwa katikakuzalisha bidhaa hizi nakuzipatia umaarufu. Pengine msomaji atashangaa kuona kuwa kuna bldhaa mbili nyingine za lineni na kazi zimechukua nafasi nzuri vile vile. Hii ni kwa sababu ya umuhimu wa vazi la kaki kwa kazi na lineni kwa hali ya hewa hapa nchini. Wakati huo huo viwanda vya nguo vimeipatia nchi fedha za kigeni kiasi cha shilingi 15,000,000 kwa kipindi cha miaka miwili 1977 na 1978. Katika mauzo hayo ya nchi za nje kiasi kikubwa kilitokana na Khangana Vitenge.
Tuchukue mfano mwingine wa kiwanda cha viatu cha Bora kilichoko Barabara ya Pugu, Dar es Salaam. Kwa muda mrefu bidhaa hii ilikuwa ikiagizwa kutoka nje nakuigharimu nchi yetu kiasi kikubwachafedhaza kigeni. Hali hii iliongeza tatizo la kudhoofisha nchi kiuchumi. Hivi sasa viatu vinatengenezwa katika kiwanda cha hapa hapa nchini na tunao wasanii katika kiwanda hiki cha viatu ambao kazi yao ni kubuni mapambo mbalimbali yanayotumiwa katika kutengenezea viatu vya miundo tofauti, kama vile wachoraji wa mapambo ya khanga wanavyobuni michoro itumikayo katika nguo.
Sanaa na Msanii Binafsi
Hapa itatubidi kwanza tuangalie kuna wasanii wa aina ngapi. Kiitikadi wasanii wote ni sawa. Msanii ni msanii awe wa fani yoyote ile lakini ni msanii. Tofauti yao kubwa iko katika lugha na ala wanazotumia wanapotaka kuutengeneza usanii wao.
Wasanii wana fani nyingi za sanaa kama kuchonga, kuchora, kufinyanga, kusuka na nyingine nyingi zote zikitafsiri sanaa za hisi au sanaa za zana. Kilamsanii hutengenezasanaa ambayo imemchepukia zaidi. Mwingine hutokea kuchepukiwa na fani nyingi, mwingine akawa katika fani moja tu. Itakuwa vizuri tukiwaweka kila mmoja na fani yake ili tuwe na picha iliyokamili.
Kwa mfano, mchongaji, hutumia mpingo ama pembe za ndovu kama nyenzo. Vifaa kama tezo, patasi, tupa na msasa ni zana. Msanii huyu ili afanikiwe na kazi yake inambidi awe na mtaji wa kutosha kununulia pembeza ndovu au mpingo. Labda tofauti iliyopo ni bei kati ya mpingo na pembe. Kwa hiyo ikiwa mchongaji huyo anataka kujiimarisha na kazi yake na awe na mtaji, itambidi aanze kwa kuchonga sanamu ndogo ndogo, mpaka atakapokuwa na mtaji wa kutosha kununua miti mikubwa au pembe.
Kutokana na hali hii, mchongaji, anapotaka kuipangia bei sanamu aliyoichonga, huangalia gharama aliyotumia kununulia nyenzo, kazi aliyoifanya, muda alioutumia kuifanya kazi hiyo, zana alizotumia na muundo aliodhamiria kuuchonga ikiwa amefikia hatua aliyoikusudia.
Soko kubwa kwa wachongaji ni nchi za nje, watalii na wakati mwingine Shirika la Uuzaji wa Sanaa hununua sanamu hizo na kuzisafirisha nje ama kuuza katika maduka yake yaliyomo humu humu nchini. Ili mchoraji afanye kazi yake, huhitaji kitambaa cha marekani, turubai ama bodi gumu kama uwanja wa kuzungumzia, rangi, mafuta ya kulainishia rangi, mafutaya kuoshea rangi nabrashi kamazana. Rangi za mafuta si rahisi kupata hapa nchini. Mradi rangi hizo zimeadimika basi inakuwa ghali mara dufu. Hivyo mchoraji akizipata anahakikisha atakapoitumia siyo penyemazungumzo madogo madogo.
Msanii huyu inambidi awe na uwezo wa kuzipata hizo rangi kwanza pamoja na kuwa na mtaji. Wengi wao wanaweza kuwa na mtaji wakashindwa kuzipata hizo rangi. Uchoraji uko wa namna nyingi. Uko uchoraji wa kutumia rangi za maji, penseli tupu, wino na mkaa kwenyekaratasi.
Hapa inategemea mchoraji alichagua kutumia zana ipi na uwanja upi wa kuundia sanaa yake. Gharama ya vifaa vya kazi, usanii wake, muda alioutumla katika usanii, dhana na hadhi ya msanii, ndio msingi wa bei ya sanaa. Wakati mwingine msanii anaweza kuajiriwa achore picha kubwa ya ukutani, hivyo bei itategemea msingi huo.
Masoko ya picha hizi za kuchora hutegemea mchoraji na vifaa alivyotumia katika kuchora. Mara nyingi picha zilizochorwa kwa rangi za mafuta ndizo zenye bei kubwa, lakini hata hivyo thamani ya picha inategemea msingi huo huo.
Msanii wa kufinyanga huhitaji shaba, chuma cha kumimina au saruji na mchanga, chokaa, udongo wa tope na maji kama nyenzo. Kazi hii huwa nzitb kutegemea na sanaa inayotakiwa kutengenezwa. Kutokana na gharamaya nyenzo, mtaji ni kitu muhimu. Kazi kama hii ikifanywa kwa maagizo maalum ni rahisi kupata nyenzo kutoka kwa mwajiri.
Msanii mwingine ni wa sanaa za kusuka. Huyu husuka vikapu, mikeka, nyungo, migono na majamvi. Kwa msukaji inategemea anataka kusuka kitu gani. Kama ni kikapu na majamvi, atahitaji milala kama nyenzo. Ikiwa anataka kusuka migono au nyungo atahitaji mianzi.
Chanzo &t&t&t&t&t&t&t&t]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-26T03:10:45Z 2021-07-26T03:10:45Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=640 <![CDATA[NAFASI YA SANAA KATIKA ELIMU TANZANIA]]>
L.A. Mbughuni
Sura ya kwanza ilijadili jinsi tunavyoweza kuunda falsafa ya Sanaa za Tanzania. Katika sura hiyo tuliona kwamba, uundaji wa sanaa hapa Tanzania, Afrika na mahali pengine pote duniani una malengo matatu muhimu ya kimsingi na ya jumuiya. Malengo hayo ni kuburudisha, kufunza maadili ya jamii au kutoa funzo maalum na kuitia jamii motisha wa kufuata na kutimiza mafunzoyenyemaadili katika maishayakilasiku.
Kwa hiyo lengo la kwanza muhimu la sura hii ni kujadili kwamba: sanaa isiyo na tumizi lolote au isiyotoa elimu au funzo lenye maadili ya jamii ya msanii, sanaa hiyo haijatimiza malengo yake mawili muhimu ya kimsingi katika uundaji wake kwani sanaa isiyonafunzo lenyemaadili ya jamii, haijakamilika, na kukomaa kisanii na msanii wa sanaa hii hajatimiza sehemu moja muhimu yawajibu wakekwajamii.
Mjadala wa kwanza wa sura hii utatumia mifano ya Sanaa za aina ya zana na zile za aina ya hisi yaani sanamu za picha za kuchora, picha za aina ya posta na vielelezo. Nia ya mjadala huu ni kufafanua jinsi sanaa itoavyo funzo au elimu wakati inapotumika katika maisha ya kila siku, mashuleni, katika vitabu, majarida, magazeti na katika matangazo ya biashara.
Lengo la pili muhimu la sura hii ni kutoa mifano maalum inayodhihirisha uhusiano mkubwa uliopo kati ya sanaa na elimu kwa kuhaklkisha kwamba, sanaa kamilifu halplngani na misingi ya asili yake au chimbuko lake. Kwa hlyo mjadala wa lengo la pili na la sura hii, nia yake ni kudhihirisha kwamba: Sanaa inayopoteza lengo na matumizi ya asili yake, sanaa hiyo hupoteza hadhl yake na hatlmaye Itafifia kisanii katika jamii yake, mpaka uundaji wa sanaa hiyo ulimbuke katika misingi na matumlzi mengine katika Jamii nylnglneau ya msanil.1
Quote:1Tangu awali sanaa ya aina va lipiku, lengo lake ni elimu na sherehe za jando baadhi ya jamu ya Makonde Jamn nyingi za Ulaya huheshimu lipiku kama sanaa bila ya kuiali matumizi yake kwa Wamakonde Na jamii mpya, huhifadhi sanaa hiyo makumbusho na kufundisha historia ya Wamakonde.
Lengo muhimu la tatu la sura hii ni kujadili na kutoa mifano michache itakayoonyesha na kudhihirisha kwamba sanaa Inaweza kutumika kikamilifu katika kufunza jamii na katika kudumisha misingi ya Taifa la Tanzania ya Elimu ya Kujitegemea, kama ilivyo elezwa na Mwalimu J.K. Nyerere, katika Elimu ya Kujitegemea (1967). Elimu ya Kujikomboa (1974), Azimlo la Arusha (1967) na sera nyingine za ChamanaSerikali.
Mjadala wa lengo la tatu na la mwisho la sura hii una nia ya kuonyesha na kuthibitisha kwamba, Sanaa muhimu ya wakati wowote, katika historia ya mapambano, baina ya jamli na mazingira yake, ni ile itumiayo usanifu wa hali ya juu katika uundaji, matumizi fulani, pamoja na kuipa jamii hamasa ya kufuata maadili ya maisha ya jamii hiyo, ili jamii iweze kufikia malengo yake katika hali zote muhimu za malsha: hamasa hiyo hutolewa kama elimu na kishawishi cha Sanaa inayohusika:
SANAA NI EUMU
Hapa Tanzania na duniani pote, elimu ni utaratibu uliokusudiwa kuongoza maarifa ili jamii ifikle malengo yake. Kwa Tanzania, malengo ya uongozl wa maarifa ni kutayarisha – jamii yenye maadili ya kljamaa na kujitegemea.
Kuna alna mbili za utaratibu wa kuongoza maarifa hapa Tanzania na duniani pote. Aina ya kwanza ni utaratibu utumikao katika shule zetu na vyuo. Alna ya pili hutumika nje ya shule na vyuo vy.etu. Lakini alna zote mbili zilikuwepo hapa Tanzania tangu zamani na aina zote mbili hivi sasa zinatambulika na kuheshimika katika taifa letu kwamba ni muhimu kwa jamii ya Tanzania katika kufikia malengo yetu ya Ujamaa na Kujitegemea.
Kwa sababu Mwalimu J.K. Nyerere (1967) alitoa maelezo kamili kuhusu madhumuni na malengo ya elimu ya kujitegemea hapa Tanzania, hatutarudia mraelezo hayo katikasura hii.
Sasa hatuna budi kuonyesha nafasi ya sanaakatika elimu kwa misingi ya maana hii na maelezo yaliyotolewa na Mwalimu J.K. Nyerere katika Elimu ya Kujitegemea, kuhusu madhumuni namalengoyaelimu hapa Tanzania, katika kujenga na kuadilisha Jamii ya Tanzania kufuatia maadili ya ujamaa na Kujitegemea.
Ikiwa maana ya elimu iliyotolewatunaikubali, basi sanaa ni elimu ikiwa sanaa zitatumika kama’utaratibu uliokusudiwakuongozamaarifa, tokakizazi hadi kizazi, ili kuwezesha jamii yoyote kufahamu’ na kufikia lengo maalum.
Kwa hapa Tanzania sanaa za mapangoni za Kondoa Irangi au sanamu ya Askari iliyoko mtaa wa Independence, Dares Salaam ni elimu kamasanaa hiyo ni utaratibu uliowekwa kwa makusudio ya kuongoza maarifa kwa watu wa Tanzania toka kizazi hadi kizazi.
Elimu ni lengo muhimu lasanaa kwasababu, moja ya asili za sanaa ni Elimu. Sanaa zote za hisi zina mawasiliano ya lengo na ujumbe maalum, lakini ni baadhi tu ya sanaa aina ambazo zina lengo na ujumbe maalum. Kwa hiyo katika uwanda wa nadharia na mantlki, tunaweza kujadili kwamba; Sanaa isiyo toa elimu au funzo fulani kwa jamii haitimizl moja ya lengo lake muhimu. Vile vile sanaa hiyo hupingana na asili yake ikiwa haitoi elimu yenye maadili. Kwa hiyo sanaa hiyo ni sanaa lakini sio sanaa kamilifu au sanifu; wala sio sanaa muhimu na ya hali ya juu kwa jamii ya msanii.
Nia yetu ni kudhihirisha kwamba iklwa kwa mfano, chakula ni sehemu muhimu ya afya na uhai wa viumbe, binadamu hula chakula ili aishi wala haishi ili ale chakula: kwa hiyo chakula kisicho muhimu kwa afya na uhai wa kiumbe slo chakula muhimu na cha hali yajuu kwa afya na maisha ya binadamu. Chakula hicho ni chakula, lakini ni cha hali ya chini. Hicho slo chakula bora.
Kwa hiyo, kwa kufuatia mfano huu huu wa chakula, afya na maisha; tunaweza kujadili kimantiki kwamba, sanaa isiyo na tumizi lolote au isiyo toa elimu au funzo lenye maadili fulani ya jamii inayohusika, sanaa hiyo siyo ya hali ya juu na wala siyo sanaa muhimu ya wakati ilipoundwa kwa jamii yake. Kwa sababu haifuati asili na lengo lake ambalo ni elimu wala haina tumizi lolote.
Kimantiki tunaweza kujadili na kuamua kwamba, kitu ambacho hupingana na misingi ya asili, iliyokifanya kitu hicho kiwe kitu, kitu hicho huonekana na hatimaye kutoweka au kugeuka kuwa kitu kingine, kama vile chakula kinavyoweza kugeuka sumu na kuhatarisha afya na maisha ya kiumbe, badala ya kuwa msingi wa afya na maisha bora ya binadamu.
Maswali muhimu, hapa yanayohitaji majibu ni haya: Asili ya Sanaa ni nini? Malengo yake ni yapi? Asili na malengd hayo yana uhusiano gani na elimu ya jamii? Kuna falsafa na nadharia tatu muhimu za asili yasanaa hapa Tanzania, Afrika na duniani pote, na zote zinasehemu inayohusishasanaa katikaelimu.
Nadharla ya falsafa ya sanaa kwanza hutambulisha sanaa kama kitu cha kuiga, klnachoundwa na binadamu wala sio wanyama, ingawaje kuna wanyama waliojipatia sifa mbalimbali kwa ajili ya utundu na ujanja wao kama vile sungura, nyani na sokwe. Nadharia ya falsafa hii Ina hoja tatu muhlmu za asili ya, Sanaa:-
Quote:(1) Kwambabinadamu ni kiumbe muigaji kwaasili na ana uwezo mkubwa wa kuiga kubunia na kutafsiri kushinda wanyama wengine wote.
Quote:(2) Kwamba binadamu tangu mwanzo wa maisha yake hujifunza kutokana na mazingira yake kwa kuiga.
Quote:(3) Kwamba binadamu hupendezewa sana na kazi za kuiga tuitazo Sanaa za hisi.
Hoja ya kwanza hujibu swali: Kwa nini binadamu anaunda Sanaa? Jibu lake ni kwamba ana uwezo mkubwa wa kuiga kwa asili na hutumia uwezo huo kwa kuunda sanaa: Sungura, Nyani na Sokwe hawana uwezo huo na ndio maana hawaundi sanaa.
Hojaya pili nayatatu hujibu swali: Sanaa inafaida gani kwa binadamu tangu akiwa mchanga hadi mwisho wa maisha yake? Jibu kwamba Sanaa ni elimu na kitambulisho cha ukuzi wa akili ya binadamu. Hojaya pili naya tatu hutoa maelezo ya kutosha kuhusu swali. Sanaa ni elimu kwa jinsi gani? Na hoja ya kwanza ambayo ndio msingi wa falsafa wa nadharia, yake huegemea sana uundaji wa Sanaa utokanao na asili ya binadamu mwenyewe. Baadhi ya sanaa hutumika hasa kwa madhumuni ya kuyatawala mazingira ya msanii kamavilesilaha.
Mjadala wa nadharia ya falsafa ya kwanza kwamba asili ya sanaa ni uwezo wa binadamu wa kuigiza mazingira yake. Na sanaa ni elimu kwa vile binadamu hujifunza njia za kutawala mazingira yake wakati anapoigiza mazingira kwa kuunda sanaa.
Mantiki ya falsafa na nadharla hii Imeegemea katika taaluma ya uundajl sanaa na jinsi binadamu alivyopata uwezo wa kuunda sanaa, akilinganishwa na wanyama wengine wenye akili kama vile Sungura, (katika methali za Afrika), Nyani na Sokwe.
Falsafa na nadharla ya pili ina mjadala mmoja muhlmu ambao pla unawelekeo wa kutoa funzo na elimu, Ingawaje mwelekeo huu hautamkwl hivyo wazi wazi. Falsafa na nadharia yake hujadili kwamba: asili ya sanaa ni mawazo na hisia za msanii kuhusu jamii na mazingira yake. Hoja na mantikl ya nadharla hil hudhlhlrlsha kwamba, msanii huhuslsha hlsla zake na mawazo yake, kuhusu jamli na mazinglrayake kwa nla ya kutoa elimu au funzo fulani kwa jamil hlyo, na kulpa hamasa jamii hiyo kutenda mambo fulani au kulshi maisha ya aina fulani, kama mambo hayo yanavyowakilishwa katika dhamira na ujumbe wa sanaa.
Mantiki na hoja za falsafa hii huegemea katika umuhimu wa dhana katika asili ya Sanaa, dhana ambayo lengo lake kubwa ni kutoa mafunzo kwajamii wakati sanaa inatoa kiburudisho kwa jamii.
Kwa kutumia sanaa kama nyenzo au zana ya kujipatia chakula na kumshambulia adui zake, kame hadi karne, binadamu alipata elimu kubwa ya kuyatawala mazingira yake aliweza kuishi maisha marefu na bora yeye na jamaa yake.
Katika mapambano haya binadamu wa asili hapa Tanzania, Afrika na mahala pengine duniani alianza kuunda zana za kujipatia chakula katika uwindaji, uvuvi, na hatimaye ukulima wakati alipojifunza kujenga mahali pa kuishi, na kufuga wanyama. Zana hizo hizo za kujipatia chakula, alizitumia kwa kuwashambulia maadui zake. Zana hizo ni kama shoka za mawe, silaha za miti, na baadaye alipendelea zaidi, mkuki na ngao, upinde na mishale.
[Image: p084.jpg]
Vielelezo vya zana na silaha za miti toka enzi ya kale Tanzania
Sanaa hizi tunaziita elimu ingawaje wakati binadamu wa mwanzo alipoziunda, bila shaka alizipamba kwa nakshi ili zipendeze, au alizipa umbo fulani ambalo ni la kupendeza ingawaje umbo hilo na nakshi hizo havikuwa na uhusiano kamili na kazi ya kumpatia chakula au kushambulia adui zake; bali jambo lililo muhimu kwa mjadala wa sehemu ni kwa kutumia sanaa kama nyenzo au zana, karne hadi karne, binadamu alipata mafunzo naelimu kubwayakutawala mazingira yake ili aweze kuishi maisha marefu nabora. Elimu hii iliporithishwa toka kizazi hadi kizazi na kukuzwa na vizazi mbali katika historia ya binadamu, imekuwa chanzo na kisa kinachoendelea cha maendeleo ya binadamu tangu kale hadi leo, kama inavyoonekana katika historia ya sanaa na ya zana za binadamu.
Sehemu hii imejadili kwamba, Sanaa ni elimu kwa vileasili mojawapo muhimu yasanaani elimu nalengo
kubwa mojawapo la sanaa ni kutoa funzo au elimu fulani kwa jamii ya msanii, na binadamu hujifunza mbinu za kutawala mazingira yake wakati akiunda sanaa za kumsaidia kuyafahamu na kuyatawala mazingirayake.
SANAA NI ZANA YA ELIMU
Tangu enzi ya ukoloni wa Kiingereza hadi leo sanaa za aina mbalimbali zimefundishwa katika mashule ya Tanzania na sanaa za aina nyingi zinatumika kama zana ya kuwakilisha ujumbe, katika mawasilianobainaya mwalimu na mwanafunzi.
Wakati wa ukoloni (1895 – 1961) na hata 1980, ni shule chache tu ambazo zimefundisha sanaa kama somo lenye uzito sawa sawa na masomo mengine kama vile hesabu na sayansi. Kati ya miaka 1895 na 1960, shule chache ambazo Waafrika walikuwa wanasoma zilifundisha somo la sanaa tangu shule za ukuzi hadi shule za sekondari na vyuo vyaelimu. Shule hizo chache ni kama vile Tabora Shule ya Sekondari, Tanga na Chuo cha Waalimu cha Butimba na Mpwapwa. Lakini wakati huohuo, mashule yote ya wanafunzi wa Kizungu na wa Kihindi, katika ngazi zote za elimu sanaa ilifundishwa kama masomo mengine, wala sio kama kiburudisho baada ya masomo kama ilivyofanyika katjka mashule mengi yaWaafrika.
Hata hivyo, umuhimu wa somo la sanaa katika ngazi mbalimbali za elimu tangu shule za ukuzi hadi Chuo Kikuu ulifahamika hapa Tanzania tangu enzi ya ukoloni hadi leo. Chuo Kikuu cha Makerere cha Uganda ambacho kilipokea wanafunzi wa Diploma ya sanaa toka Tanganyika kilifunguliwa 1940 na tdara ya Sanaa za Maonyesho ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilifunguliwa mwaka 1967, lakini Idara ya Sanaa ilifunguliwa 1974.
Suala la sanaa na elimu ya sanaa katika Chuo Kikuu halinabudl ilchunguzwe ndani ya misingi ya Chuo Klkuu chenyewe, kwa kuchunguza suala zima la lengo, madhumuni na wajlbu wa Chuo Klkuu katika nchl Inayoendelea. Katika mljadala mingi Inayoendelea Juu ya suala hili, Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, Mwalimu J.K. Nyerere, alitoa matamshi katika hotuba yake wakatl wa sherehe ya kufungua Chuo Klkuu cha Dares Salaam mwaka 1970, kuhusu wajlbu na lengo la elimu ya Chuo Klkuu kwa Jumla, ambayo yanatoa mwongozo wa kimsingi.
Mwalimu J.K. Nyerere alieleza kwamba tegemeo la jamil kwa kila taaluma ya Chuo Klkuu ni kutafltl ukweli wa kitaalamu katika kila taaluma kufuatla mslmamo unaojitambulisha na mategemeo ya jamii.
Vilevile, Mwallmu alieleza kwambawajlbu wakila taaluma ya Ohuo Klkuu ni kufunza watu wenye uwezo wa kuflkirl kulingana na mabadiliko ya jamii inayoendelea.
Lakinl, Mwalimu alionya na kusisitiza kwamba ingawaje, kila taaluma Ina uhuru wa kutafiti ukweli bila woga au upendeleo, taaluma hazitaweza kukuza elimu na kusaidla Jamli, kama matokeo ya Juhudl hiyo, hayatajali hatari yakekwajamli.
Kwa hlyo kila taaluma ya Chuo Klkuu: nla, wajibu wakutafutamaananaukweli bila yawogalaklnlwakatl huohuo, inawajibuwakutumlkiajamli.
Ingawaje Mwalimu aliyasema haya yote kuhusu kila taaluma na Idara ya Chuo Klkuu, mambo haya ndiyo msingl wa wajibu na malengo ya elimu ya sanaa na nafasi ya sanaa katika Chuo Kikuu kama inavyohusu taaluma zote nyingine.
Malengo na wajlbu huo pia umetamkwa katika katibaya Chuo Kikuu, yaani kuhifadhi elimu ya sanaa tangu kizazi kihgine hadi vingine, kufanya utaflti katika sanaa na kutafuta ukweli wa viwango vya juu katika sanaa bila woga, na kufunza wataalamu wa sanaa, katika viwango vya juu ili watimize mahitaji ya taifa ya wataalamu wa Sanaa.
Kwa maelezo zaidl, kuhusu wajibu na malengo ya sanaa na elimu ya sanaa katika Chuo Kikuu, soma hotubaya Mwallmu J.K. Nyerere, Agosti 1970, Uk. Wa 8 – 13.
Kwa hiyo nafasi ya sanaa na elimu yasanaa katika shule za sekondari, vyuo vya Waalimu na Chuo Kikuu ni kutimiza mahitaji ya taifa hili, ambayoni uundajiwa sanaa na kutoa wataalamu wa viwango mbalimbali katika taaluma ya sanaa kwa madhumuni ya kutumikia raifa la Tanzania kama mwalimu alivyoeleza katika hotuba zake mbalimbali kuhusu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wajibu wake kwa taifa la Tanzania.
Katika viwango vya mwanzo sana vya elimu hapa Tanzania tangu wakati wa zamani hadi leo, sanaa na elimu ya sanaa ina nafasi muhimu nne:
Quote:1. Sanaa ni zana ya mawasiliano baina ya mwalimu na mwanafunzi.
2. Sanaa ni zana ya uthamini wa ukuzi wa mawazo na akili ya mtoto tangu umri wa miezi 6 hadi miaka 10.
3. Sanaa ni chombo au zana ya kuhimiza ukuzi wa mawazo na akili ya mtoto wa umri uliotajwa.
4. Sanaa ni zana ya kutambulisha ufahamu wa binadamu na matokeo ya ufahamu huo.
Nafasi ya Sanaa Katika Elimu Tanzania
Sanaa kama zana ya elimu hutumika kwa maana hiyo hiyo katika kuelimisha watu wazima ambao hawajui kusoma na kuandika, kama inavyoonekana katika vitabu vingine sana hapa Tanzania vilivyoandikwa kwa ajili ya elimu ya watu wazima tangu mwaka 1969 hadi 1981. Vitabu hivyo ni kama vile Jifunze kusoma (1968), Jiendeleze kusoma (1970), Jifunze kusoma: Kilimo Bora cha Pamba (1970) na vinginevyo.
Zaidi ya sanaa kutumlka kama kielelezo cha mwalimu, chakuwakilishia ujumbe wa elimu toka kwake au ‘kltabuni hadi kwa mwanafunzi wake, kumfunzia mtoto na mtu mzima kusoma na kuandika; elimu ya saikoiojia ya watoto sasa imethibitlsha kwamba, sanaa ni zana muhimu sana katika uthamini wa ukuzl wa fikra na akili ya mtoto. Vile vile saikolojia ya elimu ya watoto imethlbitishwa kwamba sanaa iliyochorwa na mtoto yaweza kutumika katika uchunguzl wa kuelewa maendeleo na matatizo ya mtoto anayehusika. Kwa mfano, mtoto huweza kuchora magarl au ndege kwa sababu anapenda sana ndege na magari, au mtoto anaweza kutishika sana hata akaota ndoto za jinamizi akiona picha za vitu anavyoviogopa sana. Vile vile maumbo fulani na mistari ya sanaa ya kuchora, vinatafsiri mbalimbali kwa wataalamu wa saikolojia kuhusu akili ya msanii akiwani mtoto au mtu mzima.
SANAA NA ELIMU YA JAMII
Hapa Tanzania na mahali pengi duniani, sanaa ilitumika kama zana kuelimishia jamii kuhusu mambo muhimu katika maisha yao ya kila siku kati ya mwaka 1969 na 1980, sanaa za aina ya Posta na Vielelezo zimetumika kwa faida kubwa sana kwa jamii mbali mbali za Tanzania katika kampeni mbalimbali za kitaifa, kama vile kampeni za Afya Bora, Chakula bora, uchaguzi naukulimabora.
Katika maisha ya kila siku ya jamii ya Tanzania sanaazaaina ya zana hutumika sana kuelimishajamii, mambo mbalimbali kwa njia ya sanaa za ishara. Elimu hiyo hutokana na ujumbe unaowasilishwa na sanaaya ishara kwa Jamii. Ilani ya hatari kwenye nguzo za umeme hukutahadharisha na kifo, au kukulazimu ugundue njia ya kuepuka kifo kutokana na hatari ya umeme. Ishara za barabara hutoa ujumbewenyeelimu kwa njia hiyo hiyo ingawaje ishara hizo hizo pia hutumika katika elimu au kampeni za usalama wa barabarani.
Kuna aina nyingi za zana ambazo walimu hutumia kwa madhumuni ya kufundishia katika viwango mbalimbali vya elimu; Baadhi ya zana hizo ni sinema, radio na sanaa ya aina ya vielelezo.
Matumizi ya sanaa katika kutoa funzo na elimu fulani fulani, ni tofauti na yale ya msanii ambaye huingiza funzo lake katika dhana ya sanaa wakati akiunda sanaa hiyo. Kwa hiyo jamii nupata funzo la sanaa kutokana na tafsiri ya lengo la dhana ya sanaa hiyo, yaani ujumbe wa sanaa hiyo.
Sanaa hutumika kama zana ya elimu ya kufundishia wakati Inapotumika kama zana ya kuwakilishia ujumbe, ambao ni funzo, kutoka kwa mwalimu hadi kwamwanafunzi.
Kwa njia hiyo hiyo, sanaa hutumika kama zana ya kutoleaujumbewenyefunzotokakwamtu mmojahadi kwa mtu mwingine, taifa moja kwa taifa jingine au jamii moja kwa jamii nyingine.
Katika viwango vya mwanzo sana vya elimu kwa mfano, sanaa za kuchora hutumika kama msingi na zana ya kufundishia kusoma na kuandika. Sanaa za kuchora hutumika kama vielelezo vya mambo na mawazo ambayo ingekuwa vigumu kumwelimisha mtoto mchanga kwa maneno, bila ya kumchosha, kumtatanisha akili au kuvunja nia yake ya kujifunza kusoma na kuandika. Kwa hiyo vitabu vya elimu vya kiwango hiki cha mwanzo sana cha elimu huwa na maneno machache, maelezo mafupi au majinayavitu na picha za kuchora kama vielelezo.
Kwa kutumla kielelezo cha picha ya kuchora, mwalimu wa shule ya ukuzi hufanikiwa zaidi na kwa urahisi kumweleza mtoto mdogo wa shule ya ukuzi mama na baba ni nani kwa kutumia kielelezo cha picha ya baba na ya mama. Zana hii hil huweza kutumika kumweleza mtoto mambo mengi kama wanyama ambao hajawaona au vitu ambavyo havifahamu, au anavifahamu lakini hajui majina yake.
[Image: p090.jpg]
Kinyamkera cha Wazaramo
MAADILI YA JAMII MPYA KAMA DHANA YA SANAA
Sehemu hii inayohusu maadiliyajamli mpyakama dhana za sanaa katika harakati za ujenzi wajamii mpya itajadili na kujaribu kujibu maswali matatu muhlmu:
Maadili hayo yanajitokeza vipi katika sanaa za wakati huo, (1954-1980 -)? Maadili hayo yanafahamika vipi na kueleweka vipi kwa jamii? Maadili hayo ni yapi na yanapatikanawapi?
Adili ni nini? Adili ni funzo linalohusu maisha ya jamii naimanizake; misingiya imani hiyokatikaelimu, uchumi, siasa na utamaduni; tabia, mila na desturi, malengo, madhumuni na mategemeo ya jamii kuhusu hayayote.
Lengo kubwala adili au maadili yajamii ni kujenga misingi ya imani za maisha zinazo kubaliwa na kufuatwa na jamii katika mawazo na akili za watu wa Jamii hiyo, hasa watoto navijana, ili Jamii iwezekufikia na kudumisha malengo na mategemeo yake, toka kizazi hadi kizazi.
Kwa hiyo katika sehemu hii, neno adili litakuwa na maana hii; na maadili ya jamii mpya ya Tanzania ni matokeo ya mchujo au mchekecho wa hali ya juu wa maandishi na matamshi muhimu au sera muhimu za Chama na Serikali.
Mchujo au mchekecho huo hufanywa na watu wenyewe katika ngazi zao mbalimbali za maisha ya kila siku tangu nyumbani chini ya uongozi wa baba na mama, mashuleni chini ya uongozi wa mwalimu, serikalini chini yaviongozi wake; hadi katikachamana ngazi zake mbalimbali. Matokeo ya mchekecho huo ndio mafunzo ambayo hutumika kuiadilishajamii.
“Maisha bora ni Vijijini”, kwa mfano ni adili litokanalo na mawazo ya Mwalimu J.K.Nyerere, katika Maendeleo Vijijini. “Ukulima Utu Bora” vile vile ni adili ambalo lilichekechwa kutokana na kitabu hicho hicho. Kuna mifano mingine mingi ya maadili ya ujenzi wa jamii mpya yaliyopatikana kufuatia utaratibu huu, na kutumika kama dhana au dhamira ya fani mbalimbali za sanaa hapa Tanzania tangu 1954, kama yanavyoonekana katika mifano hii michache.
Quote:Jitegemee usiwe kupe
Ubepari ni Unyama, ujam aa ni utu
Uhuru wa Bara zima la Afrika ni fukumu letu
Unyonyali kwetu ni haramu
Njia kuu za uchumi zlwe chini ya wakulima na wafanyakazi Elimu kwa wote.
Hii ni mifano michache ya maadili ambayo yalichujwa na kutumika kama dhana au dhamira ya sanaa kutokana na “Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, “Azimio la Arusha, “Madhumuni ya TANU” Azimio la Arusha na Elimu ya Kujitegemea.
Katika jamii zetu za asili hapa Tanzania na Bara la Afrika, maadili ya maisha ya jamii hizo yalitolewa kwa njia mbalimbali, hasa kwa kutumia mithali au vigano na maadili fulani yakiwa ni dhamira kuu ya mithali au vigano, kwamfano:-
Quote:Usipoziba ufa, utajenga ukuta
Pole pole ndio mwendo
Haraka haraka, haina mbaraka
Usiposikia la mkuu yatakupata makuu.
Hapa tumeona maana ya maadili na jinsj maadili hayo yanavyopatikana na baadhi ya njia za kuya wakilisha kwa jamii.
Je, maadili ya jamii mpya ya Tanzania tangu 1954 hadi leo ni yapi na maadili hayo yanapatikana wapi?
Sehemu moja ya swali hili imekwisha jibiwa kwa ufupi sana na sehemu ya pili tutajaribu kuijibu kwa ufupi vile vile, kwa vile sera za Chama na Serikali, matamshi muhimu, maandishi ya Chama naSerikali ni mengi mno nafasi ya kuyataja na kuyajadili hayo yote haipokatikasura hii. Na hata kama nafasi yaainahiyo ingepatikana ni vigumu kuorodhesha katika kitabu kimoja maadili yote ya jamii yo yote. Kwa hiyo hapa tutatoa mifano michache tu.
Maadili ya ujenzi wajamii ya Tanzaniayanatokana na mchujo wa falsafa na mawazo yaliyomo katika maandishi ya Mwalimu J.K. Nyerere maandishi ya Chama na Serikali, mikutano semina, vikao vyaChama namatamshi yotemuhimu yaChamanaSerikali.
Machache baadhi ya maandlshi muhimu kwasura hii ni kama vile. Azimio la Arusha (1967). Ujamaa (1968). Elimu ya Kujitegemea(1967). Maendeleo Vijijini (1967), “Elimu ya Kujikomboa” (1974), Mwongozo (1971) na baadhi ya matamko muhimu ni kama lile ‘Tamko la Musoma kuhusu Elimu ya Kujitegemea”, Semina ya Kibaha, kuhusu Mwongozo, utekelezaji wa “Operesheni Vijiji vya Ujamaa” na “Operesheni Maauka”.
Moja ya sehemu yenye maadili muhimu yahusuyo’ tabia, desturi na mwenendowaviongozi wajamii mpya imo katika Azimio la Arusha.
Sehemu hiyo inaelekeza kwamba:
Quote:1. Kiongozi wa TANU (sasa CCM) au wa Serikali sharti awe mkulima au mfanyakazi, na asishiriki katikajambololotela kibepari au ukabaila.
2. Asiwe na hisa katika Makampuni yoyote.
3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.
4. Asiwe na mishahara miwili.
5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
Mfano mmoja wa adili litokanalo na sehemu hii ni kama vile, “Kiongozi wa CCM hanyonyi wala hanyonywi”. Huu ni mfano mmoja tu wa maadili mengi yanayoweza kuchujwa kutokana na sehemu hiyo na yakatumiwa kama dhana au dhamira ya fani mbali mbali zasanaa.
Je, maadili hayo yanafahamika na kueleweka vipi kwawatu waTanzania?
Baada ya miaka 10 tangu Elimu ya Kujitegemea na vitabu vingine vilivyotajwa vichapishwe hadi leo bado jamii na wasanii wa Tanzania wanajadili na kujitahidi kuyaelewa vyema ili kuyatekeleza mawazo nafalsafaza maandishi hayo, lakini utekelezaji huo haujafikia kiwango cha ufanisi kilicho tegemewa na Chama na Serikali. Sababu tatu muhimu zinazokaribiana zimetolewa kueleza hali hii mpaka sasa sehemu ya kwanza ni kwamba, hatukuielewa vyema sisi watu wa Tanzania falsafa ya siasa ya Elimu ya Kujitegemea, hasa Viongozi na Vyombo vya umma vya utekelezaji. Kama ilivyoelezwa katika Azlmlo la Baada ya Miaka Kumi.
Katika fani mbalimbali za sanaa harakati za utekelezaji wa siasa ya Elimu ya Kujitegemea zilifanyika na ushahidi huo ni mifano mingi ya sanaa zilizoundwa na zenye maadili ya siasa hii kama dhana au dhamira ya sanaa hizo.
Tatizo linalohusu kuelewa vyema, tafsiri sahihi na utekelezaji bora wa falsafa na siasa iliyotolewa katika maandishi na matamshi ya Mwalimu J.K.Nyerere Chama na Serikali, ulijitokeza katika maandishi mengine muhimu ya wakati wa ujenzi wajamii mpya, chini ya misingi ya ujamaa na kujitegemea. Kuna wasanii kwa mfano waliokuza wazo ambalo si sahihi katika sanaa zao na akili za wananchi, kwamba kila mtu mwenye tumbo kubwa ni mnyonyaji au kila mtu aliyekonda konda au aliye na umbile la kadiri sio mnyonyaji. Huu ni mfano mmoja tu wa mingi inayothibitisha kwamba hata baadhi ya wasanii walipata matatizo haya.
Kutokana na ushahidi huu wa shughuli za utekelezaji wasiasa, madhumuni, na harakati zaujenzi wa jamii mpya ya Ujamaa na Kujitegemea, ni wazi kwamba, ujuzi wa maadili ya ujenzi wa jamii mpya bado unaendelea na tahadhari kubwa inatakiwa ili tufikietafsiri ambazoni sahihi nasiasayetu.
Pili, tafsiri sawa na sahihi za siasa na falsafa za ujenzi wa Jamii mpya utategemea kuelewa vyema na kutoa tafsiri sawa na sahihi za utekelezaji wa maandishi, matamshi, na sera zote muhimu za Chama na Serikali.
Tatu, tuna hitaji kufunua akili zetu, muda na juhudi kubwa ya kuyachunguza na kuyaelewa madhumuni, imani malengo na mategemeo ya ujenzi wa jamii mpya, ili maadili tutakayo chuja au chekecha kwa madhumuni ya kuadilisha jamii mpya yawesawa na misingi ya ujamaa na kujitegemea.
Nne, ujuzi wa imani, malengo, madhumuni na mategemeo ya ujenzi wa jamii mpya unaojengwa juu ya ujuzi wa sera moja, tamshi moja, kitabu kimoja, au ibara chache zilizonakiliwa kutokana na moja ya hayo yote, huo ni ujuzi wa bandia na ujuzi wa aina hiyo ni hatari, kwa vile una uwezo mkubwa sana wa kutupotoshakatikamaadili yetu.
Ujuzi wa aina hii hautamwezesha mtu wa Tanzania au mtu ye yote kutoka nje ya Tanzania kuelewa sanaa zenye maadili yaujenzi wajamii mpya na hasa maadili yenyewe.
Maana ya sehemu hii ni kwamba, ikiwa mtu hajui historia ya vita vya Maji Maji, mtu huyo anaweza ashindwe kuelewa kwa urahisi tafsiri ya dhana na ujumbe wasanamu au pichaya vitavyaMaji Maji.
Au ikiwa mtu hajui kisa cha kusulubishwa kwa Bwana Yesu, sanaa za kusulubishwa kwa Bwana Yesu zitamuwia vigumu kwa jinsi hiyo hiyo. Na ikiwa mtu haelewi au hajui chanzo cha vitavya ukombozi dhidi ya uvamizi wa Fashisti idi Amini kwa Tanzania, sanaa zenye dhana au dhamira ya vita hivi pia zitamtatanisha kama ilivyoelezwa.
Kwa ufupi sana, sehemu hii imeeleza jinsi matatizo yanavyoweza kuzuka na aina ya matatizo yaliyokwisha zuka katika kuelewa maadili ya ujenzi wa jamii mpya na yanaweza kutokea wakati wa kuyatumia katika fani mbalimbali za sanaa, ili kuadilisha jamii ya msanii.
Je, maadili haya hujitokeza vipi katika sanaa za ujenziwajamii mpya?
Maadii hayo hujitokeza kama tafsiri ya mawazo na hisia za msanii kuhusu jamii mpya na mazingira yake.
Vile vile maadili hayo hujltokeza kama dhamlra kuu au dhana ya sanaa, baada ya msanil kupata mahamasa kutokana na kuelewa kwake imani, madhumuni, malengo na mategemeo ya ujenzi wa jamil mpya, au siasa, falsafa mawazo, na shughuli za utekelezajl wa siasa ya ujamaa na kujitegemea.
Kwa mfano, picha ya P.P. Ndembo dhana yake ni elimu ya watu wazima na lengo la picha hii ni kuwashawishi watu wazima kuelewa umuhimu wa kujua kusoma na kuandika. Picha hii vile vile imetokana na kampeni nyingi za elimu ya “watu wazima zilizoendeshwa hapa Tanzania na Wizara ya Elimu ya Taifa kati ya 1969 na 1980.
Tangu mwaka 1969 hadi 1980, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ikishirikiana na wizara mbalimbali za serikali. Chama, na vyombo vya utangazaji wa habarl, iliendesha kampeni nylngi sana za elimu ya watu wazima. Baadhi ya kampeni hizo ni kama vile;
“Uchaguzi ni wako (1970)”, “Wakati wa Furaha (1971)”, “Kupanga ni Kuchagua (1972)”, “Mtu ni Afya (1973),” “Chakula ni Uhai (1974),” na nyinginezo ambazo zilikuwa na marengo mbalimbali
Picha hii imefanikiwa kufikisha ujumbe wake; kwa hiyo ilikuwa picha nzuri na muhimu ya wakati huo wa kampeni zilizotajwa. Vile vile yaelekea msanii alitumia usanii wa hali yajuu katikauundaji wapichahii.
Jambo jingine ambalo ni muhimu kuhusu.plcha hii ni kwamba, msanii wa picha hii hakujishughulisha na kunakili andishi lolote muhimu, bali alitoa tafsiri yake kuhusu utekelezaji wa kampeni yaelimu kwawatu wazima. Na wasanii wengine wengi walifanya hivyo hivyo kuhusu Elimu ya Kujitegemea, Azimio la Arusha, “Ukombozi wa Afrika , Tabla za uongozi”. “Imani na madhumuni ya Chama”na mengineyo.
Tangu mwaka 1954, wasanii wengine wengi wa Tanzania wamejishughulisha na uundaji wa sanaa katika fani mbalimbali, wakitoa tafsiri ya hisia na mawazo yao juu ya shughuli za ujenzi wajamii mpya kwa madhumuni ya kustarehesha watu, kuwapa watu ‘ari na kuwaadilisha chini ya misingi ya malengo na mategemeoyajamii mpya.
[Image: p097.jpg]
Elimu ya Watu Wazima, Picha ya Kuchora: P.P. Ndembo, 1978. (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.)
Ujumbe wake, kama vile: “Ujamaa Vijijini”, “Ujamaa”, “Umoja ni Nguvu”, “Watu wanalima Shambani”, “Elimu ya Watu Wazima”, “Vita vya Ukombozi wa Afrika”, “Wake wa Wagombea Uhuru”, “Kijiji cha Ujamaa”, Sanamu na picha nyingi za Mwalimu J.K. Nyerere, viongozi wengine wa Chama na Serikali, badala ya picha za Malkia au Magavana wa Kiingereza kama ilivyokuwa kabla ya 1954. Mifano micheche ya sanaa za wakati huu ni kama vile:
Quote:1. Seif Salimu: Mwalimu J.K. Nyerere na Rals S. Machel, (1977) Mozambikiy/Tanzania Instituteof Foreign Relations, Dares Salaam.
2. Pejume Alale: “Umoja ni Nguvu”, sanamu ya mpingo, (1976), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
3. E. Jengo: “Wanamuziki” (1969), Kalenda ya Baraza la Taifa la Sanaa.
4. E. Tunginie: “Maji Safi kwa Wote” (1969), Kalenda ya Baraza la Sanaa la Taifa.
5. S. J. Ntiro: “Mnara wa Azimio la Arusha” (1974), Acusha.
6. E Jengo: “Mnara wa Tabora” (1974), Tabora.
7. J. G. Somola “Mnara wa Iringa” (1977), Iringa, Toka Maisha ya ubinafsi kuelekea kwenye Maisha ya kijamaa.
Kwa wakati huu wote inaelekea sanaa ziliundwa kwa madhumuni muhimu matatu, sanaa zilitumika kama utaratibu wa kufundishia au kama zana ya elimu. Pili sanaa ziliundwa kama tafsiri ya hisia na mawazo msaniiyanayostareheshawakati jamii inaadilishwa. Na tatu, sanaa ilitumika kama adilisho lenye kutia hamasa na ari ya kufikia malengo na mategemeo ya ujamaa na kujitegemea. Katika Chuo cha Elimu cha Butimba, Mwanza na Kigurunyembe, Morogoro, sanaa zilitumika kufundishia historia fupi ya mapambano muhimu na marefu yanayoendelea ya ujenzi wa jamii mpya; hasa katikakuelezea historia yaukombozi wa Tanganyikana mchango wa Mwalimu J.K. Nyerere, kama shujaa mkubwa, baadhi ya mashujaa wengi waliojihusisha na mapambano haya.
Katika elimu ya watu wazima, mashuleni na vyuoni, sanaa za aina ya hisi na zana zilitumika kama zana ya kufundishia elimu ya siasa na maadili ya jamii mpyayaujamaanakujitegemea.
Katika gazeti la kila siku la Kiswahili la Uhuru na Mzalendo kuna sehemu ya picha za makaragosi zilizotoa maadili kwa kutumia wahusika waitwao, “Bwanyenye”, “Polo” na “Chakubanga.”
Nyingi ya baadhi ya picha za mhusika “Chakubanga” na “Bwanyenye” zimetoa maadili mbalimbali ya kuijenga na kusifu siasa ya ujamaa na kujitegemea kwa kukanusha au kupinga destuh na tabiaza “unyonyaji” “uzururaji”, “ombaomba”, wizi na mengineyo.
Mpaka sasa picha nyingi za “Chakubanga” zinatoa mafunzo au maadili ya kujenga ari ya kupinga tabiaza unypnyaji katika maisha ya kilasiku yajamii na kujenga ari ya kujitegemea. Kwa kutumia wahusika hawa maadili mengi yamekwisha tolewa kwa jamii chini ya dhamira kama vile: “Jitegemee Usiwe Kupe”, “Usafiri wa Mazingira”, “Kilimo cha Kufa na Kupona”, “Tuhamie Vijijini”, uigaji mbaya wa mila na desturi za Kigeni nakugusia matatizoya kila siku yajamii.
Chanzo&t&t&t&t&t&t]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-24T16:54:29Z 2021-07-24T16:54:29Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=637 <![CDATA[SANAA YA MAJIGAMBO]]> MAJIGAMBO ni sanaa ya unenaji yenye utendaji na inayotumiwa na wasanii kujigamba ama kujinaki na kutangaza sifa zao.
Ni sehemu muhimu ya fasihi similizi. Msanii hujigamba kishairi na hutumia lugha iliyoteuliwa ili kutoa hisia zinazowaathiri wasikilizaji ama wasomaji kwa namna ya kipekee.
Shairi la Majigambo ni shairi la kujisifia na kujikweza kwa mtu.
Washairi wa Kiswahili wa kizamani kama vile Muyaka bin Haji na hata wa kisasa wamekuwa wakijipa lakabu au majina ya kishairi.
Ndiposa utakuta watu wanaojitambulisha kama: Malenga wa Mvita; Malenga wa Mrima; Malenga wa Ziwa Kuu; Malenga wa Bara; Malenga wa Karne Moja; Malenga wa Vumba; Dafina ya Umalenga;Jungu Kuu, Nyamaume n.k.
Lakabu
Jambo hili la washairi kujipa lakabu litadhihirika pia, pindi ukifungua ukurasa wa Ushairi Wenu katika gazeti la Taifa Leo siku ya Jumamosi na lile la Taifa Jumapili.
  Utakuta washairi wakiandika mashairi ya kujisifu kwa ukwasi na ubingwa wao wa fani hii ya ushairi. Humo utakuta lakabu kama vile:Ustadh Halua Chungu (ni kweli ipo halua chungu?), Al-Ustadh- luqman, ngariba-mlumbi, Barry M’bara, Sauti ya Mbali, Malenga wa Jangwani, Mwana wa Mambasa n.k.
Upana
Wakati mwingine mashairi ya majigambo huchukua upana kwa sifa za aina nyingine kama vile jamii, lugha na utamaduni.
Asili ya majigambo ya namna hii na hasa yale ya kusifu viongozi labda ni fasihi simulizi.
Aidha mafanani na manju walikuwa wakiwatungia wafalme mashairi na kuwaimbia huko Ikulu, au pengine katika kuwatayarisha mashujaa kihamasa kabla hawajaenda vitani.
Kauli
Kwa mfano mshairi huyu katika Kauli ya Umma anausemea Umma
Mimi ndiye umma, mimi ndiye Nyundo
Najua kukoma, nyendo za ukondo
Anayenikama, kwake sina pendo
Nielewe vyema, mimi ndiye nyundo.
Majigambo mara nyingi ni mkusanyiko wa sifa za mtu binafsi, ukoo wake, kikundi anachowakilisha au kabila lake kwa kutumia majina ya majisifu.
Miongoni mwa Wazulu wa Afrika Kusini Majigambo yanaitwa ‘izibongo’ Katika majigambo haya msanii hurejelea maisha ya Wazulu: kujieleza kwao katika jamii na kitamaduni;pia husifu nchi yao; wanasiasa wao; mifugo wao na shughuli zao za kiuchumi.
Ujasiri
Miongoni mwa mwa Wabasotho, vitendo vya kishujaa ndio uti wa mgongo wa majigambo yao.
Simulizi zao zinasifu ujasiri, ushupavu na ujuzi wa vita.
Wakuria nchini Kenya na Tanzania wanaita mashairi ya majigambo ‘amaiboko’
Vita
Katika tamaduni nyingi za ulimwengu, ushairi wa majigambo ulihusishwa na vita vya mara kwa mara; mapambano na wanyama; safari za usasi na hatari za kimaumbile.
Ushairi huuhuu umeshamiri sana miongoni mwa jamii zenye sifa za ufugaji.Ili kuuelewa ushairi huu, ni muhimu kuwa na ufahamu wa kina wa mfumo wa jamii na utamaduni husika.
Mathalan, ili kufahamu sifa na nafasi ya ‘ izibongo’ itatubidi tuelewe utamaduni wa Wazulu; ili tufahamu ‘Lithoko’ tunalazimika kuelewa utamaduni wa Basotho; ili kufahamu ‘Ekeyevugo’, hatuna budi kuzama kwenye utamaduni wa Bahima; na ili kufahamu ‘Pakruok’  tunalazimika kutalii utamaduni wa Waluo.
Tathmini
Kwa hivyo, utamaduni una nafasi kubwa katika kufungulia njia ya kutathmini ushairi wa majigambo. Kwa hakika, mfumo wa jamii ndio chanzo cha sanaa hii ya majigambo.
Mashairi ya majigambo hutaja watu, koo, matukio ya kihistoria, mila na itikadi.
Na kwa sababu ushujaa ni sifa muhimu katika jamii za Kiafrika, majigambo mengi hujishughulisha nao. Manju wengi wa Kiafrika kama vile ‘Jeli’ wa makabila ya Mandingo; ‘Gando’ wa Fulani; ‘Gemel’ wa Wolof; ‘Azimaris’ wa Ethiopia na Marombe wa Washona wamewahi kusifu ushujaa wa watu mbalimbali wa jamii zao.
Mfano
Mfano wa majigambo:
    Mimi ni Shikwekwe mwana wa Amuli
    Ninaitwa simbamwene wa Matioli
    Ningurumapo waoga hukimbilia malili.
    Ukali wangu washindana na pilipili
     Nishikapo adui zangu
     Hata wakibeba sime na mkuki
     Hujinyia na kuomba samahani hurumia
     Nimevikomoa vichaka vya Msumbiji
     Nimekomesha na Angola majangili
     Omwana wa Amuli nawika!
*Zingatia:   Omwana ni ‘mtoto wa’. Msumbiji na Angola ni vikundi vya majangili yaliyosifika kwa ukatili wa kuvamia watu majumbani mwao usiku katika maeneo ya Magharibi ya Kenya. Maudhui ni ushujaa wa Shikwekwe.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-24T12:44:06Z 2021-07-24T12:44:06Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=630 <![CDATA[SANAA YA MAJIGAMBO KATIKA NYIMBO ZA KIZAZI KIPYA]]>
Kwa hakika sanaa ya majigambo yaijapotea Barani Afrika, isipokuwa imebadilika tu kulingana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Katika kujadili mada hii, kwanza tutaanza kufafanua dhana ya majigambo kwa kuwatumia wataalamu mbalimbali huku tukitoa maana yetu kutokana na mawazo ya wataalamu hao, pia tutaelezea kwa ufupi kuhusu chimbuko la muziki wa kizazi kipya, kisha tutaingia katika kiini cha mada tajwa kwa kuonesha jinsi gani majigambo yalivyojitokeza katika nyimbo mbili za kizazi kipya ambapo tumetumia wimbo wa msanii Prof Jay “Ndiyo mzee” na wimbo wa Sugu “Sugu”. Kisha hitimisho.
Kwa mijibu wa Simiyu (2011), majigambo ni maigizo yanayotoa mwanya kwa wahusika kujisifu kwa sababu ya matendo fulani ya kishujaa au mafanikio katika nyanja fulani za maisha.
Mulokozi (1996), vivugo (majigambo) ni ghani la kujisifia. Kwa kawaida hutungwa na kughanwa na muhusika mwenyewe. Kivugo hutungwa kwa ufundi mkubwa kwa kutumia mbinu kama sitiari, vidokezi, ishara, takriri na wakati mwengine hata vina.
Wamitila (2003), hii ni aina ya maghani (sifo) yanayohusu kujisifu au sifa. Aghalabu kuhusu kutongoa utungo wa kujisifu kuhusiana na kitendo fulani, ushujaa, urijali au matendo muhimu. Wamitila (Kishatajwa), majigambo au vivugo haya ni maigizo ambayo yanaonesha kujitapa (kujigamba) kwingi kwa mtu ambaye labda ni shujaa au ametenda mambo ya kishujaa au yenye uzito fulani. Watu wanaopatikana katika majigambo ndiyo watambaji au wasimuliaji wa majigambo yenyewe. Ni kawaida ya majigambo kuwa na lugha nzito iliyojaa tamathali zenye taswira au picha za undani na yenye hisia na mawazo mazito. Mtambaji anaweza kujitapa kwa jambo lolote lile.
Wataalamu wote wanashabihiana katika kutoa maana ya majigambo kwani wote wanaelezea kuwa majigambo huhusika na matendo ya kishujaa.
Kwa hiyo tunakubaliana na fasili ya Wamitila (2003), ambaye ameenda mbele zaidi na kueleza kuwa kuna matumizi ya lugha ya kisanaa. Pia mtambaji anaweza kujigamba au kujitapa kwa jambo lolote lile na siyo lazima liwe jambo la kishujaa tu.
Kwa asili kivugo huwa hakiandikwi, hutungwa kichwani kabla au wakati wa utambaji. Siku hizi watu wameanza kutunga au kutungiwa kwa kuandika na baadaye kusoma kivugo hicho. Hii ni kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoashiria mabadiliko ya sanaa ya majigambo. Nyimbo za kizazi kipya ni zao la mabadiliko ya sanaa ya majigambo.
Muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania ulianzia kama muziki wa Hip Hop na kwamba inaelekea kuwa mwaka 1980 na 1990 watoto wa Kitanzania kutoka kwenye familia zenye uwezo kiuchumi ndiyo waliosaidia kuleta muziki wa Hip Hop waliporudi kutoka likizo walikuja na kanda, video na majarida ya muziki kuhusu wasanii wa Hip Hop wa Marekani, Uingereza. Kwa namna hiyo muziki ulikuwa na baadaye vijana wengi walijiunga ingawa muziki huu unaendelea lakini jina la “Bongo Fleva” lilishika kasi.
Kwa kutumia wimbo wa “Ndiyo Mzee” ulioimbwa na Prof Jay na wimbo wa “Sugu” ulioimbwa na Sugu tunaweza kuthibitisha kuwa ni kweli sanaa ya majigambo haijapotea barani Afrika.
Wimbo wa “Ndiyo mzee” ulioimbwa na msanii Prof Jay, ni wimbo unaohusu sera zilizokuwa zikitolewa za mwanasiasa fulani wakati wa kampeni za uchaguzi. Pia wimbo wa “Sugu” ulioimbwa na Sugu ni wimbo ambao msanii anajitamba kwa sifa alizonazo yeye, kwamba, hawezi kulinganishwa na msanii mwingine yoyote yule.
Sanaa ya majigambo imejitokeza katika nyimbo hizi katika sifa zifuatazo:-
Watu huigiza kwa kutumia lugha nzito ya tamathali, picha na taswira zenye hisia na mawazo mazito. Katika wimbo wa “Ndiyo mzee” msanii ametumia lugha nzito  ya tamathali, picha na taswira, katika ubeti wa kwanza mtambaji anajigamba kuwa:-
“Nadhani nimeletwa niokoe hiki kizazi”
“Mimi ni mwanasiasa niliyebarikiwa na Mungu”
“Mimi ni mteule kusini mwa jangwa la Sahara”
Hapa msaniii ametumia lugha hii kujitofautisha na wanasiasa wengine. Pia msanii ametumia tashibiha katika kujigamba pale asemapo:-
“Nataka kuigeuza Tanzania kama ulaya”
 “Kwenye mahospitali nitamwaga dawa kama mchanga”
Msanii ametumia lugha ya picha pale asemapo:-
“Mabomba yatatoa maji na maziwa nchi nzima”
Hapa hadhira inapata picha ya nchi ya Tanzania kuwa yenye mabomba ya kutoa maji na maziwa:-
                    “Nitajenga kumbi nyingi sana za starehe baharini”
Hapa hadhira inapata picha jinsi kumbi zitakavyojengwa kwenye bahari, jambo hili si la msingi analojigamba nalo mwanasiasa huyu kwa kuacha masuala muhimu kama kujenga daraja la Kigamboni pale kwenye kivuko nk.
Pia katika wimbo wa “Sugu” msanii ametumia tashibiha.
“Sauti yangu kwenye mic inasambaa kama upepo”.
 Ametumia pia lugha nzito, lugha ya picha na tashibiha.
“Kuna kitu kimoja watu hawajajua huwezi kuzuia mvua na Sugu ni kama mvua kama ananyesha ananyesha”
Pia ametumia sitiari.
“Mimi ni dume la mbegu”
Majigambo huwa na matumizi ya chuku. Katika wimbo wa “Ndiyo Mzee” msanii ametumia sana chuku.
Kwa mfano:-
“Nataka mpaka Matonya afundishe chuo kikuu”
 “Wanafunzi wafanyie practical mwezini”
 “Nitafungua account kwa kila mtoto mchanga“
 “Nikiwa kuliko mfalme Suleiman msiwe na wasi”
Majigambo husaidia kuelimisha, kuadilisha na kuhifadhi mila na kuzipokeza kwa vizazi vipya. Wimbo wa “Ndiyo mzee” unaelimisha wananchi hasa kwenye ubeti wa pili pale mwimbaji Juma Nature anapomkosoa mwanasiasa kwa kueleza kuwa, yale yote aliyojigamba nayo mwanasiasa huyo ni ya uongo na wala hatoweza kuyatimiza. Kwa hiyo anaelimisha jamii isikubali uongo wake. Wimbo huu unaweza kutumika kwa vizazi vya sasa na vijavyo ili kuelimisha wananchi juu ya wagombea wa kisiasa wanaoomba kura kwa wananchi.
Pia katika wimbo wa “Sugu” msanii anasema kwamba:-
                   “Napata matatizo natatua bila chuki”
Mtambaji hutumia jina halisi au jina la sifa la muhusika. Katika wimbo wa “Ndiyo mzee” msanii ameanza kwa kujitamba kwa kutumia jina lake halisi pale anaposema:-
“Ok ok naitwa Joseph Haule mwana wa Msolopa Ganzi”
Vilevile katika wimbo wa “Sugu” msanii anajitapa kwa kuanza:-
 “Wananiita Mr two kwa jina jingine Sugu, sasa nakubali kuwa mimi ni dume la mbegu”
Mtambaji huahidi kutenda mambo makubwa zaidi kwa ajili ya mkubwa wake ambaye anaweza kuwa mzazi, mtawala au umma.
Katika wimbo wa “Ndiyo mzee” mtambaji prof Jay anatoa ahadi kadha wa kadha kwa wananchi kama vile:-
“Nitahakikisha kila baamedi anamiliki benz”
“Wanafunzi watafanyia practical mwezini”
“Kwenye mahospital nitamwaga dawa kama mchanga”
 “Nitafungua account kwa kila mtoto mchanga”
 “Nitafadhili wachawi waweze kutengeneza ndege”
Pia katika wimbo wa “Sugu” mtambaji pia anajitapa kwa kusema kuwa:-
“Nataka kuwa kama 2pac”
Pia majigambo huwa na tamati, kujikabidhi rasmi kwa mkubwa. Katika wimbo wa “Ndiyo mzee” kuna tamati ambayo imetambwa na Mc Babu Ayoub ambaye anamkabidhi mgombea kwa hadhira kwa kuiuliza hadhira kama ifuatavyo:-
“Ndugu wananchi kuna mtu anaswali kutoka kwa mgombea? Nauliza nasema hivii kama mtu anaswali basi ajitokeze aweze kuuliza swali”
Kwa kuhitimisha ni kuwa kutokana na athari za lugha za kimagharibi, majigambo ya muziki wa kizazi kipya yamekumbwa na mwingiliano mkubwa wa lugha kwani si ajabu kuona mtambaji akichanganya lugha ya kiingereza na lugha ya Kiswahili. Hii ni athari ya lugha kukua na kuathiriana kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia. Lakini majigambo ya hapo awali yalitumia lugha za asili za jamii husika na hivyo kuudumisha utamaduni wa kiafrika.
VIAMBATIZI.
Prof Jay – Ndiyo mzee.
Kibwagizo.
Naam ndugu wananchi
Mc wenu babu ayubu
Ninawaleteeni habari japo kwa kifupi kuhusiana na huyu mgombea wetu Joseph Haule
Mpeni kura za ndiyo kwa sababu yeye ni mpenda watu, nimpenda amani na ni mtu mwenye huruma kwa wananchi wote
Kwa hivyo basi nawaomba ndugu wananchi mumpe kura ya ndiyo.
Naam basi hivyo basi ndugu wananchi tafadhali na mkaribisha mgombea wetu bwana Joseph Haule ili aje aweze kuzungumza na wananchi karibi karibu.
 
Ubeti wa kwanza
Ok, ok naitwa Joseph
Haule mwana wa msolopo ganzi,
Nadhani nimeletwa niokoe hiki kizazi
Mimi ni mwanasiasa niliyebarikiwa na Mungu
Nimeletwa kwenu waungwana niwapunguzie machungu
Mimi ni mteule kusini mwa jangwa la Sahara
Ndiyo maana nimetunukiwa cheti cha juu cha utawala
Na hekima kuliko mfalme Suleiman
Msiwe na wasi
Na hii nitadhihirisha pindi mtakaponipa nafasi
Actually nimedhamiria kuwasaidia
Taifa lenye nguvu duniani liwe Tanzania
Jamani makofi tafadhali basi jamani……
Ni mambo madogo tu
Nadhani ntarekebisha mkinipa visiku vichache
Uchumi utapanda ile ghafla bin vuu
Nataka mpaka Matonya afundishe Chuo Kikuu
Nchi ya Tanzania itang’ara ile kishenzi
Na nitahakikisha kila baa med anamiliki benz
 Si mtafurahi dada zangu jamani..
ndiyoooooo
Basi endeleeni kunisifu kwa nyimbo na mapambio
Nipeni hiyo nafasi jamani hamuoni hali ni mbaya
Nataka kuigeuza Tanzania kama Ulaya
Cha kwanza nitakachofanya nitafuta umasikini
Wanafunzi mkafanyie practical mwezini
Kwenye mahospitali nitamwaga dawa kama nchanga
Nitafungua account kwa kila mtoto mchanga
Mabomba yatatoa maji na maziwa nchi nzima
Watu wa vijijini mtasahau habari za visima
Nitafadhili wachawi waweze kutengeneza ndege
Kila mtu awe na yake makonda na wapiga debe
 
Kiitikio.
Si mtafurahi Watanzania jamani…
…..ndiyooo mzeee
Si ni kweli nakubalika jamani…
ndiyooo mzeeee
Basi mimi ni mkombozi wenu jama..
ndiyo mzeee
Na nitafuta shida zenu zote..
ndiyo mzeee
Hivi ni nani ni vijimbamambo …
ndiyo mzeee
Na vinanikera kweli kweli mimi..
ndiyo mzeee
Basi hali itabadilika sawa..
ndiyo mzeee
Na hatamu tutaishika ok….
 ndiyo mzeee
Ubeti wa pili
Wafanyakazi wa serikalini nashangaa hamna magari Yaani hata mikweche hahaaaa hii ni hatari
Ninampango wa kuongeza mishahara iliyo minono
Mara mia ya ile ya mwanzo ilifayofanya mfanye mgomo
 Nitawapa nyumba nzuri na magari ya kifahari
Watu watashangaa mtakapopita kila mahali
Mkulima kila mmoja nitampatia trekta
Nadhani hiyo kidogo itasaidia kunyanyua sekta
Mtauza nafaka zenu bilioni kwa mabilioni
Watu midomo wazi kama wamekamatwa ugoni
Walimu zawadi zenu amm nimezificha moyoni
Nadhani mtazimia siku mkizitia machoni
We acha tu mtafurahi nyinyi
Ila hapo hapamfahi mtu mwingine niwekeni mimi
By the way polisi wote ninawasifu
Jinsi mnavyokwenda sahani moja na wahalifu
Sasa kila mmoja nitampatia helicopta
Nadhani hiyo wote hapo hamjawahi kuota
Raia wa Tanzania mtalala milango wazi
Infakti nauhakika wa kuthibiti ujambazi
Nitajenga barabara tano tano juu na chini
Nitajenga kumbi nyingi sana za starehe baharini
 Ninaupendo kuliko wa mshumaa kumulikia wenzangu
Mtakaoyumba kiuchumi tutagawana vya kwangu.
 
Kiitikio.
Kibwagizo
Ndugu wananchi kuna mtu anasawali kutoka kwa mgombea?
Nauliza hivii kuna mtu anaswali basi ajitokeze ili aweze kuuliza swalii..
Ubeti wa tatu
Nyie ndugu zangu huyu msimpe uongozi siyo vizuri
Muongo tu mnafiki na kiburi kimsuli
Anaongopeeaaaa saaanaa sijui kazaliwa muda gani alfajiri au alasiri Au wakati wa mvua zile za kipindi kile
Amepita pita school lakini mambo yake si mazuri
Wala tusimtetee atatuangamiza
Labda angesubiri kwanza uchaguzi umekwisha
 Tumemfuma mwenyewe kwa kalmanzira anasafishwa
Kalumanzira akamwambia ehee shida yako
Elezea fasta fasta kabla jini hajapanda
Mmmmhhhh chyaaaaaaa
 Hajakaa vizuri mashetani si yakamuanza
Kakurupuka kwa kasi kimbunga amejichanja
Tukamsikia akisema kwa kasi sauti kubwa ya kukaripia
Iihiiii chyaaaaaaaaaa
Waungwana mnisaidie ndiyooo nitamweleza
Uongo mtupu babake ameliwa
Waungwana wamempeleka jau mpaka kaibiwa
Yupo hamna……………………….amewehuka
Hajatulia huyu mpepeeni upuuuuffff upuuuuffff
Ni sauti iliyosikika kutoka kwa mzee wa pembeni
Sijui msaidizi mganga au mpelelezi
Na kwa taarifa yako uongozi hupati ng’oo
Labda urudi kwenu uende ukavunje tunguli
 Na hao waganga wako waeleze hupati kitu hapa
 Hata utoe chapaaaa.
Kiitikio.
Je wananchi mmenisikia..
ndiyo mzeee
Kuwa huyu jamaa hatufai…
ndiyo mzeee
Na inafaa kumchukia..
ndiyo mzeee
Hatumtaki aondoke zake..
ndiyo mzeee
Tusizubae na maneno yake..
ndiyo mzeee
 Tunahakikisha hatumchagui..
ndiyo mzeee
Asitufanye siye wanafiki…
ndiyo mzeee
Sugu – sugu
Kiitikio.
Wanakuita sugu x 3
Ubeti wa kwanza.
Wanaita Mr. two kwa jina jingine Sugu
Sugu mtu wa vurugu
Wengi sasa wanakubali mimi ni dume la mbegu
Yaani ni mtu ambaye nipo
Na hata nisipokuwepo sauti yangu itakuwepo
Nataka kuwa kama 2pac
Itikadi zangu nazieleza kwenye mic
Napata matatizo natatua bila chuki
Shukrani za dhati kwa mashabiki
Mwanzo nilikataa mliponiita
Super star
Lakini sasa nakubali siwezi tena kukataa
Ninapopita sehemu nyingi nakutana na watu wa aina nyingi
Mara nyingi wananiuliza maswali mengi
Wengine wananiuliza eti kama navuta bangi
Nakataa kujibu maswali yasiyo ya msingi
Sababu nina mambo mengi Kila siku kwenye ziara kama vile rais
Hata mama anajua mimi ni mtu wa mitikasi ila tu basi
Na naweza kuwakamata watu nuksi
 
Na sipo longolongo ninapojimix na fix
Dawa ya mabishoo ni kuwa bishoo zaidi yao
Sugu na mbalimbali zaidi yao
Napata message kwenye voda kutoka kwa madem zao
Mi ndo sugu
Hata mtoto wa demu wangu ananiita uncle sugu.
Ahaaaaa staraa.
Kiitikio.
Ubeti wa pili.
Nayajua matatizo zaidi yako
Na hata kama ni msoto nimepata zaidi yako
Usinione brothemen kwa kuwa nipo na mkoko
Shoko utazima zako
 Kasheshe zangu nzito
Hautaweza peke yako
Dar es salaam bongo yangu
Wa kwapi machizi wangu
Kokote kule mliko naomba muite jina langu (suguuu)
Napata flag kila ninapopita
Hata watoto wadogo wakiniona wananiita
Naitika bila kusita
Nikiamua kukomaa mbaka promota anadata
Popote heshima ilipo hapo mimi ndipo napenda niwepo
Sauti yangu kwenye mic inasambaa kama upepo
Narudia  kusema tena muziki ni kazi yangu
Nawaombe kwa mungu mashabiki wangu
Na mamc wote ambao ni kama wadogo zangu
Kuna kitu kimoja watu wengi  hawajajua
Huwezi kuizuia mvua
Sugu ni kama mvua kama kunyesha nanyesha
Kama barozi kwenye chat napandisha
Wananiita sugu machizi wote sema sugu oyaaaa sugu
Mambo namna gani sugu na siwezi kukataa kuitwa sugu
Wakati mimi ni sugu.
Kiitikio
MAREJEO:
Mulokozi, M.M. (1996), Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam. TUKI.
Wamitila. K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi. Istilahi na nadharia. Focus Publishers Ltd. Nairobi. Kenya.
Simiyu, W. (2010). Kitovu cha Fasihi Simulizi. Serengeti Bookshop. Makoroboi. Mwanza.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-16T11:07:22Z 2021-07-16T11:07:22Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=585 <![CDATA[Matumizi ya Dhana ya Sanaa za Maonyesho za Jadi katika Tamthiliya za Leo]]>
.pdf   Matumizi ya Dhana ya Sanaa za Maonyesho za Jadi katika Tamthiliya za Leo.pdf (Size: 199.3 KB / Downloads: 6) ]]>
false