MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Mitihani]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ 2024-04-28T20:42:59Z MyBB MwlMaeda]]> 2021-11-11T06:10:51Z 2021-11-11T06:11:13Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1451 <![CDATA[OSW 232: FONETIKI NA FONOLOJIA YA KISWAHILI (JARIBIO KUU – 2020)]]> [Image: 5636e5c6-342c-4362-98aa-a55c7675d3d3-1.jpg]]]> false MwlMaeda]]> 2021-11-11T03:28:38Z 2021-11-11T03:30:21Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1439 <![CDATA[KF 120: MASWALI YA VIKUNDI]]> [Image: maswali.png]
  1. “Vipengele vya kibunilizi na utumiaji wa wahusika katika kujadili dhamira kwenye kazi nyingi za  fasihi andishi ya kiswahili umekuwa ukibadilika toka enzi moja kwenda nyingine”. Muwe huru kutumia kazi zozote za kifasihi kithibitisha ukweli wa hoja hiyo.
  2. “Shaaban Robert katika Adili na Nduguze amefanikiwa kujenga dhamira zake kwa kutumia motifu ya safari”. Jadili.
  3. Huku ukirejelea mawazo na tafiti za wataalamu mbalimbali jadili asili ya riwaya na mchango wa wajerumani kama koloni katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili kihistoria.
  4. Huku ukirejelea mawazo na tafiti za wataalamu mbalimbali jadili asili ya tamthilia na mchango wa Wakenya katika kukua kwa tanzu hiyo.
  5. Huku ukirejelea mawazo na tafiti za wataalamu mbalimbali jadili asili ya ushairi  na mchango wa wareno na waarabu katika kuenea kwa tanzu hiyo.
  6. Huku ukirejelea mawazo na tafiti za wataalamu mbalimbali jadili asili ya ushairi na mchango wa wareno na waarabu katika kukua kwa tanzu hiyo.
  7. Bainisha kwa mifano mchango wa Shaaban Robert katika maendeleo ya fasihi andishi ya Kiswahili.
  8. Jadili jinsi Naratolojia katika Wasifu wa siti bint Saad unavyozipambanua dhamira kirahisi ndani ya riwaya hiyo .
  9. Utomeleaji katika diwani ya Kiswahili na Malenga unaonekana kuwa na faida na hasara katika kujadili dhamira kwenye diwani hiyo. Jadili.
  10.  Wahusika katika riwaya za kingano wanamchango gani katika kujadili dhamira za kazi ya fasihi kihistoria?
  11. Mgogoro wa mswahili ni nani unaathiri vipi maendeleo ya fasihi ya Kiswahili hususani kwenye upande wa dhamira?
  12. Eleza mchango wa wataalamu wafuatao katika kuibuka na kuendelea kwa riwaya ya Kiswahili:
  13. Edward Steere
  14. Carl Veltten
  15. Edwin Brenn
  16. Graham Hyslop
  17. Jadili faida na hasara ya vipengele vya kimajaribio katika kuchunguza dhamira kwenye kazi za fasihi ya kiswahili.
  18. Plato na Aristotle waliweka msingi katika uundaji wa kazi za kisana. Jadili uzuri na ubaya wa misingi hiyo katika kujadili dhamira ndani ya kazi za fasihi ya Kiswahili.
  19. Kujadili dhamira za kifasihi kistoria kuna hasara kubwa zaidi ukilinganisha na faida nyingi tuzipatazo pindi tunapojadili dhamira za kifasihi kwa mtindo mwingine. Tumia mifano lukuki kueleza ukweli wa hoja hii.
  20. Riwaya ya Bwana Muyombekere na Bibi Bugonoka ni miongoni mwa riwaya za Kiswahili za mwanzo kabisa. Jadili dhamira na ufundi unaojitokeza katika riwaya hii.
  21. Maisha ni nini? Wanafalsafa katika fasihi ya Kiswahili wanatoa majibu gani juu ya swali hili?. Je,majibu yao yanakidhi matakwa ya kidhamira enzi hizi za sayansi na teknolojia? Uwanja ni wenu kutoa mifano kun‘tu.
  22. Chunguzeni jinsi Epistemolojia katika fasihi ya Kiswahili inavyokinzana kimaudhui kati ya enzi kabla ya uhuru na baada ya uhuru.
  23. Miaka ya 1970 nadharia ya unegritudi ilitumika sana kuhakiki dhamira katika kazi za kifasihi. Muwe huru kutumia mifano mtakavyo kuthibitisha ukweli wa hoja hiyo.
  24. “Mlimbua nchi ni Mwananchi.” Katika kujadili dhamira za fasihi ya Kiswahili kihistoria methali hii imejipambanua vipi?
  25. “Vipera vya semi vimetumiwa sana na waandishi wa fasihi ya Kiswahili katika kujadili dhamira kihistoria.” Tumia Kiswahili na Malenga na Haki ya Mtu Haipotei kukanusha au kuunga mkono kauli hii.
  26. Huku ukitumia mifano ya kazi za kifasihi, hakiki mabadiliko ya kihistoria kidhamira katika vipindi vifuatavyo:
        (a)  Kabla ya ukoloni
        (b) Wakati wa ukoloni
        ©  Baada ya uhuru

      26. “Mashairi ya Bongo Fleva nayo hayapo nyuma katika kudidimiza na kuibua historia mpya ndani ya jamii ya Waswahili.” Hakiki kauli hii kwa kutumia wanamuziki wanne ndani ya Afrika ya Mashariki.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-10T10:23:55Z 2021-11-10T10:24:34Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1434 <![CDATA[MBINU ZA KUFUNDISHIA - MITIHANI (OUT)]]> [Image: 28c8b248-c4e7-495f-b64f-bc02ea56ba50-707x1024.jpg] [Image: 050badf1-0b8f-45ea-b788-cb2c08aeb61f-684x1024.jpg] [Image: 78c89fb3-fb03-47a9-86a2-2049be3d94eb-706x1024.jpg] [Image: 684a46f6-1aab-4d1d-b6f1-3bd48ab3b6a6-753x1024.jpg] [Image: b9eb6b98-df47-4af6-90f0-02ee14fa5d88-647x1024.jpg] [Image: c5fbf539-c32c-4cea-9f49-48ddbdaf4357-717x1024.jpg] [Image: c57cd9ea-a1aa-49d3-8aaa-3e240fd125af-717x1024.jpg]]]> false MwlMaeda]]> 2021-06-27T12:21:49Z 2021-06-27T12:32:44Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=320 <![CDATA[SWALI: AINA ZA VIRAI KWA MUJIBU WA MASSAMBA NA WENZAKE]]> SWALI:
Jadili mtazamo wa Massamba na wenzake kuhusiana na aina za virai ukilinganisha na mtazamno wa wanazuoni wengine.
UTANGULIZI
Kirai ni dhana pana na yenye mkanganyiko mkubwa kiasi cha kuwaibua wanazuoni mbalimbali ambao kila mmoja amejitahidi kwa uwezo na uelewa wake kufafanua dhana hii. Kwa mahitaji ya swali hili tutatalii mitazamo ya wataalamu mbalimbali akiwemo Massamba na wenzake katika kufasili dhana hii ya kirai na aina za virai.
KIINI
FASILI YA KIRAI
Kwa kuanza na tuangalie fasili ya kirai kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali Massamba na wenzake (2009), wanasema kuwa kirai ni kipashio cha kimuundo chenye zaidi ya neno moja na ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu.
Fasili hii ya Massamba na wenzake inaelekea kutuaminisha kuwa kirai ni lazima kiwe na zaidi ya neno moja. Swali la kujiuliza hapa ni je, neno kuu linalotambulisha aina ya kirai likisimama peke yake haliwakilishi aina husika ya kirai? Ukweli ni kwamba kila neno kuu la kirai lisimamapo pekee huwakilisha aina husika ya kirai hata bila ya kuambatana na kijalizo chochote cha kirai.
Mfano:
Kirai Nomino
Kirai
hiki chaweza kuwa nomino pekee au nomino na kijalizo.
(a) Mtoto mzuri
           KN
(b) Mtoto
        KN
Kihore na wenzake (2007), wanasema kuwa kirai ni kipashio cha kimuundo chenye neno
moja au zaidi lakini bila uhusiano wa kiima kiarifu. Kwao mahusiano ya kiima
kiarifu ni yale yanayoonesha anayetenda jambo na tendo linalotendwa, anayetenda
jambo ni kiima na tendo linalotendwa ni kiarifu.
Mfano:
Mtu mnene/ anachoma nyama.
   Kiima                kiarifu
TUKI, (2011), wanadai kuwa kirai ni kipashio chenye zaidi ya neno moja lakini ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu.Maana hii ya TUKI inawiana na ile ya Massamba na wenzake.
Mdee, J.S (2007) anasema kuwa kirai ni neno au kifungu cha maneno chenye neno kuu moja. Kwa mujibu wa Mdee kirai kinaweza kuwa neno moja au kifungu cha maneno. Uhusiano kati ya neno kuu na maneno mengine (vijalizo) ndio hutambulisha na kutofautisha aina ya kirai.
Fasili zote hapo juu zinashadadia mambo ya msingi kuwa kwanza kirai sharti kijikite katika mahusiano baina ya maneno ambapo huwa kuna neno kuu moja linalotawala aina ya kirai, pili neno kuu la kirai huweza kusimama pekee au kuambatana na kijalizo kimoja au zaidi. Hivyo basi kirai kinaweza kusimama kama neno moja au zaidi iwapo tu kuna neno kuu linalotawala na kumiliki maneno mengine.
AINA ZA VIRAI
Kuhusu aina za virai wataalamu pia wametofautiana, tofauti zao zipo hasa katika aina na idadi lakini pia matumizi ya istilahi zao.
Massamba na wenzake (2009) wanatambua aina tano za virai ambazo ni:
·      Virai – nomino
·      Virai – vitenzi
·      Virai – vivumishi
·      Virai – vielezi
·      Virai – viunganishi
Zabron, T.P (2017) yeye anatambua na kutetea aina sita za virai ambazo ni:
·      Kirai – nomino
·      Kirai – kitenzi
·      Kirai – kivumishi
·      Kirai – kielezi
·      Kirai – kihusishi 
·      Kirai – kibainishi
Naye Mdee, J.S (2007) anatambua aina tano za virai ambazo ni kama zifuatazo:
·      Kirai – nomino
·      Kirai – kitenzi
·      Kirai – kivumishi
·      Kirai – kielezi
·      Kirai – kihusishi
Ukichunguza kwa makini miongoni mwa wanazuoni waliorejelewa katika kazi hii utabaini kuwa kuna mfanano juu ya idadi kati ya Massamba na Mdee isipokuwa Zabron ambaye anatambua aina sita. Baada ya uainishaji huo hapa chini tutaonesha tofauti baina yao kwa kurejelea aina wanazotofautiana na misingi ya utofauti huo.
TOFAUTI ZA AINA ZA VIRAI
Kwa kuanza na kundi la Massamba na wenzake, wao hawatambui kirai kihusishi badala yake wanatambua kirai kiunganishi. Kiunganishi kinaelezwa kuwa ni neno linalounganisha pande mbili zenye hadhi sawa kisarufi. Msingi wa tofauti hii ni kutokana na ukweli kwamba maneno yanayotumika kama kiunganishi ndiyo pia hutumika kama kihusishi.
Maneno hayo ni kama vile: Ingawa, Na, Kwa kuwa, Bila, Pasipo, Sembuse, Lakini,
Mfano:
Baba alifika ingawa mama hakumuona
Shule imejengwa na mafundi wameondoka
Wanafunzi walifeli kwa kuwa walimu hawakuwafundisha ipasavyo
Kwa upande wa Mdee, J.S (2007) na Zabron, T.P (2017) wanatambua kirai kihusishi kama aina moja wapo ya virai na hawatambui kirai kiunganishi. Mdee, (ametajwa) anasema kirai kihusishi ni kirai ambacho neno kuu ni kihusishi na Kihusishi ni neno linaloonesha uhusiano baina ya pande mbili zenye hadhi tofauti kisarufi.
Mifano ya maneno yaundayo kirai kihusishi ni kama vile:
Kwa, ya, na, au katika
Mfano:
–       Alienda kwa miguu
–       Atakuja kwa amri yako
–       Anasoma na mama
–       Amelala katika chumba
Kwa upande mwingine Zabron, T.P (2017) yeye pamoja na kutambua kirai kivumishi kama wengine pia ameongeza aina moja zaidi
ijulikanayo kama kirai kibainishi (KB). Anafafanua zaidi kuwa KB ni kirai ambacho neno kuu ni kibainishi. Vivumishi vibainishi vinaundwa na maneno kama vile: wawili, changu, kile, wote, hawa au wangu.
Mfano:
–       Wanafunzi wale pale
–        Kitabu hiki
–       Wachezaji wote hawa
Wapo wanaoona kuwa aina hiyo ya kirai ni sehemu tu ya kirai kivumishi na pengine ndio sababu ya kutoainisha kama aina ya
kirai inayojitegemea.
HITIMISHO
Kwa ujumla dhana ya kirai ni pana na yenye utatanishi mkubwa usioweza kumalizwa kwa urahisi. Ikumbukwe kuwa dhana hii inaukilia zaidi misingi ya kisarufi ya umiliki na utawala wa kategoria za maneno ambapo maneno makuu humiliki na kutawala maneno mengine katika msululu wa kategoria za maneno. Watangulizi katika taaluma hii walianza kwa kuainisha aina tano za maneno makuu ambazo ndizo zilizotumika kama kigezo kikuu cha kuamulia aina ya kirai. Hivi leo mitazamo inazidi kuibuka kutokana na mwamko wa wanazuoni wa kisasa katika kushughulikia dhana hii. Hata kazi hii itabaki kuwa kwego ya kuendelezea mpando wa kitaaluma katika kuifikia kweli ilipo.
MAREJELEO:
Massamba D.P.B na wenzake (2009) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA): Sekondari na vyuo, TUKI, Dar es salaam.
Mdee, J.S (2007) Sarufi ya Kiswahili: Sekondari na Vyuo, DUP, Dar es Salaam.
Kihore Y.M na wenzake (2007) Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA): Sekondari na Vyuo, TUKI, Dar es salaam. TUKI
(2011) Kamusi ya Kiswahili Sanifu.  TUKI, Dar es salaam.
Zabron, T.P (2017) Miundo Msingi ya Sarufi ya Kiswahili. Karljamer Publishers Ltd, DSM.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-27T12:06:38Z 2021-06-27T12:06:38Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=319 <![CDATA[OSW 121 / OSW 131 : UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU –JARIBIO KUU MAALUMU —Alhamisi , 05]]>
.jpg   JARIBIO KUU.jpg (Size: 52.63 KB / Downloads: 9) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-27T12:01:10Z 2021-06-27T12:01:10Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=318 <![CDATA[OSW 226: USHAIRI WA KISWAHILI—JARIBIO KUU—-Ijumaa , 10 February 2012]]>
.jpg   JARIBIO KUU.jpg (Size: 50.21 KB / Downloads: 3) ]]>
false