MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Nukuu]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ 2024-05-02T07:30:27Z MyBB MwlMaeda]]> 2022-04-29T03:50:32Z 2022-04-29T03:50:32Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2536 <![CDATA[KITABU CHA MWANAFUNZI- KISWAHILI 2- (TET)]]>
.pdf   KIDATO CHA 5&6 KISW-2.pdf (Size: 68.71 MB / Downloads: 47) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2022-04-29T03:46:04Z 2022-04-29T03:46:04Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2535 <![CDATA[KITABU CHA MWANAFUNZI- KISWAHILI 1- (TET)]]>
.pdf   KIDATO CHA 5&6 KISW-1.pdf (Size: 88.53 MB / Downloads: 48) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-12T06:57:42Z 2021-12-12T06:57:42Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1715 <![CDATA[UHAKIKI WA RIWAYA YA VUTA N’KUVUTE]]>
.pdf   UHAKIKI-RIWAYA-YA-VUTA-NKUVUTE.pdf (Size: 644.09 KB / Downloads: 16) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-12T06:16:20Z 2021-12-12T06:19:09Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1709 <![CDATA[VIPENGELE VYA MTINDO]]> FASIHI ni sanaa inayotumia lugha na ambayo hujishughulisha na binadamu pamoja na maisha yake na hugusa au huacha athari fulani na hupatikana katika umbo ambalo linatambuliwa na jamii.
Kwa ujumla fasihi ni sanaa inayotumia lugha na yenye maudhui yahusuyo taratibu za maisha ya binadamu katika jamii husika.
Baada ya kuangalia dhana ya fasihi kwa ujumla sasa tuangalie dhana ya mtindo na nafasi yake katika fasihi.
Senkoro (1982) anasema mtindo katika kazi yoyote iwayo ya fasihi ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi hiyo na kuipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kaida zilizofuatwa (za kimapokeo) ama ni za kipekee.
Anaendelea kusema, mtindo ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hutokeza au huonesha nafsi na labda upekee wa mtunzi wa kazi hiyo.
Katika fasili hii tunaweza kuona anachokieleza mtaalamu huyu ni kwamba mtindo huhusiha upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi ambapo upangaji huu hutegemea upekee alionao msanii.
Kwa maana nyingine, unaposoma kazi fulani ya fasihi unaweza kumwona mtunzi wa kazi hiyo kulingana na jinsi alivyoiandika, kwa maana kwamba jambo moja linaweza kuongelewa na wasanii wawili tofauti lakini namna linavyowasilishwa likatofautiana na hii ni kulingana na upekee wao.
Wamitlia (2003) naye anasema mtindo ni jumla ya mbinu au sifa zinazomwezesha mwandishi kuwasilisha ujumbe wake. Huelezea mwandishi anavyounda kazi yake.
Anaendelea kusema, dhana ya mtindo hurejelea sifa maalumu za mwandishi au mazoea ya mwandishi fulani ambayo hujionyesha kwenye fani yake, mazoea hayo ya mwandishi ya kuandika, kuteua msamiati, tamathali za semi, taswira, uakifishaji, sentensi na kadhalika ndio yanayompambanua mwandishi huyu na mwenzake.
Kitu anachokisema hapa Wamitila hakitofautiani na Senkoro. Kinachoongelewa hapa ni upekee wa mwandishi husika, lakini Wamitila kasema kitu kimoja zaidi ambacho inaonekana Senkoro hakukiweka bayana, kwamba msanii anaonekana kuwa na mtindo fulani kwa sababu amezoea kutunga kazi zake za fasihi kwa namna fulani ambayo inadhihirisha upekee wake.
Kwa kauli hii ya Wamitila, tunaweza kusema kwamba mtindo wa mtunzi huonekana baada ya kuandika kazi zake kadhaa na kimsingi hii ndio huleta maana halisi ya mazoea.
Nakubaliana na kauli hii kwani hata hivyo huwezi ukahitimisha kuwa mtunzi fulani mtindo wake ni huu kama umesoma kazi yake moja tu. Kwa hiyo mtindo (upekee) wa mwandishi huweza kubainishwa baada ya kupitia kazi zake kadhaa.
Kwa ufupi tunaweza kusema kuwa mtindo ni ule upekee alionao mtunzi wa kazi ya fasihi katika kuipa kazi yake sura fulani kifani na kimaudhui ambapo mtunzi mwingine hawezi kufanya hivyo hata kama kitu kinachoongelewa ni kilekile.
Ni namna ambavyo msanii hutunga kazi na kuipa kazi hiyo uzuri kifani na kimaudhui. Mtindo huambatanishwa na tabia ya utungaji ambayo humpambanua mtunzi mmoja kutokana na mwingine.
Katika muktadha huu, mtindo hubainika katika jinsi mtunzi anavyoteua kujieleza kwa kuchanganya ndimi, kutumia methali na mafumbo au kufumbata ujumbe kwenye ufupi au urefu wa sentensi zake.
Aidha, dhana ya mtindo huenda ikajumuisha wasanii wa kipindi fulani cha kihistoria na sifa zao za uandishi kwa kutegemea matumizi ya lahaja au maneno ya kale.
MTINDO
Tunapotaka kujua mtindo wa msanii katika kazi husika hususani riwaya tunaangalia matumizi ya lugha; matumizi ya daiolojia; namna na nafsi ya usimulizi; ukuaji wa wahusika; hisia za mwandishi; namna anavyopanga sura au matukio katika hadithi; tamathali za semi; mandhari na uteuzi wa msamiati.
Baada ya kuangalia dhana ya mtindo, ni vyema sasa tukaangalia nafasi yake katika fasihi. Kwa ujumla, mtindo una nafasi kubwa tu katika kazi ya fasihi.
Mtindo humtambulisha mtunzi wa kazi ya fasihi. Watu hupenda kazi ya msanii fulani kwa sababu mtindo anaoutumia huwavutia wasomaji wake.
Mtindo ndicho kipengele kinachotenganisha kazi nyingine za kisayansi au za kawaida. Bila mtindo, kazi za kifasihi zisingepata mashabiki wengi. Kwa hiyo mtindo ndio huibua hisia na kuwafanya wapende zaidi kusoma kazi za msanii husika.
Kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, tunapozungumzia dhana ya mtindo tunakuwa tunarejelea mwandishi husika, kwa maana kwamba ubinafsi wake ndicho kile kinachoonekana kwenye kazi yake.
Kwa hiyo tunaposema hadithi fulani ina taswira nyingi, ina sitiari nyingi au lugha yake ni rahisi au lugha yake inavutia, imetumiwa kwa uwazi, ufiche au ugumu na kadhalika tunakuwa tunarejelea mtindo wa mtunzi husika.
Kwa mantiki hiyo dhana ya mtindo kama ilivyokwisha jadiliwa inaonekana kwa namna mtunzi anavyopanga kazi yake kifani na kimaudhui, yaani namna anavyotumia lugha, anavyopanga visa na matukio, uteuzi wa mandhari, falsafa anayoiwasilisha, ujumbe anaoudhamiria na kadhalika.
Kiufupi mtindo unagusa haya:
  • Taharuki
  • Msukumo pofu/mficho wa matukio
  • Matumizi ya nafsi
  • Mtindo wa Dayalojia/Masimulizi
  • Matumizi ya Barua
  • Matumizi ya hadithi ndani ya hadithi
  • Matumizi ya maneno ya mtambaji
  • Matumizi ya kicheko
  • Matumizi ya nyimbo
  • Matumizi ya ngoma
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-12T06:11:10Z 2021-12-12T06:11:10Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1708 <![CDATA[DHIMA YA UHURU WA MWANDISHI]]>
  • Mwandishi atakuwa huru kuikosoa jamii au tabaka lolote litakaloenda kinyume nautaratibu wa jamii bila matatizo.Mwandishi atakuwa huru kuonyesha dhuluma, ukatili na ujangili unaofanywa katika jamii na tabaka lolote bila matatizo yoyote.
  • Kukiwa na uhuru wa mwandishi, msanii atakuwa na falsafa inayoeleweka pamoja na utashiwake.Hii itamfanya mwandishi awe na msimamo unaoeleweka.Msimamo  wake utamsaidia kuifundisha na kuielimisha jamii bila uoga.Ataijiulisha jamii hali yake na ataonesha jamii njia za kufikia haja na kutatua matatizo ya jamii bila uoga
  • Mwandishi atakuwa huru kutoa mwongozo katika jamii kwa kuikomboa jamii kutoka katika fikra mbovu za kugandamizwa,kunyonywa na kuonewa na tabaka tawala ili jamii ipate haki na heshima bila woga wa kuliondoa tabaka ambalo ndilo lenye mamlaka yote katika jamii.
  • Uandishi wa kikasuku utapungua, waandishi au wasanii huacha tabia ya kuwa vipaza sauti vya tabaka fulani katika jamii, wasanii makasuku huandika mambo bila kufikiri na kurudiarudia  mawazo yaliyokwisha semwa na wanasiasa majukwaani bila fikra mpya kwa hali hii hupotosha jamii.Hivyo kunapokuwa na uhuru wa mwandishi wa kutosha hali hii haiwezi kutokea kwa sababu mwandishi ataandika mambo mbalimbali yanayojitokeza katika jamii na hataweza kujikomba au kujipendekeza kwa tabaka tawala lenye mamlaka yote katika jamii.
  • Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi fasihi inakuwa chombo cha kuikomboa jamii kiuchumi,kisiasa, kiutamaduni na kifikra (kimawazo). katika jamii ya kitabaka fasihi ni mali ya tabaka tawala na hutumia fasihi kutetea na kulinda maslahi yao.Hivyo inapokuwa mali ya jamii nzima inatumiwa na jamii hiyo katika kuwakomboa wanajamii wote.
  • Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi, mwandishi anakuwa huru kuichokoza na kuisukasuka (kuichochea)jamii bila matatizo yeyote. Mwandishi atachokoza jamii ya wakulima na wafanyakazi kufikiri ili waweze kulichunguza tabaka tawala kwa jicho pevu na kutoa hadharani uozo uliopo katika kunyonywa, kupuuzwa,kuonewa, kugandamizwa na kunyanyaswa na tabaka tawala
  • Mwandishi atakuwa huru kuelimisha na kuishauri jamii katika mambo muhimu yanayojitokeza katika jamii bila woga.Mwandishi ataishauri jamii kuhusiana na mambo kama vile afya, elimu na ichague mambo gani yanafaa kuhifadhiwa na yapi hayafai vile vile msanii anakuwa huru kuirekebisha jamii bila woga kwa kuangalia yapi ni mazuri na yapi ni mabovu yanayotendeka katika jamii
  • ]]>
    false
    MwlMaeda]]> 2021-11-20T06:51:40Z 2021-11-20T06:51:40Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1506 <![CDATA[UHAKIKI WA DIWANI YA FUNGATE YA UHURU]]> KITABU: FUNGATE YA UHURU
    MWANDISHI: MOHAMED S. KHATIBU
    WACHAPISHAJI: DUP
    MWAKA: 1988
    UTANGULIZI
        Fungate ni kipindi cha siku saba baada ya harusi..Ni kipindi ambacho Bwana na bibi harusi hula na kunywa tena milo ya kuchagua wakati wote wa fungate.Fedha na vifaa vitumiwavyo na maharusi huwa ni vya kuazima au kuchangiwa(si lazima viwe vyao) Wanapewa  kutoka kwa ndugu na jamaa na hata na vijana wa kuwahudumia.Wachangaji hufanya hivyo kwa sababu wanajua kuwa fungate ni ya muda mfupi(siku saba tu),hivyo huvumilia.
    Fungate ni lazima iwe na kikomo.Ikizidisha kikomo hicho ibadili jina labda iitwe unyang’anyi,ulimbwende,uvivu,uzembe au jina lolote lenye kashfa hasa unafiki au usaliti.Mwandishi wa diwani hii ameimwaga ghadhabu hiyo kwa hao maharusi waliohesabu ukarimu wao kuwa ni upumbavu.
    Uhuru:Uhuru ni neno linalopendwa sana na wanasiasa wa ubepari au ujamaa.Hekaheka za uhuru(kudai,kuomba au kupigania) zinaweza kufananishwa na shughuli za kutafuta mchumba,kupeleka posa kulipa mahari,na kufunga ndoa.
    Katika kipindi chote cha uhuru, watu, hususani viongozi,hufurahi na kufanya sherehe ambazo huwagharimu raia-mali na vitu mbalimbali.Lakini kwa kuwa uhuru ni kitu cha thamani kama maharusi,raia hukubali kugharimia sherehe hizo.Lakini pia sherehe za uhuru kama fungate hutazamiwa iwe ya muda mfupi –labda mwezi  mmoja au miwili.
    Raia wanchi zilizopata uhuru barani Afrika walikuwa na shauku ya kupata maendeleo lakini hawajafikia lengo lao hadi sasa kwa sababu viongozi wetu wanaendeleza Fungate ya Uhuru.Hivyo viongozi wanchi za Afrika wamewasaliti wananchi wao waliowachagua.Katika utangulizi mwandishi anasema ;
    Nikate tama,
    Kwani tuendavyo,hatufiki,
    Vile ipasavyo,hayakamiliki,
    Mambo yalivyo,ni unafiki,
    Tumesalitiwa!
    MAUDHUI
        Fungate ya Uhuru ni diwani inayojdili kwa mapana sana juu ya matatizo mbalimbali yanayokwamisha ujenzi wa jamii mpya hapa Tanzania.Matatizo hayo ni kama vile usaliti,unafiki,wizi,hujuma,udanganyifu,rushwa pamoja na uongozi mbaya.
    Dhamira Kuu: Ujenzi wa jamii mpya.
    Mwandishi anajadili kwa kiasi kikubwa suala la ujenzi wa jamii mpya.Mwandishi anaitaka  jamii  itupilie mbali unyonyaji , uonevu, dhuruma, udanganyifu, wizi, unafiki,  umasikini, uongozi mbaya na ukandamizaji wa watu wa tabaka la chini ili kuijenga jamii kwa upya.Jamii ambayo hatamu zote za uongozi (utawala,siasa na uchumi) zitakuwa mikononi mwa wakulima na wafanyakazi kwa misingi ya haki na usawa.
         Itikadi ya kujenga jamii mpya ilijengeka juu ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo ilitangazwa mwaka 1967 baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha.Hadi 1988,mwandishi anaandika kitabu hiki anaonesha kuwa bado hatujafanikiwa kujenga jamii mpya hapa Tanzania.Hii inatokana na sababu zifuatazo;
      Kwanza,bado kuna dhuruma, usaliti,unyonyaji na wizi wa mali za umma.katika  shairi la “Wingu’’  mwandishi anasema;
    Bado:
    Wingu limetanda,
    Limetanda,
    Na kutughubika ghubi,
    Mvua:
    Lakini hainyeshi,
    Hainyeshi,
    Ukame umetanda waa!
    Mimea:
    Tulipanda kwa miongo,
    Kwa miongo,
    Yote imekauka!
    Pia katika shairi la “Wizi”mwandishi ameonesha dhahiri kuwa wizi umo ikuluni, bomani, kanisani, misikitini, na hekaluni.Mwandishi ameonesha kuwa dini zawabariki wezi, polisi hulinda wezi, na majeshi huhalalisha wizi.katika ubeti wa 1 mwandishi anasema;
    Wizi umo;
      Kanisani,
    Msikitini,
    Kasirini,
    Na bomani,
    Wanyang’anywao ni waumini.
    Pili, mwandishi ameonesha kuwa bado kuna matabaka katika jamii zetu.Ameonesha kuwa kuna tabaka la wenye nacho na tabaka la wasionacho.Tabaka la juu (utawala) unaolinyonya tabaka la chini(tawaliwa).Mfano katika shairi la “Fungate” mwandishi ameonesha jinsi tabaka tawala linavyofurahia maisha kwa kuishi katika majumba mazuri, kutembelea magari ya faharin, n.k.
    Katika shairi la”Waja wa Mungu”mwandishi anaonesha jinsi tabaka la chini linavyoishi kwa shida.Kwa mfano, kula kwa shida, kulala kwa shida, kuvaa kwa shida, hawapati elimu na huduma nzuri za afya.
    Tatu, mwandishi ameonesha kuwa, bado kuna uongozi mbovu katika jamii zetu.Mfano katika shairi la “Viongozi wa Afrika” mwandishi anashutumu vikali viongozi wanaotumia  madaraka  yao  vibaya na kugandamiza watawaliwa.Anasema;
    “Viongozi wa Afrika,
    Wanaotawala kwa mabavu,
    Kujifanya ni washupavu,
    Wao wachache na werevu,
    Na umma wote ni mpumbavu,
    Wanafiki,
    Wazandiki”.
    Pia shairi la “Njama”  mwandishi anaonesha  jinsi viongozi wanavyotumia njama mbalimbali kulinyonya tabaka tawaliwa.Viongozi wanatumia njama mbalimbali ili kuhakikisha kuwa hakuna anayewapinga wala kuhoji hata kidogo.
       Nne, mwandishi anaonesha kuwa, kuna unyonyaji wanaofanyiwa wakulima katika kuuza mazao yao.Ameonesha kuwa wakulima hunyonywa na kudhurumiwa na kupewa bei kidogo wakati kuuza mazao yao.Shairi la “Naona”mwandishi  linadhihirisha haya katika ubeti wa 6,ansema;
       Naona
      Wanakwenda gulioni
    Mazao kuyazabuni
          Wanapata bei duni
    Na kubaki maskini
    Unyonge ulele.
           Ni kutokana na matatizo hayo ya wizi, rushwa, uongozi  mbovu, dhuruma, uonevu na unyonyaji ndiyo maana tumeshindwa kujenga  jamii mpya.
    Mwandishi ameonesha mbinu mbalimbali ambazo jamii inapaswa kuzitumia ili  kuijenga   jamii mpya na hizo ndizo  dhamira ndogo ndogo za diwani hii kama zifuatazo;
    1.Kuwa na uongozi bora
     Uongozi mbaya ni kikwazo kikubwa  katika ujenzi wa jamii mpya.Shairi la”Fungate” Mwandishi ameonesha jinsi viongozi wanavyotumia madaraka yao vibaya kwa kuwanyonya wananchi wa kawaida.katika ubeti wa 1 mwandishi anasema;
      Fungate ya uhuru,bado inaendelea,
    “Harusi” wana nuru,wazuri wanavutia,
      Wengi inawadhuru,na tena wanaumia
         Mwandishi anaeleza kuwa tangu tupate uhuru hadi leo bado viongozi wetu wapo Fungate wakila na kunywa huku wananchi wakiendelea kuteseka na maisha magumu,hivyo mwandishi anaitaka jamii kuung’oa  uongozi mbaya na kusimika uongozi uliobora unaowajali wananchi wake .
    Shairi la “Viongozi wa Afrika”mwandishi anakemea viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya kwa kujinufaisha wao wenyewe, wenye hisa katika viwanda, mabenki, makampuni au mashamba ya mabepari kuwa ni wasaliti.Anawakemea wale viongozi wenye upendeleo, wanaotumia pesa za umma kwa kuendeshea sherehe.Mwisho anawakemea viongozi wanaopokea rushwa na amewaita magaidi au mafisadi.
      Shairi la “Utawala” mwandishi amehimiza kuuangusha utawala wa kibepari ambao unawanufaisha wachache na walio wengi hunyonywa, hugandamizwa, huonewa na kunyanyaswa na hao wachache.
    Shairi la “Kinyang’anyiro” mwandishi anaonesha jinsi viongozi walivyokimbilia kushika madaraka (hasa enzi za uhuru) lakini wanashindwa kuleta maendeleo hapa nchini.
        Kwa ujumla mwandishi anapendekeza kuwa, ili tujenge jamii mpya lazima tuwe na uongozi bora .
    1. Kuwa na umoja na ushirikiano
    Mwandishi anaona kuwa  ili  tujenge jamii mpya ni muhimu tuungane  sote tuwe kitu kimoja “Katika shairi la “Unganeni” mwandishi anawataka wananchi wote wa Afrika kuungana ili kuendeleza mapambano ya kuleta haki na usawa. Anasema:-
    “Wafanyakazi wa Afrika, tuungane,
    Na wakulima kadhalika, tushikamane,
    Makabwela  mnaosumbuka, tukutaneni,
    Tujiandae kwa mapambano, yalo marefu,
    Ushindi ni wetu”.
       Mwandishi anaitaka jamii hasa tabaka la chini kuungana na kuendeleza mapambano dhidi ya viongozi wanafiki, mabepari, mamwinyi wanaonyonya, wanaonyanyasa, wanaowatesa, wanaowadhurumu na kuwagandamiza watu wa tabaka la chini.
    Mwandishi katika shairi la “Nikizipata Bunduki ‘’anapendekeza  matumizi ya silaha ili kuondokana na matatizo hayo yote. Hivyo ili tujenge jamii mpya ni lazima tuungane tuwe kitu kimoja kwani  ‘’Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu’’.
    1. Ujasiri na kujitoa mhanga
    Mwandishi anaona ili kuijenga jamii kwa  upya ni muhimu kuwa na ujasiri,kutoogopa vitisho. Katika shairi la “Gorila” ubeti wa 1 mwandishi anasema;
    Gorila,jasiri!
         Wa Afrika ,shujaa,mshupavu,umevinjari,
          Mtutu shika,mevaa,ukakamavu,uko tayari,
          Gorila,ruwaza,wa kizazi kipya
      Mwandishi anaitaka jamii hasa vijana kuwa majasiri na mashujaa katika harakati za kuleta mapinduzi. Pia wanamapinduzi wanatakiwa wawe wavumilivu kwa sababu ujenzi wa jamii mpya sio lelemama, ni safari ndefu.
       Vile vile katika shairi la “Umma”  mwandishi anahimiza ujasiri katika kuleta mapinduzi katika jamii. Mwandishi nasema:-
    “Umma,
    Uliovinjari, kuangamiza  mtabaka,
    Hima,
    Uwe tayari na usiwena shaka,
    Ongoza mapambano,ya wafanyakazi, hadi ushindi.
    Hivyo mwandishi anaitaka jamii ijitoe mhanga ili kufanikisha suala la ujenzi wa jamii mpya.
    1. Kufanya mageuzi (mapinduzi)
    Mwandishi anapendekeza mbinu ya kufanya mageuzi ili kufanikiwa katika suala zima la ujenzi wa jamii mpya. Katika shairi la “Umma” mwandishi anawaasa wanajamii wajiandae kuangamiza matabaka yaliyokithiri katika jamii.
    Mwandishi anapendekeza mbinu mbalimbali za kufanya mageuzi (mapinduzi), kwanza, jamii hasa watu wa tabaka la chini waungane ii kuondoa viongozi wanaotumia madaraka waliyopewa kwa manufaa yao binafsi. Katika shairi la  “Ungameni” mwandishi anasema;
      Msimamo wa kitabaka,tuwekeni,
     Bepari wote kuwashika,wawe ndani,
     Na mamwinyi bila ya shaka,wambaroni,
     Tusizubae,kazi ianze,twangoja nini?
      Wakati ni huu.
       Pili,mwandishi anapendekeza kutumia silaha katika mageuzi hayo ikiwa unyonyaji hautaondoka kwa amani. Mfano shairi la “Siku Itafika” na “Nikizipata Bunduki” .Pia Katika shairi la “Utawala” mwandishi anapendekeza yafanyike mgeuzi  ili kuuangusha utawala unaojinufaisha na kuendeleza matabaka katika jamii. Katika shairi la “Mjamzito” mwandishi anaonesha jinsi watu wanavyoogopa harakati za mapinduzi katika jamii zetu. Katika mashairi ya “Ni vita si Lelemama” na “Maendeleo ya Umma” mwandishi anaonesha jinsi suala la mageuzi lilivyo gumu, ingawa ana matumaini kuwa umoja na ushirikiano wetu utatufanya tushinde. Pia anaamini kuwa unyonyaji na uonevu hautadumu milele, kwani kuna siku, saa, dakika na nukta itafika uovu wote utaondolewa kwa nguvu.
    Katika shairi la “Joka La Mdimu”  mwandishi anatoa mfano wa tawala dhalimu zilizoondolewa kwa nguvu kwa ushirikiano wa tabaka la chini. Katika shairi hili mwandishi anaonesha jinsi wananchi walivyoshirikiana katika kuutokomeza ukoloni hapa nchini.
    Hivyo ili nasi tufanikiwe kujenga jamii mpya hatuna budi kufanya mapinduzi (mageuzi).
    1. Kuwa na uzalendo katika nchi
    Uzalendo ni ile hali ya kuipenda nchi kwa dhati na hata kuifia. Msimamo wa mwandishi ni kuwa hataihama nchi yake hata kwa kutishiwa njaa, maafa au umaskini. Pia ataipigania nchi yake ili iwe salama. Hivyo hata sisi hatuna budi kuipigania nchi yetu kwa hali na mali ili kuondoa udhalimu uliopo. Katika shairi la  “Nchi Yangu”  mwandishi anasema;
     Naipenda nchi yangu,
    Naipenda,naipenda nitakufa naipenda.
    Tailinda nguvu zangu,tailinda,
    Tailinda kwa maafa tailinda,
    Sitakwenda kwa wenzangu,
    Sitakwenda,sitakwenda hata sifa sitakwenda,
    Nitakwenda hku kwangu,nitaganda,
    Nitaganda kwa ulofa nitaganda.
       Mwandishi anaona kuwa, tukiwa na uzalendo na nchi yetu tutafanikiwa kujenga jamii mpya, kwani usaliti wa viongozi wetu utaanguka na kila mmoja ataipenda nchi yake kwa  dhati.
    1. Kupiga vita ukoloni mamboleo
    Ukoloni mamboleo ni ile hali ya nchi kupata uhuru wa bandia (kisiasa) lakini njia zote za uchumi hutawaliwa au hubaki mikononi mwa mabepari au watu wa nchi nyingine.Katika shairila “Ruya”  mwandishi anasema;
    Ruya,menitoa shamba,mji kuuramba niwe utumwani?
                 chini umwinyini,
                nimo kifungoni!
               Ni ‘’huru’’ machoni!
    Ruya,hivyo wanitimba,kunifunga kamba,za ukoloni,
             Njozi niondokee!
           Mwandishi anaona kuwa wazungu ndio walioondoka katika ardhi ya Afrika lakini unyonyaji bado upon a unaendelea. Viongozi waliochukua madaraka baada ya uhuru bado wanaendeleza zile taratibu zilizoachwa na wakoloni.
    Katika shairi la “Kunguru” mwandishi anaonyesha  pia athari za ukoloni mamboleo hapa nchini. Katika shairi hili mwandishi anazungumzia juu ya kuondoka kwa ukoloni mamboleo. Hivyo mwandishi anaonesha kuwa ili tujenge jamii mpya ni lazima tupige vita ukoloni mamboleo ili tuwe na uhuru wa kuamua mambo y etu wenyewe.
    1. Kupiga vita wizi wa maliya umma
    Mwandihi wa diwani hii ameshindwa kuficha hasira yake dhidi ya wizi. Ameutaja wazi kuwa umo kanisani, msikitini, ikuluni na bomani. Waandishi wengi kukwepa kutaja ukweli kama huu. Asemacho mwandishi ni kwamba, sehemu zote za jamii zimeoza. Zamani watu wengi waliamini kuwa viongozi wa dini wana maadili wasiyoweza kuyakiuka. Kwa hiyo, maovu hayo yasingetokea huko. Lakini sasa viongozi hao na wale wa Ikulu wamejiunga na wahalifu. Lililo baya zaidi ni kuwapo kwa “Walinzi” wanaolinda hao wezi.. Shairi hili la “wizi” mwandishi anasema;
    Wizi umo;
           Kanisani,
           Msikitini,
           Hekaluni,
    Wanyang’anywao ni waumini.
    Kwa kifupi wizi umehalalishwa na kubarikiwa .
     Mwandishi  hasemi tufanyeje  Lakini kwa mtiririko na mantiki ya mashairi yake mengine, mwandishi anashauri ufumuaji na usafishaji wa jamii nzima.Katika  shairi la“Kunguru”  mwandishi pia anajadili Suala la wizi . Japo amefumba  lakini anawaelimisha wasomaji kuhusu wezi waliotimuliwa na kutawanywa. Baada ya muda wezi wakajitayarisha kwa mbinu tofauti na kuendeleza wizi wao. Mwandishi  anatanabaisha raia kuhusu kuwapo kwa wezi hawa na marafiki zao. Katika shairi la “Joka la Mdimuni” mwandishi anatanabaisha watu kuhusu uwezekano wa wakoloni kurudi kwa umbo tofauti lakini kwa athari zile zile. Katika shairi la “Naona “  Mwandishi anaonesha taabu wanazopata wakulima na malipo duni wanayopewa kwa mzao yao. Anamaliza kwa msimamo huu;
    ”Naona
    Ni fukara wakulima
    Wamepigwa alitima
    Kwa wengine ni neema
    Kwao wao ni nakama
    Wamekosa haki!
    1. Kupiga vita ukasuku wa viongozi wetu
       Mwandishi amekemea tabia za viongozi na watendaji wengine kukubali kila lisemwalo bila kufikiri au kwa hofu tu, si nzuri. Tabia hii ya ukasuku anauita ugonjwa unaohitaji tiba  (tiba yenyewe hakuitaja). Ugonjwa huu hudunisha  akili. Mwandishi anaonyesha  chanzo na athari zake.Katika shairi la “Ukasuku” mwandishi anasema;
    “Kupea kwa ukasuku
    Rais huhubiri
    Wabunge hukariri
    Wasomi huhariri
    Na taifa husimama”  .
    Mwandishi  anawachunguza viongozi wa bara la Afrik na kuwaona kuwa ni mabepari, madikteta, wenye ukabila, wabadhirifu wasiojali raia wao wapenda hongo. Wote amewakemea na kuwakanya wasitende hivyo. Amewapa majina yanayowafaa- wahaini, wasaliti, majasusi n.k. Mwandishi anastahili pongezi kwa kuweza kuwakemea, badhi ya waandishi huwasifu.
    UJUMBE
    v Uongozi mbaya, wizi wa mali ya umma, rushwa na kukosekana kwa haki, ukasuku na matumizi mabaya ya mali ya umma ni vikwazo  ujenzi wa jamii mpya hapa nchini.
    v Umoja na ushirikiano ni njia moja wapo ya ujenzi wa jamii mpya hapa nchini.
    v Mfumo wa ujamaa ni mfumo pekee utakaomkomboa mtu mnyonge, yaani ndiyo utakaoleta hali nzuri kwa wakulima au wafanyakazi.
    v Ili tujenge jamii mpya ni lazima tuwe na ujasiri wa kujitoa mhanga, tuwe wazalendo na nchi yetu na tufanye mapinduzi (mageuzi ya kweli) katika jamii.
    v Ukoloni mamboleo ni kikwazo cha ujenzi wa jamii mpya hapa nchini.
    v Mapenzi ya kweli ni yale yasiyojali fedha au hali ya mtu.
    FALSAFA
    Mwandishi anatetea itikadi ya ujamaa yenye kuleta haki na usawa kwa kila mtu. Analaani wizi, dhuluma na majivuno ya kirasimu. Mwandishi angependa nchi iongozwe kwa haki na usawa. Vile vile anatetea mapenzi ya kweli katika maisha.
    MSIMAMO
    Mwandisi ana msimamo wa kimapinduzi, kwani ameonesha matatizo mbali mbali yanayozikumba jamii zetu na mbinu za kuondokana na matatizo hayo. Miongoni mwa matatizo hayo ni uongozi mbaya, wizi wa mali ya umma, rushwa na dhuluma, n.k.
    Fani
    a)Muundo
    Mwandishi ametumia muundo changamano. Kuna muundo wa tathnia (mistari 2) mfano shairi la “Mjamzito” (uk 5-6), Muundo wa tathlitha (mistari mitatu) mfano shairi la “Fungate” (uk 1), “Nataka Kusema” (uk 14), Muundo wa tarbia (mistari minne) mfano shairi la “Nahodha Mtwesi” (uk 5), “Gorila” (uk 11), “Afrika” (uk 17) , “Kunguru” (uk 19), n.k.
     Vile vile ametumia muundo wa sabilia au takhimisa (mistari mitano na kuendelea) mfano mshairi ya “Utawala” (uk 21), “Ladha ya Maji Katani”(uk 27), “Joka la Mdimuni” (uk 31), “Mkata “ (uk 15) n.k.
    b)Mtindo
    Diwani hii ina mashairi yanayofuata kanuni za ushairi wa kimapokeo na yale yanayofuata kanuni za mashairi ya kisasa. Hii ina maana kwamba, mwandishi anayakubali mashairi ya aina mbili (kimapokeo na kisasa)
    c)Matumizi ya Lugha
    Mwandishi ametumia lugha sanifu yenye lahaja ya Kiunguja. Lugha hii imejaa misemo mbali mbali, tamathali za semi na taswira.
    Misemo
    Imetumika kwawingi.
    Mfano:
    i)Nahodha mtwesi chombo chenda joshi (uk 5)
    ii)Waja wa Mungu (uk 20)
    iii)Paka shume (uk 34)
    iv)Utakiona cha mtema kuni (uk 24)
    v)Joka la mdimuni (uk 31) n.k.
    Tamathali za semi
    Tashibiha
    Mfano shairi la “Mkata” (uk 15):-
    i)Kitandani nilalapo kama dema la samaki…
    ii)Mbu ndani kama ndege wa vitani…
    iii)Matopeni hujazika mithili nimo karoni…
    iv)Nimekoni kama ndizi natokota na kufoka
    Sitiari
    Mfano shairi la “Uwapi Uzuri Wako” (uk 35)
    -Sasa ni chano cha maji, watu wajichanyatia
    -Baola mkahawani, kila mtu akaliya
    -Sasa jamvi la wageni, wajapo huwapokeya.
    Kejeli
    -Shairi la “Fungate” (uk 1) linakejeli tabia za baadhi ya viongozi wetu wanaoendelea kuifaidi Fungate ya Uhuru.
    -Shairi la “Kantu Sauti ya Kiza”  mwandishi anatumia nyuki kukejeli baadhi ya tabia chafu za watu.
    Tafsida
    Mwandishi ametumia Tafsida kuyasema maneno makali, machafu, matusi. Mfano shairi la “Paka Shume” linajadili suala la kumendea vitu vya watu kwa njia isiyo halali. Hata neno lenyewe fungate ni tafsida.
    Mbinu nyingine za kisanaa
    Takriri
    Katika shairi la “Mkata” (uk 15), “Dafina” pamoja na shairi la “Nchi Yangu”
    Mjalizo
    Katika shairi la “Mkata” (uk 15).
    Mdokezo
    Katika shairi la “Mwinyi Mpe Ndiyo”
    Ujenzi wa Taswira
    Neno Fungate linaleta taswira ya ulimbwende wa maharusi au viongozi. Shairi la “Mjamzito” (uk 5) linajenga taswira ya viongozi waoga katika jamii. Viongozi wasioweza kutatua matatizo ya wananchi. Shairi la “Paka Shume”(uk 34) linajenga taswira ya udokozi. Shairi la “Viongozi wa Afrika” (uk 15) linajenga taswira ya viongozi wanaotumia madaraka  vibaya.
    Jina la Kitabu
    Kwa ujumla jina la kitabu Fungate ya Uhuru linasadifu  yale yaliyomo ndani ya kitabu. Mwandishi  ameonesha jinsi viongozi wetu walivyo kwenye fungate ya Uhuru. Hali kadhalika wananchi bado wanaendelea kugharamia sherehe mbali mbali za viongozi kwa njia ya michango kama vile kodi, mchango wa mwenge, n.k.
    KUFAULU KWA MWANDISHI
    Kimaudhui
    v Mwandishi amefaulu Kuonesha matatizo mbali mbali ya jamii zetu na mbinu za kuyaondoa.
    Kutofaulu kwa Mwandishi
    v Mashairi mengi kyanahusu  siasa na hivyo kuwa kama mahubiri ya kisiasa.
    v Kusisitiza mfumo wa chama kimoja badala ya mfumo wa mageuzi  na kitabu kiliandikwa  wakati mfumo wa mageuzi umepamba moto dunia nzima.
    v Kumfanyia Mwinyi kampeni ni udhaifu, hii ni kutokana na ukweli kuwa Rais Mwinyi hakuweza kuondoa matatizo aliyoyajadili na ndiyo maana hadi sasa yapo.
    v Amekemea uongozi mbaya, lakini hakuonesha chanzo cha uongozi mbaya na mbinu mbali mbali za kuwapata viongozi bora hapa nchini.
    v Kutumia lahaja ya Kiunguja ni udhaifu mwingine wa mwandishi, kwani anakinyima Kiswahili sanifu uwanja wa kukua na kuenea.
    ]]>
    false
    MwlMaeda]]> 2021-08-22T08:10:48Z 2023-01-27T14:06:50Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=982 <![CDATA[MCHANGO WA FASIHI SIMULIZI KATIKA FASIHI ANDISHI]]>
    .pdf   MCHANGO WA FASIHI SIMULIZI KATIKA FASIHI ANDISHI.pdf (Size: 62.5 KB / Downloads: 3) ]]>
    false
    MwlMaeda]]> 2021-08-08T08:41:47Z 2021-08-08T08:41:47Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=801 <![CDATA[USIMULIZI]]>
    .pdf   USIMULIZI.pdf (Size: 113.8 KB / Downloads: 7) ]]>
    false
    MwlMaeda]]> 2021-07-29T12:56:05Z 2021-07-30T05:56:25Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=672 <![CDATA[TAMATHALI ZA SEMI KISWAHILI NA KIINGEREZA]]>
    .pdf   TAMATHALI ZA SEMI KWA KISWAHILI NA KIINGEREZA.pdf (Size: 147.24 KB / Downloads: 13) ]]>
    false
    MwlMaeda]]> 2021-07-27T06:37:46Z 2021-07-27T06:37:46Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=655 <![CDATA[UFAHAMU NA UFUPISHO]]>
    .pdf   Ufahamu na Ufupisho.pdf (Size: 127.44 KB / Downloads: 7) ]]>
    false
    MwlMaeda]]> 2021-07-25T09:03:55Z 2021-07-25T09:03:55Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=639 <![CDATA[ORODHA YA VITABU VYA FASIHI NA WAANDISHI WAKE]]>
    .pdf   ORODHA_YA_VITABU_VYA_FASIHI_NA_WAANDISHI.pdf (Size: 256.65 KB / Downloads: 10)


    .doc   ORODHA_YA_VITABU_VYA_FASIHI_NA_WAANDISHI.doc (Size: 644.5 KB / Downloads: 7) ]]>
    false
    MwlMaeda]]> 2021-07-20T10:44:37Z 2021-07-20T10:49:28Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=605 <![CDATA[Wahusika Katika Fasihi Andishi]]> Fasihi Andishi hutumia wahusika wanadamu, kinyume na Fasihi Simulizi ambayo hutumia wahusika changamano (watu, wanyama, mazimwi n.k). Kunazo aina kadhaa za wahusika katika kazi ya fasihi andishi kama vile: tamthilia, riwaya na hadithi fupi.
    Aina za Wahusika
    Wahusika Wakuu: hawa ni wahusika ambao wanahusishwa na takribani visa vyote katika riwaya/tamthilia. Wahusika huhusishwa kutoka mwanzo hadi mwisho.
    Aghalabu mhusika mkuu hafi isipokuwa katika trejedia/simanzi au hufa kifo cha ushujaa.
    Wahusika Wasaidizi: hawa ni wahusika wanaosaidia kujenga mhusika mkuu. Hutokeza mara nyingi katika hadithi.
    Wahusika wasaidizi wanaweza kuwa na visa vyao. Kwa mfano marafiki na aila za wahusika wakuu.
    Wahusika Wadogo: ni wahusika ambao wanafanya kazi ndogo sana katika fasihi kama vile kujenga maudhui au mandhari. Wahusika hawa wakitolewa,
    riwaya/tamthilia inaweza kuendela bila kubadilika sana. Kwa mfano mwenye duka ambalo mhusika alinunua kitu fulani.
    Wahusika Bapa â‡’ hawa ni wahusika wasiobadilika kutoka mwanzo hadi mwisho. Kwa mfano, mhusika mbaya anabakia kuwa mbaya kutoka mwanzo hadi mwisho.
    Sifa za wahusika bapa huweza kutambulika mwanzoni mwa hadithi/riwaya. Wahusika bapa hawawakilishi sifa halisia za binadamu. Nia yao ni kujenga tabia moja tu.
    Kuna aina mbili za wahusika bapa:

    Wahusika bapa-sugu – huoenyesha msimamo wao kulingana na masimulizi ya msanii.

    Wahusika bapa-vielelezo – msimamo wao hutambulika kulingana na majina yao. Msanii hutumia mbinu ya majazi au lakabu kuwapatia wahusika majina yanayolingana na sifa zao.
    Kwa mfano: Mhusika Rehema ni mwenye huruma na neema kutoka mwanzo hadi mwisho.
    Wahusika Duara: mhusika duara hubadilika kitabia katika fasihi. Hawana msimamo thabiti. Hubadilika kulingana na maudhui na mazingira. Kwa mfano, msichana aliyeanza kama mpole na mwadilifu anapobadilika na kuwa mtovu wa nidhamu, kahaba na asiyeshirikiana na mtu yeyote.
    Wahusika Wafoili: huwa katikati ya wahusika bapa na wahusika duara. Wanaweza kuchukua msimamo fulani katika maswala fulani lakini pia wanaweza kubadilisha msimamo huo wakati mwingine kulingana na hali. Wahusika hawa hutegemea wahusika duara na wahusika bapa ili kutoa sifa zao. Kwa mfano, wakiishi na mhusika bapa, wanaweza kuchukua msimamo wa mhusika huyo lakini wakikaa sana na mhusika mwengine, wanabadilika. Wahusika hawa aghalabu huwakilisha uhalisi wa binadamu.
    ]]>
    false
    MwlMaeda]]> 2021-07-18T18:11:21Z 2021-07-18T18:11:21Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=591 <![CDATA[SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA]]>
    .pdf   MATUMIZI YA SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA.pdf (Size: 1.34 MB / Downloads: 46) ]]>
    false
    MwlMaeda]]> 2021-07-17T14:53:56Z 2021-07-17T14:53:56Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=587 <![CDATA[TOFAUTI YA FASIHI NA TANZU NYINGINE ZA SANAA]]> Fasihi na tanzu nyingine za sanaa kama uchongaji, ususi, utarizi, muziki, ufumaji, uchoraji, ufinyanzi na maonyesho vinatofautiana kwa kiasi kikubwa kama ilivyoorodheshwa katika hoja hizi:
    • Kazi za fasihi hutumia lugha.
    • Kazi za fasihi hutumia wahusika.
    • Kazi za fasihi hutumia mandhari.
    • Kazi za fasihi huwa na utendaji ambao hujitokeza zaidi katika fasihi simulizi, ambapo, fanani na hadhira yake hutenda.
    • Kazi za fasihi zina fani na maudhui.
    • Huwa na uwanja maalumu wa kutendea
    • Hukutanisha fanani na hadhira ana kwa ana
    • Huweza kubadilika kulingana na wakati na mazingira mfano fasihi simulizi
    ]]>
    false
    MwlMaeda]]> 2021-07-16T10:37:35Z 2021-07-16T10:37:35Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=582 <![CDATA[KWA VIPI FASIHI NI SANAA?]]> Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa ambapo mtu hulitumia umbo hilo kueleza yale anayotaka wengine wayafahamu.
    i. Matumizi ya mtindo katika kufikisha ujumbe. Mtindo humtofautisha mwanafasihi mmoja na mwingine. Kila mwanafasihi ana mtindo wake. Ufundi unakuja pale ambapo ufundi hutumika katika mtindo ambapo mambo kama, matumizi ya barua, dayolojia, monolojia na matumizi ya nafsi hujumuishwa.
    ii. Matumizi ya muundo. Jinsi ambavyo visa hupangiliwa kwa ufundi mkubwa ili kuwezesha kuifikisha kazi ya fasihi kwa walengwa, ndiyo sanaa yenyewe. Maana yake ni kwamba, mwandishi hutumia ubunifu katika kupangilia visa na matukio.
    iii. Matumizi ya lugha. Lugha itumikayo katika fasihi ni tofauti na lugha nyingine. Katika lugha ya fasihi kuna matumizi ya tamathali za semi, misemo, nahau na ujenzi wa picha na taswira. Haya yote yanaifanya fasihi iwe sanaa.
    iv. Matumizi ya wahusika. Si kutumia wahusika pekee, bali ule uchaguzi mzuri wa wahusika huifanya fasihi iwe sanaa. Mwanafasihi anauwezo wa kuamua anataka wahusika wa aina gani katika kazi yake. Ana uwezo wa kumwacha hai mhusika mpaka mwisho wa kazi yake. Pia, ana uwezo wa kuyakatisha maisha ya mhusika yeyote.
    v.  Matumizi ya mandhari. Jinsi mwandishi anavyojenga mandhari yake kwa ubunifu ndiyo huifanya fasihi ikawa sanaa. Kadiri mandhari inavyojengwa na mwandishi ndivyo inavyosaidia kuijenga kazi ya fasihi na kuifanya ieleweke zaidi kwa wasomaji.
    ]]>
    false